Maisha ya libya huwezi fananisha na nchi yoyote africa lakini wananchi wamesema .....

mpingomkavu

Member
Nov 26, 2010
94
0
Jana wakati nasikiliza BBC kuna mchambuzi mmoja toka Libya akawa anaelezea maisha ya wananchi wa Libya kwamba, ELIMU BORE BURE,AFYA BORA BURE, UMEME NA MAJI BURE NYUMBA UNAPEWA NA SERIKALI BURE,Na zipo nyumba kama 7000 hazina watu. Mchambuzi alienda mbali zaidi kwa kusema kuwa hadhi ya hospital huwezi linganisha na MUHIMBILI,Lakini wananchi wamesema Gadaffi inatosha pisha na wengine, Leo hii Tanzania mwananchi kupata mkate wake wa kila siku ni shida, wafanyakazi wanaishi kwa mikopo tu,LAKINI BADO WANAWAPIGA KURA CCM, KWELI AKILI ZETU ZIMEFUNGWA MPAKA BABA WA TAIFA AJE KUZIFUNGUA.Nauliza hiv sisi ni nini kinatushinda?
 


Defiant Gaddafi vows to fight on

In televised speech, Libyan leader blames youths inspired by regional events for uprising and vows to die a 'martyr'. ( 23-Feb-2011 )

SWALI HUMU: UTAMADUNI WA KURITHISHA WATOTO WA WAKUBWA
UKUBWA TANZANIA CHANZO CHAKE NI WAPI???


Nani anayejua hasa darasa la huyu King of Kings?

Kwa mtaji wa hutuba aliyoitao hivi majuzi ni mara mia angjinyamazia tu hivyo tungeendelea kumfikiria mstaarabu fulani hivi. Kwa kujiunga kwake jeshini akiwa na umri wa miaka 12 (child soldier) wala hatuhitaji kuuliza kama 'ALIONEWA SANA YEYE', 'AKADHALILISHWA SANA GADDAFI' hivyo kuja kupata kamwanya wa kuongoza nchi kwa mtindo wake mwenyewe hivi sasa anarudishia ngumi kwa jamii nzima ya Libya.

Tujifunze kitu basi na sisi hapa kwamba wale tuliowahi kuwaondoa kwenye nyadhifa fulani hapa nyumbani kufuatia kashfa iliyogoma kwisha katikati yetu hadi leo, nao wakija tu kupata urais wa nchi hii mtindo wao wenyewe na tusifikirie matendo yao kutofautiana sana na ya huyu nduli hapa.

Hakika shule iliomuingia mtu na kutulia ndani mwake ni muhimu zaidi tena sana kuliko shule ya kupitia hata kama madarasa yako ni mengi kimahesabu vidoleni.

Kanali Gaddafi ajikaanga kwa ulimi wake mwenyewe. Na watoto wake , masikini ya Mungu, ndio kabisaa wanaamini taifa zima la Libya ni kama shamba binafsi la ukoo kwa baba yao.

Nikitazama ya Ben Ali wa Tunisia, nikamgeukia Hosni Mubarak wa Misri na kumtaza mzee huyu ambaye kimawazo ni 'chipukizi' tu, na mwenendo mzima wa ushiriki wa familia zao katika mambo ya utawala wa nchi, Wa-Tanzania wenzangu NAPATA MAJIBU KUBWA SANA HAPA HAPA NYUMBANI kwamba ni kwa nini kati ya marais wetu wote wanne ni wawili tu kati yao ambao waonekana kupenda saana KUWARITHISHA UKUBWA WA TAIFA HILI kimtindo!!

Endapo Hussein Mwinyi hatojiuzulu ya Gongolamboto kwa kiburi tu kama ya watoto wa marais niliotangulia kuwataja kaskazini mwa bara hili basi huenda hata UKUBWA WA ZANZIBAR unaotazamiwa kwake ukagoma lakini ya Muungano ndio kabisaaaa wa kusikia tu redioni.

Je, inamaana wazee wengine akina Salim Ahmed Salim, Sinde Warioba, Mwalimu Nyerere, Phili Mangula, Joseph Rwegasira, Salmin Amour, Seif Shariff Hamad, Duni Haji Duni, Bibi Titi, Mama Mongela, Edith Mnuo, Dr Slaa, Prof Mwandosya, Prof Baregu, Mzee Kisumo, Edwin Mtei, Kambona, na wengine wengi tu ... wao hawana watoto wa kuwea nao kutamani kuwarithisha UKUBWA???

Katika hili tayari Vijana wa Tanzania TUMEWASOMA MCHEZO MZIMA na majibu tunayo!!!
 
Yeah Mpingo mkavu unachokiongea ni kweli kwani hata kuna watz wapo huko wanasoma bure wamepewa nyumba pia free of charge hakuna mgao wa umeme wala mgao wa maji kutoka Ruvu Chini
 
Mahitaji na matarajio ya binadamu sii chakula, mavazi, malazi na huduma za afya tuu,

Hiyo ni hatua ya kwanza ya piramidi ya mahitaji.

Pengine wenzetu Libya wamefaulu hii hatua ya mwanzo muda mrefu uliopita.

Sasa wanapigania hukwea hatua ya pili.

Masikini weee Tanzania yangu.
Ndio kwaaanza tupo hatua ya kwanza kwa miaka hamsini sasa.
Na bado hatujitambui.

Inatia uchungu sana na maumivu ya moyo na roho.
 
haya machafuko yameandaliwa na wataalam wa Israel.
mfahamu kwa israel imegundua Gas reserve kubwa ktk bahari ya mediterania na hii Natural resource inauongozi wote hitaji usimamizi wa ushirikiano .ndo maana wote north africa unabadilishwa.tusubiri tuone matukio.
Did you know kuna Jewish Member of parliament in Iran anaitwa Maurice Motamed
u can read more about huyu mbunge wa Iran ambaye ni Myahudi/muisrael
ZCommunications | Iran's Jewish MP by Ewen Mcaskill | ZNet Article
its not conspiracy ndio hali halisi.Pia kiongozi wa uslama wa israel amebadilishwa ili kujipanga na matukio haya.
 
Back
Top Bottom