Mambo yaliyopita na yajayo yote ni taswira zijengekazo katika fikra ambazo si hai

Lord genesis

Member
Jan 3, 2024
25
47
Ukijifunza kuudadisi kwa undani na kwa muono usio na attachment wala judgement msongo wako wa mawazo si kitu ambacho kipo kwenye uwepo, coz uwepo wako na kipindi ambacho unathibitishwa ya kuwa upo ni SASA (NOW). Lakini ukiichunguza stress yoyote iliyomo kichwani mwako utagundua ni msongamano wa mambo yaliyopita (PAST) na matarajio ya mambo yajayo (FUTURE).

Mambo yaliyopita na yajayo yote ni taswira zijijengekazo katika fikra ambazo si hai, si hai kwasababu haupo tena kwenye kwenye wakati uliopita, wewe wa jana umeshakufa huwezi kufufuka kamwe, je unaweza kuitumia leo kubadilisha ulivyoishi jana?, jibu lipo wazi. Pia hvyo hivyo hakuna nguvu yoyote iliyopo jana iwezayo kukuzuia kutokuishi maisha yako yenye uwepo kamili leo ndani ya wakati huu uliopo ambao ndio MAISHA.

Maana yangu ni kwamba kubaki na AMANI, FURAHA, MSAMAHA (KUSAMEHE NA KUJISAMEHE) kuhusu mambo yote yaliyopita ndio kuingia kwenye kuthibitika kwako kwenye uwepo kamili na maisha.

Vilevile kwa wakati ujao ukitaka ufike mahala hutakiwi kuweka attention yako yote huko uendako na kusahau kuwa makini na hatua zako unazozipiga ili kufika huko utapotea tu.

Maisha yetu yanasongwa na matatizo ambayo yanatokana na mawazo ya visasi, chuki, huzuni, uchungu, wivu, sifa, majigambo, hofu, tamaa na uoga ambavyo si MAISHA ila ni KIFO, ni kifo kwakuwa asili yake sio wakati uliopo ila past and future kifupi vinatokana na hamna. Coz maisha ni here and now but matatizo yetu yote huletwa na PAST and FUTURE vipindi ambavyo havipo kabisa ndani ya maisha. Kwa kifupi tunaleta matatizo kwenye maisha yetu kwa kuyahusisha na mambo ambayo yapo nje ya maisha, yani ni sawasawa na kumtoa samaki ndani ya maji na kumuweka nchi kavu.

Utambulisho wa mtu ni wa ndani yake jinsi awazavyo na anavyohisi ndani yake kuhusu yeye ndivyo maisha yake ya nje yanavyokuwa. ni wazi kuwa chochote ambacho kipo kinahitaji makazi mfano. miili yetu inahitaji makazi rafiki kwa ajili ya survivor. pia mawazo na hisia zetu huitaji kuishi ndani ya wakati uliopo ili maisha yetu ya ndani yaende sambamba na amani msamaha upendo na kusudi la uwepo wetu.

Mtu ni SASA, popote unapotamka neno MIMi au I' AM huwezi kulitenganisha na present time because you refer to your PRESENCE/NOW. Ukitaka furaha na amani inakupasa kuishi kwenye maisha yako na kuwa wewe halisi kuambatanisha hisia na mawazo yako kwenye SASA badala ya kujutia JIFUNZE sasa na badala ya kutarajia KUWA sasa.

Ishi leo tengeneza hatua nzuri leo weka mawazo yako kwenye leo kwenye wakati huu wa sasa, mfano ukiwa unasafiri kutoka sehemu A kwenda B, kuyagandisha mawazo yako sehemu A ni kutokukua, kutokujongea kutokustawi na kutoendelea ni sawa na kuwa SANAMU YA CHUMVI.

Pia kuweka attention yako yote sehemu B na kusahau kuwa makini na hatua zako unazopiga sasa hivi hakika utapotea tu, safari yako haitakuwa na maana, hatua sahihi ndizo zitakazokufikisha sehemu B.

Vivyo hivyo kwenye maisha ni kuweka nguvu kwenye kuishi sasa kuwa kwenye uwepo wako kikamilifu( love, peace, joy, truth and forgiveness) li uwe responsible na kila nafasi unayoipata kwenye maisha yako ili uifikie maana ya maisha yako.

MIMI NDIMI NJIA KWELI NA UZIMA( UWEPO WAKO KAMILI NDIO NJIA KWELI NA UZIMA).
 
Back
Top Bottom