jamii01
JF-Expert Member
- Oct 1, 2010
- 1,988
- 1,437
Huwa sipendi kulizungumzia jambo hili lakini pia nimependa kuwashirikisha rafiki JF
Hakuna anayejua historia ya maisha yangu zaidi yangu na rafiki zangu wachache walio karibu sana na jamaa zangu na huwa sipendi kuwa nakumbuka kwa sababu huwa linaniumiza moyo sana.
Nilizaliwa na miaka 37 iliyopita nikiwa simjui Baba yangu wala Mama yangu,Kwa jinsi nilivyosimuliwa na Bibi yangu(japo hakuwa Bibi yangu halisi alikuwa wa kufikia)nilipokuwa na miaka 17 ndipo aliweza kunisimulia,Mama yangu alipata ujauzito wangu akiwa shule ya Secondary kidato cha Tatu,baada ya kungundulika alikuwa mjanzito shuleni alifukuzwa na Baba yangu alimkataa akisema ujauzito siyo wake kwani naye alikuwa mwanafunzi shule moja na Mama yangu.
Mama yangu alirudi nyumbani kwao baada ya kufukuzwa shule,alipofika nyumbani tu Baba yake alimfukuza(ambaye naweza kusema ni babu yangu)Mama yangu aliangaika huko na kule hakuna aliyeweza kumsaidia ndipo alipokwenda kijiji kimoja akakutana na huyu bibi akamsaidia,kilomita 54 kutoka kijijini kwa Mama yangu,bahati mbaya Bibi huyu hakuwai kubahatika kwenda kijijini kwa Mama yangu, baada ya kukaa kwa bibi kwa wiki 3 Mama yangu alijifungua(aliweza kunizaa mimi)kipindi kilipita kama miezi 3 Mama yangu aliugua Malaria akafariki,kwa hiyo Bibi ndiye aliyeweza kunilea japo alikuwa tayari na watoto wakubwa wa kwake waliniliea kwa maisha ya shida sana
Ukweli sikuwahi kutamka neno Baba wala Mama mpaka nilipoanza Darasa la kwanza baada ya kukutana na watoto wenzangu.nilichokuwa nakijua ni Bibi tu..nilisoma kwa shida sana sipendi hata kukumbuka maisha ya namna hile..kaptura zimetoboka,sina viatu,na mahaitaji mengine ya kimaisha kama mnavyofahamu.nakumbuka nikoswa kuuwawa na Mbwa mwitu,Fisi,Nyoka Vitu hivi ilikuwa kawaida kukutana navyo..Nakumbuka kipindi fulani Bibi alinifukuza kwake baada ya mbuzi 3 kupotea nililala siku 3 bila kula zaidi ya matunda pori usiku na mchana.
Kila nilipotoka shule ilikuwa kazi yangu kuosha vyombo,au kukata kuni japo mbuzi nilikuwa nikichunga pia na msimu wa mvua kazi ilikuwa ni kulima..Bibi alinilea kwa maisha ya umaskini wake nami pia niliishi kama mjukuu wake halisi wala hakuweza kunionyesha kuwa mi siye mjukuu wake.
Nilipohitimu masomo ya darasa ya saba nilchaguliwa kwenda kusoma secondary Tabora boys,enzi zile walikuwa wakiita shule za vipaji..baada ya kufaulu ukweli bibi yangu alilia sana akidai hana pesa na atakaa nani na nani atakayemsaidia ukweli alikuwa amekwisha zeeka na nguvu hana alikuwa akihitaji msaada mara kwa mara nilikosa pesa yakwenda kusoma Secondary ilinibidi nimfuate mwl.mkuu wa shule yangu ya msingi nimuombe anisaidie sababu tulifaulu watoto 4 tu kutoka shuleni kwangu.Mwl.alikataa akadai kuwa hana pesa ila atajaribu kuniombea kanisani kwake kama wataweza kunisaidia,ashukuriwe Mungu Mch.wa lile kanisa alikubali nikunisaidia baada ya kuambiwa maisha yangu yote na Bibi yangu..
Nilikwenda kusoma nilipofika form 3 Bibi yangu alifariki nililia kwa kilio cha uchungu sana sikuona maisha mengine.Nikawaza sana kila wakati kwa nini Mungu alinileta duniani kutaabika namna hiii?ilipofika kipindi cha likizo ya December ulikuwa mtihani mgumu sana,nitakwenda kwa nani likizo sina ndugu zaidi ya yule Bibi yangu ambaye sasa ni marehemu huwa namkumbuka mpaka leo na sitamsahau maisha yangu yote.
Mungu waajabu sana wakati kipindi kile nikiwaza vile nitakwenda wapi,nilikuwa nikitafutwa na Mwl.wa zamu kumbe yule Mch. aliyekubali kunilipia gharama za shule alikuja kunichukua niende kwake likizo kwani alikuwa kitokea kwenye semina Musoma.nilikaa kwake likizo ilipokwisha nirudi shule akaendelea kunilipia gharama zangu za maisha kama kawaida,nilitamani wakati mwingine nimjue Bibi yangu harisi ni nani au hata Babu yangu japo alimfukuza mama yangu nilishidwa sababu nilikuwa nimekwisha kuzoea ksema nena Bibi kwa mda wote
Nilifanya mtihani wa form four Nilifanikiwa kufauru kwa division 1.Nilichaguliwa kwenda kusoma Kibaha,yule Mch.alishangaa sana alifurahi kuliko nilivyokuwa nikitegemea kwa mda wote nilikuwa nikaa kwake.ilifikia nikaacha kumwita Mch.Nikaanza kumwita Baba na mke wake Mama..hayo ndiyo majina niliyoanza kuayaita nikiwa na miaka 20 toka nizaliwe,japo kwa mwanzoni niliona tabu sana.Ukweli Baba yangu alinitunza vuzuri kuliko hata Watoto wake wa kuwazaa nislishangaa sana(japo kwa hari ya kibadamu ni ngumu sana)
Baada ya Kusoma kidato cha Tano na Sita nilisoma kama mtoto wa Tajiri na wengine wanafunzi wenzangu na marafiki zangu walijua yule Mch.ndiye Baba yangu halisi,nilikuwa natumiwa pocket money yakutosha kitu ambacho sikuwahi kukiona nilipokuwa secondary..Ugali na maharagwe ndiyo ilikuwa chakula changu kila siku na uji usiokuwa na sukari wakati mwingine(maisha haya acheni tu hayana mwenyewe)
Nimaliza kidato cha Sita ukweli nifauru vizuri sana.Baba yangu alifurahi sana sana..nikaa nyumbani..mwaka mmoja.kipindi nasubuiri niende chuo alipata nafasi ya mie kwenda kusoma Nje,aliniambia nishangaa sana,nilipata chuo nikasoma nikamaliza degree yangu ya kwanza ya engineering nikafanya na pili.nakumbuka wakati naondoka nililia siku nzima kwanza sikuamini nakumbuka miaka ile kwenda kusoma nje ilikuwa si mchezo,na kupanda ndege..hahahaha..
Namshukuru Mungu lipomaliza shule yangu nilipata kazi kwenye Kampuni kubwa sana ya mafuta nilifanya na sasa nilihamia kwenye Company nyingine nikiendelea kufanya kazi.
Mungu ameweza kunibariki ninamke na Watoto 2,ukweli nampenda mke wangu na sipendi maisha nilyopitia na watoto wangu wapitie pia.ni maisha ya uchungu na maumivu makali sana japo kwa hapa naelezea kwa ufupi sana.Mke wangu namchukua ndeye ndugu yangu,Mama yangu,Bibi yangu huwa najisikia furaha ninapomwita majina yote ninayojisikia naye ananifurahia sana.Mungu alinipa mke mwema na mzuri ndiye aliyefuta machozi ya kutabika kwangu.
Mungu amenisaidia namkumbuka yule Mch.(Baba yangu)na family yake ndiyo wazazi wangu wa pili duniani na kila ninapokuja Tanzania likizo basi wale ndiyo ndugu zangu.Japo kwa sasa umri unawatupa lakini bado nawapenda na kuwakumbuka kila mara.
Ukweli ndani ya moyo wangu natamani ni muone Baba yangu halisi japo ni ngumu sana sijui bado yupo hai au la.natamani niwajue ndugu zangu upande wa Mama yangu nilikwisha jaribu nikashidwa..Natamani hata ndugu yangu mmoja afurahie baraka hizi..apate hata kikombe cha maji kwangu ni ngumu kuwapata..na sijui ndugu zangu wanaishi kwenye maisha ya namna gani kwa sasa..ila anayejua ni Mungu peke yake na mara zote huwa nawakumbuka kwenye sara zangu ndugu zangu wote.
Kama unaushari au maswali unaweza kuuliza.
Asante.