sepema
JF-Expert Member
- Jun 13, 2019
- 591
- 1,000
Salaam wakuu...
Kisa Cha Ibrahimu na Isaka kimeelezwa vizuri katika vitabu vitakatifu vya dini.
Katika biblia,kitabu Cha mwanzo 22 mstari wa1-14 kinaeleza tukio la Mungu kumjaribu Ibrahimu amtoe mwanae wa pekee Isaka kuwa sadaka. Ikumbukwe sadaka ilikua nikumchinja Isaka na kuuchoma mwili wake kwa Moto.
Wakiwa njiani kuelekea sehemu ya kutolea sadaka, Isaka akamuulza babake kuwa kondoo mwenyew Yuko wapi maana kisu, kuni na Moto tunavyo.
Ibrahimu alijibu kiutu uzima kuwa twende tu mwanangu, kuhusu kondoo Mungu atatupatia huko huko.
Walipofika sehemu husika, ghalfa Isaka akashangaa anakamatwa na babake nakisha kufungwa tayari kwa kuchinjwa.
Wakati kisu kinakaribia kufika shingoni, Mungu akaingilia Kati kwa kumuonyesha Ibrahimu kondoo halisi aliyekua pembeni kwenye kichaka.
Swali langu; Baada ya Ile Hali kutokea, Isaka alimchukuliaje baba yake?
Pili, Ibrahimu alimtonya mkewe kuhusu agizo la kumtoa Isaka kuwa sadaka?
Tatu, Kama Ibrahimu hakumtonya mkewe, nifundisho gani tunalipata kwa wanandoa kushirikishana Mambo makubwa na nyeti?
Mwisho; Kama Mke wa Ibrahimu hakuambiwa kuhusu tukio lile, Kuna uwezekano alikufa bila kujua kuwa mwanae alitaka kuchinjwa na babaake au labda Isaka alimhadithia mamaake avyonusurika huko porini?