Maisha ya depo

Maisha ya depo

Ah danger sanaaa, naona mkuu unakula UTAWALA kimasihara kabsaa 😄😄😄
 
MAISHA YA DEPO

SEASON-3

EPISODE 07

“Alafu jichoni umefanya nini NGURUTU mbona jekundu hivyo au mlikuwa mnavuta bangi nini” aliniuliza afande Mochiwa ambaye alikuwa akionekana kunizingatia sana usoni.

“Eti afande pale tulipowaacha kumbe mlikuwa mnapiga msuba” afande Mochiwa alikuwa akimuuliza afande Kalaghe.

“Hakuna afande kwani vipi”
“Unasema hakuna wakati mwenzenu jicho nyanya huku”
“Hamna afande litakuwa ni vumbi tu hilo la pale alipodondokea” akijibu afande Kalaghe aliyekuwa ameinama akizifunga vizuri kamba za viatu vyake.

“NGURUTU unaona vizuri?”
“Ndiyo”
“Kweli?”
“Ndiyo afande” alikuwa akiniuliza afande Mochiwa ambaye baada ya kumjibu alinifanyia lile zoezi la utambuzi wa idadi ya vidole kama alivyonifanyia afande Kalaghe tulipokuwa RESORT.

Baada ya kunifanyia zoezi hilo na kujiridhisha alimwambia afande Kalaghe “Poti chukua watu wako mkatusubiri mbele kule”.

Afande alituchukua watu wake wanne tuliokuja naye kutoka RESORT tukaondoka naye mpaka sehemu moja iliyokuwa na kidimbwi cha maji tukasimama kuwasubiri wenzetu.

Kwa mbali tuliwaona wenzetu wakisimama na kupanga mistari iliyofuatiwa na mbio ndefu huku wakiimba.

“Afande: Usinitege dada nimeokoka mwenzio

Sisi: Usinitege dada nimeokoka mwenzio

Afande: Haleluya
Sisi: Ameeeeeen amee
Afande: Haleluya
Sisi: Ameeeeeen amee”.

Walipofika tulipo walisimama kisha afande Mochiwa akamwambia mwenzake “Afande na watu wako lianzisheni basi”.

Afande Kalaghe alituambia tulalie tumbo karibu na kile kidimbwi niliyasoma mazingira kisha nikafanya reference ya kauli nilizozisikia siku za nyuma kisha nikajifanya bado sijakaa sawa hali iliyopelekea kutojumuishwa kwenye zoezi hilo.

Najua ungependa kujua ni kauli ipi niliirefer wakati huo ilikuwa ni ile ya karani wetu siku tukishangilia baada ya moja ya zoezi kusitishwa tukiwa UWANJA WA DAMU.

Nakumbuka jioni tukiwa KOMBANIA karani huyo alisema “Eti mchana WAZALENDO mlikuwa mnafurahia mvua kunyesha mkiona mmeikwepa introduction acheni kujidanganya hakuna kipindi makamanda wanaenjoy kozi kama kipindi cha mvua”.

Kauli ambayo niliruka nayo ni hapo aliposema “Hakuna kipindi makamanda wanaenjoy kozi kama kipindi cha mvua” hivyo basi nilipokiona kile kidimbwi ni kama kuna alarm iligonga kichwani na kuniambia “mtego huo”.

Sasa sikia kilichowakuta ndugu zangu ambao kwa hiari yetu tulijileta kwenye tanuri hilo tukisubiria matokeo ya kidato cha sita.

“Nimewaambia lalieni tumbo KURUTA kipi hamjaelewa au mnataka niwakande banzi kama mwenzenu kule RESORT” afande Kalaghe alikuwa akiwaambia wale jamaa zangu watatu waliokua wakinipepea nilipozima kule RESORT.

“Haya pita pale kwa mwendo wa nyoka” afande Kalaghe aliwaambia wale watu huku akinyoosha kidole kwenye kile kidimbwi.

Form six wale wastaafu ni kama walikuwa hawaamini walichokuwa wakiambiwa walisizi kwa muda mithili ya wagonjwa waliodungwa sindano ya ganzi.

“KURUTA ni kipi hamjakielewa hapo haya KROO KROO pale” awamu hii afande Kalaghe alikuwa akiwaelekeza huku akiwaburuza kwenye kile kidimbwi.

Baada ya kumaliza kupita kwenye kile kidimbwi wale jamaa watatu nikamsikia afande Mochiwa akiwaambia wafuasi wake “Nyie WADUDU mnasubiri picha ya pamoja nendeni pale” aliwaambia huku akiwasambazia mabanzi migongoni mwao.

Ilikuwa ni patashika nguo kuchanika kwani mpaka wanaisha wote yaliyotokea hapo kati siwezi kuyasimulia yote na kuyamaliza ila kwa uchache ni kuwa sikuwahi kupokea tuzo ya mwanafunzi msafi tangu niko chekechea lakini kwa wakati huo nilikuwa tayari kupokea tuzo ya KURUTA msafi endapo ingekuwepo kwa kweli nililitumia vizuri desa la karani wetu apewe maua yake.

Baada ya kumaliza tulipanga mistari yetu ya kijeshi tukanyakua zetu huku afande Mochiwa akituimbisha.

“Afande: Ewiih
Sisi: Ewaah
Afande: Ewiih
Sisi: Ewaah
Afande: Elewii
Sisi: Elewaa
Afande: Babu wa mababu
Sisi: Ana demu na nyeto anapiga
Afande: We babu wa mababu
Sisi: Ana demu na nyeto anapiga
Afande: Nasema baaabu
Sisi: Utamuua
Afande: We babu wee
Sisi: Utamuua
Afande: Haya baaabu
Sisi: Utamuua
Afande: Kakosa chiga
Sisi: Utamuua
Afande: We babu wee
Sisi: Utamuua
Afande: Kakosa ugoro
Sisi: Utamuua
Afande: We babu wee
Sisi: Utamuua”.

Sikuwa nikicheza mbali na desa la karani Jala na kama wasemavyo waswahili “za kuambiwa ongeza na zako” basi nami sikuacha kujiongeza.

Tulikuwa tukikimbia lakini mimi nikawa najifanya sina mbio yaani nilikuwa katikati ya mstari lakini nikajivuta mpaka nikawa nyuma haikutosha nikawa napunguza mwendo na ilifika hatua nikawa natembea mpaka wenzangu wakawa wameniacha umbali fulani.

“We KURUTA tunakusubiri wewe ujue FANYA GHAFLA” alikuwa ni afande Mochiwa ambaye alikuwa akinisisitiza kufanya haraka kuwafuata pale walipo.

Nilijivuta kisanii nikafika pale walipo ambapo niliwakuta KURUTA wenzangu wamewekwa kitako.

“We staff KURUTA vipi hujisikii vizuri tukurudishe ukalale zako” aliniuliza afande Mochiwa aliyenivisha cheo cha ustaff kwasababu walichokuwa wakikifanya wenzangu sikuwa nikikifanya.

Yaani kama ni kwenye gari wote tunapanda tukiwa abiria lakini abiria wengine hawalipi nauli kwa mgongo wa kuwa wao ni staff na mara nyingi hukaa ile siti nyuma dereva ama hii ya mlangoni kwa mabasi ya mkoani.

“Daah kichwa kinagonga afande na nikiwa nakimbia naona kama kinazidi yaani nakisikia kinavuta balaa”

“Basi sawa kula maisha hapo ukisikilizie”
“Poa afande”
“Umenijibuje wewe? sema sawa afande unanichukulia poa KURUTA” alinikaripia afande huku akiwa ameniwekea uso wa mbuzi.

“Sawa afande” nilimjibu kwa unyenyekevu wa kiwango cha kupokea upako kisha nikajisogeza pembeni kwa ajili ya kutizama kinachotakiwa kutokea nikajikuta nimekuwa kama U.S.A mbele ya mataifa ya ulaya kwenye Berlin Conference.

“Haya KURUTA tano zimeisha saa juu uuuup” kumbe bwana kile kitako walichojikalisha walikuwa wamepewa TANO binafsi nilishangaa kuwakuta kwenye hali kama ile nilitarajia kuwakuta wamekunja ngumi ama wakinywa VIROBA.

“Uuuup” walikuwa ni KURUTA waliokuwa wakisimama juu baada ya kupewa amri hiyo na afande Kalaghe.

Afande Kalaghe akaamua kuwarudisha utotoni kidogo nikamsikia akiimba “Simaama kaa! Simaama kaa! Ruka ruka rukaaa simaama kaa” najua hatuna ugeni na wimbo huu hivyo ni rahisi kuelewa kwamba kama wimbo unavyozungumza na ndivyo KURUTA walivyokuwa wakifanya.

Kwa tafsiri hiyo mpaka afande anaweka kituo hawa binadamu wenye muonekano wa kizombi walikuwa wamekaa chini na ndipo balaa likawa limeanzia hapo. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

................................Itaendelea……….………………...

MAISHA YA DEPO

SEASON-3

EPISODE 08

“Haya KURUTA mtaniambia au hamtoniambia”
“Tutakwambia afande”
“Mtasema au hamtasema”
“Tutasema afande”
“Mtanijibu au hamtonijibu”
“Tutakujibu afande”
“Haya nijibuni hapa ni wapi” aliwauliza afande Kalaghe ambaye mikono yake ilikuwa kiunoni akionekana kuchomekea vizuri tisheti yake.

“Hatupajui afande”
“Mnasemaje nyie mbwa?”
“Hatupajui afande”
“Haya kunja ngumi” aliwaamuru afande Kalaghe ambaye wakati huu mikono yake iliyokuwa kiunoni ilionekana kushirikiana kuuvua mkanda uliokuwa kwenye luksi zilizojipangilia kwa nafasi kukizunguka kiuno cha suruali aliyoivaa.

“Nimesema kunja ngumi KURUTA” aliendelea kusisitiza afande Kalaghe ambaye wakati huu tayari alikwisha utwaa mkanda wake kutoka kiunoni na kuukabidhisha kwenye kiganja cha mkono wake wa kuume.

“Yaani kiroho safi nawauliza mkiwa mmekalisha vikalio vyenu hamtaki kuonesha ushirikiano sasa ngoja niwanyooshe”

“Baba haya huku YANAKUVUNA” aliropoka afande Mochiwa.

“Yako wapi hayo baba”
“Hili hapa lenye kiuno kama sukani ya pawatira”
“Nyie nyie sinimewaambia mkunje ngumi achene MAPUUZA” afande Kalaghe alikuwa akiwaambia huku akiwalamba mikanda kwenye migongo.

“Nyie si mnapenda MASIMANGO mnajikuta mabubu sawa ngoja tuone”
“Haya juu chini, juu chini, chini chini chini, haya juu juu nimesema juu KURUTA haya tulieni hapo hapo sasa nione mtu akienda chini” alikuwa akiamrisha afande Kalaghe.

“Haya na wewe huko mgeni wa heshima tuambie hapa ni wapi?” aliniuliza afande Kalaghe.

“Hapana sipajui afande”
“Yaani na wewe pia hupajui!’
“Ndiyo afande”
“Haya kunja ngumi KURUTA kunja ngumi hapo hapo yaani haiwezekani nyie wote msipajue” duuh mgeni wa heshima ilinibidi nivue suti na kuukabili mgongo wa dunia.

“Haya kwa muda wenu atakayechoka ama atakayekuwa tayari kusema au ikitokea mmepakumbuka mtaniambia tuko sehemu gani hapa mimi ngoja niperuzi zangu” alituambia afande Kalaghe aliyejitwalia jiwe na kuegesha kiuno chake.

“Baba kumbe utopolo wanacheza leo” afande Kalaghe alimuongelesha afande Mochiwa.

“Sijui ngoja niangalie”
“Hata usisumbuke kuangalia nimeona hapa watakuwa kumbukumbu ya sokoine mishale ya saa kumi na wajelajela” afande Kalaghe alikuwa akimwambia mwenzie.

Kwa upande wangu maji yalikuwa yakizidi unga yaani nilikuwa dhoofulihali nilijikaza kwa muda halafu nikajibwaga chini puuh mithili ya bondia aliyekutana na ngumi peresuperesu iliyonifanya nijilaze chini.

“Baba unaua huko” afande Mochiwa alimwambia afande Kalaghe ambaye aliinuka pale alipo na kunifuata.

“KURUTA vipi”
“Safi tu”
“Una shida gani”
“Kichwa afande”
“Anhaa sawa tukupe dawa au uende ukalale”
“Hapana afande siumwi sana nilisikia kizunguzungu tu”
“We KURUTA kule nyanyua kiuno hicho acha kutegea” alikuwa ni afande Mochiwa aliyekuwa akimwambia moja ya KURUTA aliyeonekana kushusha mwili wake chini.

“Anhaa basi endelea kulala hapo umuote na demu wako” aliniambia afande Kalaghe ambaye alikuwa akiondoka kuelekea kwa wale jamaa zangu.

“We KURUTA wewe acha MAPUUZA haya nyanyua mwili huo kaza na kiuno hicho usinipime imani” alikuwa ni afande Kalaghe ambaye alikuwa akiwaambia wana huku akiwashushia mikanda kwenye miili yao ambayo kwa muda huo ilikuwa ikitambulika kama miili ya jeshi.

“Dah! ila jua linawaka afande” afande Mochiwa alikuwa akimwambia mwenzie.

“Sio poa afande hawa jamaa walioridhika kujianika juani wapewe maua yao”
“Inabidi tufanye kitu afande kwa ajili yao” alisema afande Mochiwa aliyejitwalia ndoo na kujisogeza kwenye bomba la maji lililokuwepo mahala hapo kisha kulifungulia.

“Afande tunaomba TANO afande" zilisikika sauti za chini kwa chini kutoka kwa KURUTA wakishinikiza kupewa ahueni baada ya kuelemewa na DOSO.

“Eeeeh bado hamjasema na mtasema tu na lazima mseme”alikuwa ni afande Kalaghe aliyejibu baada ya kuombwa TANO.

“Wanataka TANO afande” aliuliza afande Mochiwa ambaye alikuwa akiwasogelea KURUTA ambao vipara vyao vilikuwa vikitiririka jasho kama chupa ya maji iliyotoka jokofuni.

“Ndio baba yameanza kusanda eti yanataka tano” alijibu afande Kalaghe.

Pwaaaah! “TANO zenyewe ndiyo hizo sasa” alisema afande Mochiwa ambaye alimwagia jamaa zangu maji kutoka kwenye ndoo iliyokuwa mikononi mwake.

“We KURUTA uliyekuwa likizo hembu niletee ndoo hiyo” aliniagiza afande Mochiwa nami nikaenda kuichukua ndoo iliyokuwa bombani na kumpelekea.

Pwaaaah! Alikuwa ni afande Mochiwa ambaye alimwaga ndoo ya pili ya maji migongoni mwa KURUTA na kuniamuru nikaendelee kukinga ndoo nyingine ya maji.

“Haya ROLI ROLI ROLI Kuruta nenda kushoto” afande Mochiwa aliwaamrisha viumbe hao kubiringita kuelekea upande wa kushoto.

“Haya kulia kulia rudi kulia we KURUTA hiyo ndoo bado haijajaa”
“Ilete hivyo hivyo weka hiyo nyingine” alinisisitiza afande Mochiwa aliyeonekana kuwa mzuka wa hali ya juu usawa wa mawingu.

Pwaaah! Ilikuwa ni ndoo nyingine iliyomwagika kwenye miili ya wanangu hao wahitimu wa kidato cha sita.

Hali hiyo iliendelea mpaka zilipofika ndoo karibia saba ndipo waliojikatia tamaa wakabaki wamelala tu na kuwafanya wengine walioko upande wa pili kushindwa kuendelea na zoezi hilo.

“Aii! Mmmnh! Mama wee” ilikuwa ni miguno iliyokuwa ikisikika mahala hapo kutoka kwa KURUTA.

“Baba naona limewaingia wameshaanza kunena kwa lugha” alijinenea afande Kalaghe.

“Bado sijawasikia sijasikia kinyakyusa hapo KURUTA Twambombo, Kamwene, Togolani, Mwapanga, Ausindile, Mwivihi, Shimboni shafo, Namnani, Ndimunofuela, Mosie nzeze, Mbukweni mmeona mlivyokuwa majeuri yaani kuwasalimia kote hakuna aliyenijibu” alikuwa ni afande Mochiwa aliyekuwa akiwasalimia kwa lugha mbalimbali.

“Mwapanga mpola zako, Kamwene unogage, Tununu tumasiku, Chivyedi, Mbokwa mhanyenye, Hanoga hausindile gwegwe, Nchedi namnani” wenye lugha zao nao waliamua kujibu.

“Nzuuri nzuri iyo kaeni kitako wanangu mle TANO kaeni kitako nzuri hiyo nimeipenda” alionekana kufurahishwa afande Mochiwa baada ya kujibiwa salamu hizo.

“Mnaona KURUTA mmekula TANO na mmekula TANO kwasababu mmejibu na ndivyo tunavyotaka mkionesha ushirikiano kama hivyo tunawapa tano nyingine haya tusipoteze muda tuambieni hapa ni wapi?” aliendelea kuongea afande Mochiwa.

“Hatupajui afande”
“Eeeh”
“Hatupajui afande”
“Mnasema?”
“Hatupajui afande”
“Aaah washenzi nyie kunja ngumi” afande Mochiwa aliwaamuru watu wale kurudi walikotoka ambako sidhani kama kwa hiari yao wangekubali kufanya hivyo kwa upande wangu yangu yalikuwa ni macho.

“Oya afande malizana na watu wako tuondoke zetu” afande Mochiwa alimwambia afande Kalaghe. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

…………..….…Itaendelea…………..………
 
EPISODE 09

“Anhaah sawa ngoja kwanza nimuangalie wife kule juu” alijibu afande Kalaghe ambaye alikuwa akitazama ghorofa ya juu katika moja ya majengo yaliyokuwepo sehemu hiyo.

“Mnnh ndiyooo nishamuona mama watoto na yeye ananiangalia sasa ngoja nizidishe UNAA” alijisemea afande Kalaghe.

“Haya KURUTA KURUTA KURUTA nimewaita mara tatu haya niambieni hapa ni wapi?”
“Hatupajui afande”.

“Anhaah kumbe nyie sikio la kufa yaani mnataka mpaka tuwatoe damu ndiyo muelewe tunachokimaanisha siyo” afande Kalaghe alijaribu kuwatisha.

“Nawauliza nyie watu mnataka tuwatoe damu” aliuliza tena baada ya kukosa majibu mara ya kwanza.

“Hapana afande”
“Haya semeni hapa ni wapi?”
“Hatupajui afande”
“Wapuuzi nyie hapa mlipo ndipo zilipo appartments za maofisa wa jeshi wa kikosi hiki cha HCH KJ ni kwasababu mnanuka matope ndiyo maana sitawapeleka ilipo apartment yangu”.

“Kama zilivyo sehemu nyingine huruhusiwi kufika mahala hapa pasi na ruhusa ya kamanda wako tumeelewana NGURUTU”.

“Ndiyo afande”
“Haya kama mmeelewa semeni sasa nimewaambia hapa ni wapi?”
“Hapa ni apartment za jeshi afande”
“Endeleeni kwani nimewaambia hivyo tu”
“Umesema hutupeleki kwako kwasababu tunanuka tope”.

“Mnnnh wapuuzi kweli nyie haya lingine nililowaambia” alitabasamu afande Kalaghe baada ya kupewa jibu hilo ambalo nadhani hakutarajia kulisikia.

“Umetuambia kuwa haturuhusiwi kufika bila ya ruhusa yako”
“Pumbaavu nimewaambia bila ruhusa yangu kweli?” alihoji afande Kalaghe.

“Hapana afande”
“Enheeh nimesemaje?”
“Bila ruhusa ya kamanda”
“Haya iwekeni vizuri hiyo sentensi mkiwa mmepangilia vishazi na vinominishi pale vinavyotakiwa kuwa”.

“Haturuhusiwi kufika mahala hapa bila ruhusa ya kamanda”
“Ndiyooh! Hutakiwi kufika mahala hapa pasi na ruhusa ya kamanda wako sasa jichanganye siku nikukute mitaa hii bila ya ruhusa utanipa tofauti kati ya pepopunda na degedege”.

Baada ya mbilinge hizo afande Kalaghe alituweka kitako na kutuambia “Sasa wanangu nataka tugonge songi hapa mpaka wifi yenu ashuke kutoka kule juu aje anikumbatie mbele yenu” baada ya maneno hayo yalianza kusikika makofi paah! Paah! Paah! Yaliyousindikiza CHENJA hiyo.

“We KURUTA njoo kwa wenzako huku” aliniambia afande Kalaghe nami nikajiunga nao.

“Afande: Eeembe dodo sijalila embe dodo bwana sijalila eeembe dodo sijalila embe dodo bwana sijalia

Sisi: Eeembe dodo sijalila embe dodo bwana sijalila eeembe dodo sijalila embe dodo bwana sijalia

Afande: Na baruuua nimetuma na barua bwana nimetuma na baruuua nimetuma na barua bwana nimetuma

Sisi: Na baruuua nimetuma na barua bwana nimetuma na baruuua nimetuma na barua bwana nimetuma

Afande: Na majiiibu sijapata na majibu bwana sijapata na majiiibu sijapata na majibu bwana sijapata

Sisi: Na majiiibu sijapata na majibu bwana sijapata na majiiibu sijapata na majibu bwana sijapata

Afande: Eeembeh (paah!) eembeh (paah!) eembeh (paah!)

Sisi: Eeembeh (paah!) eembeh (paah!) eembeh (paah!)”.

“Oya mbona haji mwambieni aje basi” alikuwa akituambia afande Kalaghe baada ya kumaliza kuimba na pisi aliyotuahidi kuwa itakuja kumkumbatia haikutokea.

“Basi mwambie aje” alianza kuimba afande Kalaghe huku akionesha ishara ya kutaka kujibiwa nasi hatukuwa na hiyana tukaanza kumpa sapoti.

“Aje”
“Oooh aje”
“Aje”
“Asije peke yake”
“Aje”“Aje na wigi lake”
“Aje”
“Oooh aje”
“Aje”
“Aje basi aje”
“Aje”
“Asije peke yake”
“Aje”
“Aje na dela lake”
“Aje”

Ebwana eeh ilikuwa ni burudani chini ya mtumbuizaji wa zamu Afande Kalaghe ambaye hakuwa anaimba tu bali alikuwa akicheza pia hali ambayo ilitufanya namba kubwa ya tuliokuwa eneo hilo kufurahi.

Kusema kweli makamanda wetu walikuwa ni mfano halisi katika moja ya beti ya bwana kikulacho (Mr. Nice) ambaye kwenye moja ya nyimbo zake aliwahi kuimba “Kumbe anang’ata na kupuliza puuh kama panya buku ee”.

Hali ilikuwa hivyo kwa maafande wetu ambao waliweza kutuhenyesha kwa kututoa jasho la kutosha lakini ilikuwa kila baada ya msoto kuna tukio moja watalifanya tunajikuta tunasahau shida zote na kila mmoja wetu asipocheka basi atatabasamu.

Nahisi huwa wanapigwa msasa kabla ya mafunzo kuanza ambayo huwasaidia katika utambuzi wa hali tunazokuwa nazo kipindi chote cha mafunzo kwani wanajua sana kucheza na akili zetu wanajua ni kipindi gani cha kutukera na ni kipindi kipi cha kutupooza.

“Haya KURUTA simameni tuondoke” alituamuru afande Kalaghe huku akitabasamu.

Tulisimama ila wakatokea wachache kati yetu wakasema “Tuimbie mwingine wa mwisho afande”
“Eeeh mnataka niimbe tena”
“Ndiyo afande” awamu hii tulijibu wote kwa umoja wetu siyo kwamba tulikuwa tukipata burudani lakini pia ilikuwa ni moja ya mbinu ya kupoteza muda na kupooza machungu yaani hizi zilikuwa ni TANO fulani hivi za rejareja.

“Anhaa kwa kuwa pisi imegoma kutokea ngoja sasa tuanze kuiita ije haya nipeni biti wanangu” alitumbia afande Kalaghe tukaanza kupiga makofi paah! Paah! Paah!“

Afande: Na mchumba mbona hutokei mama wee

Sisi: Anakuja
Afande: Hii pisi mbona haitokei naisubiiri

Sisi: Itakuja
Afande: Niko hapa mwenzenu naisubiri toka alfajiri

Sisi: Inakuja……”.

Alikuwa akiimba wimbo huo afande huyo wa jeshi la wananchi huku akitizama juu ambako kulikuwa na hadhira iliyokuwa ikishuhudia kinachoendelea sina shaka zilikuwa ni familia za makamanda waliokuwa wakiishi kwenye majengo hayo.

“Oya tuondokeni zetu wanangu si mnaona pisi imegoma kuja” alituambia afande Kalaghe ambaye za ndaani kabisa tulikuja kugundua kuwa hakuwa akiishi kwenye apartments hizo.

Kifupi alikuwa akitupanga kwani hata kule anakoishi yuko peke yake yaani afande wetu ni bachela na ndiyo maana hakuna chuma chochote kilichojitokeza.

Mwisho wa wimbo huo ulikuwa ukimaanisha mwanzo wa pumzi ya moto kutoka kwa makamanda wetu kwakuwa tulishatambulishwa sehemu hiyo tulijipanga na kuondoka zetu huku afande akionekana kitufe chake cha vibe kipo ON hatukutoka kizembe akaweka CHENJA.

“Afande: Ewiih
Sisi: Ewaah
Afande: Elewii
Sisi: Elewaa
Afande: Vaileth nakupenda sana cheka kidogo nione wako mwanya

Sisi: Vaileth nakupenda sana cheka kidogo nione wako mwanya

Afande: Tulikuwa wengi maama wee wamekufa kwa mabomu mbagala eeh

Sisi: Tulikuwa wengi maama wee wamekufa kwa mabomu mbagala eeh

Afande: Nyumba ya makuti Zanzibar ina umeme wee kama unabisha panda boti ukaione

Sisi: Nyumba ya makuti Zanzibar ina umeme wee kama unabisha panda boti ukaione”. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

……….........……….…Itaendelea……………….......………
 
Sisi: Nyumba ya makuti Zanzibar ina umeme wee kama unabisha panda boti ukaione”.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

EPISODE 10

Kama kawaida nikiwa mtu wa nyumanyuma tulifika sehemu moja ambayo tulikuta shughuli mbalimbali za useremala na uchomeleaji zikiendelea isivyo bahati kulikuwa na bomba la maji lililokuwa likitumika na mafundi hao.

Kuwepo kwa bomba hilo siyo shida saana maana hata kwenye apartments tulilikuta ingawaje lilileta shida pia shida ya bomba hilo la mafundi ni pale maji yanapomwagikia.

Kwanza ulichimbwa mfereji ambao marefu, mapana na kina chake hfuuuh! (Shikamoo mfereji) kifupi maji yalikosa pakwenda yakatuama na mwishowe yakatengeneza tope jeusi asili ya ujiuji.Kwenye mtaro huo palikuwa pakisika “nziiiiiiiiiiiiiii” ambazo zilikuwa ni sauti za Mbu waliokuwa wakifurahia chakula iliyojipeleka sehemu hiyo pasi na kujua kuwa walikuwa ni askari ambao wamefika mahala hapo kuteketeza makazi yao.

Ni mshangao kuona mafundi wakiyaacha mazalia hayo ya mbu na tope lile jeusi linalonuka mithili ya yai lilikosa kuatamiwa ila naweza kuelewa kwamba huenda yakawa ni maelekezo tu waliyokuwa wakipewa kama ilivyo kwa marefa wetu wa kibongo.

Kuna uwezekano baada ya kozi kuisha panafunikwa na pale wanapowasili WAZALENDO wengine panachimbwa kwa ajili ya shughuli hiyo maana sidhani kama yupo binadamu anayeweza kuvumilia kufanya kazi kwenye mazingira hayo.

Basi bwana alipita mmojammoja kwenye tanuru lile la matope kwa kugalagala mpaka pale walipoisha wote wakawekwa pembeni na kukaguliwa yule aliyeonekana kufanya janjajanja aliamriwa kurudia kipengele hicho.

“Haya wewe na wewe nendeni mkapodoane pale” alikuwa ni afande Mochiwa aliyekuwa akiwaambia wale waliokwepesha nyuso zao wakati wa kujigalagaza hivyo wakawa wanaonekana wasafi kwenye nyuso afande akawaamuru wakapakazane matope.

“Haya na wewe kukunja ngumi ushindwe hata kujipakaza matope nako usiweze haya nenda pale” ebwana eeh awamu hii afande Mochiwa alinigeukia.

Nilikuwa nimejitenga sehemu moja ambayo nilikuwa nikihangaika kufukuza Mbu huku nimejikunyata kana kwamba ni mtu aliyekuwa akihisi baridi.

Nilisingizia kujisikia baridi, kizunguzungu na homa ila shinikizo lilikuwa ni kubwa kutoka kwa afande huyo ambaye hakuweza kushawishika na sababu hizo hivyo na mimi nilijipitisha kwenye mfereji huo.

Maafande walitupanga kwenye mistari miwilimiwili iliyotufanya kutazamana yaani ilikuwa kila mtu anatizamana na mtuwe.

Kwakweli hatukuweza kutambuana kwa kutazamana usoni muda huo kwani wote tulikuwa tukifanana usoni tukiwa tumejipodoa kwa vipodozi hivyo vya kijeshi.

“KURUTA mtizame Jirani yako huyo aliye mbele yako” alituambia afande Kalaghe.

“KURUTA acheni MAPUUZA nimesema mtazame usoni aliye mbele yako”.

“Tayari ushamuangalia eeh?”
“Ndiyo afande”
“Haya mwambie umependeza jirani”
“Umependeza jirani”
“Nzuuri hiyo ndiyo muzuri kabisa nimeipenda haya twende” alituambia afande Kalaghe ambaye alinyoosha mikono juu na kuanza kupiga makofi paah! Paah! Paah!

Afande: Honey wangu fanya ujirembe
Sisi: Honey wangu fanya ujirembe
Afande: Ujirembe nataka tutoke
Sisi: Ujirembe nataka tutoke
Afande: Mi nina mzuka na wewe
Sisi: Mina mzuka na wewe
Afande: Nina morali na wewe
Sisi: Mina morali na wewe
Afande: Haya haya kipenzi wee
Sisi: Haya haya kipenzi wee
Afande: Haya haya laazizi wee
Sisi: Haya haya laazizi wee”.

“Haya hapohapo mlipokaa kiroho safi kiroho barida niambieni hapa ni wapi”
“Hatupajui afande”
“Mnasema nini nyie watu”
“Hatupajui afande”
“Ah wapi hembu kunjeni ngumi wanangu mjue nyie ni mafala sana yaani hampajui na hapa” alituambia afande Mochiwa.

Tulizikunja na kushushiwa kisago lakini mwishowe tukasikia “Hapa ni factory sehemu ambayo vitanda mnavyolalia na thamani nyingine msizozitumia zinazalishwa”.

“Wale jamaa mnaowaona pale ndiyo wanaozitengeneza kifupi ndiyo walikuwa wanawapa jeuri ya kulala mpaka kunakucha ila kuanzia leo hii ndiyo mwisho maana mtakuwa mnakesha mpaka kunakucha na kama mnabisha nipeni mikono tushindane” aliongea afande Mochiwa huku akipita katikati yetu na kutulazimisha kutushika mikono.

“Kama zilivyo sehemu nyingine hamtakiwi kufika mahala hapa pasipo na ruhusa ya kamanda sasa ole wako utatuambia kwanini Iddi Amini hana maziwa lakini anaitwa dada” aliendelea kukazia afande Mochiwa.

Tuliondoka mahala hapo kwa mwendo mchafu kwenye barabara iliyoinama kutoka kiwandani kuelekea kule tulikotakiwa kwenda hivyo mwendo wa bingiribingiri ukawa haukwepeki.

Tulifika moja ya sehemu ambayo tulichuchumaa na kutakiwa kutembea kwa ubatabata kwenda mahala ambapo nakumbuka siku moja tulienda kushusha mahindi tuliyopakia kwenye gari baada ya kuyavuna shambani.

Katika muda huo ambao jua lilikuwa limekwishakaa pale linapotakiwa kukaa tulitakiwa kujipanga sehemu ambayo kulikuwa na sakafu kuukuu iliyokuwa imepashwa moto na jua hilihili linalochomoza mashariki na kuzama magharibi.

“Hapa ni wapi KURUTI”
“Hatupajui afande”
“Kabisaa”
“Ndiyo afande”
“Jamani haya si mahindi mliyotoka kuyavuna jana yamefikaje hapa kama hayakuletwa na nyie” alituuliza afande Kalaghe nasi tukabaki kimya tukose cha kumjibu.

“Baba YANAKUVUNA hayo hembu tuyalaze kwanza akili ziwakae sawa yanaonekana yamechoka” aliropoka afande Mochiwa akishinikiza tulale kwenye ile sakafu badala ya kusimama.

“Haya hapohapo ulipo lalia mgongo KURUTA” amini usiamini bwana afande Kalaghe alitutaka tulale kwenye ile sakafu ambayo kwa muonekano wake hapo awali ilikuwa ikitumika kama uwanja wa mpira wa kikapu kwani kulikuwepo na milingoti ya magoli iliyosimama.

Ile sakafu ilikuwa imeshika moto barabara kiasi kwamba hakuna hata mmoja kati yetu aliyemaliza dakika walau moja bila kugeuka mbavu za upande wa kulia na kushoto zilikuwa zikitumika kama mbadala wa mgongo.

Ni angalau tungevaa truck suit na masueta yake ahueni ingepatikana ila kwa mtoko ule tuliovaa haukuwa rafiki kwetu maana nafuu ilikuwepo wakati wa kuulalia mgongo angalau unaweza kukunja miguu na kuiweka mikono juu ya tumbo ingawaje maafande hawakutaka tuipate nafuu hiyo walikuwa wakituzuia wakijua fika tunapunguza ukali wa zoezi kwani nao walipita kwenye hali hiyo.

Mgongo ulipokolea moto tuliamua kulala kiubavubavu ambapo umuhimu wa kuvaa suruali ulionekana wazi kwani tukilalia ubavu sehemu za mwili zinakuwa na mgusano na sakafu moja kwa moja yaani ilikuwa ni sawa na kuweka kipande cha nyama kwenye kaa la moto vuta picha.

Kuna wakati tulipolalia ubavu tulijaribu kuiinua miguu na mikono kutoka kwenye ile sakafu kilichokuwa kikitokea ni kuwa uzito wote ukawa unaegemea kwenye nyonga hakuna rangi tuliacha kuona sehemu hiyo. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

…………………….…Itaendelea………………………………
 
EPISODE 11

Katika sehemu zote tulizopita hii haikuwa ya kusahalika hata kidogo binafsi naweza kulisau lile banzi nililokumbana nalo kule RESORT ila hii sehemu ambayo jina lake la utani huitwa “Karaini” wakimaanisha kwenye karai yaani kile chombo kinachotumika kukaangia vitafunwa na mbogamboga jikoni.

Katika kujifikirisha nikakumbuka kuwa nina ile hati ya msamaha kutoka kuzimu nikaona cha kufia nini na kwanini nijitese nikaamka zangu na kuchuchumaa.

“Haya wewe wewe nani kakwambia uamke” aliuliza afande Mochiwa baada ya kuniona nimechuchumaa.

“Baba vipi lalia mgongo acha mapuuza KURUTA” alisema afande Kalaghe huku akinisogelea.

“Haya umepatwa na nini wewe MZALENDO wa zamani”

“Daah kichwa kinagonga tena nasikia na kizunguzungu afande”

“Kumbe ni wewe KURUTA sikukuona vizuri maana sasa hivi wote mmefanana haya sogea pale utupishe hapa tuna jambo letu” aliniambia afande Kalaghe nami sikuitumia vibaya nafasi hiyo nilijikusanya na kujiweka kando ya timbwili lile.

Ingawaje sikukaa kivulini kwani eneo hilo lilikuwa ni la wazi sana ila kidogo niliipata nafuu tofauti na mwanzo nilipokuwa nimeungana na wale jamaa zangu.

Nikiwa hapo nilikuwa nikiwaonea huruma sana wana kwani nilishaonja tamu na chungu za shuruba hizo.

“Afandeee afande tunaomba tano afande” zilikuwa ni sauti za jamaa zangu wa DANGER COY waliokuwa kwenye karai wakimuomba heri afande.

“Ahahahah nzuri hiyo, Baba naona DOSO limewaingia sasa” alikuwa ni afande Kalaghe aliyejichekesha kama mwanaume aliyekutana na mwanadada aliyemtoa uvulana wake.

“Tano hazitoki mpaka pale mtakaposema hapa ni wapi” aliropoka afande Mochiwa na sauti yake nzito yenye kukwaruza mithili ya kijana mlalahoi aliyetoka kuchanganya zege.

Hali hiyo iliendelea huku wakibadilishiwa zoezi kama vile kukunja ngumi, kulalia tumbo pamoja na KUROLI mazoezi ambayo hakukuwa na hata moja lenye nafuu.

Wakati hali hiyo ikiendelea nilimuona afande Mochiwa na dada mmoja wakijadili jambo na baada ya kikao hicho kifupi nilimuona dada yule akiinuka na kuja pale nilipo.

Nilimtupia jicho na kugundua kuwa mwanadada yule hakuwa akitembea vizuri kwa Kiswahili kinachotambulika na BAKITA mwanadada huyo alikuwa akiguchia yaani alikuwa akitembea kwa kuchechemea.

Mwanzo nilifikiri kuwa huenda labda ni kutokana ukali wa DOSO alilotoka kukabiliana nalo ila nikiwa namuangalia kwa kubahatisha nikang’amua jambo kumbe kilichomfanya afande amtenge mwanadada yule ni yale yale malipo ya kila mwezi yaani mshahara.

Ile taswira ya SIX WEEK tuliyokuwa tukisimuliwa nilikuwa nikiishuhudia kwa wakati huo bi dada yule alikuwa akitokwa na damu iliyokuwa ikimchuruzika miguuni kwa kifupi kabisa ni kuwa “kipofu kauona mwezi”.

Naomba kutoa code kwa mabaharia, kama kuna mtoto wa mama mkwe mtarajiwa anakuvuruga kichwa kuwa kapoteza siku zake usihangaike kununua vipimo we mtafutie kambi inayofanya intro mpaka kamchakato kaishe atakuwa keshaziona tu maana si kwa mikikimikiki ile.

Sisemi hivyo kwa sababu ya huyo dada pekee bali tulikutana na kesi nyingi kama hizo tuliporudi kikosini wadada wengi walikutana na gari la mshahara na kupatiwa ujira wao.

Baada ya kurupushani hizo alisikika afande Kalaghe akisema “Hapa ni Godauni sehemu ambayo chakula cha kikosi kinahifadhiwa kama zilivyo sehemu nyingine inyeshe mvua liwake jua hamtakiwi kufika hapa pasipo na ruhusa ya kamanda”.

Baada ya utambulisho TULIFOLENI mistari mitatu ya kijeshi na kuondoka kwenye hilo Karai kwa mara ya kwanza njiani tulipishana na BOGI ambalo lilionekana kutoka kule tunakoelekea.

Tukiwa kwenye njia hiyo inayoelekea kwenye makutano ya njia inayokwenda REST HOUSE, utawala na ghala la kuhifadhi silaha afande Kalaghe alikuwa akituimbisha huku tukikimbia.

Afande: Ewii
Sisi: Ewaa
Afande: Ewii
Sisi: Ewaa
Afande: Elewii
Sisi: Elewaa
Afande: Danger Coy ya DEMO ndo mana morali

Sisi: Danger Coy ya DEMO ndo mana morali

Afande: Ee Dcoy ya DEMO ndo mana morali

Sisi: D Coy ya DEMO ndo mana morali

Afande: Ee Morali
Sisi: Morali
Afande: Ewii
Sisi: Ewaa
Afande: Ewii
Sisi: Ewaa
Afande: Alii alii aling’ang’ang’ang’a moraali

Sisi: Moraali
Afande: Aling’ang’ang’ang’a moraali

Sisi: Moraali
Afande: Oya oyaa moraali
Sisi: Moraali
Afande: Oya oyaa Masooja
Sisi: Masooja”.

Tulipofika kwenye makutano hayo ambapo nakumbuka ndipo nilipokutana na Matroni Anna na kupiga naye stori kwa mara ya kwanza siku ile akijing’atang’ata.

Tulishika njia inayoelekea REST HOUSE na kuweka kituo kwenye daraja lililokuwa likiunganisha mitaa ya REST HOUSE na sehemu nyingine muhimu za kikosi maafaande wakatuamuru tuingie mtoni.

Binafsi nilitaka kujifanya mgonjwa ila nilipoifikiria hali niliyonayo baada ya kujigaragaza kwenye matope kule FACTORY nikaona ni bora tu nikaingia kujisafisha.

“Chubwii chubwii chubwii” zilikuwa ni mbizi nilizokuwa nikizipiga kwenye maji ya mto huo huku nikipita chini ya miguu ya watoto wa kishua ambao walionekana kuwa waoga kuogelea.

Hazikuwa shida zangu binafsi nilikuwa nikifurahi na kujikumbushia enzi zangu nikiwa naogelea kwenye madimbwi ambayo baada ya kurudi nyumbani nilikutana na viboko vya kutosha kutoka kwa Mzee Mjuzi aliyekuwa akinikataza kuogelea kwenye maji machafu ya madimbwi hayo.

“Wooi wooi mamba huyo” zilikuwa ni kelele za wale niliokuwa nikipita chini kwa chini na kuwagusa huku nikikatiza kati katikati yao nikasikia wakipiga makelele na kutoka nje wakidhani wameguswa na kiumbe huyo.

Baada ya kutoka mtoni tulijipanga kama ilivyokuwa ikitakiwa kisha afande Kalaghe akatuambia “Zoezi la kunyakua”.

“Chini kuna moto juu kuna miba tunaondoka afande uup uup uup uup” tulimjibu na kuanza kukimbia tukipandisha kimlima ambacho kwa mara ya kwanza tulipita njia ambayo ilionesha tayari kuna watu wameshapita.

Kwa lugha nyepesi ni kwamba sehemu zote tulizopita hapo kabla tulikuwa wa kwanza faida ambayo watakutana nayo MABOGI yatakayofuata nyuma kwani huenda yasikutane na baadhi ya madimbwi ambayo tutakuwa tumeshayakausha ila si kwa pale FACTORY kwa kweli lile tope hakuna wa kulikausha.

Tukiwa tumeshika njia hiyo tulipishana na BOGI ambalo walionekana DOSO kuwaingia kwelikweli ingawaje sipingani yaliyosemwa na wahenga kuwa “nyani haoni kundule” lakini lugha yao ya mwili haikuacha kuongea. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

………………………….…Itaendelea…………………………
 
Mgongo ulipokolea moto tuliamua kulala kiubavubavu ambapo umuhimu wa kuvaa suruali ulionekana wazi kwani tukilalia ubavu sehemu za mwili zinakuwa na mgusano na sakafu moja kwa moja yaani ilikuwa ni sawa na kuweka kipande cha nyama kwenye kaa la moto vuta picha
Duuh siyo poa
 
Naomba kutoa code kwa mabaharia, kama kuna mtoto wa mama mkwe mtarajiwa anakuvuruga kichwa kuwa kapoteza siku zake usihangaike kununua vipimo we mtafutie kambi inayofanya intro mpaka kamchakato kaishe atakuwa keshaziona tu maana si kwa mikikimikiki ile.
😆😆😆 aah basi wameisha hii siiachi hii pale Lugalo na ndugu zao Twalipo patakua kama maabara au duka la madawa hivyo wanizoee🤣🤣🤣
 
MAISHA YA DEPO

SEASON-3

EPISODE 09

“Anhaah sawa ngoja kwanza nimuangalie wife kule juu” alijibu afande Kalaghe ambaye alikuwa akitazama ghorofa ya juu katika moja ya majengo yaliyokuwepo sehemu hiyo.

“Mnnh ndiyooo nishamuona mama watoto na yeye ananiangalia sasa ngoja nizidishe UNAA” alijisemea afande Kalaghe.

“Haya KURUTA KURUTA KURUTA nimewaita mara tatu haya niambieni hapa ni wapi?”
“Hatupajui afande”.

“Anhaah kumbe nyie sikio la kufa yaani mnataka mpaka tuwatoe damu ndiyo muelewe tunachokimaanisha siyo” afande Kalaghe alijaribu kuwatisha.

“Nawauliza nyie watu mnataka tuwatoe damu” aliuliza tena baada ya kukosa majibu mara ya kwanza.

“Hapana afande”
“Haya semeni hapa ni wapi?”
“Hatupajui afande”
“Wapuuzi nyie hapa mlipo ndipo zilipo appartments za maofisa wa jeshi wa kikosi hiki cha HCH KJ ni kwasababu mnanuka matope ndiyo maana sitawapeleka ilipo apartment yangu”.

“Kama zilivyo sehemu nyingine huruhusiwi kufika mahala hapa pasi na ruhusa ya kamanda wako tumeelewana NGURUTU”.

“Ndiyo afande”
“Haya kama mmeelewa semeni sasa nimewaambia hapa ni wapi?”
“Hapa ni apartment za jeshi afande”
“Endeleeni kwani nimewaambia hivyo tu”
“Umesema hutupeleki kwako kwasababu tunanuka tope”.

“Mnnnh wapuuzi kweli nyie haya lingine nililowaambia” alitabasamu afande Kalaghe baada ya kupewa jibu hilo ambalo nadhani hakutarajia kulisikia.

“Umetuambia kuwa haturuhusiwi kufika bila ya ruhusa yako”
“Pumbaavu nimewaambia bila ruhusa yangu kweli?” alihoji afande Kalaghe.

“Hapana afande”
“Enheeh nimesemaje?”
“Bila ruhusa ya kamanda”
“Haya iwekeni vizuri hiyo sentensi mkiwa mmepangilia vishazi na vinominishi pale vinavyotakiwa kuwa”.

“Haturuhusiwi kufika mahala hapa bila ruhusa ya kamanda”
“Ndiyooh! Hutakiwi kufika mahala hapa pasi na ruhusa ya kamanda wako sasa jichanganye siku nikukute mitaa hii bila ya ruhusa utanipa tofauti kati ya pepopunda na degedege”.

Baada ya mbilinge hizo afande Kalaghe alituweka kitako na kutuambia “Sasa wanangu nataka tugonge songi hapa mpaka wifi yenu ashuke kutoka kule juu aje anikumbatie mbele yenu” baada ya maneno hayo yalianza kusikika makofi paah! Paah! Paah! Yaliyousindikiza CHENJA hiyo.

“We KURUTA njoo kwa wenzako huku” aliniambia afande Kalaghe nami nikajiunga nao.

“Afande: Eeembe dodo sijalila embe dodo bwana sijalila eeembe dodo sijalila embe dodo bwana sijalia

Sisi: Eeembe dodo sijalila embe dodo bwana sijalila eeembe dodo sijalila embe dodo bwana sijalia

Afande: Na baruuua nimetuma na barua bwana nimetuma na baruuua nimetuma na barua bwana nimetuma

Sisi: Na baruuua nimetuma na barua bwana nimetuma na baruuua nimetuma na barua bwana nimetuma

Afande: Na majiiibu sijapata na majibu bwana sijapata na majiiibu sijapata na majibu bwana sijapata

Sisi: Na majiiibu sijapata na majibu bwana sijapata na majiiibu sijapata na majibu bwana sijapata

Afande: Eeembeh (paah!) eembeh (paah!) eembeh (paah!)

Sisi: Eeembeh (paah!) eembeh (paah!) eembeh (paah!)”.

“Oya mbona haji mwambieni aje basi” alikuwa akituambia afande Kalaghe baada ya kumaliza kuimba na pisi aliyotuahidi kuwa itakuja kumkumbatia haikutokea.

“Basi mwambie aje” alianza kuimba afande Kalaghe huku akionesha ishara ya kutaka kujibiwa nasi hatukuwa na hiyana tukaanza kumpa sapoti.

“Aje”
“Oooh aje”
“Aje”

“Asije peke yake”
“Aje”“Aje na wigi lake”
“Aje”
“Oooh aje”
“Aje”
“Aje basi aje”
“Aje”
“Asije peke yake”
“Aje”
“Aje na dela lake”
“Aje”

Ebwana eeh ilikuwa ni burudani chini ya mtumbuizaji wa zamu Afande Kalaghe ambaye hakuwa anaimba tu bali alikuwa akicheza pia hali ambayo ilitufanya namba kubwa ya tuliokuwa eneo hilo kufurahi.

Kusema kweli makamanda wetu walikuwa ni mfano halisi katika moja ya beti ya bwana kikulacho (Mr. Nice) ambaye kwenye moja ya nyimbo zake aliwahi kuimba “Kumbe anang’ata na kupuliza puuh kama panya buku ee”.

Hali ilikuwa hivyo kwa maafande wetu ambao waliweza kutuhenyesha kwa kututoa jasho la kutosha lakini ilikuwa kila baada ya msoto kuna tukio moja watalifanya tunajikuta tunasahau shida zote na kila mmoja wetu asipocheka basi atatabasamu.

Nahisi huwa wanapigwa msasa kabla ya mafunzo kuanza ambayo huwasaidia katika utambuzi wa hali tunazokuwa nazo kipindi chote cha mafunzo kwani wanajua sana kucheza na akili zetu wanajua ni kipindi gani cha kutukera na ni kipindi kipi cha kutupooza.

“Haya KURUTA simameni tuondoke” alituamuru afande Kalaghe huku akitabasamu.

Tulisimama ila wakatokea wachache kati yetu wakasema “Tuimbie mwingine wa mwisho afande”
“Eeeh mnataka niimbe tena”
“Ndiyo afande” awamu hii tulijibu wote kwa umoja wetu siyo kwamba tulikuwa tukipata burudani lakini pia ilikuwa ni moja ya mbinu ya kupoteza muda na kupooza machungu yaani hizi zilikuwa ni TANO fulani hivi za rejareja.

“Anhaa kwa kuwa pisi imegoma kutokea ngoja sasa tuanze kuiita ije haya nipeni biti wanangu” alitumbia afande Kalaghe tukaanza kupiga makofi paah! Paah! Paah!“

Afande: Na mchumba mbona hutokei mama wee

Sisi: Anakuja
Afande: Hii pisi mbona haitokei naisubiiri

Sisi: Itakuja
Afande: Niko hapa mwenzenu naisubiri toka alfajiri

Sisi: Inakuja……”.

Alikuwa akiimba wimbo huo afande huyo wa jeshi la wananchi huku akitizama juu ambako kulikuwa na hadhira iliyokuwa ikishuhudia kinachoendelea sina shaka zilikuwa ni familia za makamanda waliokuwa wakiishi kwenye majengo hayo.

“Oya tuondokeni zetu wanangu si mnaona pisi imegoma kuja” alituambia afande Kalaghe ambaye za ndaani kabisa tulikuja kugundua kuwa hakuwa akiishi kwenye apartments hizo.

Kifupi alikuwa akitupanga kwani hata kule anakoishi yuko peke yake yaani afande wetu ni bachela na ndiyo maana hakuna chuma chochote kilichojitokeza.

Mwisho wa wimbo huo ulikuwa ukimaanisha mwanzo wa pumzi ya moto kutoka kwa makamanda wetu kwakuwa tulishatambulishwa sehemu hiyo tulijipanga na kuondoka zetu huku afande akionekana kitufe chake cha vibe kipo ON hatukutoka kizembe akaweka CHENJA.

“Afande: Ewiih
Sisi: Ewaah
Afande: Elewii
Sisi: Elewaa
Afande: Vaileth nakupenda sana cheka kidogo nione wako mwanya

Sisi: Vaileth nakupenda sana cheka kidogo nione wako mwanya

Afande: Tulikuwa wengi maama wee wamekufa kwa mabomu mbagala eeh

Sisi: Tulikuwa wengi maama wee wamekufa kwa mabomu mbagala eeh

Afande: Nyumba ya makuti Zanzibar ina umeme wee kama unabisha panda boti ukaione

Sisi: Nyumba ya makuti Zanzibar ina umeme wee kama unabisha panda boti ukaione”.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

……….........……….…Itaendelea……………….......………
Anyway Nimeikubali ulivyoweka hyo code HCH =838kj maramba😂
 
Tokea Nyerere aanzishe Kambi za JKT, ukimwi ulienea sana majeshini,
Endeleeni kuambukizana HIV ndio kazi munayoiweza
 
MAISHA YA DEPO

SEASON-3

EPISODE 11

Katika sehemu zote tulizopita hii haikuwa ya kusahalika hata kidogo binafsi naweza kulisau lile banzi nililokumbana nalo kule RESORT ila hii sehemu ambayo jina lake la utani huitwa “Karaini” wakimaanisha kwenye karai yaani kile chombo kinachotumika kukaangia vitafunwa na mbogamboga jikoni.

Katika kujifikirisha nikakumbuka kuwa nina ile hati ya msamaha kutoka kuzimu nikaona cha kufia nini na kwanini nijitese nikaamka zangu na kuchuchumaa.

“Haya wewe wewe nani kakwambia uamke” aliuliza afande Mochiwa baada ya kuniona nimechuchumaa.

“Baba vipi lalia mgongo acha mapuuza KURUTA” alisema afande Kalaghe huku akinisogelea.

“Haya umepatwa na nini wewe MZALENDO wa zamani”

“Daah kichwa kinagonga tena nasikia na kizunguzungu afande”

“Kumbe ni wewe KURUTA sikukuona vizuri maana sasa hivi wote mmefanana haya sogea pale utupishe hapa tuna jambo letu” aliniambia afande Kalaghe nami sikuitumia vibaya nafasi hiyo nilijikusanya na kujiweka kando ya timbwili lile.

Ingawaje sikukaa kivulini kwani eneo hilo lilikuwa ni la wazi sana ila kidogo niliipata nafuu tofauti na mwanzo nilipokuwa nimeungana na wale jamaa zangu.

Nikiwa hapo nilikuwa nikiwaonea huruma sana wana kwani nilishaonja tamu na chungu za shuruba hizo.

“Afandeee afande tunaomba tano afande” zilikuwa ni sauti za jamaa zangu wa DANGER COY waliokuwa kwenye karai wakimuomba heri afande.

“Ahahahah nzuri hiyo, Baba naona DOSO limewaingia sasa” alikuwa ni afande Kalaghe aliyejichekesha kama mwanaume aliyekutana na mwanadada aliyemtoa uvulana wake.

“Tano hazitoki mpaka pale mtakaposema hapa ni wapi” aliropoka afande Mochiwa na sauti yake nzito yenye kukwaruza mithili ya kijana mlalahoi aliyetoka kuchanganya zege.

Hali hiyo iliendelea huku wakibadilishiwa zoezi kama vile kukunja ngumi, kulalia tumbo pamoja na KUROLI mazoezi ambayo hakukuwa na hata moja lenye nafuu.

Wakati hali hiyo ikiendelea nilimuona afande Mochiwa na dada mmoja wakijadili jambo na baada ya kikao hicho kifupi nilimuona dada yule akiinuka na kuja pale nilipo.

Nilimtupia jicho na kugundua kuwa mwanadada yule hakuwa akitembea vizuri kwa Kiswahili kinachotambulika na BAKITA mwanadada huyo alikuwa akiguchia yaani alikuwa akitembea kwa kuchechemea.

Mwanzo nilifikiri kuwa huenda labda ni kutokana ukali wa DOSO alilotoka kukabiliana nalo ila nikiwa namuangalia kwa kubahatisha nikang’amua jambo kumbe kilichomfanya afande amtenge mwanadada yule ni yale yale malipo ya kila mwezi yaani mshahara.

Ile taswira ya SIX WEEK tuliyokuwa tukisimuliwa nilikuwa nikiishuhudia kwa wakati huo bi dada yule alikuwa akitokwa na damu iliyokuwa ikimchuruzika miguuni kwa kifupi kabisa ni kuwa “kipofu kauona mwezi”.

Naomba kutoa code kwa mabaharia, kama kuna mtoto wa mama mkwe mtarajiwa anakuvuruga kichwa kuwa kapoteza siku zake usihangaike kununua vipimo we mtafutie kambi inayofanya intro mpaka kamchakato kaishe atakuwa keshaziona tu maana si kwa mikikimikiki ile.

Sisemi hivyo kwa sababu ya huyo dada pekee bali tulikutana na kesi nyingi kama hizo tuliporudi kikosini wadada wengi walikutana na gari la mshahara na kupatiwa ujira wao.

Baada ya kurupushani hizo alisikika afande Kalaghe akisema “Hapa ni Godauni sehemu ambayo chakula cha kikosi kinahifadhiwa kama zilivyo sehemu nyingine inyeshe mvua liwake jua hamtakiwi kufika hapa pasipo na ruhusa ya kamanda”.

Baada ya utambulisho TULIFOLENI mistari mitatu ya kijeshi na kuondoka kwenye hilo Karai kwa mara ya kwanza njiani tulipishana na BOGI ambalo lilionekana kutoka kule tunakoelekea.

Tukiwa kwenye njia hiyo inayoelekea kwenye makutano ya njia inayokwenda REST HOUSE, utawala na ghala la kuhifadhi silaha afande Kalaghe alikuwa akituimbisha huku tukikimbia.

Afande: Ewii
Sisi: Ewaa
Afande: Ewii
Sisi: Ewaa
Afande: Elewii
Sisi: Elewaa
Afande: Danger Coy ya DEMO ndo mana morali

Sisi: Danger Coy ya DEMO ndo mana morali

Afande: Ee Dcoy ya DEMO ndo mana morali

Sisi: D Coy ya DEMO ndo mana morali

Afande: Ee Morali
Sisi: Morali
Afande: Ewii
Sisi: Ewaa
Afande: Ewii
Sisi: Ewaa
Afande: Alii alii aling’ang’ang’ang’a moraali

Sisi: Moraali
Afande: Aling’ang’ang’ang’a moraali

Sisi: Moraali
Afande: Oya oyaa moraali
Sisi: Moraali
Afande: Oya oyaa Masooja
Sisi: Masooja”.

Tulipofika kwenye makutano hayo ambapo nakumbuka ndipo nilipokutana na Matroni Anna na kupiga naye stori kwa mara ya kwanza siku ile akijing’atang’ata.

Tulishika njia inayoelekea REST HOUSE na kuweka kituo kwenye daraja lililokuwa likiunganisha mitaa ya REST HOUSE na sehemu nyingine muhimu za kikosi maafaande wakatuamuru tuingie mtoni.

Binafsi nilitaka kujifanya mgonjwa ila nilipoifikiria hali niliyonayo baada ya kujigaragaza kwenye matope kule FACTORY nikaona ni bora tu nikaingia kujisafisha.

“Chubwii chubwii chubwii” zilikuwa ni mbizi nilizokuwa nikizipiga kwenye maji ya mto huo huku nikipita chini ya miguu ya watoto wa kishua ambao walionekana kuwa waoga kuogelea.

Hazikuwa shida zangu binafsi nilikuwa nikifurahi na kujikumbushia enzi zangu nikiwa naogelea kwenye madimbwi ambayo baada ya kurudi nyumbani nilikutana na viboko vya kutosha kutoka kwa Mzee Mjuzi aliyekuwa akinikataza kuogelea kwenye maji machafu ya madimbwi hayo.

“Wooi wooi mamba huyo” zilikuwa ni kelele za wale niliokuwa nikipita chini kwa chini na kuwagusa huku nikikatiza kati katikati yao nikasikia wakipiga makelele na kutoka nje wakidhani wameguswa na kiumbe huyo.

Baada ya kutoka mtoni tulijipanga kama ilivyokuwa ikitakiwa kisha afande Kalaghe akatuambia “Zoezi la kunyakua”.

“Chini kuna moto juu kuna miba tunaondoka afande uup uup uup uup” tulimjibu na kuanza kukimbia tukipandisha kimlima ambacho kwa mara ya kwanza tulipita njia ambayo ilionesha tayari kuna watu wameshapita.

Kwa lugha nyepesi ni kwamba sehemu zote tulizopita hapo kabla tulikuwa wa kwanza faida ambayo watakutana nayo MABOGI yatakayofuata nyuma kwani huenda yasikutane na baadhi ya madimbwi ambayo tutakuwa tumeshayakausha ila si kwa pale FACTORY kwa kweli lile tope hakuna wa kulikausha.

Tukiwa tumeshika njia hiyo tulipishana na BOGI ambalo walionekana DOSO kuwaingia kwelikweli ingawaje sipingani yaliyosemwa na wahenga kuwa “nyani haoni kundule” lakini lugha yao ya mwili haikuacha kuongea. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

………………………….…Itaendelea…………………………

MAISHA YA DEPO

SEASON-3

EPISODE 12

Katika moja ya ishara ya wazi inayonipa nguvu kusema hayo ni kuwa kama unakumbuka siku ambayo SERVICE MAN waliharibu kazi kuna afande mmoja aliyevurugwa alikuwa akijimwagia maji yeye mwenyewe basi ndiye afande aliyeambatana na BOGI lile.

Lilikuwa ni BOGI kutoka KOMBANIA ya BRAVO likiwa na afande huyo aliyefahamika kwa jina la Shona tulia ambaye nilivyomtupia jicho niligundua kombati yake ilikuwa imelowa.

Inasemekana mwamba kipindi wanapandisha kwenda REST HOUSE alitumbukia mtoni na kombati zake akapiga nazo mbizi kwa lugha ya jeshini nikiri kuwa mwamba ni MNAA yaani ni mnoko kupitiliza usiombe ujae kwenye mfumo wake.

Kwakuwa hazikuwa shida zetu tulishika njia yetu na kwenda tulikotakiwa kwenda kama kawaida afande Kalaghe hakupoa alikuwa akituimbisha.

“Afande: Ewii
Sisi: Ewaa
Afande: Ewiiih
Sisi: Ewaaah
Afande: Elewii
Sisi: Elewaa
Afande: Nauliza why
Sisi: Wanajifanya wanaongea ngeli
Afande: Repart agaiiin
Sisi: Wakija wazungu wanakimbia ee
Afande: Sema nauliza why
Sisi: Wanajifanya wanaongea ongee
Afande: Oya epart agaiiin
Sisi: Wakija wazungu wanakimbia ee
Afande: What is my name
Sisi: Mi sijui
Afande: Ooh my name
Sisi: Mi sijui
Afande: Sema what is my name
Sisi: Mi sijui
Afande: Ooh my name
Sisi: Mi sijui”

Tulikimbia na kavibe hako mpaka tulipofika kwenye uwanja wa moja ya nyumba iliyoonekana kupendeza japokuwa ilionekana kuwa ni kuukuu yaani ya siku nyingi na kuna uwezekano kuwa ilijengwa zama za mkoloni.

Ukongwe wa jengo hilo halikuwa kizuizi cha kupendezeshwa kwake bila ya kuingia ndani tuliweza kuona hilo kupitia kibaraza chake ambapo palikuwa na mapambo mbalimbali.

Mbali na mapambo tuliyoyakuta kwenye kibaraza hicho lakini pia hata uwanja wake ulizungukwa na maua mbalimbali ambayo yalipendezesha mazingira kulizunguka jengo hilo.

Kwa jinsi tulivyopakuta hapakujificha hata kidogo palionekana dhahiri kuwa kuna wenzetu walikwishatangulia eneo hilo.

Kama ilivyo ada walituuliza na tulivyokuwa mabandidu hatukutoa jibu walilolitaka hali iliyowapelekea kutufanya walichojisikia ila sio walichokitaka.

Baada ya kuridhika kwa walichotufanyia ndipo tukasikia “Sikia kutoka kwangu NGURUTU, wadudu, vipawatira vya jeshi hapa ni REST HOUSE yaani Ikulu ya kikosi kama mnavyoiona” alisema afande Mochiwa.

“Hapa ndipo yalipo makazi ya mkuu wa kikosi awapo kikosini sasa kama ushawahi kumuona fala yeyote akiingia Ikulu pasi na kuruhusiwa na watu wa usalama ningependa na fala wewe ujichanganye kufika sehemu hii bila ruhusa ya kamanda” aliendelea kukazia afande Mochiwa.

“Yaani kifupi kama mtakuwa mmemuelewa afande hii ndiyo mara yenu ya mwisho kuiona sehemu hii na sehemu ambayo mtakuwa mkiiona na kufika hovyo kila mtakapojisikia ni jikoni kwa MZABUNI na chooni kukata gogo na siyo sehemu hii” alidakia afande Kalaghe.

Baada ya kutambulishwa tuliondoka sehemu hiyo kwa kila aina ya mwendo usiokuwa mzuri na awamu hii makamanda waliturudisha zama za mawe nafikiri ni zile za mwanzo kabisa kwani walitutembeza kwa aina nyingine ya mwendo uliofahamika kama mwendo wa nyani mzee.

Kwa kupitia mwendo huo tulitakiwa kuinamisha migongo halafu tunatembea kwa kutumia miguu na mikono ulikuwa ni mwendo wa kibabe sana kwani baada ya kumaliza tu mapaja, kiuno na mgongo havina hali kabisa.

Tulifika lilipokuwa moja ya geti tulilokuta likiwa na ulinzi mzuri sijui ni kwa siku hiyo pekee ama ndivyo inavyokuwa siku zote ila siku hiyo tulikutana na walinzi wehu kwelikweli tofauti na mageti mengine.

Sifa kubwa ya walinzi tuliowakuta ilikuwa ni unoko kule jeshini wao wanaita UNAA kwanza walitumwagia maji ya kutosha pia KUTUDOSOA vilivyo huku wakisaidiana na makamanda tuliokuja nao kifupi walikuwa WAKIJILA yaani walifanya majukumu yasiyowahusu.

Varangati hilo liliendelea mpaka pale iliposikika sauti ya afande Kalaghe akisema “Msiopajua mnatakiwa kupajua mahala hapa na yeyote asiyepajua anatakiwa kunikopesha sikio lake na kunisikiliza kwa makini ili apajue vizuri mahala hapa”.

“Hapa tulipo ni upande wa Mashariki wa kikosi na geti mbele yenu ni geti la Mashariki maarufu kama geti la kuzimu”

“Mnnnh” ilikuwa ni miguno iliyopita kati katikati yetu.

“Fyokooo nyie jigunisheni tu ila ukweli ndiyo huo sasa kwakuwa mmening’ong’a ngoja nimuachie afande awaambie sababu za hapa kufahamika kama geti la kuzimu maana naona mmepoteza imani na mimi”.

“Eeh ndiyo afande aisee nyie KURUTA mkiwa mnatoroka tumieni mageti yote ya kikosi ila msije mkajichanganya mkatorokea geti la huku hawa jamaa wanaolinda hili geti wamepewa ruhusa ya kufyatua chochote ambacho wana mashaka nacho”.

“Kudhihirisha hilo jiulizeni tumepita sehemu ngapi na tumepishana na mapoti wangapi kule dukani, zahanati, resort, factory mmeona kuna poti yeyote aliyewasogelea kuwadosoa kama hawa wa huku?”.

“Jibu ni hapana kwasababu hiyo ruhusa ya kufanya chochote waliyopewa hawa jamaa inatoka kwenye mamlaka ya juu sana na ndiyo maana hata sisi hatukuweza kuwazuia kuingilia majukumu yetu”.

“Hakuna kitu ambacho makamanda hatupendi kama kuingiliwa kwenye majukumu na kuingiliwa huko mnakokumaanisha nyie” alikuwa ni afande Mochiwa aliyetufanya tuangue vicheko kwa maneno hayo.

“Kimya NGURUTU kama mnavyokuona kunashawishi mno mtu kuingia na kutoka kuona hivyo ndiyo ikawa sababu ya kuimarisha ulinzi kiasi kwamba askari wa zamu wameruhusiwa kufanya chochote kwa asiyekuwa na maelezo ya kutosha”

“Sasa wewe ROBUROBU kipande hiki au ujifanye ni nunda utorokee geti hili halafu afande wa zamu akuone unapotelea hata kwa mbali aisee Mwenyezi Mungu ailaze roho yako panapostahiki” alimazia kutujuza afande Mochiwa.

“Aisee msichukulie poa hili swala na ndiyo maana tunawasisitiza kama utakuwa umemsikiliza vizuri afande amesema hata ukionekana unaishia kwa mbali risasi inakuhusu akiwa na maana kuwa ukiwa karibu inakuwa ni rahisi kuhojiwa”

“Sasa tuulizane kitu je, ukiwa mbali watawezaje kukuhoji? Jibu ni vigumu siyo! kwahiyo huduma ya kwanza utakayopatiwa ni kufyatuliwa risasi hukohuko uliko halafu ndiyo watakusogelea sasa mawili wakikukuta uko hai ina maana bwana yu nawe na utakuwa umebarikiwa mno wakati huo”

“Vinginevyo wakakukuta Israel ndo yuko nawe hakuna haja ya mahojiano tutakachofanya ni kutenganisha kichwa na kiwiliwili halafu kiwiliwili tutakitupa kule bwawani iwe halali ya mamba kuhusu kichwa hatutowaambia tutakifanyaje” alikazia Afande Kalaghe. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

……………….………….…Itaendelea…………………………
 
EPISODE 13

“Mwisho na kwa msisitizo ni kuwa ulinzi wote huo ni kwaajili ya kukabiliana na mamluki wanaoweza kujipenyeza na kuchota siri za kambi na ndiyo maana tukikuona unatokomea kwa mbaali wewe ni halali yetu“

“Haijalishi utakuwa umevaa GREEN VEST juu chini ukavaa kipensi chako hatutokuhurumia hata kidogo maana mamluki huwa wana mbinu nyingi na ndiyo maana tunawasisitiza hata kama ikitokea mnatoroka torokeeni mageti mengine siyo hili wanangu vuta picha linaitwa geti la kuzimu we huogopi” alimalizia kwa kauli hiyo afande Kalaghe.

Baada ya utambulisho huo uliotukuka na wenye vitisho kedekede tulishika njia na kurudi tulikotoka kusema kweli hali haikuwa shwari kabisa nakumbuka baada ya kutoka mtoni tulipandisha kwenda REST HOUSE mpaka geti la Mashariki tukikimbia lakini kwa wakati huu amini usiamini hakukuwa na mbio yoyote ilikuwa ni mwendo mbaya kwenda mbele.

Kikubwa kilichokuwa kinashawishi ni hali ya mteremko wa barabara ile yaani tulikua tunaelekea bondeni kama ilivyokua uelekeo wa mito ambayo mara zote hupatikana bondeni.

Yote hayo yakiendelea afande Mochiwa alikuwa akinigomea kabisa kila pale nilipozuga najisikia vibaya na hata yule dada aliyekuwa akitokwa na damu kule factory alimkazia na kumtaka aungane na wengine kifupi muda wa kudeka uliisha.

Hatukuwa na namna ilibidi tukubaliane na hali huku tukihenyeka tulitambulishwa aina nyingine ya mwendo ambao ulikuwa ni ahueni kwetu.

Mwendo huo ulifahamika kama kuendesha ndege ama helkopta ambapo ulikuwa ukitutaka kukimbia kwa umbali fulani halafu tunasimama na kulalia mgongo na baadaye tunanyoosha miguu juu na kuichezesha mithili ya mtu anayenyonga pedeli za baiskeli.

Unafuu tulikuwa tukiupata wakati wa kukimbia ambapo alipokuwa akituamuru tusimame tulijifanya hatujasikia na kuongeza umbali kiasi kisha ndiyo tunasimama na kuendelea na kulalia mgongo.

Maafande ni kama walitusanukia wakatamani kuturudisha ila hawakuwa na jinsi kwani walitakiwa kuturudisha nyuma ambako kulikuwa na MABOGI mengine kwakweli tuliitumia vizuri fursa hiyo.

Tulipofika mtoni tulitumbukia kwa mara nyingine kwani tulikuwa hatutamaniki kwa kile kilichotutokea REST HOUSE, kule getini na njiani wakati wa kurudi lakini hata hivyo niligundua maafande walikuwa wakipenda sana kutuona tumetota hali ambayo ilipatana mno na mazoezi yao ya kugalagazana kwenye kidongo kile cha mgongo wa ardhi wa kikosi.

Tulitoka mtoni na kujipanga kwenye mistari kisha tukatembea kwa mwendo wa nyoka mpaka kwenye makutano ambapo siku moja tukitoka REST HOUSE kufanya usafi nilisimama na kusalimiana na matroni Anna.

Tulipofika hapo tulishika barabara inayoelekea mapokezi wanakochukua PARTICULARS na kuweka kituo katikati ya barabara hiyo kwenye jengo moja ambalo mbele yake kulikuwa na bendera ya Taifa, ile ya Jkt na nyingine ambazo hazipo kwenye kumbukumbu kwa sasa.

Kiburi tulichokuwa nacho hakikuacha kutuponza eneo hilo baada ya kuwajibu makamanda wetu kuwa hatupajui na wala hatukuwahi kufika sehemu hiyo.

Hakukuwa na jipya tena zaidi ya kutushikisha adabu na baadaye wakatufungukia na kusema “Hapa ni Utawala yaani Administration office kama wanavyopaita wazungu na hapa ndipo kilipo kitovu cha kikosi” alisimama kuongea na kumeza mate afande Mochiwa.

“Hii ni sehemu moja muhimu mno hivyo hatutegemei kukutana na mdudu yeyote asiyekuwa na ruhusa ya kamanda na mpitapo eneo hili mnatakiwa kupita kwa utulivu wa hali ya juu ili msiwasumbue wakuu waliomo ndani tumeelewana nyie wadudu”

“Ndiyo afandeee”tulimjibu afande Mochiwa.

Baada ya kutoka hapo kwa mwendo wa hovyo tulirudi tena mpaka yalipo makutano ya barabara zile nne tukashika ile inayokwenda UWANJA WA DAMU ashukuriwe Mungu mzunguko ulikuwa unakaribia kukamilika.

Tuliishika njia hiyo huku tukitembea ubatabata kusema kweli tangu tulipokimbia kipindi tukipandisha kwenda REST HOUSE hatukukimbia tena zaidi ya kutembea kwa mamimwendo ya hovyohovyo.

Tukiwa tunatembea mwendo huo afande Mochiwa alikuwa akituimbia wimbo mmoja uliofanana na zoezi hilo ambao ulitufanya tujichekee zetu tukasau shuruba tulizokuwa tukikabiliana nazo.

“Afade: Nampenda bata kwa kunyakunyaa na mwendo wake wa madoido (imba KURUTA)

Sisi: Nampenda bata kwa kunyakunyaa na mwendo wake wa madoido

Afade: Nampenda bata kwa kunyakunyaa na mwendo wake wa madoido

Sisi: Nampenda bata kwa kunyakunyaa na mwendo wake wa madoido”.

Tulifika kwenye jengo moja kuukuu lililokuwa likitumika kuhifadhi silaha tukapanga mistari vizuri kisha tukatakiwa kukunja ngumi na ikasikika sauti “NGURUTU nani hapajui hapa” aliuliza afande Kalaghe swali hilo la kikuda nasi tukamkalia kimya.

“Nyie viumbe nawauliza nani hapajui hapa”
“Kimya maana yake mnapajua sivyo”
“Hatupajui afande”
“Sasa nawauliza mnanikalia kimya mnategemea ije mizimu ya bibi zenu iwaambie mbwa nyie haya hembu ibebeni dunia kwanza akili ziwakae sawa”.

Ebwana ee lilikuwa ni zoezi lingine kiboko kabisa lilifanana na kukunja ngumi ila mikono inakuwa kiunoni yaani unanyoosha miguu kama kawaida halafu komwe ndilo linagusa ardhi badala ya mikono.

Kwa upande mwingine mikono inakunjwa na kuwekwa mgongoni kama vile wafanyavyo wachezaji haswa mabeki pindi wanapokwenda kumkaba mpinzani ambaye amekwisha kuingia kwenye 18 hivyo anachukua tahadhari ya kukwepa kusababisha mkwaju wa penati.

Puuh! Puuh! Puuh! Vilikuwa ni vishindo vya miili iliyokuwa ikijitupa chini kila baada ya sekunde moja baada ya kukosa balance kwani zoezi hilo halikuwa la kitoto lilikuwa likihitaji balance ya mwili ambapo wengi wao hatukuwa nayo.

Baada ya muda afande Kalaghe alisema “Hapa ni AMALA sehemu ambayo silaha zinahifadhiwa ni kama moyo wa kikosi hivyo hamtakiwi kuwepo mahala hapa bila ya ruhusa ya kamanda”.

Tulipomaliza kutambulishwa sehemu hiyo kwa mwendo usiotamanisha tuliuzunguka UWANJA WA DAMU upande ambao kwa kumbukumbu nzuri nilipita ile siku niliyonusurika kuivuruga Master PARADE baada ya kutonywa na moja ya afande wa zamu.

Muda huo uwanja ulionekana kuwa mtupu hakukuwa na kundi lolote lililosalia ama kurudi ni dhahiri kuwa sisi ndiyo tulikuwa wa kwanza kufika sehemu hiyo ya kuanzia. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

…………………………….…Itaendelea…………………………………
 
EPISODE 14

Kwa kupitia njia hiyo tulinyoosha moja kwa moja hadi mtoni ambako maafande walituamuru kuingia humo na kuoga kwa mara nyingine.

Muda huu nafikiri walikuwa wakitutafutia pumzi kwani tukiwa ndani ya maji walitutaka wote kuzama ndani kabisa pasi na kuruhusu kichwa cha mmoja wetu kuonekana.

Kwakuwa si wote walikuwa wakiweza kufanya hivyo kuna kipindi ilibidi tutolewe kugaragazwa kwenye udongo hali iliyonifanya nikumbuke zile tahadhari tulizokuwa tukipewa na SERVICE MAN kuwa makamanda hufaidi mno kozi ikifanyika kipindi cha mvua kuliko kiangazi.

Hisia zinanishawishi kuwa siku hiyo ya utambulisho ingetokea mvua imenyesha basi hata mara moja kutoka eneo moja kwenda lingine tusingekuwa tunakimbia na badala yake makamanda wangependelea mwendo wa kugalagazana zaidi.

Hii ni kutokana na hali ya ushawishi wa matope na ndiyo maana hakuna dimbwi hata moja tulilolipita bila kuambiwa “pakausheni hapa”.

Mtoni hapo kazi ilikuwa ni kuzama kwenye maji na baada ya muda tunatolewa na kugalagazwa kwenye matope baada ya kufanya kosa la kuibuka kabla ya muda hivyo tunatolewa mtoni na kwenda kugalagazwa.

Kipindi zoezi hilo likiendele waswahili wanasema “Macho hayana pazia” kuna tuvituvitu fulani vilikuwa ni adimu kujizuia navyo haswa tukiwa katika hali kama ile.

Kutokana na ingia toka hizo ilikuwa ni vigumu kuacha kuziona zile zinaitwa saa sita maarufu kama chuchu konzi haswa katika kipindi ambacho vitu vimelowana haswa yaani vilikuwa ndembendembe.

Achana na hizo saa sita kuna zile namba nane na mizigo ya asili pia ilikuwa ni kama pembe la ng’ombe yaani ni vigumu mno kufichika mimi yakwangu yalikuwa macho nilikuwa nikipata burudani ya bure.Baada ya muda tulitolewa mtoni na kuelekea UWANJA WA DAMU tukiwa tumejipanga mistari yetu mitatu na kutembea mdogomdogo huku tukiimba na kamanda wetu.

“Afande: Eeembe embe dodo eeh eeembee embe dodo tamtam

Sisi: Eeembe embe dodo eeh eeembee embe dodo tamtam

Afande: Maji ya kisima mama sintoyanywa tena matumbili na manyani wanaogelea

Sisi: Maji ya kisima mama sintoyanywa tena matumbili na manyani *wanaogelea

Afande: Maji ya kisima mama sintoyanywa tena matumbili na MAKURUTA wameogelea

Sisi: Maji ya kisima mama sintoyanywa tena matumbili na MAKURUTA wameogelea

Afande: Eeembe embe dodo eeh eeembee embe dodo tamtam

Afande: Maji ya kisima mama sintoyanywa tena MADAWILI wa Danger COY wameyaogelea

Sisi: Maji ya kisima mama sintoyanywa tena MADAWILI wa Danger COY yameogelea*

Afande: Na MANGORONGORO ya Danger COY yameyajambia

Sisi: MANGORONGORO ya Danger COY yameyajambia

Afande: Eeembe embe dodo eeh eeembee embe dodo tamtam

Sisi: Eeembe embe dodo eeh eeembee embe dodo tamtam

Afande: Maji ya kisima mama sintoyanywa tena MAKURUTU ya Danger COY yamekojolea

*Sisi: Maji ya kisima mama sintoyanywa tena MAKURUTU ya Danger COY yamekojolea”.

*Tulifika UWANJA WA DAMU na kuwakuta waliofika hapo kabla yetu kutoka COY nyinginezo ingawaje kwa upande wa KOMBANIA yetu ya D-COY tulikuwa BOGI la kwanza kurudi.

Bila ya kupoteza muda na kujitafutia mabalaa tulijitwalia zetu kipande cha ardhi na kuiweka miili yetu iliyokuwa ikitota maji katikati ya jua kali lililokuwa likiwaka muda huo.

Tukiwa kwenye kipande hicho ndani ya ardhi tukufu ya HCH KJ tulimsikia afisa mmoja wa jeshi mwenye nyota zake mbili begani akiuliza “Wako wapi Danger COY”.

“Tuko huku mkuu” alijibu afande Kalaghe huku akitupa ishara ya kututaka tusimame nasi tukasimama.

Afande Kalaghe aliiweka vizuri kofia yake kichwani na kutuambia tusimame bila kutikisika alipofika afisa yule afande Kalaghe alibana kinyeo na kuukunja mkono wa kulia na kuweka kiganja chake mbele ya komwe lake halafu kwa sauti ya unyenyekevu akasema “Jambo afande”.

“Jambo” alijibu afisa yule huku na yeye akipandisha kiganja chake cha mkono wa kulia kwenye kofia yake na kuushusha kisha akamwambia afande Kalaghe “mwili legeza” ndipo tulipopata kumuona kamanda wetu Kalaghe akishusha mkono na kulegeza kinyeo chake.

“Hawa ndiyo Danger COY wote afande”
“Hapana mkuu hii ni PLATUNI ya kwanza wengine hawajafika bado”
“Anhaa asante kwa taarifa ngoja tuyasubiri hayo MANANGA”
“Sawa mkuu”

Kipindi tukiwasubiri wenzetu tulikuwa tukipiga soga na afande huyo aliyefahamika kwa jina la LUTENI Novath ambaye alituambia kuwa ndiye atakayekuwa O.C. wetu kipindi cha mafunzo yaani Operation Commender.

Punde si punde liliwasili BOGI lingine lililoungana nasi ingawaje jamaa zetu walitota ila hawakuwa kama sisi inaonekana safari yao haikuishia mtoni kama ilivyokuwa kwetu.

Miili ikiwa imechoka kwa DOSO hali iliyotufanya wengine kusinzia tulikuwa tukimuona LUTENI kama Zuchu kwani tulipoteza kabisa morali ya kumsikiliza mbaya zaidi alikuwa akitumia sauti ya kwanza na robo kuongea na sisi.

Wakati LUTENI akiendelea kutubembeleza likaja BOGI la mwisho la D-Coy kwakweli lilidamshi kinoma watu wake walikuwa hawatamaniki kuwatizama tulishindwa kujizuia na kuangua vicheko ilibidi afande Novath awaamuru waende mtoni wakaoge kwanza na warudi wasafi.

Kucheka kule kulitutoa kwenye hali ya usingizi tukaendelea kumsikiliza afande Novath ambaye alikuwa akitulazimisha kuimba wimbo tusioujua na tulipomwambia hatuujui alishangaa kutoujua kwetu akidai ulikuwa ni wimbo maarufu.

Alitusikilizisha wimbo huo kupitia simu yake ulikuwa ni wimbo ulioimbwa na msanii mmoja wa hip-hop kutoka pale kwa jirani na mashemeji zetu wa Kikuyu na Kiluhya afahamikaye majukwaani kwa jina la Juliani.

“Makamanda kwenye KOMBANIA zenu nipatieni lokoo” ilikuwa ni sauti ya makamu mkuu wa kikosi aliyewasili mahala hapo.

“ST yuko wapi” aliuliza LUTENI Novath
“Nipo afande”
“DABO” Jamani msisahau na mimi ni ST na hapa alikuwa akitakiwa adabo ni mimi ambaye ndiye niliyemjibu kuwa nipo maana yule mmakonde ST wa kike sidhani kama alikuwa na kumbukumbu kuwa na yeye ni ST maana si kwa DOSO lile.

Nilijikokota kwenda kule aliko LUTENI nikiwa naelekea huko afande Kalaghe alinisemesha “Eeeh kumbe na wewe ni ST!”

“Ndiyo afande”
“Aaah baba huyu si ndiye jamaa yetu wa RESORT huyu” alidakia afande Mochiwa
“Ndiyo baba” “Vipi hastahili” aliuliza LUTENI Novath. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

…………………………………Itaendelea…………………………………
 
Sisi: Maji ya kisima mama sintoyanywa tena MADAWILI wa Danger COY
yameogelea*

EPISODE 15

“Hapana mkuu anafaa sana ila kuna madhira amekutana nayo ndo yamenifanya nistuke kidogo”

“Madhira gani hayo hembu tuambieni tumjadili ikibidi tumteue mwingine”

“Naomba lokoo zenu zioneshe idadi ya wale waliofanikiwa kufika mwisho wa zoezi walioishia njiani na hata waliokumbwa na dhoruba za hapa na pale” aliendelea kusisitiza Matroni daboli N ambaye ndiye makamu mkuu wa kikosi.

“Sawa mkuu nitawasimulia tuchukue lokoo kwanza” alijibu afande Kalaghe huku akitabasamu.

“Hili zoezi bila msaada wa makarani siyo jepesi kama hawapo naomba mkawaite ofisi zao tunajua ziliko” ulikuwa ni msisitizo kutoka kwa Matroni Neema.

Tulipomaliza afande Kalaghe alisimulia yale niliyokutana nayo akasimulia lile tukio baina yetu alipofika ile sehemu niliyomwambia “Ina maana afande ndo nimekufa kweli”

KOMBANIA nzima iliangua vicheko vilivyofanya KOMBANIA nyinginezo kutushangaa.

“Naona ndugu zetu pale mshakamilisha lokoo maana mnapata mpaka mnapata muda wa kucheka siyo bure haya naombeni mniletee lokoo kwa mliomaliza”.

“Halafu makamanda mkisaidizana na makarani naomba kwenye lokoo zenu iwepo idadi ya wale wambea wanaojifanya wanaijua kambi kabla hawajatambulishwa na mniambie mlikowapeleka hatuwezi kuishi na mamluki kikosini” aliongea Matroni daboli N.

Baada ya kukamilisha lokoo tulikusanyika pamoja aliko matroni na kipindi makarani wakiwasilisha lokoo zao kwa matroni walipewa nafasi maafisa wa jeshi watusalimie akaanza LUTENI Novath.

“KURUTA wii”
“Waah”
“Ewaa”
“Ewii”
“Poleni kwa zoezi na hongereni kwa kufanikiwa kufika mwisho wa zoezi”
“Asante afande”.

“Kwanza nishukuru kwa nafasi hii tuliyopewa na matroni kipindi hiki anaweka sawa hesabu kwa ajili ya kutambua idadi ya marehemu waliopatikana kipindi cha utambulisho wa kikosi” alianza kututisha afande huyo.

“Mbona mmekuwa wanyonge au njaa zinawauma”
“Ndiyo afandeeeee”
“Msijali mtaenda kula muda si mrefu subirini kidogo Bosi wangu hapa aweke hesabu vizuri kila kitu kitakuwa sawa”
“KURUTI wiih”
“Waah”
“Kuna wimbo mmoja tulikuwa tukiimba na jamaa zenu wa Danger COY pale DANGER simpo”
“Tupo afandee”
“Haya tupeni vibe tuanze kuimba pigeni makofi KURUTA” alituamuru afande Novath kupiga makofi nasi tukafanya hivyo paah! Paah! Paah!

“Luteni: Niko njaa na siwezi karangaa
Sisi: Niko njaa na siwezi karangaa
Luteni: Hoohe hahee shaghalabaghalaaa
Sisi: Hoohe hahee shaghalabaghalaaa
Luteni: Niko tayari kulipa gharamaa
Sisi: Niko tayari kulipa gharamaa
Luteni: Sitasimama maovu yakitawala
Sisi: Sitasimama maovu yakitawala”.

Baadaye ulifuata uchambuzi wa tulichokuwa tukikiimba LUTENI akatuambia “Niko njaa na siwezi karanga ina maana ya kuwa ni mtu aliyekuwa na njaa kali na hakuwa na chochote kitu cha kuweka mdomoni ndiyo mana akaimba siwezi karanga akimaanisha kuwa hana chakula”.

“Hohehahe shaghalabagala ni masikini asiyekuwa na mbele wala nyuma yaani haeleweki na hana chochote mfukoni kwa kiswahili cha kule mtaani tunamuita kabwela”.

“Niko tayari kulipa gharama, Sitasimama maovu yakitawala hapa mtunzi anafikisha ujumbe kuwa yuko tayari kugharamia chochote kile ila hayuko tayari kuona maovu kama vile ufisadi, rushwa, unyanyasaji na udhalili mwingine wa aina yoyote ile ukitawala yaani ukitendeka mbele yake na asipaze sauti kukemea”.

“Kwa majumuisho ni kuwa mtunzi anasisitiza kwamba hata kama mkiwa katika hali mbaya kiasi gani mkakosa mali na hata chakula isiwe sababu ya nyie kuruhusu maovu yatokee na ninyi mkakaa kimya na kuwa miongoni mwa wale watakaounga mkono maovu hayo kutokana na njaa hiyo” hiyo ndiyo ilikuwa tasfiri kwa mujibu wa LUTENI huyo.

“Na hilo ndiyo lengo la ninyi kuwa hapa sasa hivi mnaitwa KURUTA ila kama mnakumbuka masaa machache yaliyopita mlikuwa mnaitwa WAZALENDO sivyo”
“Ndiyo afande”.

“Hicho ni cheo cha kwanza jeshini vipo vyeo kedekede mbeleni mkidumu kundini mtakutana navyo ila kuna sababu ya hiki cheo kuwa cha awali”.

“Kwa mfano ukiachana na mimi na hizi nyota zangu begani wapo majenerali na mabregedia lakini ukichunguza hao wote wamepitia kwenye cheo kinachoitwa MZALENDO”.

“Maana yangu ni kwamba mwanajeshi yeyote awe PRIVATE, STAFF SAJENTI, LUTENI, JENERALI na hata BREGEDIA ambaye usipomkuta ofisini ukaikuta kofia yake tu unatakiwa kuipigia SALUTI nayeye kiasili ama ukimpekua kwa ndaaaaani kabisa utagundua kuwa ni MZALENDO”.

“Kwahiyo haijawa sababu siku ya leo umeitwa KURUTI ukaudharau uzalendo ilimradi upo jeshini tukakupatia mafunzo na kukukabidhi cheti hatiamaye ukarudi kwenu ukiwa na hicho cheti hata kama kikaliwa na panya ama ukakichana jua ya kuwa wewe ni MZALENDO mpaka siku yako ya mwisho unafukiwa kaburini aidha kwa mitutu ama kwa njia nyingine yoyote”.

“Nasisitiza kuwa ilimradi tutakupatia cheti na ukawa kwenye kanzi-data makao makuu ya jeshi basi jeshi linatambua kuwa mtaani yupo MZALENDO aliyepata mafunzo ya kikamanda na MZALENDO huyo ni wewe”.

“Hii inamaanisha kuwa tangu ile siku unapokelewa kule getini ukaandikisha PARTICULARS zako na ukaambiwa umekuwa MZALENDO kuanzia siku ile basi unatakiwa kuyaishi maisha hayo mpaka siku ya kuhifadhiwa kwenye kifusi cha tani sita”.

“Tambua kwamba ukomo wa cheo cha UZALENDO ni ile siku roho inapotengana na mwili sasa ni juu yako vimetengana ukiwa kitanda cha nyumba ya wageni ukiwa mwenyeji, ukiwa vitani kulipambania taifa lako ama Mwenyezi Mungu akakukumbuka ukiwa zako nyumba ya ibada hiyo ni juu ya wewe” alikuwa akiongea huku Matroni akionekana kuinuka tayari kuhutubia.

“Mwisho kabisa nikirejea kwenye wimbo tuliotoka kuuimba ambao nao unatusisitiza uzalendo siyo bahati mbaya cheo chako cha kwanza jeshini kuwa MZALENDO kwani tungeamua uanze kuitwa KURUTA au SERVICE MAN tusingezuiwa wala kushtakiwa popote pale”.

“Ndiyo maana nikawaambia hata BRIGEDIA alikuwa MZALENDO kwa mantiki ya kuwa kila mwanajeshi ni MZALENDO lakini sio kila mwanajeshi atakuwa JENERALI hivyo uzalendo siyo cheo tu bali ni maisha ya kila siku kwa kila binadamu aliyepata mafunzo ya kijeshi”.

“Na tukiizungumzia misingi ya uzalendo inakutaka uwe mstari wa mbele kukemea, kupinga na kuzuia uovu wa aina yoyote mahala popote iwe ni kazini, bar, chuoni, kwenye ofisi za taasisi binafsi ama za umma, sijui gesti, shuleni, iwe ni nyumba ya ibada na ikiwezekana hata nyumbani kwenu hutakiwi kufumbia macho uhuni wa aina yoyote ile”. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

……………………………….…Itaendelea……………………………………
 
EPISODE 16

“Namuona Bosi wangu hapa ananivuta shati hivyo sina budi kumpisha nayeye atoe yaliyokuwa moyoni ila kabla sijamkabidhi nafasi hii adhimu niwasisitize kwa kupigia mstari maneno niliyoyasema awali”.

“Kama MZALENDO jukumu lako kubwa unatakiwa kuwa mstari wa mbele kukemea na kufichua maovu elewa neno mstari wa mbele naomba mshikilie hapohapo huku mkijiandaa kumsikiliza Matroni bwana yesu asifiwe sana”.

“Milele na milele Amina” alijibiwa afande Novath aliyeamua kumaliza kwa mfumo huo.

“Anhaah asante sana mtumishi ila kusema kweli leo tumejichanganya yaani kitendo cha kukuruhusu baba paroko uongee kabla yetu nisiwe mnafiki umenifilisi nimejikuta nimekuwa hohehahe kabisa maana kila nilichopanga kuongea naona kama ushakiwasilisha labda niwape fursa wenzangu kama kuna mwenye la kujazia”.

Hakukuwa na hata mmoja aliyeonesha nia ya kuzungumza badala yake wote walidai kuwa wamefilisiwa na baba paroko LUTENI Novath cha ajabu baba paroko alisema “Kama wao hawana basi nipewe mimi hiyo nafasi nimalizie niliyobakiza maana nimeishia njiani kwa ajili yako mkuu”.

Kauli hiyo iliwafanya maafisa wenzake waangue vicheko na matroni akasema “Baba paroko wewe subiri kwanza utaongea baadaye usijali kunywa kwanza maji upooze koo”.

“Hamna sina kiu mkuu lakini pia kama ni maji naweza kunywa huku naongea siumeona koromeo langu lilivyokuwa kubwa” alikuwa akiongea afande Novath huku akiinua kichwa kuonesha koromeo lake.

Baada ya mazungumzo hayo yaliyokuwa ya utani mwingi ndani yake alianza kuungurumu daboli N akisema “KURUTA wiih”
“Waah”
“Wii”
“Waah”
“Awaa”
“Awii”.

“Sikia kutoka kwangu KURUTA, maneno aliyoyasema mheshimiwa baba paroko ni maneno sahihi kabisa kama nilivyosema awali mtumishi amenifilisi sina la kuongeza ila muhimu mnatakiwa myachukue na kuyafanyia kazi”.

“Lakini pia msichokijua ni kuwa siyo kwamba tunamuita baba paroko kwakumtania hapana ni ukweli mnaotakiwa kuujua kuwa afande aliyetoka kuongea ni mtumishi wa Mungu kabisa”.

“Hivyo basi kwa yeyote atakayepata shida ya kiroho amtafute atamsaidia na nimatumaini yangu kuwa atawaachia namba zake japo tunajua kwamba simu tumewapokonya ila mjitahidi mumtumie vizuri”.

“Habari iliyokuwa nzuri ni kwamba wapo baadhi ya watu siku za ibada watakuwa wanasalia KOMBANIA si kwa ubaya afande hivi umesema ni O.C wa COY ipi? ”

“Danger COY mkuu” alijibu afande Novath baada ya kuulizwa na Matroni juu ya KOMBANIA anayoisimamia.

“Eeeh kama nilivyosema kwahiyo huenda ndugu zetu wa Danger COY wakawa wanasalia KOMBANIA yaani watakuwa wakitoka MABIO wanafanya usafi wakimaliza wanafoleni KOMBANIA kwa ajili ya ibada ila wakizingua mtumishi awaambie bwana yesu asifiwe na wasijibu mtumishi atalivua joho na kuvaa gwanda halafu anawadosoa hapohapo” maneno hayo yalitufanya tuangue kicheko karibia kundi lote la watu zaidi ya elfu mbili.

“Au nakosea mtumishi”
“Hapana mkuu hata maandiko yanasema usimnyime mtoto kiboko” yalikuwa ni majibu ya O.C wetu kwa Matroni yaliyozidisha vicheko miongoni mwetu.

“Itoshe kusema watu wa danger mmebarikiwa sana na nadhani mtakuwa mmebarikiwa kuliko KURUTA wote kikosini”.

“Na O.C wa KOMBANIA yao amebarikiwa pia” alidakia LUTENI Novath hali iliyomfanya Matroni kubaki mdomo wazi kwa muda huku akionekana kutabasamu.

“KURUTA Ewii”
“Awaa”
“Awaah”
“Awiih”
“Maswala ya baba paroko tuyaweke pembeni kwa sasa nataka nikazie jambo ambalo nafikiri tulishaliongea awali ila kwa wakati huu nataka kukazia kidogo”.

“Mmeshakuwa wakubwa sasa na hatimaye mnafahamika kama KURUTA ingawaje baba paroko keshawaambia hata mpande vyeo mkawe MAJENERALI lakini swala la uzalendo liko palepale kilichobadilika ni cheo tu ila sifa kuu ya mwanajeshi inasalia palepale”.

“Jambo ninalotaka kuwasisitiza ni kuwa katika kipindi hicho cha UKURTA mtakachodumu nacho ndani ya siku 42 sawa na wiki sita ukiachana na nidhamu lakini pia mnatakiwa kuwa shupavu na watiifu kwa siku zote bila kusahau ukakamavu na kutodoji FATIKI”.

“Kitendo cha kuitwa KURUTA maana yake unatakiwa ufanye vitu kwa uharaka hivyo nategemea kuwaona mkikimbia muda wote yaani ukienda kwenye FATIKI nenda kwa kumbia sijui umeenda kufoleni MESI nenda kwa kukimbia ni muda wa KOMBANIA nenda ukiwa unakimbia hata ukienda chooni nenda huku unakimbia huu ndiyo msingi wa ukakamavu ninaouzungumzia hapa KURUTA muda wa kutembea unautoa wapi!”. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

………………....…….…….…Itaendelea……………..……...........……
 
………………………….…Itaendelea……………..…………

MAISHA YA DEPO

SEASON-3

EPISODE 17

“Tukiachana na hilo naomba nitambulishe uongozi mtakao kuwa nao kwenye KOMBANIA zenu katika kipindi chote cha mafunzo”.

“Uzuri nyinyi wote ni wasomi tofauti na wale wenzenu wa kujitolea ambao huwa tunaletewa wengine darasa la saba na wanakuwepo darasa la nne mpaka darasa la pili wanakuja wakiwa hawajui kusoma wala kuandika”.

“Kwahiyo sina shaka kuwa elimu mliyokuja nayo ni kubwa sana na jambo la manufa zaidi inalingana hivyo nashawishika kuwa mtakuwa na uelewa uliokuwa sawa na wa haraka zaidi tofauti na wale ndugu zetu wa memkwa”.

“Kuna kitu sisi wangoni tunakiita Organization structure yaani Muundo wa taasisi kwa Kiswahili, msicheke hiyo imezeni na mtulie nayo wala hamtakiwi kuitapika hata kama ikiwa chungu” Matroni alituambia hivyo baada ya kugundua kuwa ametubutua na kitu Kizito.

“Ninaposema taasisi namaanisha nini? Ni kuwa hapa jeshini tuna taasisi mbalimbali zilizo katika mfumo wa makampuni yaani tukisema ALFA COY hiyo COY mbele ni ufupisho wa neno la kingoni yaani COMPANY”.

“Ni vile hatuna chaki wala ubao ila kwakuwa tushakubaliana kuwa nyie ni wasomi kwenye neno COMPANY ukichukua herufi mbili za mwanzo yaani C na O ukachukua herufi moja ya mwisho yaani Y then ukaziunganisha utapata neno COY tumeelewana KURUTA”.

“Ndiyo afande”
“Kumbe sasa tukisema BRAVO COY tunamaanisha taasisi au kampuni ya BRAVO sivyo KURUTA”
“Ndiyo afande”.

“Na ndiyo maana nikasema nyinyi ni wasomi yaani ndani ya nusu dakika mmekwishanielewa ila wale wenzenu wa darasa la saba mpaka la pili zilituchukua siku saba kueleweshana hili” Matroni alikuwa akiongea maneno hayo yaliyotufanya tuangue vicheko.

“Yaani karibia wiki nzima tulikuwa tukifoleni kuwaelewesha maana ya neno COY halafu wanapanga foleni ya kula wakimaliza wanafoleni KOMBANIA tunawaelewesha tena mpaka wiki inakata ndiyo unakuta wameelewa Mwenyezi Mungu awarehemu kwa kweli”.

“Tuachane nao hao ngumbaro jambo lingine ni kuwa kama taasisi lazima iwe na uongozi wake ambao unaelezewa vizuri kupitia muundo wa taasisi ambao kwa kingoni nimesema unaitwaje?”.

“Organization structureeeeee”
“Sijasikia vizuri unaitwa” aliuliza matroni ambaye aliweka mkono sikioni akiashiria kutaka majibu.

“Organization structureeeeee”
“Makamanda wangu mnasikia KURUTA wanavyoichapa lugha adhim ya kingoni” Mataroni alikuwa akiwauliza maafisa wenzake wa jeshi ambao walionekana kutabasamu.

“Hongereni sana wasomi wenzangu nisiongee sana nikaonekana mbaguzi ila wale ndugu zenu kutamka tu hilo neno aah subuuutu ziliwachukua siku zaidi ya mbili wote kuweza kulitamka tu hilo neno”.

“Hivyo kwa ruhusa yenu naomba nitambulishe viongozi wa taasisi zenu ili muwatambue japo wengine walishajitokeza huko kwenye KOMBANIA mkawaona ila si vibaya nikawatambulisha mbele yenu wote mkawaona kusudi hata akiulizwa KURUTA wa Danger COY kuhusu kiongozi yeyote wa Eagle COY awe anamjua kwani jeshi ni moja na mbaya zaidi japo si kwa ubaya kikosi ni kimoja”.

“Bila kupoteza muda mana naona hapo mlipo mnachungulia kwa MZABUNI kunaendeleaje hivyo naomba nianze na ma-Operation Commander yaani ma-O.C ambao ndiyo viongozi wa juu kwenye KOMBANIA zenu naomba ma-O.C wangu mjipange mbele kikombania kusudi KURUTA wawajue”.

“Mtashangaa mbona wako watano na taasisi ziko sita ipoje Ipo sawa kabisa hiyo wala haina shida maana mimi mwenyewe ni O.C wa KOMBANIA fulani na mimi nimejikatia KIBANGALA changu kwahiyo mkinijumlisha si tunafika sita”.

“Ndiyo afande”
“Haya tuanze utambulisho nikianza mimi mwenyewe Alfa COY enhee afande pale”
“BRAVO”“
mkurya na wewe”
“CHARLIE muraa”
“Enheeh baba paroko hapo”
“DANGER bwana yesu asifiwe”
“Matroni na wewe”
“EAGLE mkuu”
“Na kule mwisho”
“FOX mkuu”.

“Sawa naona utambulisho huo umekamilika na wote mmetufahamu hivyo basi nategemea wewe KURUTA wa Fox COY ukiulizwa O.C wa A-COY bila shaka utanyoosha kidole kwangu na wewe wa CHARLIE ukiagizwa kwa O.C wa DANGER sina shaka utaelekea kwa mtumishi pale baba paroko na wewe wa BRAVO ukiagizwa kwa O.C wa EAGLE nina uhakika utamkimbilia Matron pale chap kwa haraka tumeelewana KURUTA”.

“Ndiyo afande”
“Baada ya hapo wanaofuatia ni ma-SIR MEJA naomba SIR MEJA msogee mbele kwa ma-O.C ili KURUTA wawaone”.

Walijipanga maafande hao walioonekana ni wazee kwa umri tofauti na ma-O.C ambao umri ulionekana kudai wazee hao wakiwa na vifimbo vyao mkononi upande wa Danger COY tulipangiwa mpemba mmoja aitwaye Ashiru huku Alfa COY wakipangiwa yule afande mwenye tumbo la kwenda aitwaye SAJENTI Pastima. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

………………...…..…..….…Itaendelea……………...….....……………

LogoMakerCa-1743852388260~2.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom