Maisha ya Arusha sio

Maisha ya Arusha sio

Mkuuu sing'isi kitaa chetu ni sehemu salama sana kwa sasa


Sing'isi huko wiz ndo umejaa kuanzia kwenye mashamba Yan Kama n mgen utaumia kagiza kakianza tuu hiace hazisimami wanajua wameru wanaeza fanya yao
 
hii
Wakuu salama, Sina. Mengi ya kuandika hapa,
Nina. Miaka kadhaa hapa Arusha lakini kuna baadhi ya mambo hunishangaza kidogo

1) Ujambazi, wezi wa hapa hawaogopi chochote, mfno mzuri usiku wa. Leo wameingia kwenye nyumba ya mjeda, mwanamke na mume wake wote ni wajeda lakini cha kushangaza wazee wa kazi wameingia ndani ya ukuta wamechukua piki piki na kusema.
Mwezi Uliopita pia waliingia kwa mjeda mwingine huko kwa morombo wakachukua kombati. Lilikuwa kwenye kamba lime Anika.

2) Ugomvi kidogo mtu anachomoa kisu. Na hapepesi anakupa cha kichwa au cha tumboni. Si mwanamke si mwanaume wote ni visu wanakushikia na hawaogopi.

3) Kubwa zaidi kuliko yote ni Bangi na. Mirungi
Si wanaume si wanawake Bangi na Mirungi huwaambii kitu. Tena Mirungi ya siku hizi wanaagiza Nairobi wanaita wenyewe ndo gredi one

Mijanamke ya hapa kukuta yanapiga mizinga ya nyagi huku yanachanja Yan kawaida sana.

4) No story no ushost kila mtu na laifu Lake, kila mtu hapa anamaindi mambo yake.
Katika mitaa ambayo haikaliki ni matejoo, ugalimi, na Ngarenaro Yan huko hata polisi wamenyoosha mikono.
Japo patrol ya. Polisi ni usiku na. Mchana lakini vijana hawasikii na hawaelewei
hii ndio chuga mzee
 
Arusha ya sikuhizi imepoa saana tena saana.

Rudi 2005 kwenda nyuma saa 12 kila mtu anawahi kwake.
 
Huko chuga kawaida sana.

Embu waje dar watembelee sehemu hizi

Mburahati ,vingunguti, gongo la mboto, chanika , ukonga moshi bar, yombo buza, mbagala , keko kitoroli , nk.
Yani dar ilivyokosa "USIRIAZ" mpaka ukitaja hiyo mitaa hatari mtu anadhani unamchekesha eti KITORORI...aisee mburahati apaelewa vizuri.
 
Arusha siku hizi hamna sana mambo ya kuchomana visu hata ujambazi umepungua au tuseme kuisha kabisa.

Zamani hukai siku hujasikia tukio la ujambazi na mtu kuuwawa. (Tutofautishe jambazi na kibaka). Matukio ya vibaka ni kawaida karibu kila mkoa TZ.

Issue ya bangi na miraa ni kawaida pia maana bangi kila mahali TZ inavutwa na miraa ni kwasababu tu inapatikana hapa jirani Kenya na Upareni ndio maana watu wa hapa wanatumia.

All in all Arusha ni sehemu nzuri tu na salama as long as unafata mambo yako. Hizi stroy mingi mingi ni exaggerations tu za watu ambao hata hawapajui Arusha.
 
Yaelekea huyu aliondoka arusha 1995!! Anaongelea habari ya unga ltd na ujambazi leo? Haijui hata mitaa hatarishi kwa sasa,ngoja nimdokeze kidogo- pandisha barabara ya sanawari,panda juu kabisa hadi ukute daraja,ukishavuka hilo daraja sasa jiendee tu slow slow,maana muda wowote unakabwa,umeshaisikia kidin'ga? Basi bora usiisikie, (2)panda mianzini kutokea kwenye mataa pale, nenda juu kama kilometa 5 hivi,kuna mtaa kule wakaaji wote wanajuana,ukiwa hueleweki basi wenyeji wanakupora kila kitu mbele ya kadamnasi, in short Arusha ina washamba flani wachache tu (mleta mada akiwemo) ambao hawajawahi kutoka nje ya arusha na ambao wanadhani ni arusha tu ndiyo kuna vibaka,wanadhani ni arusha tu ndiyo kuna wavuta bangi,na wanafikiri ni ujanja kuvuta bangi huku unatembea barabarani,au kutembea na beto na bisibisi wanaona ni uselaaa! Hao washamba wachache ndiyo wanaotuharibia sifa ya kamji chetu!!! Najisikia salama mno kutembea unga ltd saa saba za usiku kuliko kukatiza temeke saa 12 jioni,
Hahahaa
 
Haha huu uzi umenithibitishia msemo wa MTU KWAO kama kibwagizo cha mchoraji NATHAN MPANGALA pale ITV
 
Hii ndio Chuga arifu,ukizingua kidogo unapewa dozi,wanaume wa huku hawarembi kama wa Dar.
Unashangaa mjeda kuibiwa,haushangai wazee wa mzigo kwenda kupiga selfie kwenye kambi ya jeshi,hii Chuganistan.
Acha kusifia upuuzi mkuu!
 
Halafu Arusha maisha ya huku hayana uhalisia.Kiwanja cha 20X20 nje ya Mji unaweza uziwa hata mil10 kitu ambacho Dar au Mwanza unaweza pata kwa mil1 au 2.Barabara unaweza uziwa mil3.Thamani ya nyumba Arusha haina uhalisia kwa maisha ya sasa.Yaani kama vile haka kamji kapo Kenya!
 
Back
Top Bottom