Habari wadau..
Nilikuwa natazama kwenye TV kipindi cha arobaini ya mtoto wa Babu Tale. Hiyo nyumba ya Babu Tale ni ndoto za wasomi wengi kuimiliki. Ni wasomi wachache sana wanaimiliki tena wengi ya hao wachache ni kwa rushwa, na ufisadi, sio kwa hela halali.
Mahojiano ya Fella pia nyumbani kwake Mbagala napo maisha yake yanaonekana yana financial freedom kubwa kuliko hata ya kaka yangu ambaye ni lecturer Mzumbe kwa miaka mingi na ni mbahili sana huyo bro ila hana maisha na vitega uchumi kama vya Fella na bro ana umri mkubwa kuliko Fella na amefanya kazi miaka mingi kama mhadhiri.
Mwisho kabisa Kanumba. Hadi mauti yanamkuta alikuwa na miaka 28 ila aliacha kampuni yake, magari kadhaa ikiwemo Lexus na hiace na account yake benki ilikuwa na milion 40 savings.
Je wasomi wangapi wenye miaka 28 wana uwezo wa kuwa na savings ya milion 40 na huku maisha mengine yanaenda kama kawaida tena maisha ya anasa sio ya kula matembele.
Sijamtaja Diamond sababu kila mtu anajua mchango wake.
Naomba tuelezane ukweli wasomi tunakosea wapi kiasi ikifika tarehe 23 tu humu thread za mishahara imechelewa zinakuwa nyingi sana na wengine tunakopa hadi elfu 10 ili zisogeze siku mbele.
Tutasema ni vipaji hatuna, je Babu Tale au Fella wana kipaji gani? Mbona hawaimbi wala hawana studio tuseme ni ma producer ila wana maisha mazuri tu.
Je degree zetu zinatusaidia kweli au zinaturudisha nyuma?
Kuna thread ya visa humu watu wengi wanalalamika kunyimwa visa na balozi hasa wa Marekani na Canada na tena wengi ya wanaolalamika ni wasomi wana elimu kubwa sana na wanashangaa kina Fella au Babu Tale wakipeleka documents tu visa wanapewa na wanasafiri mara nyingi kama JK vile kushangaa dunia ila wasomi hatuwezi hata kuweka mazingira ya kumshawishi mzungu akupe visa ukatembelee nchi yake.
Dick sound mfunga mziki wa magari Magomeni wengi waliokaa Magomeni wanamjua na amewahi kuwauzia maji kwenye madumu ya mkokoteni pale Magomeni anasukuma mkokoteni anauza maji kipindi ametoka kwao Iringa. Angalia leo alipo ana nyumba kibao mpaka mama yake kamjengea nyumba Dar na angalia gari zake anavyozibadili kila mwaka angalia umri wa dick hata 35 sizani kama amezidi.
Swali kwa wasomi wote ambao tumeajiriwa na tunalalamika mishahara ikichelewa, au ikikosa increments je hizi degree zinatusaidia kweli au zinatufelisha?