Maisha ya kijijini yalivyo na furaha

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,542
22,049
Miongo kadhaa iliyopita, nayawaza maisha yangu yalivyokuwa kijijini.
Nimetokea familia ya wafugaji, kwa hiyo maisha yote yalikuwa ni porini mda wote nikichunga ng'ombe.

Hakukua na chai kama huku mjini! Asubuhi tulipikiwa ugali kwa lugha nyingine (cha mchungaji -yaani break fast). Ni chakula tulichokuwa tunakula asubuhi kabla ya kuondoka na mifugo porini.

Kule machungani ufahari tulizidiana kutokana na mifugo tuliyokuwa nayo;
Mchunga mbuzi alimzarau mchunga kondoo na mchunga ng'ombe alionekana bora kuliko mchunga punda.

Hata kiafya tu, mchunga mbuzi alionekana kukonda sana kwakuwa mbuzi hawatulii kitu ambacho mchunga mbuzi lazima awe na mbio, maana mbuzi hula kwa kuruka ruka na pengine kukimbilia mashamba ya watu jambo ambalo mchunga mbuzi lilimfanya aongoze kwa kesi za malisho.

Kifupi mchunga mbuzi hana raha kisaikolojia! Mchunga kondoo, huyu ndiye aliyekuwa mtu mjinga kuliko wachungaji wote, akili ya mchunga kondoo imezubaa kama kondoo wenyewe; mliokulia vijijini mtanielewa.

Raha tuliyojivunia
kule porini kuna mchezo wa kugombanisha mafahari ulitawala, ilikuwa ni burudani sana asikwambie mtu.

Ushamba wa magari
Kusema ukweli enzi hizo kuiona Gari ilikuwa nadra sana, nakumbuka tulikuwa tunapanda mrima na miti mirefu ili kuona Gari zilizokuwa zinapita barabara Kwa mbaali mithili ya kilomita zaidi ya ishirini.

Maajabu ya msituni
Tulizoea porini kiasi kwamba tulizoea, hatukuogopa lolote, tulicheza na kupuliza mziki porini, tulipiga zeze na marimba pamoja visiki Vya miti, burudani ilizidi kuwa taam maeneo ya milimani;

Maajabu ya milima
Kuna mlima ulikuwa na mawe yaani ukiongea na lenyewe linaitikia mwangwi mfano "Helloooo! Na jiwe nalo linaitikia " Hellooooooooooh! Ilikuwa zaidi ya muvi ya tazani.

Tulishindana kuporomosha mawe kutoka mlimani; na yaliporomoka kwelikweli. Tulitengeneza manati na michezo mbalimbali ya kurusha mawe kwa kombeo; kombeo kwetu ilikuwa ni zaidi ya bastola; (kombeo ni kamba ndeefu yenye jiwe katikati tulioizungusha na kurusha.

Video na sinema siku za sikukuu
Yaani kulikuwa na zile sinema za kuzungushwa kwenye baisikeli; jamaa walizunguka kijiji hadi kijijii kingine, burudani ilitawala pale jamaa wakifika kijijini kuonesha video.

Ilikuwa ni furaha sana japo ile Tsh.50/= ya kiingilio sikuwa nayo! PICHA zilioneshwa usiku, japo zilitangulizwa kwa kuonyeshwa trailer " (PICHA ya utangulizi) wale wenzangu na mimi tulitumia mda huo kukariri kila kitu na tunahadithia kuliko hata aliyetazama picha nzima.

Picha la usiku tulisubiri fungulia mbwa, yaani dakika kumi kabla picha kuisha! Daah ni maisha ya kule kijijini nikiwa na marafiki zangu.

Kweli Mungu Muacheni aitwe Mungu; kwasasa kila mmoja ana maisha yake mjini hapa; wengine tunamshukuru Mungu sasa tunamiliki makampuni na maduka kadhaa, rafiki zangu sasa wengine ni mawaziri na wakuu wa mikoa na wilaya.

Kijijini kuna watu muhimu sana wakipatiwa fursa wanaweza.
Kitu gani hutakisahau ulivyokuwa kijijini enzi hizo?

=========
Michango ya wadau

Nakumbuka nilipoteza Ng'ombe mmoja kutokana na ubize wa kutega ndege aisee nilichapwa sana nyumbani siku ya pili alfajiri nilipelekwa na brother kumtafuta Ng'ombe aliyepotea jana yake kwa bahati mbaya tukapita pale nilipokua natega ndege si ndege akakurupa akanasa weeee kaka anajua mchezo mzima wa jana kumbe kisa cha kupoteza mfugo ni kutega ndege fimbo zikaanza upyaaaa

Nakumbuka kuchapwa na kushtakiwa kwenu endapo mifugo yako itakula shamba la watu.

Wali ni chakula cha sikukuu
Wakati wa sikukuu kama jana nguo mpya ni muhimu ununuliwe otherwise hata kuchunga hutaenda kwa moyo mmoja.

Kuangalia video kwa watu na kwenye mabanda ya video kiingilio ni Tsh 100 ila kuipata labda upewe kwenu au uibe somewhere

Ukisikia kesho mama atafiri nawewe kwenda mjini au mkoani mtapanda basi aisee haulali kila muda unastuka kuangalia kama mama kakuacha usiku unakua mrefuuu.

Kuona gari mpaka uende mjini au lipite gari kijijini kwenu Mara nyinyi yalikua magari ya makanisani( wakatoliki wazungu)
Tukimuona mzungu tunamuomba ela tuliamini wazungu wote ni matajiri
Yapo mengi sana nakumbuka
----
Zamani sana umenikumbusha
kuwinda sungura kama huna mbwa mawindo yatayopatikana
Hulambi kitu ukiwa muoga wa
Kupigana utakuwa tingo wa
Kurudisha mifugo isiende mbali
Kama una mifugo michache wewe
Ni fala mbele ya wenye mifugo
Kugombana na wenye mashamba
Kisa mifugo yako hawataki uchunge kwenye shamba lake
Kesi za mifugo kula mazao ya watu Kuiba miwa karanga mahindi mihogo viazi kwenye mashamba ya watu
kwenye sekta hii mimi nakuwa kinara nilikuwa bingwa wa kuiba miwa na nikaondoka eneo la tukio bila kujulikana
Nilikuwa nakata miwa katikati
Ya shamba halafu naifunga mitatu
Mitatu nachukua kama namfungia ng'ombe mguuni anakuwa anaivuta mpaka natokomea mbali tunaenda kula
Duuuh! Kuna mengi sana tumeyafanya kijijini ambayo siwezi kuyasahau
----
Haliitwi kombol linaitwa KOMBEO kama lile la stori ya Daudi na Goliati kwenye biblia. Nilikuwa mtaalam sana wa kurusha hii kitu (kombeo).

Siku moja tulikuwa tunapim umbali wa kurusha tunashindana ns anatumwa mtu sehemu ya mbali afu yeye ndiye atakuwa mwamuzi sikumoja nikambahatisha rafiki yangu bonge la ngeu damu mpaka akazimia. Niliogopa sana mama yake alianzisha msala nyumbani kwetu kwamba akifa basi tujue wapi tutampeleka

Raha nyingine kuwinda sungura na madogi nawakumbuka mbwa wa brother wangu kwa majina, PIROT, Pop, Chui, simba,tiger na Tax hawa umbwa kwa nyakati tofauti walikuwa ni noma sana.
----
Dah umenikumbusha mbali sana wakati huo wa utotoni. Kundi la mbuzi na kondoo, mbuzi wanakimbia huku na kule tofauti ya kondoo wao kutembea kikundi wakiwa wavivu wa mwendo.

Nakumbuka katika hao kondoo kukawa na madume ambao tuna washindanisha kupigana vichwa kundi lako likishinda wee ndio mbabe wa vikosi vingine.
Siku ambayo sitahisahau ni siku moja dume ktk kundi langu kumpiga mama mmoja alikwenda kuokota kuni hadi kumvunja mguu. Siku hyo nilitamani hata ardhi ipasuke maana msaada sikuwa nao Yule mama alikuwa analia kwa sauti kubwa hadi watu wa mbali wakaja. Niliswaga kundi langu japo mida ya kurudi ilikuwa bado na ikaniwia ngumu maana hao mbuzi na kondoo walishazoea kusoma mida ya kurudi.

Waligoma na baada ya kuona vile kuna dalili ya kuchezea mboko niwaacha na kutimua mbio hadi nyumbani nikatoa habari. Story ni ndefu na ndio ilikuwa mwanzo wa kuchunga. Kweli maisha ya kijiji ni ngumu sana kusahau
 
Ni dhahili shairi maisha ya kijijini yana changamoto zake hivyo nimechunga sana mbuzi wakati huo bado nasoma elimu ya secondary hivyo niliacha kuchunga mbuzi baada tu ya kufaulu kujiunga form five namshukuru Mungu mpaka sasa nimemaliza chuo mwaka 2015 hivyo natafuta kazi tu coz nilisoma mambo ya civil engineering DIT
 
kutega ndege kwa kutumia nywele za mkia wa ng'ombe (butinga)
kurina asali za kwenye milingoti..
kuwinda sungura..(hapa mwenye mbwa ambaye ana spidi kila siku sherehe
Hahahaha umenikumbusha sungura alivyokuwa hakamatiki kirahisi; kuna jamaa alivamia zinga nyuki aling'atwa balaa
 
Ni dhahili shairi maisha ya kijijini yana changamoto zake ivo nmechunga sana mbuzi wakati huo bdo nasoma elimu ya secondary ivo niliacha kuchunga mbuzi baada tu ya kufaulu kujiunga form five namshukuru mungu mpaka sasa nmemaliza chuo mwaka 2015 ivo natafuta kazi tu coz nilisoma mambo ya civil engineering DIT
Halloo hongera sana mkuu
 
Yaani nakumbuka tu enzi za kuchunga ng'ombe kijijini kwetu tumekula sana mtunda fulani hivi yakiitwa mambolesi, tumetengeneza vimipira vinavyodunda yaan vimdundo kwa kutumia utomvu wa miti flan hv, tumeokota sana matunda yakidondoshwa na nyani.... enzi hzo tumekula sana viazi vitamu na magimbi tukiyachoma kwa stail tuliyoiita kabhunguja na mambo mengine meng

Sasa ni miaka ming sana imepita nikienda kijiji huwa nadata sana nikiangalia kwa mbali yale maeneo.
 
Enzi hizo nipo kijijini nikisoma gazeti la Sani nilikuwa najua Madenge anaishi Dar
 
Nimeelezea Kwa walio mjini ili kuonyesha ukinzani; sasa kosa hapo lipo wapi?
Nakuzingua usichukulie serious mwee!! Sijazaliwa kijijin ila nilikua naenda sana utotoni mwangu.... kuna vitu navikumbuka huwa nabaki nasmile...ile situation ya kwenda kuvua samaki mto kandete....kula usipa na mbasa...kwenda mtoni kutafuta majani flan ivi kwa ajili ya kusukia mikeka basi nilikua naona burudaaani!! Utoto bwana
 
Nakumbuka nilipoteza Ng'ombe mmoja kutokana na ubize wa kutega ndege aisee nilichapwa sana nyumbani siku ya pili alfajiri nilipelekwa na brother kumtafuta Ng'ombe aliyepotea jana yake kwa bahati mbaya tukapita pale nilipokua natega ndege si ndege akakurupa akanasa weeee kaka anajua mchezo mzima wa jana kumbe kisa cha kupoteza mfugo ni kutega ndege fimbo zikaanza upyaaaa

Nakumbuka kuchapwa na kushtakiwa kwenu endapo mifugo yako itakula shamba la watu.

Wali ni chakula cha sikukuu
Wakati wa sikukuu kama jana nguo mpya ni muhimu ununuliwe otherwise hata kuchunga hutaenda kwa moyo mmoja.

Kuangalia video kwa watu na kwenye mabanda ya video kiingilio ni Tsh 100 ila kuipata labda upewe kwenu au uibe somewhere

Ukisikia kesho mama atafiri nawewe kwenda mjini au mkoani mtapanda basi aisee haulali kila muda unastuka kuangalia kama mama kakuacha usiku unakua mrefuuu.

Kuona gari mpaka uende mjini au lipite gari kijijini kwenu Mara nyinyi yalikua magari ya makanisani( wakatoliki wazungu)
Tukimuona mzungu tunamuomba ela tuliamini wazungu wote ni matajiri
Yapo mengi sana nakumbuka
 
Sitosahau jinsi nilivyokimbizwa ni nyuki,nikawachenga kwa kujifukia na udogo wakarudi porini wakashambulia ngombe mmoja akambia akaanguka kwy shimo wakaanza kudung'a mpk akafa! Maisha ni safari ndefu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom