Fohadi
JF-Expert Member
- Jul 24, 2020
- 770
- 2,410
Kuna watu wana amini maisha ya Dar ni magumu (kufanikiwa ni ngumu) wengine wanasema maisha mikoani ni rahisi (kufanikiwa ni rahisi)... Je, ugumu wa Dar uko wapi na urahisi wa mikoani uko wapi? (Huu ni mtazamo wa wengi humu kwa utafiti wangu mdogo nilioufanya humu ndani kwa muda kidogo).
Ningefurahi kama hii thread ichukuliwe serious na watu waweze kuweka strong arguments ambazo zitawasaidia wengine kutoa tongotongo machoni mwao (kujifunza) na kuona opportunities za kimaisha na kuchukua hatua kabla hawajaamua sehemu ya kuishi. Tofauti ya maisha mikoani na Dar ni ipi kiasi cha kuja na hitimisho kuwa Dar kugumu kuliko mikoani..Je ni kweli Dar ni kugumu kuliko mikoani?
Ni hoja zipi zinatumia katika kutoa hiyo conclusion hapo juu?. Mitazamo na hoja zetu wote zina manufaa na zina umuhimu wake hapa kwajili ya kujifunza zaidi. Ila pia nitafurahi zaidi kusikia kutoka kwa haya makundi mawili:-
1. Watu waliofeli mikoani wakafanikiwa Dar
2. watu waliofeli Dar wakafanikiwa mikoani
Karibuni tujifunze kwa hoja.

NB: Kuna watu tuta/watajifunza mambo mengi sana kupitia hapa. Sasa wale wenye lugha za kuudhi na kukejeli kila muda, itabidi wajifikirie na kujitathimini utimamu wao wa akili kabla hawajawavunjia wengine heshima..Ni bora/ vyema kukaa kimya bila kuandika chochote ikiwa utakachoandika kitakuwa kina lengo la kutukana au kuboa au ku attack watu personally.