Maisha ya depo

Maisha ya depo

Wadogo zangu wote hawajaenda Kwa mujibu tulikataa na wanangu hawataenda,mateso matupu
Wa kiume ungewaacha waende. Kuna Cha kujifunza. Wa kike naunga mkono maana mateso yakizidi wengi wanagawa Ili yapungue. Tuliwaambia madawili wetu tupo tayari kuteseka kwa ajili yao ikiwa watawakataa maana sana sana hawezi kukupa adhabu peke yako anagawa kwa kombania au platoon au kibangala.
Tulikubaliana lengo letu ni kwenda chuo na sio ukimwi ila Kuna waliogawa kwa Raha zao. Mwisho tunapimwa HIV waliongezeka tofauti na tulivyopimwa mwanzoni. Maana hairuhusiwi mgonjwa kushiriki mazoezi.
 
Aseehh..inaumiza mnooo...ni WA kike watupu Kwa kweli jeshi ni mtihani mtupu
 
Wa kiume ungewaacha waende. Kuna Cha kujifunza. Wa kike naunga mkono maana mateso yakizidi wengi wanagawa Ili yapungue. Tuliwaambia madawili wetu tupo tayari kuteseka kwa ajili yao ikiwa watawakataa maana sana sana hawezi kukupa adhabu peke yako anagawa kwa kombania au platoon au kibangala.
Tulikubaliana lengo letu ni kwenda chuo na sio ukimwi ila Kuna waliogawa kwa Raha zao. Mwisho tunapimwa HIV waliongezeka tofauti na tulivyopimwa mwanzoni. Maana hairuhusiwi mgonjwa kushiriki mazoezi.
Kwa iyo mwishoni wenye ngoma walikua wengi
 
MAISHA YA DEPO

SEASON-3

EPISODE 17

“Tukiachana na hilo naomba nitambulishe uongozi mtakao kuwa nao kwenye KOMBANIA zenu katika kipindi chote cha mafunzo”.

“Uzuri nyinyi wote ni wasomi tofauti na wale wenzenu wa kujitolea ambao huwa tunaletewa wengine darasa la saba na wanakuwepo darasa la nne mpaka darasa la pili wanakuja wakiwa hawajui kusoma wala kuandika”.

“Kwahiyo sina shaka kuwa elimu mliyokuja nayo ni kubwa sana na jambo la manufa zaidi inalingana hivyo nashawishika kuwa mtakuwa na uelewa uliokuwa sawa na wa haraka zaidi tofauti na wale ndugu zetu wa memkwa”.

“Kuna kitu sisi wangoni tunakiita Organization structure yaani Muundo wa taasisi kwa Kiswahili, msicheke hiyo imezeni na mtulie nayo wala hamtakiwi kuitapika hata kama ikiwa chungu” Matroni alituambia hivyo baada ya kugundua kuwa ametubutua na kitu Kizito.

“Ninaposema taasisi namaanisha nini? Ni kuwa hapa jeshini tuna taasisi mbalimbali zilizo katika mfumo wa makampuni yaani tukisema ALFA COY hiyo COY mbele ni ufupisho wa neno la kingoni yaani COMPANY”.

“Ni vile hatuna chaki wala ubao ila kwakuwa tushakubaliana kuwa nyie ni wasomi kwenye neno COMPANY ukichukua herufi mbili za mwanzo yaani C na O ukachukua herufi moja ya mwisho yaani Y then ukaziunganisha utapata neno COY tumeelewana KURUTA”.

“Ndiyo afande”
“Kumbe sasa tukisema BRAVO COY tunamaanisha taasisi au kampuni ya BRAVO sivyo KURUTA”
“Ndiyo afande”.

“Na ndiyo maana nikasema nyinyi ni wasomi yaani ndani ya nusu dakika mmekwishanielewa ila wale wenzenu wa darasa la saba mpaka la pili zilituchukua siku saba kueleweshana hili” Matroni alikuwa akiongea maneno hayo yaliyotufanya tuangue vicheko.

“Yaani karibia wiki nzima tulikuwa tukifoleni kuwaelewesha maana ya neno COY halafu wanapanga foleni ya kula wakimaliza wanafoleni KOMBANIA tunawaelewesha tena mpaka wiki inakata ndiyo unakuta wameelewa Mwenyezi Mungu awarehemu kwa kweli”.

“Tuachane nao hao ngumbaro jambo lingine ni kuwa kama taasisi lazima iwe na uongozi wake ambao unaelezewa vizuri kupitia muundo wa taasisi ambao kwa kingoni nimesema unaitwaje?”.

“Organization structureeeeee”
“Sijasikia vizuri unaitwa” aliuliza matroni ambaye aliweka mkono sikioni akiashiria kutaka majibu.

“Organization structureeeeee”
“Makamanda wangu mnasikia KURUTA wanavyoichapa lugha adhim ya kingoni” Mataroni alikuwa akiwauliza maafisa wenzake wa jeshi ambao walionekana kutabasamu.

“Hongereni sana wasomi wenzangu nisiongee sana nikaonekana mbaguzi ila wale ndugu zenu kutamka tu hilo neno aah subuuutu ziliwachukua siku zaidi ya mbili wote kuweza kulitamka tu hilo neno”.

“Hivyo kwa ruhusa yenu naomba nitambulishe viongozi wa taasisi zenu ili muwatambue japo wengine walishajitokeza huko kwenye KOMBANIA mkawaona ila si vibaya nikawatambulisha mbele yenu wote mkawaona kusudi hata akiulizwa KURUTA wa Danger COY kuhusu kiongozi yeyote wa Eagle COY awe anamjua kwani jeshi ni moja na mbaya zaidi japo si kwa ubaya kikosi ni kimoja”.

“Bila kupoteza muda mana naona hapo mlipo mnachungulia kwa MZABUNI kunaendeleaje hivyo naomba nianze na ma-Operation Commander yaani ma-O.C ambao ndiyo viongozi wa juu kwenye KOMBANIA zenu naomba ma-O.C wangu mjipange mbele kikombania kusudi KURUTA wawajue”.

“Mtashangaa mbona wako watano na taasisi ziko sita ipoje Ipo sawa kabisa hiyo wala haina shida maana mimi mwenyewe ni O.C wa KOMBANIA fulani na mimi nimejikatia KIBANGALA changu kwahiyo mkinijumlisha si tunafika sita”.

“Ndiyo afande”
“Haya tuanze utambulisho nikianza mimi mwenyewe Alfa COY enhee afande pale”
“BRAVO”“
mkurya na wewe”
“CHARLIE muraa”
“Enheeh baba paroko hapo”
“DANGER bwana yesu asifiwe”
“Matroni na wewe”
“EAGLE mkuu”
“Na kule mwisho”
“FOX mkuu”.

“Sawa naona utambulisho huo umekamilika na wote mmetufahamu hivyo basi nategemea wewe KURUTA wa Fox COY ukiulizwa O.C wa A-COY bila shaka utanyoosha kidole kwangu na wewe wa CHARLIE ukiagizwa kwa O.C wa DANGER sina shaka utaelekea kwa mtumishi pale baba paroko na wewe wa BRAVO ukiagizwa kwa O.C wa EAGLE nina uhakika utamkimbilia Matron pale chap kwa haraka tumeelewana KURUTA”.

“Ndiyo afande”
“Baada ya hapo wanaofuatia ni ma-SIR MEJA naomba SIR MEJA msogee mbele kwa ma-O.C ili KURUTA wawaone”.

Walijipanga maafande hao walioonekana ni wazee kwa umri tofauti na ma-O.C ambao umri ulionekana kudai wazee hao wakiwa na vifimbo vyao mkononi upande wa Danger COY tulipangiwa mpemba mmoja aitwaye Ashiru huku Alfa COY wakipangiwa yule afande mwenye tumbo la kwenda aitwaye SAJENTI Pastima. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

………………...…..…..….…Itaendelea……………...….....……………

View attachment 3294186

MAISHA YA DEPO

SEASON-3

EPISODE 18

Baada ya utambulisho wa ma-SIR MEJA walifuata ma-ODARI KOPLO wakaja makamanda akina Mochiwa, Kalaghe na wengineo mwisho wakamalizikia makarani na mwisho japo si kwa muhimu ila ni muhimu tukatambulishwa ma-ST ambapo muundo ulikamilika kwa mfumo huo.

“Haya makamanda wangu mnaweza kwenda kukaa nafikiri wamekwishawaona” Matroni aliwaruhusu viongozi hao walioko mbele kutawanyika.

“Eeh yote kwa yote nafikiri tumemaliza maana naona mmenuna KURUTA zisije laana zenu zikanushukia hapahapa nilipo maana kusema kweli DOSO jumlisha njaa duu siyo poa Mungu awape ahueni kwa kweli”.

“Baba paroko nakumbuka nilikukatisha nikakwambia nitakupa nafasi mwishoni sasa nafasi yenyewe ni hii ila wakati huu unaipata kwa masharti yaani utakachoongea kiwe kifupi mno”.

“Sawa mkuu huohuo muda mfupi unanitosha sana” alijibu LUTENI Novath.

“Sasa afande nawaona kabisa hawa watu wa Mungu wamenuna sasa ombi langu ni kuwa kabla hawajaenda kula nataka watabasamu ili wakila wale wakiwa na furaha kwenye nyuso zao”.

“Sawa mkuu”
“Utaweza?”
“Hata usijali mkuu”
“Bwana usijekuongea muda mrefu ujue utawakera hawa binadamu”
“Hata usiwaze nakuhakikishia Bosi wangu”.

“Sawa hakuna shida mwanzo niliwaona KOMBANIA nakumbuka mlicheka sana meno thelathini na mbili yote yalikuwa nje sasa nina uhakika nimechagua mtu sahihi naomba kwa dakika chache watu hawa nao nione meno yao angalau kumi yakiwa nje”.

“Anhaah sawa afande asante sana kwa kunipa fursa hii namuomba yule KURUTA St wa kiume Danger COY aje mbele” baba paroko aliniita nami bila kuchelewa nikadabo pale alipo.

Nilipofika afande alilielezea tukio alilosimuliwa na afande Kalaghe tukiwa KOMBANIA nakumbuka uwanja mzima uliripuka kwa vicheko vilivyochukua muda kukoma.

“KURUTA wiih”
“Waah”
“Wiih”
“Waah”
“Ewaah”
“Ewiih” Matroni ilibidi awakatishe kutoka kwenye vicheko vile.

“Uzuri mhusika mwenyewe tuko naye hapa ngoja tumsikilize hujambo KURUTA”.

“Sijambo”
“Enheeh unajisikiaje kwa sasa?”
“Najisikia vizuri tuu”
“ mwanzo ulikuwa unajisikiaje?”
“Aah hali haikuwa nzuri afande”
“Kwanini?”
“Nilikuwa naona mapichapicha tu usoni”
“Mapicha gani hayo tuambie”.

“Kusema kweli afande kuna muda nilikuwa namuona Israeli anapita mbele yangu sijakaa vizuri naona kama jeneza linapita usoni mwangu halafu waliolibeba siwaoni mara kuna kipindi naona watu wanachimba kaburi yaani yalikuwa ni mauzauza matupu” bwana wee watu waliangua vicheko siyo poa.

“Daah hii kali unaitwa nani KURUTA” aliniuliza jina langu Matroni Neema nami nikamtajia.

“Anhaah jina siyo geni wewe sio yule rafiki yake na KOPLO wa dukani aliyekuita pale KOMBANIA usiku”“Ndiyo mimi afande”.

“Aaah we dogo wewe sawa bwana asante kwa kutuvunja mbavu mana nilitegemea meno angalau kumi ila kusema ukweli nimeyaona meno yoote thelathini na nje mbili haya bana rudi kwa wenzako KURUTA”.

“KURUTA wiih”
“Waah”
“Ewaah”
“Ewiih”
“Kwanza tukushukuru baba paroko na KURUTA pale ama kweli hatukukosea kuwachagua mmeupiga mwingi ni kama watu wanataka kuhamia Danger COY vile itoshe kusema watu wa DANGER mmebarikiwa sana”.

“Wakaribie tu tutawapokea kwa ukarimu maana hata maandiko yameibariki nyumba yenye kupokea wageni” alidakia LUTENI Nova.

“Asante sana mtumishi, sikia kutoka kwangu KURUTA”
“Niwape poole kwa yoote mliyokumbana nayo siku ya leo japo bado haijakamilika ila kuna kitu cha muhimu mno kukazia kabla sijawaruhusu mkamsalimie MZABUNI japo najua muda umeenda ila mnipe sekunde chache tu mtanishukuru”.

“Jambo la kwanza kukazia ni kuwa hiki mlichokutana nacho leo ni sehemu ya kile mtakachokutana nacho siku arobaini na mbili za wiki sita hivyo mjiandae kiakili na kisaikolojia hilo la kwanza”.

“Jambo la mwisho niliwapa kazi makamanda wangu ya kuwatambulisha maeneo ya kikosi na nina uhakika wamefanya hivyo sasa sina shaka waliwaonesha hayo maeneo kuwasisitiza kutofika bila ruhusa yao”.

“Sasa kwa kukazia ni kwamba si maeneo hayo tu mliyotambulishwa bali hata yale msiyotambulishwa hamtakiwi vilevile na isije ikatokea ukaenda ukiwa peke yako ama bila ya ruhusu ya kamanda wako hili ni onyo na mimi nawapatia”.

“Zingatieni hili na mwisho kabisa niwapongeze kwa awamu nyingine kwa hatua hii mliyofikia mwisho wa yote hakuna la ziada niwaruhusu mtawanyike kwenda kwenye chakula tukutane tena KOMBANIA baada ya mlo na niwatakie mlo mwema.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Huu ni mwisho🔚 wa msimu wa tatu wa simulizi ya MAISHA YA DEPO.

Oya doja la doso Aiylan wasalan na ndugu yangu zee la masongi kabwela wa kutupa Poor boy bila kuusahau mdomo wa mafulusi moneytalk na swahiba wangu MombaDier njooni tumalizie hii halafu tukutane msimu ujao 🔚.

🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜
LogoMakerCa-1743852388260~2.jpg

🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜
 
Kwa jinsi unavosimulia kupitia location mbalimbali hii ,inaonesha moja kwa moja ni 838KJ
Swahiba yangu Toofast tumekamilisha utambulisho wa camp vipi kwa ukiangalia maeneo yaliyotambulishwa bado unasimamia hiki ulichokisema? 😊
 
View attachment 3295808
🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜
Asante mkuu kwa burudani
Vipi tuutarajie lini tena muendelezo wake
 
One love mwanangu
 
HEY kichekesho cha kambi, asante kwa burudani kaliii,, nasubiri nione msimu unaishaje, je kuna watu wanashuka daraja au wote mnatobo!!!!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom