SoC01 Maisha si leo tu, Utawala Bora unaanzia nyumbani

Stories of Change - 2021 Competition

etton1999

Member
Oct 28, 2020
5
2
“Most people do not really want freedom, because freedom involves responsibility, and most people are frightened of responsibility.”

Sigmund Freud

”Watu wengu hawataki uhuru wa kweli, sababu uhuru unahusisha jukumu, na watu wengi wanaogofya jukumu”

Sigmund Freud​

Wakati tunaendelea na taratibu za kila siku za utafutaji wa mali na chakula, wacha nikushirikishe jambo moja adimu sana ambalo wengi hawafundishi na kupata wanaofundisha ni wachache sana, na huenda ukachukizwa lakini utaelewa kwa sababu utapona. Maisha yako haya uliyonayo yanatokana na maamuzi, na fikra zako ulivozipeleka, yaani matokeo ya maisha ya sasa ni vile wewe ulikua unafikiria hapo awali labda ulijiona ni mdogo sana hata ushindwe kufanya jambo fulani la maemdeleo ama uliona wanaokutawala wanaweza kuishi milele.

Sasa ni hivii maamuzi yanayofanyika sasa pia ndio maisha ya baadae ebu geuza fikra zako na utafakari chanya juu ya maisha ya baadae kuna jambo lenye maendeleo wahitajika kulifanya anza sasa maana itapofika wakati wenyewe wa kutimilika hilo swala utashindwa maana utaanza kukumbuka ulivyopoteza awali badala ya kutazama hilo jambo na ulitimize, mfano wa mwanafunzi wakati aliambiwa soma kwa bidi yeye akazembea alipowatazama rafikize wanasoma kwa bidii alijipa moyo na kusema ”siku za mimi kusoma bado hazijafika mitihani ikikaribia nitasoma na nitafaulu” baada ya muda kuendelea hatimaye siku ya mtihani ilifika na akajikuta anahitajika asome vitu vingi kwa muda mfupi vitu ambavyo angelipambana navyo hapo awali bhasi angekuwa na wakati mzuri wa kusoma vitu vichache ama kujikumbushia pekee, alipoingia ndani ya mtihani akiangalia kila swali anaona linamshinda na akikumbuka alishawahi kuona majibu yake kwenye kitabu ila haliwezi kujibu ndipo anaacha kufanya mtihani na kuanza tafakari ” ningelisoma hapo awali ningelishinda hili swali na mtihani mzima” pia anaanza kukumbuka maneno ya waliokua wanasema nae kuhusu kusoma hatimaye saa zinazidi kwenda na muda wa kuandika mtihani unatimilika hata hakuna cha maana alichojibu kwenye mtihani mzima.

”WAKATI WA AMANI NDIO WAKATI WA KUTENGENEZA AMANI, LAKINI WAKATI WA VITA NI WAKATI WA HUZUNI, MAJONZI NA MANUNG’UNIKO MENGI”​

Wakati uliokubalika ni sasa wa kuanza kuandaa mabadiliko kwa wakati ujao na hata wakati huu pia maana ufanyapo jambo linamatokeo ila usipofanya hakuna matokeo yatatokea, usisubiri aliye juu yako akuamulie maana hatakaa juu milele ipo siku ataanguka nawe utapaswa kuwa juu je ni nani atakuamulia kwa huo wakati.

Kila mtu anayeonekana kwenye huu ulimwengu amezaliwa na amelelewa na kikundi cha watu iwe ni wazazi, ndugu ama jamii inayomzunguka. Nataka kusema mtawala anayeonekana kwenye kila juu ya kiti amelelewa na watu na aina ya hao watu ndio wanaomfanya aonekane vile alivyo, kama wazazi ndugu na jamii ingekua inapata wasaa wa kueleza watoto wao namna waweza kuishio na watu wengine kwa kutenda haki kwa jamii ya karibu na mahali pote waendako.

Jamii zetu kiujumla zinamfundisha mtoto atakapokua kua ajali kwanza watu wa nyumbani mwake kuliko wa nje, tena anapoanza kuingia darasani tu huyu mtoto anafundishwa kusoma kwa bidii ili aje aikomboe familia yake kama sio familia yake basi asome ili aje ajikomboe mwenyewe kwenye maisha yake.

Siku moja mtoto alikua anatembea na mamaye njiani walikutana na mtu anayeokota mabobo ya plastiki ( chupa za plastiki) yule mtoto alimuuliza mamaye ”eti mama kwanini huyu mtu anaokota chupa walizotupa watu njiani?” mama wa mtoto akamjibu ”soma mwanangu ili usije kuwa kama huyo yeye hajasoma ndio maana anaokota chupa zilizotupwa na wengine njiani”.

Yule mtoto alikutana na rafikize shuleni akawambia ”msome msije kuwa kama muokota machupa” mwalimu alikua karibu yake akawaambia ”someni ili muweze kuwasaidia waokota makopo wasiokote tena”.

Tuwafundishe watoto wetu maisha ambayo hata baadae hayatoleta shida kwa watu wengine wataokuja kuwaongoza, viongozi tulionao sasa ni matokeo ya kile walichoambiwa na jamii zao hapo awali. Wanatimiza kile walichoambiwa sio tatizo lao binafsi, wamejengwaje. Na vile wapo chini ya muongozo usiowabana lazima watimilize kile walichoelekezwa kuwa ni sahihi kutoka kwa jamii na wazazi wao.

Sasa ili kupunguza ama kuondokana na tatizo hili linalosumbua jamii kubwa ya Waafrika lazima torati/ sheria za utawala zibadilike na ziwe ngumu zenye uelekeo wa kusaidia jamii nzima na si ile sheria inayompatia mamlaka makuu mtawala. Sheria zetu inabidi ziipe mamlaka sawa ama mamlaka makuu wananchi/ jamii tawaliwa yenye vipaumbele visivyobadilika ambavyo mtawala yeyote atapoingia asimame katika hivyo wala si kama vile ilivyo sasa mtu mmoja anaamua ni nini cha kufanya juu jamii nzima ndipo hapo unakuta anafanya vile ambavyo alifundishwa na wazazi wake, lazima kujitoa kama wananchi tunao hitaji uhuru wa kisheria na utawala bora. Leo inajengwa inapoanza, kesho inajengwa na leo. Siku zijazo zinajengwa na kizazi hiki, tengeneza uzao unaochipukia ili ukutunze baadae hata uwe msaada kwa jamii nzima nao wapate kukubariki kutokana uzao wako.

“These then are my last words to you. Be not afraid of life. Believe that life is worth living and your belief will help create the fact.”

William James

“Most people do not really want freedom, because freedom involves responsibility, and most people are frightened of responsibility.”

Sigmund Freud​
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom