Maisha Vs Muda,...Unatosha?!

Duh..gurudumu langu haliendeshi hata mkokoteni...needs big tym fixing!
Thanks Mbu...leo umetoa tiba badala ya maradhi!
hahahaaaaaaaaa.... yaani wengine tumegeuza magurudumu yetu yamekua kama embe au hata mstatili

Good one for the day
 
Yule miss J ndoa ndio dawa yake mana pale hakuna mjanja inaonekana anaingia katika ile ndoa akiamini 1+1=2 kumbe hakuna hio kule jibu ni 11.

Ataijua sawa sawa.
Ila huyu Mbu bana naona kakosea kujiita Mbu
Haya mapost anayoweka hapa JF hayafanani kabisa na jina lake
Yaani akianzisha mada, akachangia M'JamiiOne utafikiri ni mtu na mke wake.
Nampa wazo afikirie kulibadilisha if posibo.
 
Ataijua sawa sawa.
Ila huyu Mbu bana naona kakosea kujiita Mbu
Haya mapost anayoweka hapa JF hayafanani kabisa na jina lake
Yaani akianzisha mada, akachangia M'JamiiOne utafikiri ni mtu na mke wake.
Nampa wazo afikirie kulibadilisha if posibo.

Loh watu wengine wachokozi! Sasa ID ya Mbu, kuchangia kwa Mjw1 na kuwa mkewe kuna uhusiano gani wajameni!!?
 
I am a failure when it comes to balancing my time..... All blames to TBL/SBL. Why on earth are they brewing this kind of drinking liquid? ...When I get out of my office the only thing in my addicted mind is Beer......... and only Beer!


Yaani unapanga kwenda kwenye ibada (kujaribu kurejesha uhusiano wako na Muumba wako)....ukiwa njiani unapigiwa simu....njoo hapa baa mpya, nipo na A, B na Y....
Ratiba inabadilika....unasahau njia ya kwenda nyumba ya ibada....
Damn...I surely need a life mechanic.....
 
Ataijua sawa sawa.
Ila huyu Mbu bana naona kakosea kujiita Mbu
Haya mapost anayoweka hapa JF hayafanani kabisa na jina lake
Yaani akianzisha mada, akachangia M'JamiiOne utafikiri ni mtu na mke wake.
Nampa wazo afikirie kulibadilisha if posibo.


mimi jina la mbu nalipenda ila avata si ya ukweli haijaka sana kikaka atafute mbu dume kweli kweli alafu hizi pea naona kama zipo zipo na kama tight

hapa jamvini sijui kweli nisaidie kwa hilo nipate jibu.
 
Kama maisha ambavyo ni mzunguko, kila kitu kina kiasi. Basi tujiweke tayari kupokea lolote litakalotukabili katika maisha wakati huo huo tukifanya bidii kuhakikisha tunatimiza wajibu wetu ipasavyo. The wheel of life lisukumwe bila kuweka 100% expectations kwamba ukitimiliza yote hayo utakuwa umefanikiwa na furaha ya milele itakuwa kwenye himaya zetu.

"You can have anything you really want but you cannot have everything you want."
 
Mkuu Issue inakuja kwenye umasikini.....

Hii RAT RACE, inaumiza wengi..., mtu unakuta financially sio Stable kwahiyo ili to make ends meet watu unakuta 24/7 wapo busy wanatafuta pesa ili hiyo relationship and romance iweze ku-survive.....

Kwahiyo unakuta hayo yote mengine ni misamiati...., No Fun at All..., unless labda hio kazi anayofanya ndio aibadilishe kuwa FUN, kuangalia Afya yako???, thats another msamiati., sababu pesa ni za mafungu....

So there are some factors which are beyond the person power to overcome.., kutokana na kwamba factor moja muhimu ya "Financial" haitoshelezi hence hata kama mtu angeongezewa masaa 12 katika hayo 24 huenda still asingeweza ku-make ends meet
 
....dah, kwanza nawashukuru nyote mliokwisha changia mpaka muda huu. WoS, nice to see you back japo hiyo ya huyo baba aliyeonyeshwa ushuhuda na muumba maisha yake imeniuma sana. Kwakweli twahitaji ku balance haya maisha jamani.

Nitakuja na maoni na michango tofauti bdae.
 
happy_circle.png

The wheel of life is a valuable tool to help you evaluate what’s working and what’s not working in your life.

...ni kawaida kusikia mtu anakujia na excuse ya,."..sikuwa na muda!"...lakini je? huwa unajipangia mambo yako kwa mujibu wa muda, au ndio umejikubalisha muda utawale sehemu kubwa ya maisha yako?


Evaluate maisha yako kisha ujiulize;

  • una muda wa kutosha kukaa na kubadilishana mawazo na familia yako? Unawasaidia watoto homeworks zao, kujua maendeleo yao kimaisha? ...vipi kutembelea ndugu, jamaa na marafiki?
  • una muda wa kutosha na mpenzi/mke/mume wako, ...mwenza wako halalamiki hutulii nyumbani?
  • umejiwekea muda wa kutosha kujiburudisha akili, hii ni recreational activities hata kama ni kwa kibustani cha mboga..., michezo etc? , una muda wa kutosha kufanya ibada?
  • una muda wa kutosha kujiangalia afya yako, kufanya mazoezi, regular check ups? au mpaka uumwe ndio unakwenda hospitali?
  • Una muda wa kutosha kufanya kazi zako bila kuelemewa na kurudi nazo nyumbani? Wengine 'hushikika' hata kula wanasahau. Nawe ni mmoja wao?


    see-best-color-life-glasses-cloud-blue-reflect.jpg


    "You can have anything you really want but you cannot have everything you want."

    reflect-on-life.jpg


    "To know yourself is the first and most important step to pursuing your dreams and goals." – Stedman Graham
Badala ya kulaumu hali ngumu, jilaumu mwenyewe kwa kushindwa kujipangia yaliyo na umuhimu katika maisha yako. Kila siku iendayo hairudi Nyuma. Usilolifanya leo na kuliweka kiporo kwa kisingizio utalifanya kesho jua umeshaharibu mtiririko wa mpangilio wa maisha yako. Jiepushe kulimbikiza shughuli.

Liwezekanalo kufanyika leo, usilisubirishe. Ni wangapi kufumba na kufumbua wamejishtukia tayari retirement age ishawafikia ilhali hawakukumbuka kuwekeza?

Fainali uzeeni!....tusisubiri kukurupushwa ilhali kushakucha!...Hakuna awezaye kukupangia mkaisha yako ila wewe mwenyewe. Tuanze kujipangia maisha yetu kuanzia sasa kisha mtaona uwiano mzuri wa maisha, furaha, amani na mapenzi yanavyorudi tena majumbani mwetu.
Otherwise,

kwanini unaamini hauna muda wa kutosha (ku balance maisha yako?)

Mbu ahsante sana kwa uzi mwingine mzuri sana. Kwa maoni yangu kuwa na maisha ya kila siku ambayo yanaendana ni hilo gurudumu la maisha ni ngumu mno! Unaweza kabisa kupanga siku au hata wiki iwe hivi lakini kuna mambo mengine ambayo yatajitokeza na kuvuruga kabisa ule mpangilio ulioutaka kwa siku ile au wiki ile.

Kama alivyosema MTM maisha ya leo kikubwa zaidi ni career na finance hivyo utaona hapo ndio kuna mkazo mkubwa katika maisha ya kila siku ya watu wengi duniani ikiwemo Watanzania

Mimi ushauri wangu mara nyingi hasa kwa wale wenye familia ni kujitahidi tu kuhakikisha kuwa familia yako inaona juhudi zako za kila siku katika kuhakikisha unaboresha maisha ya kifamilia kwa namna moja au nyingine. Hata utakapokuwa haupo duniani na wao kuendelea kuwepo waweze kutamka bila hati hati kwamba Baba/Mama yetu alikuwa mzazi mwema ambaye alijitahidi kila awezalo kuhakikisha tunakuwa na maisha mazuri ikiwemo kupata elimu nzuri pia. Mume/Mke wangu alikuwa ni mwenzi mema na siku zote alijitahidi kwa kila hali kuboresha maisha ya familia yetu. Kama unaweza na kumshukuru Mungu kila siku unayoamka na kujikuta wewe na wale wote uwapendao mko salama basi hapa ni lazima kushukuru ukitilia maanani Wanadamu wengi sana duniani hawana bahati kama hiyo.
 
Yule miss J ndoa ndio dawa yake mana pale hakuna mjanja inaonekana anaingia katika ile ndoa akiamini 1+1=2 kumbe hakuna hio kule jibu ni 11.
Jamani tusifikirie kila ndoa mbaya.. Pengine Miss Judy kapata mtu aliye compatible naye.. Hebu msameheni jamani.
 
Wow,shukrani Mbu na wachangiaji waliotangulia....honestly, sina balanced life,nahisi asilimia 80 ya akili yangu kwasasa inawaza kazi tu na matatizo ya kazini,nikijaribu tu kufanya kitu kupumzisha akili ndo worse kabisa kwa kuwa naona kama kila kitu kinasimama kazini.....nimejifunza kitu na nitajitahidi sasa kupanga muda zaidi kwa ajili yangu na familia.....maisha mengine,Mungu atusaidie!!!
 
Lol maisha yetu wengine mwenzangu mh......unapanga weekend uende beach na mtoto mara wapigiwa simu ijumaa jioni unatakiwa kusafiri Ntwaraaaaaaaaa........... miezi miwili!! Ukirudi wakuta meza inakusubiria na mkoloni ndo kasimama tititi!! kutahamaki miezi miwili hujaonana na rafiki wala kukaa na familia!
Mie ndio maana nikiona maji ya shingo nabeba mwanangu na mdada wake naenda nao safari hukohuko kwenye kazi
 
Actually Mbu najialumu sana mwenyewe kwa kuweka mbele career and finance ambavyo vimekula kabisa spiritual, personal growth, health

relationship na family navyo nisipokua makini vitanitupa mkono

I am going to try something to reverse this... the only challenge ni kazi/career success na pesa... they are more addictive than anything i have ever experienced

...well said MTM. unajua twaweza zifanyia maskhara dalili za maisha yanavyoweza kutuelemea, kisha tukaishia laumu uchumi na watu wenginbe ilhali power ya mabadiliko imo mikononi mwetu.

Ni ukweli usiopingika, masaa ya kazi (8hrs) kwa wengi wetu yanakula theluthi moja ya kila siku (24hrs!)
Tuseme theluthi ya pili, ukiigawanya mara mbili....masaa manne wayatumia kwenda kazini na kurudi nyumbani,...hayo masaa manne yalobakia wayatumia vipi?

...Iwapo kwenye theluthi ya tatu (8hrs) wayatumia kulala, kweli kuna sababu mke/mume kulalamika humjali?
Nadhani tuna haja ya kujiangalia katika haya masaa 24 tunayatumiaje?
kisha tuangalie weekend, au off days nazo twazitumiaje.

Isije ikawa masaa yanatupita bila hata kugundua.

shem, what can i say??
....this is a very good reminder about our life purpose, the only challenge niionayo ni ile definition ya success kwa community zetu, including those we love most... what if i balance all of them and end up with less income and stunted career path, my love may never give me the same respect

its a challenge really, especially now you find in many couples wote wanakua career people
 
Hii hali inawapata watu wengi sana wenye kazi/majukumu yenye kuwategemea sana hasa middle and senior cadre of workers/experts. Ndio maana taasisi nyingi zenye malipo makubwa kitu kikubwa kinachowafanya wawe "waajiri wabaya" ni ile work-life balance.They scored very poorly hadi wanatafuta hadi mikakati ya kuimprove na inashindikana maana ule mzunguko wa kazi uko palepale!

Tukiacha mchango wa waajiri katika kukosekana balance, kuna upande mwingine pia ambao unachangiwa na familia zenyewe. Huwa nasema wazee wetu waliostaafu ambao walitulea kwa kipato chao walichokipata kwenye mishahara na ambao hawakujisikia kusukumwa kuongeza kipato, walifanya vizuri kuliko siye wa zama hizi za kukimbiza shilingi isiyokamatika!

Mwanao MTM leo anataka "toys" ambazo siyo toys bali ni "hi-tech gadgets" zinazouzwa mamilion ya shilingi, umlipie ada ya mamilioni, atoke kutembea na kuburudika kwa gharama kubwa, akifunga shule aende holiday,avae mavazi yaendanayo na world trends.... the list is long!

Mamaa naye anataka aishi maisha mazuri, mjenge au mpangishe nyumba ya kiwango, usafiri wa binafsi, maisha bora kwa kifupi.Je usipochacharika unadhani familia itakuwa na amani na wewe? Je unadhani utajivunia heshima kwa ndugu jamaa na marafiki kwa kutokuhangaika... nikimaanisha urudhike na kipato cha kijungu-jiko kisichokuweka kwenye level ya wewe kujiskia confident kujichanganya nao?

Ukija kwenye kujijali afya, ukiwa huna pesa ( unayoitafuta kwa kujinyima muda wako na kuuwekeza kwenye kazi) utamudu AAR na bima nyingine za afya assuming haulipiwi na muajiri.

Nina mengi ya kuchangia kwenye hili kuonyesha its becoming almost impossible kuligawanya hilo gudumu alilotuwekea MBU na kutoa nafasi sawa.

Ninapoandika huu mchango wangu, nimekumbuka video moja tulionyeshwa miaka ya nyuma kuhusu management and leadership kwa kifupi ikionyesha baba aliyejitesa sana kutafuta ili aipe familia yake maisha mazuri.Katika kimbizana hiyo akaja kupata heart attack akafa! Alipokufa akaenda mbele ya Muumba, na akaulizwa jitetee kwanini upate paradiso na siyo jahanamu.Utetezi wake ulikuwa kwamba alihangaikia sana familia yake hadi akajikuta umauti unamfika!

Cha ajabu na kilichonishtua ( miaka ile) ni kwamba Muumba alimuuliza tena " je una uhakika familia yako ilifurahia hali hiyo?" Akajibu ' nina uhakika maana hawakukosa chochote walichohitaji".
Muumba akamwambia " subiri tuthibitishe kama kweli familia yako ilirIdhika". Ikaonyeshwa Re-play ya maisha ya yule bwana na familia yake...jamaa alishtuka kuona jinsi mkewe alivyokuwa ananung'unika kwa vile muda mwingi hayuko nyumbani hata pale alipokuwa na watoto wadogo, watoto walipoumwa, mke alipoumwa, yalipotokea matatizo mbalimbali kwenye familia etc. Kisha akaonyeshwa jinsi hakuwepo kuona wanae wakikuwa kwa haraka, wakianza shule, wakifanya homework na kushiriki michezo mbalimbali.Watoto walihudhunika baba hakuwepo kuwapa support nk.

In short jamani hakuna jema.Haya maisha ya sasa ni ubatili mtupu!

Mimi mwenyewe ninajiangalia na kujiuliza itakuwaje kama naulizwa maswali aliyoulizwa huyo bwana hapo juu. Je na nyie wengine majibu yenu yatakuwa vipi?
Je mtastahili paradiso?
Pole kusoma kitu kirefu lakini ni vema kushirikishana.

WoS, kiukweli post yako imenipa changamoto kwa jambo ambalo hata mimi nina kauzembe.
Ni kweli siku ya siku tutajikuta mbele ya muumba na 'filamu ya maisha,' ...itapokuwa rewinded tutajikuta
twajiinamia chini kwa fadhaa!

Maisha ni discipline, ...utapojipangia na kuzingatia muda, mipango na utekelezaji wake, kidogo kidogo muda utatosha.
Hivi ni wangapi miongoni mwetu wanajua mida yao ya kulala?...au ndio wana vijisababu mpaka utapopatikana usingizi?

Kujipangia muda wa kufanya ibada ni jambo jema sana. Sawa na kujipangia angalau mara moja kwa siku mtu ukae mezani kula na familia yako. Ukishafanikiwa kujipangia muda wako kwa siku nzima, sidhani kama itakuwa ngumu kujipangia ratiba ya wiki nzima.

'Unexpected Circumstances' zitakuwapo, ambazo iwapo tutakuwa twajipangia plan B za maisha yetu, ni rahisi kuwa kurudia kwenye mstari likishapita. Issue ya masaa ya kazi nitaigusia nitapomjibu Mwj1...

Yaani unapanga kwenda kwenye ibada (kujaribu kurejesha uhusiano wako na Muumba wako)....ukiwa njiani unapigiwa simu....njoo hapa baa mpya, nipo na A, B na Y....
Ratiba inabadilika....unasahau njia ya kwenda nyumba ya ibada....
Damn...I surely need a life mechanic.....
 
Ni kweli lakini Mbu ukiangalia kiundani zaidi ni wazi kuwa kila kitu kiko mikononi mwetu!! If we strictly stick to our job description (kwa walioajiriwa) ni wazi kuwa utawezajipangia na kuweka limit ya ufanyaji wako wa kazi but kwangu mimi (Sijui wengine) najikuta kwenye dilema kwa kuwa kuna kale kamstari kasemako......and any other work assigned by my employer...yaani hii inanifunga hata akinambia unatakiwa kuja jumamosi au uunganishe safari juu kwa juu hata miezi miwili nashindwa kumwambia siwezi.......nilisign mwenyewe ule mkataba ujue!!
But I think there is a need to reflect some aspects!

But kitu kingine ni how do we get satisfied?? especially ukiwa na kazi ambazo yaani zinalipa? mfano safari zenye per diems nzito na masurufu mengineyo (Posho za kibunge lol) how can we sacrifice that only to spend some quality time with our loved ones?
Mwe!! Mtihani

hhaaa hha! BaK wasemaje? twahitaji masaa 48?....
Mimi nakwambia tuanze kwanza kujiuliza haya masaa 24 tuliojaaliwa tunayatumiaje.
Ukishaweza weka hayo masaa kwenye mchanganuo unaoeleweka, wallahi utajikuta wacheka mwenyewe unavyo waste!

Katika shughuli muhimu za mwanadamu,....una masaa 8 ya lazima kufanya kazi (wengi wetu)
Kisha, una masaa 6-8 ya kupumzika (kulala!).... masaa nane 8 yaliyobakia unayatumiaje?
Kumbuka,...hayo masaa nane "8" * 7 days a week = 56 hrs!!! ni zaidi ya 48 hours ulizosema kaka.

MwanajamiiOne,...
Tatizo la wengi wetu tufanyao hizi kazi za kuajiriwa tuna nidhamu ya uwoga!...
Kwanza ni haki ya muajiriwa kudai Job description!...msinambie eti Bongo hakuna hiyo....
Haya, hata kama wafanya kazi kwa mhindi... masaa ya kazi ni yale yale,...either 8- 4/5pm!
Hakuna Muhindi ambaye anataka kufanya kazi/biashara zake zaidi ya masaa nane...chunguza!

Kwa wakazi wa Dar, jioni mtawaona hawa wenzetu waasia wamejazana kwenye gari na wake zao na watoto haooo Coco Beach kula upepo wa bahari na madafu. Tukirudi kwa wabantu wenzangu na mie,...waajiriwa tukishatoka maofisini/vibaruani, wengi wetu tunaishia 'vikaoni' na washkaji kupoozea mbili tatu kabla ya kurudi nytumbani. Tena usipoonekana kikaoni utaulizwa, unakimbilia nini nyumbani?!

Kuhusu hizo worrk overloads,...kiukweli kuna kila dalili nasi twachangia kujitwisha hayo ma home work!....Hivi kuna raha gani upo nyumbani na mkeo/mumeo, badala ya kutumia masaa machache baada ya mihangaiko ya kutwa kuwasaidia watoto homework, kula pamoja, na kubembelezana kwenye kochi kabla ya kwenda kulala...wewe mke/mume unakuwa busy na mafaili yako ya ofisini? Hasta huo muda wa kubadilishana mawazo unakuwepo kweli?

By the time mke/mume huyo anakwenda kulala, tayari mwenziwe anakuwa keshaboreka...keshajilalia zamani. Au kama mume ndio ana roho ndogo, atajionea bora akazurure nje...awe anarudi nyumbani kulala tu. There's alimit kwa kila kitu,...kuna kazi za dharura, hizo ni kawaida kufanyika nyumbani,...lakini si vizuri kujenga mazoea Monday to monday mke/mume yupo busy na mafaili ya ofisi,...au nakosea jamani?

Binafsi, I can tolerate baadhi ya kazi, lakini zile nionazo mke wangu anazidiwa kiasi kwamba huko kazini wanahataraisha maisha ya ndoa yangu, maisha ya mke wangu, na watoto wetu...sitasita kumjengea tabia ya kuanza kuacha mafaili huko huko ofisini. Tena akirudi nyumbani na simu zizimwe. Haiwi ati bosi yupo Kempinski na mkewe, anampigia mamsapu eti a submit report by 6am... unless mke wangu nae ni mzito wa kumaliza kazi zake huko ofisini.... that's another case.

Mbu we need a 48 hours day :) instead of 24 hours only :) in order to balance our daily lives
 

hhaaa hha! BaK wasemaje? twahitaji masaa 48?....
Mimi nakwambia tuanze kwanza kujiuliza haya masaa 24 tuliojaaliwa tunayatumiaje.
Ukishaweza weka hayo masaa kwenye mchanganuo unaoeleweka, wallahi utajikuta wacheka mwenyewe unavyo waste!


Mbu tayari tuna uthibitisho wa kutosha kwamba 24 hours hazitutoshi ili kuweza kuendana sambamba na hilo gurudumu la maisha, hivyo labda saa moja iwe na dakika 120 :) badala ya dakika 60 au tupunguze masaa ya kufanya kazi kwa siku badala ya masaa manane iwe ni manne tu tena kwa ujira ule ule wa masaa manane (Waajiri kamwe hawatalikubali hili) labda Wanadamu tutafanikiwa kuweza kuendana na hilo gurudumu la maisha, vinginevyo itabaki kuwa ni ndoto tu.

NB: Nina baadhi ya marafiki ambao wanaupanga muda wao kila siku wakitoka kazini watafanya hili watafanya lile n.k. na kila siku huwa nawauliza katika ile schedule yako ya jana ulikamilisha mangapi? Kila siku jibu linakuwa sikuyamaliza yote kutokana na hili na lile na hawa ni watu ambao wanajitahidi sana katika kupanga mambo yao kila siku iendayo kwa Mungu.
 
Mbu tayari tuna uthibitisho wa kutosha kwamba 24 hours hazitutoshi ili kuweza kuendana sambamba na hilo gurudumu la maisha, hivyo labda saa moja iwe na dakika 120 :) badala ya dakika 60 au tupunguze masaa ya kufanya kazi kwa siku badala ya masaa manane iwe ni manne tu tena kwa ujira ule ule wa masaa manane (Waajiri kamwe hawatalikubali hili) labda Wanadamu tutafanikiwa kuweza kuendana na hilo gurudumu la maisha, vinginevyo itabaki kuwa ni ndoto tu.

NB: Nina baadhi ya marafiki ambao wanaupanga muda wao kila siku wakitoka kazini watafanya hili watafanya lile n.k. na kila siku huwa nawauliza katika ile schedule yako ya jana ulikamilisha mangapi? Kila siku jibu linakuwa sikuyamaliza yote kutokana na hili na lile na hawa ni watu ambao wanajitahidi sana katika kupanga mambo yao kila siku iendayo kwa Mungu.

kaka, kwa kiwango kikubwa walaumu muda wa kazi kwa kuathiri mipango yako. Kwani mwenzetu wafanyakazi masaa mangapi bana? Najua, idadi kubwa waliopo Ughaibuni hujitutumua kufanya double jobs (totalling 14- 16hours a day)...
Hao siwalaumu sana.

Ila kama una familia ughainbuni, ina maana wanao wanaishia kucheza na X-box, wakati mke anakesha aki reminice na Facebook friends. Hali ya maisha ughaibuni si mchezo, lazima kujipinda kisawasawa mkono uende kinywani, lasivyo waweza rudisha familia Bongo!
Hata hivyo, hiyo haiondoi ukweli kwamba unastahiki kwa masaa machache (unapokuwa off,) kwenda kufanya ibada, kutembelea marafiki, na kuspend Quality time na wanafamilia.

'Kubondwa bondwa' na haya maboksi kiasi kwamba muda unaopata ni kuitumikia pauni au dolari, na kulala... ina maana ipo siku afya itakuletea mgogoro, wakati huo tayari wewe na familia yako mwaonana strangers!...Hapo lazima Depression nayo itagonga hodi.

Tujipangie tu muda bro, hatuna jinsi...muda utatosha tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom