Maisha ya Arusha sio

Maisha ya Arusha sio

Sasa hizo share za jeshi za nini? Wajeda wakikubananisha wakakupa kichapo unaanza kumlilia mama.
 
Nenda katembeee tembee unga LTD usiku uone arusha vile tamu.

Karibu arusha am sure huna hata miezi 3. Baada ya mwaka njoo utupe mrejesho.
 
Umeleta story za kuambiwa tena na mzazi wako ambae aliishi chuga akiwa kijana, haya mambo uliyoandika mengi ni story now, matejoo sasa hivi pamekuwa fresh sana maana hakuna tena mashamba ya kahawa na migomba ambayo ilikuwa kichaka cha wezi, matejoo now vijana wengi wameenda shule na wapo sehemu tofauti ulimwenguni matejoo ya sasa imejengwa sana na makabila tofauti na zamani walikuwa wazawa peke yao, bangi ni kila mahali TZ inavutwa, kila mtu ku mind mambo yake ndio maisha chuga kila mtu anatafuta pesa, mwanamke anaamka saa 11 anaenda kwenye mishe zake, nyumba nyingi kwa mromboo, uswahilini zimejengwa na wanawake wajasiriamali, hakuna mtu anakaa kibarazani asubiri agongee nyagi au banana, ananunua week end kwa pesa yake, miraa inaliwa sana ndio lakini wananunua...bro wewe ishi Dar ukae kijiweni usubiri kutia story na wake za watu.
 
Acheni uongo chuga ipi hiyo ya mambo ovyo, haahaa!

Arusha ya sasa imepoa sana unaweza tembea usiku sana usiwe na wasiwasi wowote.

Sehemu zote ulizozisema maisha ni salama kabisa. Unaanika nguo usiku asubuhi unazikuta, haaahaaa.
Acheni mastori ya kuambiwa.

Njoeni Arusha week-end hii mje mfanye utalii wa ndani wa hiyo mitaa jamaa aliyoisema.
 
hii ni story umeisikia kwa mtu in real aspect arusha ya sasa hv kote huko matejoo ngarenaro ni pakawaida sana yani ungalimited pamepoa ni viwanda tupu kasoro ngarenaro msingi kidogo kwa umbalii bado kuna vibaka afu eti watu wa arusha kuchomana bisi bisi au visu mbona hizo story hamna huku watu n amani tu afu i can gurantee u arusha iko top 2 ya miji isiyo lala mapema maana trip za morombo na uswahilini zinaisha saa saba na sehemu kama mianzini nimeishi miaka 20 kwanzia 2014 mianzini hawalali watu barabarani ni 24 hours acheni story za vijiweni njooni mtembee afu haipiti siku uzi wa arusha haujafunguliwa humu jf
 
Wakuu salama, Sina. Mengi ya kuandika hapa,
Nina. Miaka kadhaa hapa Arusha lakini kuna baadhi ya mambo hunishangaza kidogo

1) Ujambazi, wezi wa hapa hawaogopi chochote, mfno mzuri usiku wa. Leo wameingia kwenye nyumba ya mjeda, mwanamke na mume wake wote ni wajeda lakini cha kushangaza wazee wa kazi wameingia ndani ya ukuta wamechukua piki piki na kusema.
Mwezi Uliopita pia waliingia kwa mjeda mwingine huko kwa morombo wakachukua kombati. Lilikuwa kwenye kamba lime Anika.

2) Ugomvi kidogo mtu anachomoa kisu. Na hapepesi anakupa cha kichwa au cha tumboni. Si mwanamke si mwanaume wote ni visu wanakushikia na hawaogopi.

3) Kubwa zaidi kuliko yote ni Bangi na. Mirungi
Si wanaume si wanawake Bangi na Mirungi huwaambii kitu. Tena Mirungi ya siku hizi wanaagiza Nairobi wanaita wenyewe ndo gredi one

Mijanamke ya hapa kukuta yanapiga mizinga ya nyagi huku yanachanja Yan kawaida sana.

4) No story no ushost kila mtu na laifu Lake, kila mtu hapa anamaindi mambo yake.
Katika mitaa ambayo haikaliki ni matejoo, ugalimi, na Ngarenaro Yan huko hata polisi wamenyoosha mikono.
Japo patrol ya. Polisi ni usiku na. Mchana lakini vijana hawasikii na hawaelewei
We kunguni kwanini unawaita Binadamu wenzio Mijanamke???

Mama, dada na shangazi zako pia unawaita hivyo?
 
Back
Top Bottom