MAISHA: Nilinusurika kwenda Jela baada ya mke wa mtu kuoenekana kama kafia kitandani kwangu (sitasahau)

Inamafundisho lkn kwangu mm inamapungufu mengi ili niiamini kuwa ni stori iliyokutokea kwa mtiririko huo.
 
Ndo maana fidi q alisema siitaji marafiki kwa usela wa kishamba kama huu pole mkuu ni mapito ya dunia haya.
 
Naona watu wanaongea mengi kuhusu wanajeshi mara oooh wasingekuacha mara umeongeza chumvi suala ni kwamba *mke wa mtu sumu*
 
Nimejikuta naikumbuka siku kama ya leo miaka mitatu nyuma nilivyonusurika kufungwa kwa kifungo cha kunyongwa ama maisha ama miaka thelathini kulingana na upelelezi ambao ungetoa majibu ya hatia iliokuwa ikiniandama wakati huo.

Inshu ilikuwa hivi....

Nilikuwa na rafiki yangu wa damu yani nikisema damu namanisha kweli yani wa kufa na kuzikana langu lake lake langu.

Tulikuw wote tangu utoto na hadi utu uzima wa miaka ya kuwa watu wazima huku shule zote tukisoma pamoja na tukaja kuachana baada ya kuhitimu kidato cha sita mi nikaenda kujiunga na idara flani ya ulinzi hapa nchini nae akaendelea na masomo ya chuo kikuu...
Badae nikapata matatizo flani huko nilikokuwa nimeajiriwa na nikawa nipo bila kazi huku nikijaribu kutafuta maisha kwa elimu yangu ya kidato cha sita na nikafanikiwa kupata mkoani Dodoma kama afisa mwajiri kampuni flani ya kizungu (ina tawi Dodoma)

Rafiki yangu alimaliza chuo na hakuwa na pa kwenda wakati akisubiri ajira na hapo nikaamua kumchukua na kuishi nae huku tukijaribu kuona namna gani atapata kazi wakati akingoja ajira.

Sasa kutoka kwangu ni Ahsubuh na kurudi jioni kila siku,rafiki yangu nae akapata wenyeji na akaanza kutembea na mke wa mtu mtaani pale nilipokuwa nikiishi na walikuwa wakikutana pale kwangu kwa siri bila mimi kujua...

Waliendelea hivyo hadi siku mbaya ilipokuja kutokea na kufanya lizuke tatizo kubwa sana siku hiyo.

Tofauti na siku zote ambazo huwa narudi jioni sana ila siku hiyo nilirudi mapema baada ya kuwa nimejisikia vibaya na nikaona siwezi kuendelea na kazi.

Nilikuta mlango upo wazi bila kufungwa,sikujali sana nikapita hadi sebleni na kujitupa kwenye kikochi chakavu kilichokuwa pale sebuleni kwangu ila nikaona viatu vya kike vimetupwa chini na kufuli la kike lilikuwa chini,nikaita jina la rafiki yangu bila mafanikio nikaamua kwenda chumbani mana nilihisi hali si nzuri pale ndani..

Macho yangu yakatua juu ya mwili wa mwanamke akiwa uchi juu ya kitanda changu huku povu jingi likimtoka mdomoni, nilichanganyikiwa kwa picha ile pale ndani.
Ili kujiweka mbali na ushahidi walau kidogo nikachukua mfuko mdogo wa rambo na kuuvaa, kisha nikamsogelea yule mwanamke na nilipomgusa sehemu kadhaa za mwili wake nikastuka zaidi hakuonesha dalili ya uhai.....

Nilipagawa sana huku nikishindwa cha kufanya,Mara nje mlango ukagongwa kwa fujo...

Nikajivika ujasiri wa kioga huku nikitetemeka nikatoka sebleni na kabla sijaufikia ule mlango wakaingia wanaume wawili wakiwa wamevaa mavazi ya kijeshi...

Mmoja akanitazama kwa gadhabu,kisha akaniuliza

"mke wangu yuko wapi?"
Niligwaya jama..
Baada ya malumbano mengi kati yangu na wale jamaa hatimae wakaviona vile viatu na chupi,mara moja jamaa alieonekana kuwa ndie mwenye mke akakimbilia chumbani kwangu na gafla nikasikia kishindo cha mtu kuanguka sote tuliokuwa pale sebuleni tukaelekea huko

Yule mwanajeshi alikuwa ameanguka chini na kuzimia baada ya kuona mkewe yupo uchi kitandani kuashiria alikuwa anakazwa...

Mwanajeshi mwingine nae akataka kunikoromea zaidi,huku akinitishia kuwa nimeua mtu na mkewe....

Nikaona nikizubaa zaidi yatanifika makubwa ikabidi nitumie utalamu kidogo kumdhibiti yule mwanajeshi mana alianza kusumbua kwa kuchanganyikiwa hasa kwa matukio anayoyaona mle ndani...
.watu nje wakaanza kujaa bada ya kusikia kelele za hapa na pale mle ndani kwangu...

Punde wakaongezeka wanajeshi wengine wawili ambao nadhani walikuwa nje lengo ni fumanizi pale kwangu...

Wakashangaa mwenzao yupo chini huku nikiwa nimemdhibiti mwingine ikabidi watumie maarifa ya mazungumzo sio vita...
Nikawaelekeza kwa kifupi hali halisi na hapo muafaka ukawa ni kupiga simu polisi ambao sikuwa naishi nao mbali na punde wkafika....hapo itifaki ikazingatiwa na nikawekwa chini ya ulinzi na kisha nikawekwa kwenye karandinga na wale wengine wakipelekwa hospital ya mkoa...

Mengi yalitokea bada ya hapo ila muda wote yule rafiki yangu hakuonekana na wala sikujua alipo,ndugu pekee wakawa ni wafanyakazi wenzangu waliopigana kufa na kupona ili nitoke hasa baada ya yule mwanamke kuzinduka na alisemekana alikuwa na ugonjwa wa kifafa na yule mumewe nae alirejewa na fahamu... Ila majirani walisaidia bila kinyongo kuwapa ushirikiano polisi na kuweka bayana kuwa mimi sikuwa na mpakuwa mke wa yule jamaa bali ni mtu niliekuwa naishi nae...

Ila pia kozi kadhaa nilizopitia zinaeza kuwa zilinisaidia kununua ujasiri flani wakati wa tukio sijui mtu wa kawaida angelikuwaje....

Lakini niwaombe vijana wenzangu ishi vizuri na watu hasa majirani na watu unaofanya nao kazi ipo siku wema wako utakulipa...
Hakuna ndugu yangu ambae alifika na pia sikutaka mama yangu ajue mana anaugonjwa flani ambao naamini ungemtoa uhai endapo angelipata taarifa za hayo masahibu yangu mana yale yalionikuta wakati nafanya kazi ya kwanza yalimuweka hospital mara kadhaa....

Namshukur pia afande mmoja tuliewahi kukutana miaka ya nyuma na siku hiyo tulikutana akiwa na wadhifa kidogo nami ni mtuhumiwa bado alisimama kuhakikisha askari njaa hawanihujumu....

Kuweni makini na wake za watu jamani.......
Duh pole sana mkuu wake za watu ni watamu mno ila tatizo ndo hilo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wanaleta mahitimisho kwa hisia zao tu,hivi fikiria watu wametoka kijiweni tunakwenda kufumania mke,huyu kunguni anayemchukua atatukoma.

Wanafika hapo,wanakuta unshangashangaa tu kuuliza anauliza mmoja mwenye mke anakimbilia chumbani,lengo akute baby amekaa au anavaa,hamad anakutana na picha ya maiti,ule mshituko baada ya gia kibadilikia angani mwenye mke anazimia,huyu mjeshi mwingine akiwa hajapewa jibu kwanini unakula mke wa mwenzake-inabidi ajue sasa kwamba huyo mke ni marehemu na mwenzake pia kaanguka hajitambui.

Kuna wajinga hapa wanadhani wanajeshi wangeanza kukurusha kichura🤩🤩🤩.pole kwa matatizo mkuu,na pia hongera kwa kunasuka kwenye hii kimeo.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana. Umenikumbusha issue za mademu WENYE pepo. Niliwahi chukua demu GETO la mshkaji wangu makini yakatokea kabla sijammega. Nilikimbikia nje, busara ikanituma kumuomba mama mwenye nyumba,aksbonga nayo yakahoji naoa au, nikajibu mie raha tu, yakakataaa. Yule mama tukiwa nje akanishauri siku nyingine kwenye mahaba nisishike nywele za utosini, km ana majini lazima yatokee. Kwa vile mzuri nilijipanga siku nyingine nikaenjoy fuluuuu. Dah, demu alikuwa bora sana lkn si wa kuoa, lkn uvamiwe tu labda uwe na vyombo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ila huwa ni hatari sana kukaribisha watu na kkuishi nao hata kama ni rafiki wengi wameibiwa vitu vyao n wengine wameingizwa matatizoni na hao wanaokaribishwa
 
Wewe ni mmoja ya watu wachache sana hapa duniani wenye bahati. Yaani ulimdhibiti mwanajeshi mmoja chini huku mwenzao mmoja na mkewe wamelala hawajulikan kama hai au mfu then wanajeshi wengine waliokuja kufumania mkawa mnajadiliana kwa utulivu mpaka walipopigiwa simu polisi?

Kudo plz mi huwa nakuheshimu nawe niheshimu hata kidogo. Tunaposoma hiz threads si wote ni division 5 wengine tupo tuna akili angalau kidogo. Tuheshimiane please siyo kutukanana kwa style hii.
😂😂😂😂😂 jamaa chenga kweli, yani mmwajeda wamekuja kufumania yeye akafanikiwa kuwadhibiti bila hata kula mitama? Huyu kuna scene kazificha
 
Ukitaka kujua hii ni chai. Tanzania hakuna wanajeshi wastaarabu kiasi hicho. Lazima wangekula kwanza 0713 alafu mengine yangefuata.
Soma between lines jamaa alimthibiti jamaa mwingine jamaa alikua mtu wa IDARA, maana kwenye mafunzo pia wamo
 
Back
Top Bottom