Maisha ya kijijini

Maisha ya kijijini

Mie niliendaga Rombo Mkuu kumtembelea mjomba. Wenyeji wa huko (Wachaga wa rombo) ni very hardworking. Mashamba yao yako mbali sana; wanalima mpakani na Kenya. Mama akiondoka asubuhi saa 12 kurudi kwake ni saa moja jioni! Kivumbi ndo kiko hapo saa ya kurudi. Mama anaporudi ataanza kazi ingine ya kulisha mifugo kama mbuzi, ngombe nk. Kazi hii inaisha saa 2 au 2.30 usiku ndo aanze shughuli za chakula cha usiku. Bwana wee! Siku mbili za mwanzo nilitaka kupiga kelele kwa njaa kali. Chakula huiva saa 5 au sita usiku! Ukimaliza kula, jogoo za mwanzo unazisikia! Wachana na maisha ya kijijini aisee!
 
mh,me nakumbuka meng sana kijijin. kusenya kuni,kuchota maji mton,kupuliza moto. bas kulikuwa na chuma flan hv km bomba tulikuwa twalitumia kupulizia moto linaitwa "fududu" wenyej wa kule kwetu watakuwa wanalipata. afu na kuogelea mtoni. dah nkikumbuka huwa nacheka sana!

Umenikumbusha Friji asilia za kijiini. Ikinunuliwa nyama inatundikwa juu jiko .ule moshi wa jiko utaikausha nyama basi itadumu hata kwa kwa mwezi. Maana vijiji vingine hakuna bucha zanyama na ng'ombe wanachinjwa kwa msimu La sivyo kutafuta nyama tu inaweza kubidi utembee mpka kilmita tano

hahahaaa!
Charminggirl nini unafurahia na sisi tuwe charmed
 
Last edited by a moderator:

mh,hyo kikwetu inaitwa nyama singisi.
 
Last edited by a moderator:
Nadhani ni pole, lakini nipo kujifunza kwa watu halisi na sio Juma na Rosa :smile-big:
Gaijin
Kutokana na avatar yako nadhani utakuwa na mengi ya kutupa kwenye maisha ya Boadrding skuli. Kama ulisoma hata boarding skuli ya kijijini chakachua thread . teh teh sijui mazinde juu huu mazinde chini .........
 
Last edited by a moderator:
Nakumbuka kwenda kufua nguo za shule mtoni kila jmosi,kuogelea na kuvua visamaki flani vinafanana na kambale mto karanga moshi
 
Gaijin
Kutokana na avatar yako nadhani utakuwa na mengi ya kutupa kwenye maisha ya Boadrding skuli. Kama ulisoma hata boarding skuli ya kijijini chakachua thread . teh teh sijui mazinde juu huu mazinde chini .........

Hapana sijawahi kwenda boarding school na nashukuru kwa hilo. Ningeyaweza wapi mie!

Mie home schooled kwenye mambo ya house keeping :wave:
 
Nakumbuka mkitoka shamba na mzgo wa kuni,halafu nyakat za ji0n maeneo ya PORIN,INAWEZA ZUKA HARUFU YA WALI,AU MIHOGO YA KUCHEMSHA .
-mkienda mtoni,wanawake wanaoga wakiwa na chup! Za taiwan hasa nyekundu na blak,wengine wana magagulo,then wanaume wanazo za V.I.P,
 
Mi kule kila kitu ni raha.Ntawasimulia kesho.

Loh?
Pole Mama Ashrat, naona coment yako wameipotezea, wana roho mbaya sana hawa member wazoefu.
Mimi nimezaliwa Ocean Road, nimesoma Msasani Msingi, Kibaha Sec. na Azania, nimeishi Mikocheni A, na Mungu akijalia nitazikwa makaburi ya Kinondoni.
Zeafoo ai noo nasingi kuhusu kijijini.
 
Last edited by a moderator:
Hapana sijawahi kwenda boarding school na nashukuru kwa hilo. Ningeyaweza wapi mie!

Mie home schooled kwenye mambo ya house keeping :wave:

Basi mpaka miaka ya karibuni mtoto wa kikeaumwanamke kuvaa suruali kijijini kwetu ilichukuliwa ni uhuni. Sasa sijui watunza mila na desturi wakija mijini wakiona kinadada na kinama mama wakiwa na skin tight tena tight hasa wanaonaje ......
 
Mwanamke kavaa serewili na matiti yamepigwa jeki!
 
  • Kijijini akifariki mtu kazi zote zinasimama sijui hii bado inaendelea?
  • Haurusi au sherere ya kijijini haina kadi . Ni diso vumbi kwa kwenda mbele. Dj lazima awe na kanda ya lucky dube
 
Back
Top Bottom