Maisha ya Ibrahimu na mwanae Isaka yalikuaje baada ya lile jaribio la kumchinja kuahirishwa?

sepema

JF-Expert Member
Jun 13, 2019
591
1,000
Salaam wakuu...

Kisa Cha Ibrahimu na Isaka kimeelezwa vizuri katika vitabu vitakatifu vya dini.

Katika biblia,kitabu Cha mwanzo 22 mstari wa1-14 kinaeleza tukio la Mungu kumjaribu Ibrahimu amtoe mwanae wa pekee Isaka kuwa sadaka. Ikumbukwe sadaka ilikua nikumchinja Isaka na kuuchoma mwili wake kwa Moto.

Wakiwa njiani kuelekea sehemu ya kutolea sadaka, Isaka akamuulza babake kuwa kondoo mwenyew Yuko wapi maana kisu, kuni na Moto tunavyo.

Ibrahimu alijibu kiutu uzima kuwa twende tu mwanangu, kuhusu kondoo Mungu atatupatia huko huko.

Walipofika sehemu husika, ghalfa Isaka akashangaa anakamatwa na babake nakisha kufungwa tayari kwa kuchinjwa.

Wakati kisu kinakaribia kufika shingoni, Mungu akaingilia Kati kwa kumuonyesha Ibrahimu kondoo halisi aliyekua pembeni kwenye kichaka.

Swali langu; Baada ya Ile Hali kutokea, Isaka alimchukuliaje baba yake?

Pili, Ibrahimu alimtonya mkewe kuhusu agizo la kumtoa Isaka kuwa sadaka?

Tatu, Kama Ibrahimu hakumtonya mkewe, nifundisho gani tunalipata kwa wanandoa kushirikishana Mambo makubwa na nyeti?

Mwisho; Kama Mke wa Ibrahimu hakuambiwa kuhusu tukio lile, Kuna uwezekano alikufa bila kujua kuwa mwanae alitaka kuchinjwa na babaake au labda Isaka alimhadithia mamaake avyonusurika huko porini?
 
Hutopata unachotaka! Jiongeze biblia imejaa mafumbo
 
Zamani ilikuwa ni kawaida kuwatoa watoto dhabihu kwa Mungu eti kwamba sadaka ya kuteketezwa ile unayoipenda zaidi ndio nzuri zaidi. Mnajua Jephta alimtoa mwanaye wa kike na nani sijui aliwajengea wanae katika kuta za hekalu/ukuta sijui.

Muendelezo wake ndo kama sasa hivi mtu akikushawishi kumtolea Mungu mali kubwa 'itakayokuuma' eti ndio utakuwa umeonesha kumpenda zaidi.

Ifahamike wazi Mungu hajawahi kuhitaji sadaka all along, na hata kama ukikaza shingo kwamba ni lazima kumtolea toaga tu kwa mapenzi yako sio eti kama ni kitu anakihitaaaaaaaaaaji🤨.

Kwa mtazamo mama yake, na mwanae hawangemchukulia baba yao kama katili binafsi, no hard feelings. Wangeshukuru tu kwa pamoja na waliendelea kupendana zaidi. Maana mtoaji na mtolewaji wote walikuwa na hisia kwamba hilo ni jambo zuri sana. Mtoto labda hata aliona kapendelewa, kapendwa zaidi, kutolewa ikawa ni ishara ya upendo zaidi kuliko ukatili.

Mnakumbuka yule binti wa jephta/sijui joshua pia. Hata yeye atakuwa aliona yeye kutolewa ni jambo sahihi kabisa. Msiwaone wa ajabu, au msione kifo ni kitu kibaaaaaaya. Kufa kwa ajili ya kusudi/worthy goal huendelea kuchukuliwa kitu cha heshima. Wanaokufa RUSSIA NA UKRAINE ni uthibitisho tosha. Kilichobadilika ni goals tunazozichukulia ni worthy kulingana na utamaduni wa wakati husika
 
Kwenye mafundisho yakislam yanasema Ibrahim alimwambia is-haka juu ya mungu kumtoa sadaka,Isaka akasema Kama ni amri toka kwa mungu nipo tayari kwa hiyo Isaka alipewa tarifa.
 
Isaka alijua kuwa baba yake alijaribiwa. Nae aka'appreciate Imani ya baba yake.

Isaka hakumwambia mama yake. Mambo ya wanaume ni ya wanaume. Huo ndo uanaume. Siku hizi wanaume wamekuwa masnitch kama wanawake.
 
Back
Top Bottom