Maisha ni magumu utadhani nchi iko Vitani

Maisha ni magumu utadhani nchi iko Vitani

My Son drink water

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2016
Posts
4,930
Reaction score
13,333
Hatimaye kesho narudi zangu Perth kuendelea na vibarua vyangu vya kuchunga kondoo.

Hali ya maisha ya Watanzania wenzangu ni ngumu kupindukia. Si mijini wala vijijini pote ni vilio utadhani Taifa liko vitani,watanzania wamekata tamaa na wengi wao wame run crazy baada ya kufilisika Biashara zao na kufukuzwa kazi kwa uonevu eti walifoji vyeti wakati mfukazaji mkuu naye Elimu yake imejaa utata.

Ugumu wa maisha ya Tanzania kwa sasa hauna Tofauti na Burundi na Somalia.

Burundi ukimkosoa Nkurunzinza unapotea Kama ilivyo Tanzania, nimeenda Burundi family nyingi zimepoteza ndugu kwa kuwa wapinzani wa Nkurunzinza.

Hakuna tena pa kushika Tanzania, mzunguko wa pesa umekufa na pesa haina thamani tena. Vijana wamechanganyikiwa kwa ugumu wa maisha huku wakikimbilia CCM ili kusifia wapenda sifa ili wapate kula.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom