Mwambie mdogo wako mambo haya

Street brain

JF-Expert Member
Oct 24, 2022
486
606
"Mwambie mdogo wako chuoni hakuna adhabu wala viboko, ila adhabu atayoipata ni supp na carry ikiwa hatazingatia kile kilichompleka."

"Mwambie akifika chuoni atakutana na watu wa mikoa tofauti na hata majiji ila akumbuke kuwa anatokea kijijini tena ndani ndani kbsa..."

Mwambie makundi makundi humaliza boom lake mfukoni

(Mwambie marafiki wa chuo hubadilika kila semester kuendelea kung'ang'ania ataisoma namba)

(Mwambie ajiandae kupokea lawama na hata kuachana na mpenzi wake aliyemwacha nyumbani)

"Mwambie lecturers wa kitanzania wanajua kila kitu na wako juu ya sheria kama ni wa kike ajifunze"

"Mwambie kama ni wa kike marafiki zaidi ya watatu hatoweza kudumu nao, watagombana kwa kuwa in nature marafiki wa kike mara chache kupendana na kuelewana"

*Mwambie chuoni kuna makanisa na misikiti kuna wanafunzi zaidi ya 1000 lakini wanaosali ni wachache sana,. Akumbuke kusali kwa juhudi zote......."

"Mwambie kwa "kapuku" kila mtu huwa anataka kuwasaidia wazazi wake ila inakuwa ya uwezo wetu"

*Mwabie chuoni ni sehemu ya kutengeneza connection na watu muhimu siyo sehemu ya kuambatana na marafiki wasio na faida"

Mwambie migomo na mihemko yenye uovu aviepuke maana si kila mtu amekuja kusoma wengine ndio wako kazini..

"Mwambie zile Bata alizokuwa akisikia zikibadilika na kuwa dagaa asishangae
Mwambie baada ya kumalizana na chuo hajawin maisha hapo ndipo msoto mpya wa maisha unapoanzia..."

"Mwambie mdogo wako wa kike kuhusu mavazi. Asipunguze zile sketi zake ndefu nagauni za heshima alizonazo asipunguze kwa ushawishi wa rafiki zake...."

"Mwambie tena maisha ni mafupi sana,Adumu kumcha Mungu na kumtukuza na kufanya mambo mazuri... LASTLY ASIMDHARAU MTU YEYOTE"

IKIKUPENDEZA YAFANYIE KAZI
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom