Maisha Vs Muda,...Unatosha?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maisha Vs Muda,...Unatosha?!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mbu, Jun 30, 2011.

 1. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  The wheel of life is a valuable tool to help you evaluate what's working and what's not working in your life.

  ...ni kawaida kusikia mtu anakujia na excuse ya,."..sikuwa na muda!"...lakini je? huwa unajipangia mambo yako kwa mujibu wa muda, au ndio umejikubalisha muda utawale sehemu kubwa ya maisha yako?


  Evaluate maisha yako kisha ujiulize;

  • una muda wa kutosha kukaa na kubadilishana mawazo na familia yako? Unawasaidia watoto homeworks zao, kujua maendeleo yao kimaisha? ...vipi kutembelea ndugu, jamaa na marafiki?
  • una muda wa kutosha na mpenzi/mke/mume wako, ...mwenza wako halalamiki hutulii nyumbani?
  • umejiwekea muda wa kutosha kujiburudisha akili, hii ni recreational activities hata kama ni kwa kibustani cha mboga..., michezo etc? , una muda wa kutosha kufanya ibada?
  • una muda wa kutosha kujiangalia afya yako, kufanya mazoezi, regular check ups? au mpaka uumwe ndio unakwenda hospitali?
  • Una muda wa kutosha kufanya kazi zako bila kuelemewa na kurudi nazo nyumbani? Wengine 'hushikika' hata kula wanasahau. Nawe ni mmoja wao?


   [​IMG]

   "You can have anything you really want but you cannot have everything you want."

   [​IMG]

   "To know yourself is the first and most important step to pursuing your dreams and goals." – Stedman Graham
  Badala ya kulaumu hali ngumu, jilaumu mwenyewe kwa kushindwa kujipangia yaliyo na umuhimu katika maisha yako. Kila siku iendayo hairudi Nyuma. Usilolifanya leo na kuliweka kiporo kwa kisingizio utalifanya kesho jua umeshaharibu mtiririko wa mpangilio wa maisha yako. Jiepushe kulimbikiza shughuli.

  Liwezekanalo kufanyika leo, usilisubirishe. Ni wangapi kufumba na kufumbua wamejishtukia tayari retirement age ishawafikia ilhali hawakukumbuka kuwekeza?

  Fainali uzeeni!....tusisubiri kukurupushwa ilhali kushakucha!...Hakuna awezaye kukupangia mkaisha yako ila wewe mwenyewe. Tuanze kujipangia maisha yetu kuanzia sasa kisha mtaona uwiano mzuri wa maisha, furaha, amani na mapenzi yanavyorudi tena majumbani mwetu.
  Otherwise,

  kwanini unaamini hauna muda wa kutosha (ku balance maisha yako?)
   
 2. Mayasa

  Mayasa JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 587
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ngoja niisome kwa makini niangalie wapi panapwaya.. Asante sana kwa kutukumbusha!
   
 3. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #3
  Jun 30, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  It is a very good advice and remainder Mbu........Seriously wengi wetu hatuna huo utaratibu wa kupangilia kila kitu kama hiyo Wheel of Life inavyofanya...........but mbona inaonekana kama inadefine maisha toooo serious?! what about tose adhocs zinazotokea in-between? where do we put them?
   
 4. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160

  ...hebu weka na mifano basi naweeeeee....lol!
   
 5. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #5
  Jun 30, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Lol maisha yetu wengine mwenzangu mh......unapanga weekend uende beach na mtoto mara wapigiwa simu ijumaa jioni unatakiwa kusafiri Ntwaraaaaaaaaa........... miezi miwili!! Ukirudi wakuta meza inakusubiria na mkoloni ndo kasimama tititi!! kutahamaki miezi miwili hujaonana na rafiki wala kukaa na familia!
   
 6. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...habibty,...nimeishiwa kauli hapa.
  Sasa hiyo ni job enrichment au ni kukomoana?

  So, how do you cope with that situation?
  si umeona nimeandika hakuna awezaye kukupangia maisha, ni wewe mwenyewe?

  Binafsi una maoni gani ku balance angalau kidogo maisha yako?
  si wajua maisha ni mlingano,...ukielemea zaidi upande, ukaupunja mwingine
  kuna athari zake baadae?

  Hebu tujadiliane...
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Jul 1, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Actually Mbu najialumu sana mwenyewe kwa kuweka mbele career and finance ambavyo vimekula kabisa siritual, personal growth, health

  relationship na family navyo nisipokua makini vitanitupa mkono

  I am going to try something to reverse this... the only challenge ni kazi/career success na pesa... they are more addictive than anything i have ever experienced
   
 8. The great R

  The great R Senior Member

  #8
  Jul 1, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  I appreciate MBU mana kuna watu wanahangaika mabo kwenda kombo kumbe hawakua wakijua ho wthey are suppose to go about
   
 9. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #9
  Jul 1, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145

  Ni kweli lakini Mbu ukiangalia kiundani zaidi ni wazi kuwa kila kitu kiko mikononi mwetu!! If we strictly stick to our job description (kwa walioajiriwa) ni wazi kuwa utawezajipangia na kuweka limit ya ufanyaji wako wa kazi but kwangu mimi (Sijui wengine) najikuta kwenye dilema kwa kuwa kuna kale kamstari kasemako......and any other work assigned by my employer...yaani hii inanifunga hata akinambia unatakiwa kuja jumamosi au uunganishe safari juu kwa juu hata miezi miwili nashindwa kumwambia siwezi.......nilisign mwenyewe ule mkataba ujue!!
  But I think there is a need to reflect some aspects!

  But kitu kingine ni how do we get satisfied?? especially ukiwa na kazi ambazo yaani zinalipa? mfano safari zenye per diems nzito na masurufu mengineyo (Posho za kibunge lol) how can we sacrifice that only to spend some quality time with our loved ones?
  Mwe!! Mtihani
   
 10. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #10
  Jul 1, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  MTM cmn bana I know you
  You have a lot to share with us in this thread.....tell me how can we balance hii wheel aisee?
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Jul 1, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  shem, what can i say??
  ....this is a very good reminder about our life purpose, the only challenge niionayo ni ile definition ya success kwa community zetu, including those we love most... what if i balance all of them and end up with less income and stunted career path, my love may never give me the same respect

  its a challenge really, especially now you find in many couples wote wanakua career people
   
 12. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #12
  Jul 1, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Hii hali inawapata watu wengi sana wenye kazi/majukumu yenye kuwategemea sana hasa middle and senior cadre of workers/experts. Ndio maana taasisi nyingi zenye malipo makubwa kitu kikubwa kinachowafanya wawe "waajiri wabaya" ni ile work-life balance.They scored very poorly hadi wanatafuta hadi mikakati ya kuimprove na inashindikana maana ule mzunguko wa kazi uko palepale!

  Tukiacha mchango wa waajiri katika kukosekana balance, kuna upande mwingine pia ambao unachangiwa na familia zenyewe. Huwa nasema wazee wetu waliostaafu ambao walitulea kwa kipato chao walichokipata kwenye mishahara na ambao hawakujisikia kusukumwa kuongeza kipato, walifanya vizuri kuliko siye wa zama hizi za kukimbiza shilingi isiyokamatika!

  Mwanao MTM leo anataka "toys" ambazo siyo toys bali ni "hi-tech gadgets" zinazouzwa mamilion ya shilingi, umlipie ada ya mamilioni, atoke kutembea na kuburudika kwa gharama kubwa, akifunga shule aende holiday,avae mavazi yaendanayo na world trends.... the list is long!

  Mamaa naye anataka aishi maisha mazuri, mjenge au mpangishe nyumba ya kiwango, usafiri wa binafsi, maisha bora kwa kifupi.Je usipochacharika unadhani familia itakuwa na amani na wewe? Je unadhani utajivunia heshima kwa ndugu jamaa na marafiki kwa kutokuhangaika... nikimaanisha urudhike na kipato cha kijungu-jiko kisichokuweka kwenye level ya wewe kujiskia confident kujichanganya nao?

  Ukija kwenye kujijali afya, ukiwa huna pesa ( unayoitafuta kwa kujinyima muda wako na kuuwekeza kwenye kazi) utamudu AAR na bima nyingine za afya assuming haulipiwi na muajiri.

  Nina mengi ya kuchangia kwenye hili kuonyesha its becoming almost impossible kuligawanya hilo gudumu alilotuwekea MBU na kutoa nafasi sawa.

  Ninapoandika huu mchango wangu, nimekumbuka video moja tulionyeshwa miaka ya nyuma kuhusu management and leadership kwa kifupi ikionyesha baba aliyejitesa sana kutafuta ili aipe familia yake maisha mazuri.Katika kimbizana hiyo akaja kupata heart attack akafa! Alipokufa akaenda mbele ya Muumba, na akaulizwa jitetee kwanini upate paradiso na siyo jahanamu.Utetezi wake ulikuwa kwamba alihangaikia sana familia yake hadi akajikuta umauti unamfika!

  Cha ajabu na kilichonishtua ( miaka ile) ni kwamba Muumba alimuuliza tena " je una uhakika familia yako ilifurahia hali hiyo?" Akajibu ' nina uhakika maana hawakukosa chochote walichohitaji".
  Muumba akamwambia " subiri tuthibitishe kama kweli familia yako ilirIdhika". Ikaonyeshwa Re-play ya maisha ya yule bwana na familia yake...jamaa alishtuka kuona jinsi mkewe alivyokuwa ananung'unika kwa vile muda mwingi hayuko nyumbani hata pale alipokuwa na watoto wadogo, watoto walipoumwa, mke alipoumwa, yalipotokea matatizo mbalimbali kwenye familia etc. Kisha akaonyeshwa jinsi hakuwepo kuona wanae wakikuwa kwa haraka, wakianza shule, wakifanya homework na kushiriki michezo mbalimbali.Watoto walihudhunika baba hakuwepo kuwapa support nk.

  In short jamani hakuna jema.Haya maisha ya sasa ni ubatili mtupu!

  Mimi mwenyewe ninajiangalia na kujiuliza itakuwaje kama naulizwa maswali aliyoulizwa huyo bwana hapo juu. Je na nyie wengine majibu yenu yatakuwa vipi?
  Je mtastahili paradiso?
  Pole kusoma kitu kirefu lakini ni vema kushirikishana.
   
 13. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #13
  Jul 1, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Umeona eee shem!
  Lakini ni nzuri kweli kwa afya yetu but mh..........halafu kuna kitu nimekigundua hawa waajiri wetu wanatufanyia.....ukiwa unafanya kazi kama umetumwa na kijiji basi utatupiwa kila kitu................. matokeo yako mzigo mzima wa shirika unakuwa mgongoni mwako! wakati wengine wanakula maisha na familia zao wewe unabebeshana na malaptop hadi nyumbani weekend !!
   
 14. Tulizo

  Tulizo JF-Expert Member

  #14
  Jul 1, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 849
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Thanks for a very useful remainder.

  Hicho ulichosema hapo juu ni dream life ya kila mtu. But let's review the constraints. Kwa nini tunashindwa? ni jamii? mazingira? Partnership na wapenzi wetu? Kama tutaweza kutambua hizo contraints za hapo itakuwa tumepiga step one ya kuelekea kwenye "dream life" ..naweza sema hiyo ndiyo real life..hii nyingine ni ubabaishaji..Watu wengi tunatoa sababu za kiuchumi..lakini ni wangapi wana hela na maisha mazuri lakini hakuna anayejali kama mtoto ana homework? etc..

  Nakubaliana na wewe.. tunaweza na tusisubiri kesho.
   
 15. Romance

  Romance JF-Expert Member

  #15
  Jul 1, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 587
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kweli jf kisima cha elimu.
   
 16. CPU

  CPU JF Gold Member

  #16
  Jul 1, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Aiseee . . . . Ngoja
   
 17. CPU

  CPU JF Gold Member

  #17
  Jul 1, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Yaani we acha tu Humu ndani unaweza kupata wake na waume wazuri
  Ona mfano wa Miss J anakuwa mke muda si mrefu
  Ila asipobadilika . . . . . . daaaaaaah
   
 18. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #18
  Jul 1, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,920
  Likes Received: 23,558
  Trophy Points: 280
  I am a failure when it comes to balancing my time..... All blames to TBL/SBL. Why on earth are they brewing this kind of drinking liquid? ...When I get out of my office the only thing in my addicted mind is Beer......... and only Beer!
   
 19. Romance

  Romance JF-Expert Member

  #19
  Jul 1, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 587
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Yule miss J ndoa ndio dawa yake mana pale hakuna mjanja inaonekana anaingia katika ile ndoa akiamini 1+1=2 kumbe hakuna hio kule jibu ni 11.
   
 20. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #20
  Jul 1, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,658
  Likes Received: 8,211
  Trophy Points: 280
  Duh..gurudumu langu haliendeshi hata mkokoteni...needs big tym fixing!
  Thanks Mbu...leo umetoa tiba badala ya maradhi!
   
Loading...