MAISHA: Nilinusurika kwenda Jela baada ya mke wa mtu kuoenekana kama kafia kitandani kwangu (sitasahau)

Kudo

JF-Expert Member
Nov 2, 2017
1,809
6,081
Nimejikuta naikumbuka siku kama ya leo miaka mitatu nyuma nilivyonusurika kufungwa kwa kifungo cha kunyongwa ama maisha ama miaka thelathini kulingana na upelelezi ambao ungetoa majibu ya hatia iliokuwa ikiniandama wakati huo.

Inshu ilikuwa hivi....

Nilikuwa na rafiki yangu wa damu yani nikisema damu namanisha kweli yani wa kufa na kuzikana langu lake lake langu.

Tulikuw wote tangu utoto na hadi utu uzima wa miaka ya kuwa watu wazima huku shule zote tukisoma pamoja na tukaja kuachana baada ya kuhitimu kidato cha sita mi nikaenda kujiunga na idara flani ya ulinzi hapa nchini nae akaendelea na masomo ya chuo kikuu...
Badae nikapata matatizo flani huko nilikokuwa nimeajiriwa na nikawa nipo bila kazi huku nikijaribu kutafuta maisha kwa elimu yangu ya kidato cha sita na nikafanikiwa kupata mkoani Dodoma kama afisa mwajiri kampuni flani ya kizungu (ina tawi Dodoma)

Rafiki yangu alimaliza chuo na hakuwa na pa kwenda wakati akisubiri ajira na hapo nikaamua kumchukua na kuishi nae huku tukijaribu kuona namna gani atapata kazi wakati akingoja ajira.

Sasa kutoka kwangu ni Ahsubuh na kurudi jioni kila siku,rafiki yangu nae akapata wenyeji na akaanza kutembea na mke wa mtu mtaani pale nilipokuwa nikiishi na walikuwa wakikutana pale kwangu kwa siri bila mimi kujua...

Waliendelea hivyo hadi siku mbaya ilipokuja kutokea na kufanya lizuke tatizo kubwa sana siku hiyo.

Tofauti na siku zote ambazo huwa narudi jioni sana ila siku hiyo nilirudi mapema baada ya kuwa nimejisikia vibaya na nikaona siwezi kuendelea na kazi.

Nilikuta mlango upo wazi bila kufungwa,sikujali sana nikapita hadi sebleni na kujitupa kwenye kikochi chakavu kilichokuwa pale sebuleni kwangu ila nikaona viatu vya kike vimetupwa chini na kufuli la kike lilikuwa chini,nikaita jina la rafiki yangu bila mafanikio nikaamua kwenda chumbani mana nilihisi hali si nzuri pale ndani..

Macho yangu yakatua juu ya mwili wa mwanamke akiwa uchi juu ya kitanda changu huku povu jingi likimtoka mdomoni, nilichanganyikiwa kwa picha ile pale ndani.
Ili kujiweka mbali na ushahidi walau kidogo nikachukua mfuko mdogo wa rambo na kuuvaa, kisha nikamsogelea yule mwanamke na nilipomgusa sehemu kadhaa za mwili wake nikastuka zaidi hakuonesha dalili ya uhai.....

Nilipagawa sana huku nikishindwa cha kufanya,Mara nje mlango ukagongwa kwa fujo...

Nikajivika ujasiri wa kioga huku nikitetemeka nikatoka sebleni na kabla sijaufikia ule mlango wakaingia wanaume wawili wakiwa wamevaa mavazi ya kijeshi...

Mmoja akanitazama kwa gadhabu,kisha akaniuliza

"mke wangu yuko wapi?"
Niligwaya jama..
Baada ya malumbano mengi kati yangu na wale jamaa hatimae wakaviona vile viatu na chupi,mara moja jamaa alieonekana kuwa ndie mwenye mke akakimbilia chumbani kwangu na gafla nikasikia kishindo cha mtu kuanguka sote tuliokuwa pale sebuleni tukaelekea huko

Yule mwanajeshi alikuwa ameanguka chini na kuzimia baada ya kuona mkewe yupo uchi kitandani kuashiria alikuwa anakazwa...

Mwanajeshi mwingine nae akataka kunikoromea zaidi,huku akinitishia kuwa nimeua mtu na mkewe....

Nikaona nikizubaa zaidi yatanifika makubwa ikabidi nitumie utalamu kidogo kumdhibiti yule mwanajeshi mana alianza kusumbua kwa kuchanganyikiwa hasa kwa matukio anayoyaona mle ndani...
.watu nje wakaanza kujaa bada ya kusikia kelele za hapa na pale mle ndani kwangu...

Punde wakaongezeka wanajeshi wengine wawili ambao nadhani walikuwa nje lengo ni fumanizi pale kwangu...

Wakashangaa mwenzao yupo chini huku nikiwa nimemdhibiti mwingine ikabidi watumie maarifa ya mazungumzo sio vita...
Nikawaelekeza kwa kifupi hali halisi na hapo muafaka ukawa ni kupiga simu polisi ambao sikuwa naishi nao mbali na punde wkafika....hapo itifaki ikazingatiwa na nikawekwa chini ya ulinzi na kisha nikawekwa kwenye karandinga na wale wengine wakipelekwa hospital ya mkoa...

Mengi yalitokea bada ya hapo ila muda wote yule rafiki yangu hakuonekana na wala sikujua alipo,ndugu pekee wakawa ni wafanyakazi wenzangu waliopigana kufa na kupona ili nitoke hasa baada ya yule mwanamke kuzinduka na alisemekana alikuwa na ugonjwa wa kifafa na yule mumewe nae alirejewa na fahamu... Ila majirani walisaidia bila kinyongo kuwapa ushirikiano polisi na kuweka bayana kuwa mimi sikuwa na mpakuwa mke wa yule jamaa bali ni mtu niliekuwa naishi nae...

Ila pia kozi kadhaa nilizopitia zinaeza kuwa zilinisaidia kununua ujasiri flani wakati wa tukio sijui mtu wa kawaida angelikuwaje....

Lakini niwaombe vijana wenzangu ishi vizuri na watu hasa majirani na watu unaofanya nao kazi ipo siku wema wako utakulipa...
Hakuna ndugu yangu ambae alifika na pia sikutaka mama yangu ajue mana anaugonjwa flani ambao naamini ungemtoa uhai endapo angelipata taarifa za hayo masahibu yangu mana yale yalionikuta wakati nafanya kazi ya kwanza yalimuweka hospital mara kadhaa....

Namshukur pia afande mmoja tuliewahi kukutana miaka ya nyuma na siku hiyo tulikutana akiwa na wadhifa kidogo nami ni mtuhumiwa bado alisimama kuhakikisha askari njaa hawanihujumu....

Kuweni makini na wake za watu jamani.......
 
Ukitaka kujua hii ni chai. Tanzania hakuna wanajeshi wastaarabu kiasi hicho. Lazima wangekula kwanza 0713 alafu mengine yangefuata.
Kama waliwahi kukutigo sishangai hii ikiwa ni chai mana unawajua sana bila shak
 
Back
Top Bottom