Maisha ya depo

Maisha ya depo

Mwanzilishi: Sisi wakali bwana wee
Masela: Wanaukali gani kama sisi
Mwanzilishi: Sisi wakali sana
Masela: Wanaukali gani kama sisi
Mwanzilishi: Sema wanamapanga🗡 hao, wana mabisu🔪hao watakutoa roho bure ganja 🌿wamemwaga na pepa🧻 wamechana masela utawaambia nini”

Zilikuwa ni shangwe za wanajamvi👨‍👧‍👧👫 wakipiga jaramba🏃‍♀️ baada ya kumuona mtunzi wa simulizi ya maisha ya depo akirandaranda kwenye uzi huo.

Akiwa amechoka sana baada ya kukimbia kwa umbali mrefu akajikuta anajikwaa na kuanguka ndipo BOGI lile la watu likamtwaa na kumuweka kitako na kuanza kumhoji.

“We bwana vipi mbona unatuzingua ile simulizi ulituambia itaendelea lakini mpaka leo kimya bora ungetuambia imeisha tungekuelewa🥶” alikuwa ni Aiylan wasalan aliyehoji akiwa na jazba kilo mbili huku mkono wake wa kulia ukiwa umeshika tofali lililokuwa likikaribia kwenye utosi wa mtunzi wa simulizi hiyo.

Akiwa anatetemeka kwa hofu mithili ya bonge la bwana lililofumaniwa ugoni😄 mtunzi huyo akajibu,

“Ni kweli nilisema itaendelea nikimaanisha kuwa haijaisha ila sikusema ni lini lini itaendelea🔜”.

“Aaaaah” lilidakia kundi hilo la watu lililomuweka mtu kati mtunzi wa simulizi hiyo.

“Hembu nipisheni anatuzingua huyu anajifanya anajua sana kiswahili eti kwa kuwa hajasema itaendelea lini ndiyo anatumia kama sababu ya kujitetea!😡 kwahiyo kwakuwa hajasema itaendelea lini tusubiri mpaka mwakani kwasababu hajasema itaendelea lini!😞”

alikuwa ni Kacheda mjasiliamali na rungu lake mkononi aliyekuwa akijitahidi kuwasukuma wenzake ili wampishe aende kumkabili mtunzi ana kwa ana.

“Hamna wakuu kuna vitu nilikuwa nikivikamilisha na nilijitahidi kuvikamilisha ili nianze kutuma wiki ileile ila kama wasemavyo waswahili mipango siyo matumizi nikapata dharura nikashindwa kufanya kama nilivyopanga”

alijibu mtunzi huyo huku akikinga kichwa chake baada ya kuona silaha nyingi zikiwa juu ya kichwa chake🙆‍♂️.

“Angalia sasa anajifanya anazijua sana methali eti mipango siyo matumizi haya tuambie ni dharura gani hiyo inayokufanya ushindwe kutuma hizo episode tuambie kabla sijalishusha hili rungu kwenye uso wako huo nikauvurugavuruga na kama huna bando tuambie tukusaidie”

alikuwa ni kabwela Poor boy aliyekuwa akijinadi kuharibu sura ya mtunzi akiwa na rungu mkononi mwake👨‍⚖.

“Nilipata dili moja kutoka inec ikanibidi nilizingatie lilikuwa lina maslahi 💴mazuri tu kusema kweli sikuweza kuliacha vuta picha braza unaenda semina unafundishwa halafu unapewa mpunga💰 usio na makato wala kodi yaani hii ni zaidi ya elimu bure yaani unafundishwa📊 halafu unalipwa haitoshi unapewa chakula 🍗🥪🌮na kinywaji🥤 bure hata kama ungekuwa wewe ungeiachiaje hii fursa na mnajua fika kijana wenu ni JOBLESS😂”

alijibu mtunzi huyo huku akionekana kupungukiwa na hofu na kuanza kupandisha hali ya kujiamini😲 kwa wakati huo.

“Anatupiga fix huyo inec ndo kitu gani yaani anataja vitu ambavyo hatuvijui ili apone”

alihoji moja ya watu waliokuwepo eneo hilo ambaye hakufahamika kwa urahisi akiwa ameshika panga🗡 mkononi.

“Hamna braza inec si Tume huru ya taifa ya uchaguzi zamani walikuwa wakiitwa nec ila baada ya kujitegemea na kuwa independent ndo wakaongeza I hivyo kwa sasa wanatambulika kama inec”

aliendelea kujibu mtunzi awamu hii akiwa amesimama na kujifutafuta🧍‍♂️.

“Yaani nyie kumsubiri kote kule leo hii anawapa majibu mepesi hivyo mnamuamini kirahisi hatakiwi kusimama huyu na kujiamini kiasi hiki”

alidakia ndugu Antonio de Guzman huku akiwa amemkwida tai mtunzi na kumrudisha chini.

“Haya tuambie kama kweli ulipata huo mchongo huko inec ulikuwa nani muandishi📝 au au ulikuwa unaendesha lile limashine💻🖨sijui ndiyo mnaliita li-V.A. R na waliwalipa shingapi na hiyo kazi ya watu ushamaliza au bado?”

aliendelea kuhoji mwamba huyo aliyekuwa amemkwida.

“Kusema ukweli kuhusu simulizi nishakamilisha ila hizo taarifa za watu siwezi kuwaambia🤬 chochote kama mnaweza niueni hapahapa ila hizo siri za watu siwaambii ng’oo🤐”

alijibu mtunzi ambaye alikuwa amerudishwa chini na jitu lenye miraba yake.

“Jamani jamani hembu shusheni hizo silaha🛠⛏🪓 zenu chini cha muhimu kashasema alikuwa na dharura bahati nzuri pia kasema mwenyewe simulizi imeshakamilika jambo la msingi atuambie sasa ataanza kutuma lini hizo episodes haya simama mwaya mkaka”

ilikuwa ni sauti ya kwanza yenye busara ndani yake kutoka kwa mwanadada Numbisa 🧖‍♀️aliyeenda kumuinua mtunzi huyo na kumuweka vizuri shati lake lililokuwa limekunjwa baada ya kukwidwa na jibaba la miraba🕺.

“Ndiyo atuambie atatuma lini na aache kumpotezea dada wawatu Linda 😭anahangaika na mademu wanaompa masharti na wasiokuwa na time na yeye wakati linda anahangaika kwa ajili yake kamfuata mpaka jeshini kwenye mateso lakini yeye hajali tu🤤”

ilikuwa ni sauti ya kaka mkubwa Senior Member dorge aliyekuwa akimshinikiza hayo kwa jazba 🥴 lenye uzito wa tani moja.

“Msijali mabosi zangu nimewaelewa niwahakikishie kuwa leo haipiti nitaanza kutuma”

alijibu mtunzi wa simulizi hiyo huku akionekana kutabasamu na kujiamini baada ya kupata utetezi kutoka kwa mwanadada huyo👏.

“Aaah nyie mnamuachiaje huyu kama ishakamilika si atutumie hapahapa ina maana hamkumbuki tumemsubiri kwa muda gani tukiwa tukipoteza bando kuchungulia kama katuma lakini wapi au mshasahau? Mmesahau tulikuwa tukimuuliza inaendelea lini lakini anakaa kimya huyu hapaswi kuondoka hivihivi”

hii ilikuwa ni sauti ya JF-Expert Member BLACKTIGER 🐯.

“Hamna mkuu wala usijali nilikuwa sina bando ndiyo maana nilikuwa kimya ila hata hivyo simu nimeacha chaji kwa MombaDier naelekea mbele hapo kufuata futari 🍲 nikishafuturu tu naanza kutuma”

alijibu mtunzi huyo aliyekuwa ameshika mfuko wa Magufuli mkononi.

“Aaah nawewe unafunga siku hizi ama kweli kiama kinakaribia”

alikuwa ni mtoto wa father pekupeku Alfagems aliyekuwa akimtania mtunzi.

“Ndiyo kaka na nyie mfunge maasi yapungue duniani na msisahau pia kwenda kujiandikisha kwenye daftari la kudumu🗒 ni muhimu sana” alijibu mtunzi huku akikimbia kuwahi fungu la mihogo sokoni............................🏃

Hii imeisha, yaani haina muendelezo😊😊
 
Attachments

  • LogoMakerCa-1738779454430~2.jpg
    LogoMakerCa-1738779454430~2.jpg
    205 KB · Views: 23
🤣🤣🤣😂😂😂 aiseeeee
ilikuwa ni sauti ya kwanza yenye busara ndani yake kutoka kwa mwanadada @Numbisa 🧖‍♀️aliyeenda kumuinua mtunzi huyo na kumuweka vizuri shati lake lililokuwa limekunjwa baada ya kukwidwa na jibaba la miraba🕺
 
MAISHA YA DEPO

SEASON-3

EPISODE 01

Pyeeh! Pyeeh! Pyeeh! Pyeeh! Pyeeh! Pyeeh! Pyeeh! Pyeeh! Pyeeh! Pyeeh! Pyeeh! Pyeeh! Pyeeh! Pyeeh! Pyeeh! Pyeeh! Pyeeh! Pyeeh! Pyeeh! Pyeeh! Pyeeh! Pyeeh! Pyeeh! Pyeeh! Pyeeh!Pyeeh! Pyeeh! Pyeeh! Pyeeh! Pyeeh!

Ebwana eeh msije mkadhani akaunti yangu imehakiwa ama nimewachoka na kuamua kuwarudisha utotoni.

Ulikuwa ni mfululizo wa kelele zilizotokana na filimbi zilizokuwa zikipigwa kutoka UWANJA WA DAMU na wakati huo zilikuwa zikipigwa na maafande jamii ya BAKABAKA.

Hali hii haikutofautiana na ile ya siku ambayo Service Man waliharibu kazi.

Saikolojia haikusizi baada ya kuona mfanano wa tukio hilo ni kama moyo niliisikia nafsi ikiniambia KIVUMBI LEO.

Tukiwa tunajishauri kwenda ziliko filimbi hizo zikaanza kutembea kauli ambazo bado mpaka leo sijaweza kuzitambua kama ni kejeli, kebehi, dharau ama hamasa ambazo kwa nyakati tofauti walisikika maafande wakizitoa.

“Hizi filimbi mnazozisikia siyo za Ramadhani Kayoko wa daslam ama Arajiga wa manyara wanaozipuliza ni makamanda wa jeshi la wananchi wewe KURUTA unayetembea acha kupima kina cha bahari kwa kijiti” huyu alikuwa nia afande wa kwanza.

Poti mwingine naye alisikika akisema “We KURUTA acha MAPUUZA unaposikia filimbi zinapulizwa kokote unatakiwa ufanye GHAFLA na ufoleni zinakosikika”.

Baada ya kuonekana tunashuka KOMBANIA kwa kusuasua baadhi ya maafande walikuja MAHANGANI na kuanza kutukimbiza wakitushinikiza kuelekea KOMBANIA.

Walinikumbusha kipindi niko shule ya upili mwalimu wangu wa Chemistry tuliyekua tukimuita “White hair” na yule wa Biology aliyekua akitambulika kwa a.k.a ya “Mbuyu twite” walikuwa wakitufuata mabwenini wakitufukuza kutushinikiza kwenda assemble.

Basi ilikua ingia huku, tokea kule, nenda pale pita kule mpaka pale tulipokusanyika wote KOMBANIA ambako TULIFOLENI na kujipanga kwenye maeneo yetu ya kila siku nyakati za usiku.

Alianza kusikika kubwa la maadui “Sikia kutoka kwangu daboli N naongea, aliyekuwa na masikio aendelee kunisikiliza kwa makini kwasababu ni muhimu mno kuyasikia haya nitakayoyaongea”.

Aliendelea kusema “Leo ndiyo ile siku mliyokuwa mkiiota na kusimuliwa na kitakachotokea baada kumaliza kuongea ndicho kinachotakiwa kutokea na awamu hii wahusika wakuu mtakua ni nyie KURUTA”.

“Kwa kipindi cha wiki zaidi ya tatu mlizokuwa kikosini mmekuwa mkishiriki katika majukumu mbalimbali ambayo mlistahili kuyafanya huku mkiitwa WAZALENDO”.

“Kuanzia sasa natangaza rasmi kuwavua cheo mlichokuwa nacho awali cha UZALENDO na kuwavisha kipya cha juu yake yaani kuanzia muda huu ninyi ni KURUTA”.

“Atakayekuita MZALENDO achana naye na kama ukiona anakuzingua sana njoo umripoti kwangu kwasababu kuanzia wakati huu nyinyi mmepanda cheo na kuwa MAKURUTA hembu jipigieni makofi kwanza”.

Tulipiga makofi, tukachanganya vigelegele, miruzi kidogo na kila aina ya fujo ambayo ilitafsiri maana halisi ya nderemo na vifijo mahala hapo na baada ya muda akaendelea kutamba Matroni Neema.

“Naona mmefurahi sana pongezi kwenu sasa kabla ya kuanza kazoezi ketu kanakofahamika kama INTRODUCTION TO THE CAMP naomba kwanza niwaelezee kuhusu sifa za KURUTA, je kuruta ni nani? Nawaomba wote mniazime masikio yenu”.

“KURUTA kama cheo cha pili katika jeshi la kujenga taifa yeye ni askari atakayedumu na cheo hicho ndani ya kipindi cha wiki sita ambazo ni sawa na siku arobaini na mbili kitaalamu kipindi hicho tunakiita SIXWEEK”.

“Na katika kipindi hicho huyu KURUTA atakuwa akishiriki shughuli mbalimbali kikosini zikiwepo za uzalishaji mali na mafunzo ya kijeshi ndani ya siku arobaini na mbili bila kuchoka wala kugoma”.

Alipoongea hivyo tulijikuta tukiguna hali iliyopelekea pakae kimya kwa muda mpaka aliporudi kwenye ubora wake na akaendelea kuongea.

“Mnanitukana eeh! Nyie nitukaneni tu lakini utaratibu uko hivyo kabla hata sisi hatujawa tumeukuta na nyie mtauacha kifupi hauwezi kubadilika hata kidogo”.

“Katika kipindi hicho cha siku arobaini na mbili ni marufuku kwa KURUTA yeyote kuonekana akitembea yaani popote pale utakapokwenda unatakiwa kwenda huku unakimbia”.

“Lakini pia ndani ya siku hizo tunakutarajia uwe mtiifu, mwenye adabu na kusikiliza maagizo utakayopewa na afande utakayekuwa naye wakati huo”.

“Katika yote hayo la muhimu zaidi kuzingatia ni kuwa usije ukaenda mahala popote ama kufanya chochote bila ya kupata ruhusa kutoka kwa kamanda wako”.

“Nasema hivyo kwanini? kumekuwa na tabia ya KURUTA kudoji FATIKI na kwenda kujificha kwenye mapori msichokijua ni kwamba hii ni kambi ya jeshi na kama zilivyo kambi nyinginezo tuna utaratibu wetu wa kuchukua tahadhari”.

“Kifupi nisizunguke sana kwenye hayo mapori mnayokwenda kujificha tumetega mabomu kwa ajili ya usalama nafikiri wengi wenu humu ni wapenzi wa movie za kivita sasa vile mnavyoona hakuna tofauti hata kidogo hatuwezi kujilinda kizembe”.

“Sasa tahadhari ni kwamba asitokee yeyote akajichanganya nisiwafiche ukweli ni kwamba mtalipuka mana ni wengi tuliowazika na kati ya hao ni wachache mno tuliowazika miili yao ikiwa imekamilika”.

“Kwa asilimia kubwa tumewazika vipande vipande na huwa tunawazikia kule kwenye migomba ya geti kuu nafikiri mmeshaambiwa labda mgeni atakayeripoti kesho ndiye atakuwa hajaambiwa na hatutegemei kupokea mwingine tushafunga hesabu sisi”.

“Baada ya kusema hayo naomba makamanda wangu muelekee kwenye KOMBANIA mlizopangiwa mkashirikiane na makarani kuchukua lokoo kabda ya kuanza zoezi letu”.

Walikuja kwa mbwembwe sana BAKABAKA wapatao wanane ilipo D-Coy tulihesabu kukatokea pungufu ya watu saba ambao kati yao kulikuwa na walinzi wa HANGA na wagonjwa.

Baada ya kukamilika kwa hesabu ilipelekwa taarifa kwa Matroni tukamsikia akisema “Aisee kawaiteni wenzenu wote waje hapa leo ndio leo hakuna atakayesalia kwenye HANGA lolote lile leo MAHANGA yatatusamehe yanatakiwa kujilinda yenyewe”.

“ST nendeni mkaniitie walinzi na hao wanaojiita wagonjwa, mgonjwa pekee ambaye hatutokuwa naye ni yule aliyekuwa mahututi tu ambaye hawezi kuwepo HANGANI kifupi tunategemea awe amelazwa kule zahanati”.

“Na hata kama mtawakuta mende wanaitwa KURUTA naomba mniswagie mniletee asije akabaki KURUTA yeyote HANGANI”.

Nilienda HANGANI nikazikusanya zile kondoo ambazo zilikuwa tatu nikaenda nazo dimbani. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

............................ Itaendelea ............…..………...
 
Mwisho wa pongezi hizo nilikaa chini afande Rashidi akasema “Ila mwanangu unafaa sana twende kwenye FATIKI ukatuchangamshe mana kazi ikiwa ngumu tukafurahi kama hivi inakuwa nyepesi kabisa”.
 
EPISODE 02

Wakati makamanda wakiweka hesabu sawa karani Jala alikuwa akipitisha maneno ya chinichini huku akitucheka na kutuibia siri moja muhimu sana ambayo asingetupatia hakika kitu kizito tungekutana nacho mbele ya safari.

Nikimnukuu afande Jala alisema “KURUTA huko mnakopelekwa jitahidini msiwe wambea chochote mtakachoulizwa jifanyeni hamjui mtakuja kunishukuru sana”.

“Ikitokea mkaulizwa hapa ni wapi? msijifanye wajuaji hata kama mnapajua ni MESI kwa mzabuni ambako MFOLENI mara tatu kwa siku nyie jibuni kuwa hampajui” aliendelea kutuambia karani huyo.

“Sasa mkajichanganye mseme mnapajua mtamueleza kamanda mara mwisho afande Pastima kukaa kwa juu ilikuwa ni lini” kauli hiyo ilitupelekea kuangua vicheko ikambidi karani huyo anyamaze baada ya moja ya kamanda kututupia jicho na kuonekana kutuzingatia.

Idadi ilipokamilika kwa KOMBANIA zote Matron Neema aliwaruhusu makamanda kuendelea na zoezi hilo.

Kunako KOMBANIA walitugawa MABOGI matatu kulingana na PLATUNI na kwa upande wetu tuliangukia mikononi mwa afande Kalaghe na afande Mochiwa.

Alianza kusikika afande Mochiwa akituamuru tukunje ngumi nasi tukafanya hivyo akatupigisha pushapu kadhaa kabla ya kuturukisha kichurachura.

Tulishika njia inayoelekea MESI kwa mwendo wa ubatabata na tulipofika tukasimama na kujipanga upya kwani mistari ilikuwa haieleweki kutokana na kurupushani tulizokumbana nazo.

Afande Kalaghe alitutaka tubebe viroba tukabaki kumtazama kwani tulishindwa kumuelewa alichokimaanisha.

“Acheni MAPUUZA nyie KURUTA mjue mi nawaambia mbebe viroba mnaning’olea macho mnanipima imani siyo?” alihoji afande huyo nasi tulijikalia kimya tusijue cha kumjibu.

“Haya punguzeni urefu” alituamuru afande Kalaghe nasi hatukuwa na hiyana tulichuchumaa na akatutaka tusimame kisha akapata kamchezo akawa anatuamrisha juu chini, chini juu nasi tukawa tunasinama na kuinama.

Baada ya hapo afande Kalaghe alitufafanulia alichokuwa akikimaanisha kumbe bwana kubeba viroba ni zoezi ambalo unaunganisha vidole vya mikono kisha unaweka viganja kwenye kisogo halafu sasa ndiyo unaanza kubeba viroba kwa idadi aitakayo afande yaani kamchezo ka “juu chini” ndiyo kanachukua nafasi yake huku viganja vikiwa vimeegemewa na kisogo.

Alipomaliza kutupa maelekezo hayo afande Mochiwa alituamuru tuchuchumae na akatuuliza

“Nyie KURUTA wa Mungu mnapajua hapa?” tulikaa kimya na hakuna aliyemjibu.

“Nyie KURUTA afande si anawauliza ina maana hamna midomo tuambieni tuko sehemu gani hapa?” alidakia afande Kalaghe ila bado tulimkalia kimya.

“Baba YANATUVUNA haya ngoja tuyanyooshe midomo ifunguke MANANGA haya”.

Walituamuru tukunje ngumi na kuanza kutupigisha pushapu kwa muda ambapo jasho nalo lilianza kututoka na mikono ikawa inatetemeka ndipo wakatuambia tukae kitako.

“Naona mmeshaanza kunyooka sasa vipi mnaonaje tuendelee au inatosha? ” afande Kalaghe alikuwa akipita kati katikati yetu na kutubonda makofi kwenye mapara huku akituuliza

“Inatosha afande” baadhi yetu tulijibu kwa sauti ya chinichini.

“Kwahiyo nyie watu hamna sauti ya kumjibu afande siyo, haya KUNJA NGUMI” alituambia afande Mochiwa kwa sauti ya ukali nafikiri katika mpangilio huenda ikawa ni ya sabini na tano.

Tulizikunja na tukarudishwa tena kwenye mfumo wa chini juu mpaka pale ilipoanza kusikika miguno ndipo tukamsikia afande Kalaghe akisema

“Mnnh naona mmeanza manung’uniko tulieni hivyohivyo dawa iwaingie mkitikisika tu inakatikia nyie si mnajikuta hamjui kuongea”.

Tukiwa tumekata tamaa mithili ya mateka wa kivita tulimsikia afande Mochiwa akisema “Simama juu up” harakaharaka tulisimama huku tukiwa tumelowa majasho.

Afande alitucheka na kutuamuru tuketi chini kisha akatuuliza
“Haya KURUTA wa Mungu mtaongea au mtabaki kimya kama marehemu wajao”.

“Tutaongea afande” tulimjibu kwa sauti ya chini na yenye unyonge ndani yake.

“Mnasemaje”
“Tutaongea afande”
“Sijasikia mnasemaaa”
“Tutaongea afandeeee” wakati huu tulimjibu huku sauti ikionekana kutoka vizuri.

“Mtatoa sauti hamtatoa”
“Tutatoa afande”
“Mbona sisikii sasa”
“Tutazitoa afandeeeee” sauti zilikuwa zikitoka kadri ya muda ulivyokuwa ukiongeza namba mithili ya gari lililokuwa likishuka mlimani.

“Haya niambieni hapa ni wapi” aliuliza afande Kalaghe tukaanza kusita ila tulipolikumbuka DOSO tulilotoka kukabiliana nalo ikatubidi tujibu kwa chinichini.

“Hatupajui afande”
“Mnasemaje nyie MANANGA”
“Hatupajui afande” wakati huu tulichagua kutumia karata yetu turufu tuliyopewa na karani wetu lakini haikufanya kazi kwani badala ya kupata ahueni hali ikawa tofauti tulimsikia afande Mochiwa akisema.

“Kunja ngumi” hatukuamini alichoongea hivyo tukawa tunamshangaa badala ya kufanya alichotuagiza.

“KURUTA mmegoma eeh sinimewaambia mkunje ngumi” bado hatukuamini alichokuwa akituambia tulibaki kumtizama ingawaje wapo baadhi yetu ambao nahisi ni wale viumbe kutoka kanda ya ziwa walikuwa wamekwishafanya hivyo.

“Kunja ngumi, nimesema kunja ngumi, kunja kunja kunja KURUTA” wakati huu walikuwa wakituambia huku wakitushushia mabanzi yaliyokosa idadi mithili ya mvua za masika.

Walitukanda mabao hayo bila kujali walikuwa wakitupiga sehemu gani ya mwili maana wapo waliopigwa kwenye vipara wengine walikutana nayo mashavuni na wengine yaliwashukia mgongoni.

Baada ya muda tulijikuta wote tukiwa tunausukuma mgongo wa ardhi kwenda chini huku tukiendelea kukumbana na mibanzi pamoja na mashambulizi ya mikanda kutoka kwa makamanda hao wa Jeshi la Wananchi.

“Haya KURUTA kwa mara ya mwisho hapa ni wapi?” aliuliza afande Kalaghe.

“Hatujui afande”
“Eeh”
“Hatujui afande”
“Mnasemaje nyie MANANGA”
“Hatupajui afande” kwa mbali kulikuwa kuna BOGI lingine lililokuwa likitukaribia ila sikumbuki walikuwa wakija kwa mwendo wa aina gani.

“MANANGA nyie mnajikuta mmeiva, hapa si mnakuja kila siku mara tatu kufuata chakula na KUBASTI juu”

“Anhaah kumbe ni hapa” nilijikuta nimeropoka peke yangu.

“Wewe endelea kujichanganya tu” alisikika afande ambaye ni kama alinimaindi ila niligundua alikuwa akiokoa muda kwa ajili ya kuwapisha wenzetu waliokuwa wakikaribia.

“Hapa ni jikoni au MESINI sehemu ambayo chakula kinaandaliwa kwa ajili ya makamanda na MANANGA kama nyie hutakiwi kufika hapa bila ruhusa ya afande wako tumeelewana NGURUTU”.

“Ndiyo afandeeeee”
“Haya simama juu uuuuuuuup” tulisimama kwa haraka mno maana hakuna aliyekuwa akitamani kuendelea na DOSO hilo tena.

Makamanda wetu walitutoa eneo hilo kwa mwendo wa kibabe ulioambatana na songi lililoongozwa na afande Kalaghe.

“Afande: Soja nyakua
Sisi: Nyakua
Afande: Nyakua nyakua
Sisi: Nyakua
Afande: We soja yaue
Sisi: Yaue
Afande: Yaue yaue
Sisi: Yaue”.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

........................Itaendelea………………………...
 
*“Afande: Soja nyakua
Sisi: Nyakua
Afande: Nyakua nyakua
Sisi: Nyakua
Afande: We soja yaue
Sisi: Yaue
Afande: Yaue yaue
Sisi: Yaue”.* ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

........................Itaendelea………………………...

MAISHA YA DEPO

SEASON-3

EPISODE 03

Tulikwenda na mwendo huo mpaka lilipokuwa duka la kikosi uliokuwa ukihusisha kurusha miguu ambapo goti lake lilitakiwa kufika usawa wa kifua.

Mpaka tunafika dukani hali haikuwa shwari hata kidogo maana kwa mwendo ule nilikuwa naona kabisa utumbo, firigisi, kongosho na maini kama vimechanganyikana vile nahisi tungeendelea kidogo tu bandama na nyongo vingeungana navyo sijui tumboni kungekuwa na mkutano gani sijui kama ni wa Berlin ama ule unaozikutanisha nchi wanachama wa umoja wa nchi za kusini mwa Afrika.

“KURUTA wii”
“Waah”
“Wii”
“Waah”
“Nataka kuona mistari mitatu ya kijeshi iliyonyooka na zoezi hilo haliwezi kuchukua muda haya CHAP KWA HARAKA zoezi hilo anza” ilikuwa ni sauti ya afande Kalaghe.

Tulijipanga na baada ya kumaliza tukaamriwa kuketi chini kisha afande Kalaghe akauliza
“KURUTA mnapajua hapa”
“Hatupajui afande”
“Eeeh”
“Hatupajui afande”
“Aaah ila nyie watoto ni wanafki sana ni kweli hampajui hapa?”
“Ndiyo afande”

“Baba yanakudanganya hayo nayakutaga kila siku hapa yanafuata mikate ya Bakhresa na soda” alituchongea afande Mochiwa.

“Kumbe baba! haya kunywa viroba kumi kwa kusema uongo” afande Kalaghe alituporomoshea dhahama hiyo nasi tulijizima data tukijifanya hatujui kile kinachoendelea.

“Aisee KURUTA acheni MAPUUZA mjue au mnataka tuwavunje hiyo migongo yenu ndiyo muanze kutii amri” alisema afande Kalaghe.

“Nawauliza nyie KURUTA tuanze kuwatembezea mabanzi”
“Hapana afande”
“Haya viroba hivyo kunywa”.
“Moja, mbili, tatu, nne, tano, sita, saba, nane, tisa, kumi” tulimhesabia afande huyo viroba vyake ingawaje tulikuwepo sisi tuliokuwa tukitegea yaani unakuta wengine wamesimama juu sisi tume mute chini.

Baada ya kushusha VIROBA hivyo tulikaa kitako na afande Kalaghe akatuuliza kwa mara nyingine
“Haya tuambieni sasa hapa ni wapi KURUTA”
“Hatupajui afande”
“Nyie mna masihara haya kunja ngumi” alituamuru afande Mochiwa huku akitutembezea mabanzi kwa wale waliokuwa wakisitasita kufanya hivyo.

“KURUTA sikia kutoka kwangu hapa sio pale mwalimu wenu wa hesabu aliposema hamuwezi kufika hapa mlipofika sasa ni dukani na mbele yenu ni duka la kikosi tumeelewana KURUTA”

“Ndiyo afande”
“Nauliza tena tumeelewana nyie vichwa maji”
“Ndiyo afande”
“Na kama zilivyo sehemu nyingine zote hutakiwi kufika hapa bila ya ruhusa ya afande sasa wewe jikute una njaa kupitiliza ukaja KUFOLENI hovyo bila kuruhusiwa na afande utatueleza ni kwanini maji hayapandi mlima” aliyasema hayo afande Kalaghe.

Baada ya kutambulishwa mahala hapo tulitembezwa ubatabata mpaka lilipokuwa bwalo la chakula la askari wa Jeshi la kujenga taifa yaani SERVICE MEN.

Tulijipanga mistari mitatu kwenye barabara iliyoinama toka tulipo kuelekea sehemu ya makutano inayozikutanisha njia za kwenda KIWANI, Zahanati, KOMBANIA na lilipo duka la kikosi.

Tulikunjishwa ngumi na kupigishwa juu chini za kutosha kabla ya kutakiwa kulala chini nasi tukajitabasamuisha tukaona kitonga si hii hapa.

Hatukujali kwamba tutachafuka kwani kwa vumbi lililokuwa kwenye barabara ile ukajumlisha na jasho lililotumwagika hatukustahili kulala kwenye ule udongo ila kwa wakati huo ndiyo ilikuwa nafuu kwetu.

Ghafla tukiwa juu ya godoro hilo tukasikia afande Mochiwa akisema“KURUTA zoezi linalofuata ni KUROLI uelekeo ni zahanati haya zoezi hilo anza”.

“Hah! Hah! Haah! Afande siumeona yalivyokuwa na MAPUUZA yaani badala YAROLI yamelala baba yanatuvuna haya” aliropoka afande Kalaghe baada ya kuona tumetulizana pale chini pasi na kutokea lolote.

“Baba ukiyauliza yatajifanya hayajui KUROLI we yaache ntayavunja mbavu yakawekewe za mbwa haya KURUTA biringitabiringita kuelekea chini kule ROLI KURUTA”.

Tulikuwa hatuelewi kinachoendelea ila baada ya kuambiwa tubiringite tukaanza kupata picha na afande alipoona hakuna kilichokuwa kikiendelea alienda mbele akamchukua KURUTA mmoja akamuweka mabanzi huku akimsukuma hali iliyomfanya afanye AROLI kama alivyokuwa akitaka afande.

Baada ya tukio hilo akasikika afande Kalaghe “Haya kama yeye” huku wakitupiga mibanzi hali iliyotufanya automatically tujikute wote tunafanya hivyo.

Kwa kweli ilikuwa ni patashika kwani wapo waliotumbukia kwenye msingi na wengine walikuwa wakiwapandia wale walioshindwa kuendelea kutokana na kupatwa na kizunguzungu hivyo wakajikuta wanalala tu na wasijue kinachoendelea.

Hali ya kizunguzungu iliwapelekea wengi wao kutapika na wengine kuzimia kabisa watu hao ilibidi watengwe na kupatiwa huduma ya kwanza kwa sisi ambao bado tulikuwa ngangari tuliendelea na mchakato huo na tulipofika kwenye makutano tukashika njia inayoelekea KIWANI kwa ubatabata.

Juu chini chini juu simama kaa ndiyo zilikuwa kauli za mapoti hao waliotubebesha viroba vya kutosha pamoja na pushapu za kufa mtu.

“Hapa ni wapi”
“Hatupajui afande”
“Viazi nyie nauliza tena hapa ni wapi”
“Hatupajui afande”alikuwa akituuliza afande Kalaghe ambaye baada ya kumpa majibu hayo akatunyoosha kwa DOSO la nguvu.

Akatuuliza tena “Kwa mara ya mwisho kabla sijawatemesha maini mnapajua mahala hapa?”
kuna mmoja wetu ambaye nahisi DOSO lilimuingia akaona isiwe tabu akajiropokea
“ndiyo tunapajua afande”.

“Nani huyo anayepajua simama juu up” tulisimama wote na afande akasema

“Aaah mbona mmesimama wote sasa kwani nyie ndio mliojibu haya wote rudi chini” tulitii amri hiyo na kurudi chini wote.

“Haya namtaka aliyejibu kuwa anayepajua hapa ndiyo asimame nyie wengine si hampajui hapa mtaendelea kula vumbi hapo chini mpaka mpajue”

Yule mwamba alisimama huku akituacha sisi tukihenya pale chini hatukupata nafasi ya kumuona kwani macho yetu yalikuwa yakitizamana na mgongo wa ardhi.

Afande aliendelea kuuliza kama kuna mwingine anayepajua mahala hapo wakasimama MADAWILI wawili wakawa wanaongezeka wengine afande akawazuia na kuwaambia

“Mlikuwa wapi muda wote hembu rudini chini huko"
Wale watu walikabidhiwa kwa afande Mochiwa huku sisi tukisalia na afande Kalaghe aliyetuhenyesha ipasavyo.

Tulipomaliza kutambulishwa sehemu hiyo tuliondoka kwa KUROLI mpaka tulipofika mbele ya jengo la zahanati ya kikosi.

Hatukukaa sana sehemu hiyo kwani kuna BOGI lingine lilikuwa likitukaribia hivyo ilitubidi tufanye chap na kuondoka zetu.

Tuliondoka toka mahala hapo kwa aina mbalimbali za mwendo ubatabata, kichurachura, kuroli na tukiwa njiani tulielekezwa aina nyingine ya mwendo tuliyokuwa tukiita nyoka style ama snake movement. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

............................. Itaendelea .........................…
 
EPISODE 04

Kupitia staili hiyo tulikuwa tukilala chini kifudifudi kisha tunakunja mkono mmoja na kuupeleka mbele halafu tunauvuta mwili kutoka nyuma kwenda mbele kwa wale wajuaji sana haswa waliobahatika kutizama picha za kivita na hata wale waliopitia mafunzo ya kijeshi wanaitambua kama KUKROO.

Baada ya muda afande Kalaghe alitusimamisha na kutuweka kitako kisha akaamuru tuunde mistari minne kisha akatugawa mistari miwilimiwili yenye kutizamana.

Poti huyo alituambia tushikane mikono watu wawili tunaotizamana kisha tukafanya kazoezi ka kwangu kwako.

Tukiwa tumeshikana afande akisema kwangu mmoja anajivuta kurudi nyuma huku akimvuta mwenzie aliyemshika na baadaye afande akisema kwako yule mwingine anafanya vilevile alivyofanya wa kwanza.

Afande alituuliza “Kwani hamjachoka KURUTA” tulikaa kimya tusijue cha kumjibu.

“Hembu mtizame partiner wako na umuulize hujachoka KURUTA” kusema ukweli tulikuwa tumechoka kiasi cha kutotamani kuinua mdomo hivyo tulikaa kimya kwa mara nyingine.

“Anhaa kumbe bado mnautaka haya kunja ngumi kunja kunja kunja chap kwa haraka” duuh tabu ilirejea tena kwa mara nyingine tukarejeshwa mzigoni ikawa ni DOSO dosoni.

“Yaani nawaagiza mfanye jambo mnanikalia kimya kwahiyo mmeniona mimi ni Celine Dion nawabembeleza mlale siyo” tuliendelea kuvunga tena.

“Anhaah yaani nawaongelesha bado mnanikalia kimya haya chini chini chini chini” awamu hii alikuwa akitutia mibanzi migongoni haswa wale walio waliojikuta wavivu kwenda chini.

“Haya juu juu juuu” afande alituamuru nasi tukajivuta kwenda juu kama alivyotaka.

“Ee acha dawa iwaingie simnajikuta viburi ngoja niwanyooshe na ninajua hapo mlipo mnanitukana ila hilohilo tusi mnalonitukana liwarudie wenyewe kila mkihema”.

Ilikuwa ni shoo ya mtu mmoja kutoka kwa afande Kalaghe na alipoona dawa imetuingia akatuuliza

“Haya mtanijibu au mtaendelea kukaa kimya”
“Tutajibu afande”
“Eeeeeh”
“Tutajibu afande”
“Haya simama juu up” tulisimama wote huku tukiropoka “uuuup”.

“Haya kaeni chini wanangu” tulikaa chini tukajipanga kama mwanzo afande akasema
“Mnajua KURUTA mnazingua yaani mna MAPUUZA kupitiliza afande naongea mnanikalia kimya hivi mnanichukuliaje?”.

“Eti nyie KURUTA wa Mungu mnanifananisha na nani Gigy money au Masha Love?”

“Nawauliza nyie viumbe”
“Hapana afande”
“Mapana au Tangamano mbwa nyie”.
“KURUTA wiih”
“Waah”
“Wiih”
“Waah” afande alianza kupiga makofi nasi tukamfuatisha paah! Paah! Paah!

*“Afande: Afandeeee afande tunaomba tano afandeee
Sisi: Afandeeee afande tunaomba tano afandeee

Afande: KURUTAAA Kuruta siwapi tano KURUTAAA

Afande: KURUTAAA Kuruta lalia mgongo KURUTA".

Ulikuwa ni wimbo wa kumpanga afande atoe UTAWALA fulani hivi wa kishkaji uliofahamika kama TANO.

UTAWALA huo mara nyingi hupatikana tukiwa kwenye FATIKI ama kwenye DOSO moja kali mno hivyo ukifika wakati wa CHENJA tulikuwa tukitumia wimbo huo kwa ajili ya kumtongoza afande atupunguzie mwendo kwenye tuta tupate kupunguza machungu.

Baada ya maneno hayo kutoka kwa afande tulilalia zetu migongo tukiwa katikati ya barabara inayoingia kikosini ikitokea barabara kuu.

Tukiwa tunatazama mbinguni tukishuhudia uumbaji wa Mwenyezi Mungu tulikuwa tukiona jinsi wingu jeupe likipiga doria chini ya anga yenye rangi ya samawati ghafla afande akatuamuru kufumba macho.

“Vipi mnaona nini KURUTA” alituuliza afande Kalaghe ambaye hatukumjibu chochote tukamkalia kimya kana kwamba hatukusikia chochote toka kwake.

“Yaani KURUTA kwa moyo wangu mmoja nimeamua kuwapa TANO nawauliza bado mnanikalia kimya kana kwamba mmewasha redio sasa mnasikiliza Juma Lokole akiwapa umbea wa Mondi na zari” eeh kumbe mapoti nao huwa wanafuatilia mambo ya udaku😆😆.

“Sasa nyie si mna MAPUUZA ngoja niwaoneshe kuwa dawa ya jeuri ni kiburi haya TANO zimeisha simama juu uuuuup” looh! Kumbe kweli bwana wala hakuwa anatania.

Tulisimama tukanyweshwa VIROBA kadhaa kabla ya kukunja ngumi huku afande huyo akitumia filimbi yake barabara yaani badala ya kusema “juu chini” yeye akawa anatumia filimbi iliyokuwa mdomoni mwake.

Alipopuliza pyeeeh kila mmoja wetu alinyanyua mwili kwenda juu na alipopuliza tena tukaishusha kwenda chini.

Hali hiyo iliendelea mpaka pale tulipomuona afande Mochiwa kwa mbali ndipo tukapatiwa TANO kwa kutuambia tulalie tumbo na kufumba macho.

Alipofika afande Mochiwa akaanza kuropoka “Baba yamelala”
“Ndiyo afande nimeyaambie ya KROO yamenigomea yamesema eti yanakutaka wewe mimi hapa sina cha kuwafanya yananiona kama Hamorapa vile”.

Duuh! Ngoja kwanza nifute jasho🤔 maana afande Kalaghe alijua kutuchosha sijui hayo maneno tuliyasema saa ngapi nilitamani nisimame nimwambie anadanganya sijui ni malaika gani alinishukia wakati huo nikajikuta nikijiambia “Mdomo koma”.

“Anhaah kumbe yamenimisi baba sawasawa haya NGURUTU sa juu sa juu uuuuuup”
“Uuuuuup” kama kawaida yetu tulijiropokea kama wanafunzi wa darasa la awali waliokua wakiimba ule wimbo wa kuagana na mwalimu.

Tulisimama zetu kwa haraka kwani tulikuwa tukipenda sana kusimama bila kujua ni kipi kingefuata baada ya kusimama.

Afande Mochiwa alituamuru kujipanga mistari mitatu kisha akanza kutuimbisha“

"Afande: KURUTA Wiih
Sisi: Waah
Afande: Ewiih
Sisi: Ewaah
Afande: Ewiih
Sisi: Ewaah
Afande: Kaja mwenyewe geto kaja kunitega
Sisi: Kaja mwenyewe geto kaja kunitega
Afande: Kaja na kanga moko nyingine kwenye bega
Sisi: Kaja na kanga moko nyingine kwenye bega
Afande: Atamlaumu nani
Sisi: Atajilaumu mwenyewe”.

Tulikimbia mpaka tulipofika sehemu moja ambayo kulikuwa na vibanda kadhaa vilivyosimama kwa kujitengatenga mfano wa vile vinavyopatikana kwenye bar mbalimbali za mjini.

Tulichuchumaa wakatupitisha kwenye kinjia kilichokuwa kikiingia ndani viliko vibanda hivyo kwa uchurachura na tulipofika tukakunjishwa ngumi na kugonga pushapu kadhaa.

Alianza kusikika afande Mochiwa akituuliza “Nyie NGURUTU, Wadudu, Vipawatira vya jeshi hapa ni wapi?” kwa mbali yule shetani anayepitiaga watu wengi nikamsikia akininong’oneza.

“Mjibu ni pale mwalimu wa hesabu aliposema hatuwezi kufika” nikiwa najiandaa kuropoka hayo ghafla nikasikia “Hatupajui afande” zilikuwa ni sauti za KURUTA wenzangu sauti za wengi ambazo hata ningeropoka zingesikika hizo.

“Kweli NGURUTU”
“Ndiyo afande”
“Ina maana hakuna aliyewahi kufika hapa kweli?”
“Hatujawahi afande” ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

............................Itaendelea………….......………...
 
“Afande: Afandeeee afande tunaomba tano afandeee

EPISODE 05

“Acheni uwongo KURUTA kama mnapajua semeni tuondoke zetu tusipoteze muda” alijaribu kututega afande Mochiwa ila tulisimama imara na hatukuhadaika na maneno yake tukasalia na msimamo wetu.

“Hayo endelea kuyanyoosha tu baba maana hata kama yanapajua hayatakujibu yanajikuta yamekunywa maji ya bendera” alidakia afande Kalaghe.

“Kwani yalikwambia yanatakaje ili yaseme baba? Au tukayalete ubwabwa wa Mzabuni?” afande Mochiwa alimuuliza afande Kalaghe.

“Baba yalisema yatagoma kusema mpaka pale utakapoyapeleka kule ulikoyapeleka wenzao” aliendelea kutuchongea afande Kalaghe.

“Anhaah si wale wajuaji”
“Ndiyo baba”
“Anhaa yale tumeyapa UTAWALA baba kwani hujui taratibu zetu afande”

“Najua sana poti ila nimeamua kukausha ili uje uyaambie mwenyewe huenda yakakuamini zaidi” duuh! ila huyu jamaa wa kuitwa afande Kalaghe ni mnoko acha tu.

“Wale bwana nikutoe hofu afande tumeyapa UTAWALA kama kawaida na kama kuna wengine wanaijua kambi waseme wakalale zao MAHANGANI maana hatuwezi kumfanyia utambulisho mtu anayejua sasa utamtambulisha kipi kipya”.

“Enyi KURUTA wa Danger COY Platuni ya ngapi vileee?”
“Namba moja afande” tulimjibu afande Kalaghe alitaka kujua namba ya PLATUNI hiyo ingawaje mwanzo kipindi wanagawana waliambiwa kabisa wachukue PLATUNI namba moja.

“Mmemsikia afande kama mmezichoka hizi taabu maeneo ya kikosi mnayajua vizuri semeni mapema mchukue zenu UTAWALA nasisi tukale zetu TANO mjini huko au afande hairuhusiwi kuwapa UTAWALA wote hawa” alikuwa ni afande Kalaghe aliyekuwa akitupaka mafuta kwa mgongo wa chupa.

“Why not? Nimewaacha BRAVO karibia PLATUNI mbili zinakula UTAWALA yani mule wamechomoa wajuaji mmoja mmoja mpaka ikapatikana PLATUNI moja na nusu tunapoongea hivi sasa wamewachanganya hiyo moja na nusu wanawatembeza pamoja” alitoa ushuhuda huo afande Mochiwa.

“Wacha bana” alidakia afande Kalaghe.
“Amini kwamba yaani kiuhalisia ni kuwa kuna PLATUNI moja tu ya BRAVO mpaka sasa ndiyo ipo kwenye zoezi la kutambulishwa mipaka ya kikosi”.

Kusema kweli ukiwa mzembe unaweza kunasa kirahisi kwenye huu ulimbo waliokuwa ukipakazwa mtegoni na makamanda hao wa TPDF ila kwetu ilikuwa tofauti tukaendelea kushikilia bomba huku tukiwajibu kuwa kwa herufi kubwa HATUPAJUI.

Kuona hivyo ikawabidi makamanda wetu waanze kufunguka“Hapa ni RESORT sehemu ambayo makamanda wenu wanakuja kupata ile kitu roho inapenda”

“Masanga, Kamnyweso, Maji ya dhahabu, Soda mweleka, Mkojo wa firauni na majina mengine mnayoyajua ndiyo bidhaa inayopatikana sehemu hii”

“Ukiachana na kwamba hamruhusiwi kufika bila ruhusa ya kamanda ni kwamba mnaruhusiwa kuja kupata ile kitu ya kuchamba koo ila msichoruhusiwa ni kuharibu kazi” yote hayo yalikuwa ni maneno ya afande Mochiwa aliyekuwa akiyashusha kana kwamba yaliandaliwa kwenye karatasi ya risala.

“Yaani kifupi anachosema afande ni kuwa unaruhusiwa kulewa lakini usije kuharibu kazi za watu wewe lewa unavyoweza hakuna shida na ukiona za hapa hazikutoshi we nenda hata mtaani ukalewe ila mwisho wa siku isitokee ukafanya uharibifu wowote ule” alijazia afande Kalaghe.

“Swadakta afande namimi kwa upande wangu nikikuona mahala hapa na nikajua huna ruhusa ya kamanda wala sijisumbui najua ntakupata wapi” alituambia afande Mochiwa.

“Unataka kusema kitu gani afande” alidakia afande Kalaghe.

“Hawa si najua vichwa vyao vilivyo”
“Vikoje afande”
“Unajua afande masanga ni masanga”
“Najua sana baba”

“Masanga akinywa kiumbe mwenye kichwa cha kuku kama hawa WADUDU kinachofuata ni kuharibu kazi na si vinginevyo unajua kwanini afande”

“Hapana baba hembu nijuze”
“Hawa jamaa kwenye vichwa vyao ubongo umechanganyika na makamasi kifupi bado haujakomaa na masanga ilivyo inamtaka mtu mwenye ubongo uliokaa vizuri”

“Ndiyo maana ikitokea mdudu yeyote jamii ya KURUTA akapiga kamnyweso kinachofuata ni kuharibu kazi na hapo ndipo wanapoingia kwenye mikono yangu bila kutumia nguvu yeyote ile” hayo yalikuwa ni maneno ya kamanda Mochiwa.

Ulipokamilika utambulisho wa eneo hilo tukatembea kwa mwendo wa nyoka mpaka kwenye barabara iliyochepukia kutoka barabara kuu kuelekea kikosini.

Tulipofika kwenye barababara hiyo tulisimama wima na kupanga mistari ya kijeshi kisha afande Kalaghe akatuambia “Haya KURUTA zoezi la kunyakua” tulikaa kimya kwani hatukung’amua kile alichokuwa akikimaanisha.

“Nyie viumbe sinaongea na nyie mnashangaa nini sasa au mnasubiri picha ya pamoja?” alituuliza afande Kalaghe huku akitutumbulia macho kama mwamuzi mmoja maarufu kwenye mchezo wa mpira wa miguu pale nchini Italia afahamikae kwa jina la Pierluigi Collina.

“Hatujakuelewa afande”
“Hamjanielewa kipi sasa hapo ina maana nyie kila kitu kwenu ni kipya haya kunja ngumi kunja ngumi kunja ngumi” ebwana eeh nilianza kumkumbuka karani Jala alipotuambia kuwa kipindi cha kozi huwa hakuna tofauti kati ya DOSO na mazoezi ni vile akili ya kamanda itakavyomtuma ndivyo itakavyotafsiriwa.

Tulikunja ngumi na kuchangamsha mwili kabla ya kuinuka na kupanga mistari kwa mara nyingine.

“Angalieni demo kutoka kwetu” Afande Kalaghe alituambia.

“Afande wa Jeshi la Wananchi wa bongo Zoezi la kunyakua” afande Kalaghe alikuwa akimuamrisha mwenzie.

“Chini kuna miba Juu kuna moto tunaondoka afande uuup uup uup uup” alikuwa akijibu afande Mochiwa ambaye alikunja viganja vyake kisha akaunda alama ya “X” (siyo X ya pono unayoiwaza wewe hii ni ile tunayotumiaga watu wa hesabu ku “Close multiplication”).

Alama hiyo inayofanana na kumi ya kirumi aliiundia kifuani kwake kwa kutumia mikono yake ambayo viganja vyake alikuwa amevikunja kuunda ngumi.

Kamanda huyo alipokuwa akisema Uup Uup alikuwa AKINYAKUA yaani alirusha miguu huku magoti yakiruka kuufikia usawa wa kifua chake.

Baada ya hapo afande Kalaghe akatuambia “Haya kama yeye” tukaliunga na sisi tukifanya alivyokuwa akifanya afande Mochiwa.

“AZIWEA AZIWEA AZIWEA simameni KURUTI” alituambia afande Kalaghe ambaye alikuwa akipitapita katikati ya mistari ghafla nikajikuta nimekula banzi lililohusisha sikio na jicho la upande wa kushoto nisijue chanzo ni kipi.

Nilipunguza urefu na kuchuchumaa chini nikisikilizia frequency (yaani masafa ya redio) zilizokuwa zikichangamsha masikio yangu.

Hapa nilianza kumuelewa mwalimu wangu wa baiolojia kidato cha tatu mzee wa topic pendwa alipokuwa akitufundisha topic iitwayo Uratibu yaani Coordination. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

...............................Itaendelea…………...........………
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom