bcsolution
JF-Expert Member
- Jun 7, 2013
- 394
- 177
Katika Dunia hii BINADAMU anahangaika asubuhi, mchana na usiku, ukimuuliza kwa nini? Anasema anatafuta maisha.. Maisha gani? atajibu maisha mazuri, ya namna gani? Atajibu nataka: Gari, nyumba, mke/mme mzuri, nk.. Sasa mbona kuna watu wana kila kitu lakini hawana raha katika Dunia hii?
Hebu tujiulize je maisha mazuri ni yapi?
La hasha ngoja nikupe siri ya kuwa na maisha mazuri=ni kuridhika na hali halisi ulo nayo, kuwa na hofu ya Mungu, kuishi vizuri na watu, kusamehe walokukosea, kuwa na Upendo na utu.. Hii ndo siri ya maisha mazuri.. Mungu akujalie hivi vyote...
Ewe MJA kumbuka, staili uliyoingia nayo duniani ndiyo hiyo hiyo utakayo ondoka nayo duniani. Ulikuja duniani ukilia na siku ya kuondoka duniani watalia.
Ulikuja duniani huna nguo wakakuvisha na utaondoka duniani huna nguo pia watakuvisha. Ulikuja duniani ukaogeshwa na utaondoka duniani watakuosha. Ulikuja duniani huwezi kutembea ukabebwa na utaondoka duniani huwezi kutembea utabebwa. Zinduka ewe mja, tubu haraka . Dunia ni chumba cha mtihani.
MUNGU aliumba Ardhi na Mbingu, Miti na Wanyama wala Hakujisifia lakini alipoumba kiumbe mzuri kama WEWE alijisifia na akasema "NIMEMUUMBA MWANADAMU KATIKA UMBO LILILO BORA"