Maisha Mazuri Kwa Kila Mtanzania na Kupanda Kwa Nauli...

Chuma

JF-Expert Member
Dec 25, 2006
1,324
43
Wadau naona Hali ya maisha inazidi kuwa ngumu sana....

Nauli zimepanda vibaya mno by the so called kupanda kwa mafuta, Hapo hawajasema vipuri....na takataka zake zingine. Kikubwa ni kuwa Kupanda kwa Nauli kutasababisha kila nukta ya mahitaji nayo yapande.bei za vyakula nazo zitapanda...Cost za Masomo au Tuition fee nazo itabidi zipande...sijui tunaelekea wapi....

Muungwana na Mawaziri wake un-aware of maisha magumu, sijui safari ya wiki Hii anayoifanya akiwa Tanga kama anaweza kujionea lolote....

Hawa Sumatra nao naona hawapo kwajili ya wananchi..Tunahitaji vyama vya upinzani either kwa Umoja wao au Kama chama Binafsi kuonesha kuwa wananchi hawaridhishwi na Hali hii. Believe me dola 100 Bongo huwezi fanya lolote, wakati China na India dola 100 inaweza kukusukuma kama factors zote zipo constant!!!
 
Ndo Vizuri Kupanda Huko Ili Watanzania Tujifunze.2010 Tusifanye Tena Makosa.zipande Hata Mara 1000.
 
Kwa kweli sasa wameamua kutuua kabisa!! hata wanafunzi nauli juu..!
 
Hizi nauli jamani balaa tupu, ndo serikali yetu hii tumeiweka wenyewe madarakani, yaani mwanafunzi alipe mia moja kwa njia moja? hivi kweli tutasomesha watoto? au ndo tunarudishwa vijijini kinamna?
 
Ndo Vizuri Kupanda Huko Ili Watanzania Tujifunze.2010 Tusifanye Tena Makosa.zipande Hata Mara 1000.

Sasa wewe too much hata kama ni hasira siyo hivyo ndugu.Loh!huna hata huruma kwani walivyochaguliwa tulijua ni mbwa mwitu hawa tunawachagua?
 
Wakuu hizo zinaitwa nguvu za soko huru na huria. Kwa kifupi ni kwamba mfumuko wa bei ndio huo na huu mara nyingi ukishatokea katika nyanja au sehemu moja ya uchumi kama hautodhibitiwa (sio na serikali bali na mamlaka zinazojishughulisha na huduma za fedha na uchumi) una tabia ya kusambaa katika maeneo mengine.

Kiufupi ni kwamba, kutokana na uchumi wetu kuwa mchanga, nchi haina uwezo wa kujikinga na masahibu ya kiuchumi yatokenayo mahala pengine duniani.Huu mfumuko wetu wa bei unachangiwa kwa kiasi kikubwa sana na mfumuko wa bei katika chumi kubwa duniani.

Hapa ni kuomba tu waendesha dunia waweke mambo sawa KWAO labda na sisi huku Bongo ndio tutaweza kupona.
 
nafikiri sasa hata sisi watanzania tutajifunza jinsi ya kuipressurize serikali ambapo ni kugoma tu..sasa ni pale lini? tutapiga kelele wewe kwenye kipimajoto then kwisha kazi
 
Nauli zimepanda lakini mishahara bado tunalipwa ile ile sh.80,000/=
Maisha bora yapo wapi sasa?Au maisha bora kwa kila FISADI.
 
nauli na vyenginevyo lazima vipande.......hasa kwa sababu tunategemea vitu vingi kutoka nje.

tukitaka tukae mbali na mabadiliko yanayotokea ulimwenguni tunahitaji kujitegemea zaidi. ....lakini juu ya hivyo nafikiri athari ya kupanda kwa mafuta ni kubwa mno kuwa isifike tanzania.

cha kujiuliza ni "jee kupanda kwa mafuta na kupanda kwa nauli kunatokea kwa viwango sawa?"
 
Huyu JK wetu mbona kimya hana la kusema katika lolote lile? afadhali na Bush, mafuta yamepanda juu na morgage zinz-crumble, lakini anajaribu kuwa-ashua wananchi wake kuwa mambo yatakuwa powa, JK hata cha kumumunya au cha kutafuna hana?
 
JK ni bubu ndugu zangu
Siku hizi yuko bussy na wananchi wa nchi zingine na kuwachekea tu akina GB wa Marekani na Uingireza ndugu zangu

Huu ni mzigo hasara tena vibaya sana, lugha za mitaani tunasema hii imekula kwetu, lakini poa tu maana ukiwambia watu wanakuona wewe mbaya

sasa miatano mlizokuwa mnaongwa na vijikofia na kuuza kura zenu ndio matokeo yake haya.

bwaha ha ha ha ha haaaaaa kwi kwi kwi kwi kwi BabaH umesahau walipewa pia sahani za pilau...
 
Huyu JK wetu mbona kimya hana la kusema katika lolote lile? afadhali na Bush, mafuta yamepanda juu na morgage zinz-crumble, lakini anajaribu kuwa-ashua wananchi wake kuwa mambo yatakuwa powa, JK hata cha kumumunya au cha kutafuna hana?

Hapa tunapata somo moja zuri tu kwa wale wote wanaokimbilia ikulu. Jipime na ukiona huna ubavu, kaa mbali na ikulu. Kikwete aliyataka mwenyewe na sasa yamemshinda, watanzania tumeliwa. Inanikumbusha wimbo moja siukumbuki vizuri lakini ulipigwa na vijana wa Tanga - nielekee wapi, mbele yuko simba, nyuma chui, kushoto sijui mnyama gani na kulia ndio balaa. We acha tu......
 
......endeleeni kuwapigia kura CCM ili mpate maisha bora na muendelee kusema wapinzani bado hawajakomaa!
 
Date::7/16/2008
Nauli mpya zazusha vilio toka kwa wananchi mbalimbali
Na Waandishi Wetu
Mwananchi

UAMUZI wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini, (Sumatra) kupandisha nauli za mabasi nchini kote, umekoroga fikra za wadau mbalimbali nchini.

Mamlaka hiyo ilipandisha nauli zote kwa zaidi ya asilimia 20 ya nauli za awali, zitaanza kutumika rasmi Agosti Mosi, mwaka huu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wadau walisema kuwa, hatua hiyo si tu kwamba itapandisha karibu kila bei ya kila kitu, bali pia itasababisha ugumu wa maisha kwa wananchi wengi.

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Idara ya Siasa na Utawala, Bashiru Ally, alisema kama serikali ingekuwa inawajali wananchi wa kawaida, ingesimamia vyema ongezeko la bei katika mafuta ili lisilete madhara kwao.

Alisema Serikali imekuwa ikitoa ruzuku katika mambo mengi, lakini katika suala la mafuta imelifumbia macho kwa muda mrefu, hali inayosababisha kupanda kwa gharama za uzalishaji mali na kuongezeka kwa ugumu wa maisha.

Ally alisema kama serikali ingekuwa na chombo chake cha usafiri, nauli zisingeweza kupanda kwa kiasi hicho tofauti na sasa ambapo mambo yote ya usafirishaji yanafanywa na matajiri, ambao wamekuwa wakishinikiza kupanda kwa nauli hizo ili wapate faida.

Alisema ipo haja kwa serikali kulitazama upya suala hilo la nauli kwani litaathiri uchumi wa taifa na kupunguza kasi ya maendeleo kama lisipochukuliwa hatua za kudhibiti, kwa kuandaa chombo kitakachosimamia vyema manunuzi ya mafuta ili kuwe na unafuu wa upatikanaji wa nishati hiyo.

Naye, Daktari bingwa wa upasuaji wa watoto katika Hospita ya Taifa ya Muhimbili, Dk Petronila Ngiroi, alisema kupanda kwa nauli kumetokana na kushuka kwa thamani kwa sarafu ya Tanzania ukilinganisha thamani ya fedha zingine duniani.

Alisema kupandishwa kwa nauli za wanafunzi ni sahihi kabisa kwani manyayaso ya wanafunzi yalikuwa yakitokana na Sh 50 waliyokuwa wakiilipa, jambo lililokuwa likihatarisha maisha yao.

Alisema kama serikali itaona kuwa hilo ni tatizo kwa wanafunzi, ni vema ikaandaa magari maalum kwa ajili ya kuwabeba ili wasiweze kuchelewa shuleni na kukosa masomo.

Dk Ngiroi alisema gharama za uendeshaji miradi zimekuwa zikipanda kila siku kutokana na ogezeko la bei ya nishati, hali ambayo imewafanya wafanyabiashara nao kupandisha bidhaa zao bei maradufu hivyo kuathiri gharama za maisha.

Chama cha Wamiliki wa Mabasi yaendayo mikoani (Taboa), kilisema kinakubaliana na ongezeko hilo, lakini serikali inatakiwa kuchukua hatua zaidi za kudhibiti upandaji holela wa bidhaa mbalimbali zinazohusu magari.

Mwenyekiti wa Taboa, Mohamed Abdullah, alisema kutokana na ongezeko hilo, wandeshaji wanaunga mkono, wamefarijika na watapata ahueni ingawa kiwango cha asilimia 20 sicho walichoomba.

Aliongeza kuwa, uendeshaji wa mabasi unategemea zaidi bei ya kununulia vipuri, ujenzi wa bodi, mafuta na gharama za wafanyakazi na kwamba, wasionekane kama wanataka kujitajirisha na wao ni wananchi wanajua hali halisi.

Abdullah alisema mahitaji yote hayo ni wafanyakazi ambao wanalipwa kwa shilingi ya Tanzania, huku mengine yakithamanishwa kwa dola ya Marekani, hali inayowakandamiza waendeshaji.

Aliongeza kuwa walipeleka maombi Sumatra tangu Aprili, lakini walikutana Juni 16, huku mafuta yakiwa yameongezeka kwa asilimia 15 na hadi jana yalikuwa yamefikia asilimia 20.

"Sawa tunakubali ongezeko hilo, lakini yawezekana kama hakuna udhibiti tukaenda tena Sumatra kuomba kuongeza nauli kwa sababu, mafuta yanazidi kupanda hizi asilimia 20 zilizoongezwa zitadumu kwa muda mfupi," alisema Abdullah.

Kwa upande wake, Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Usafiri jijini Dar es Salaam (Darcoboa) kimesema kuwa, hakikuridhishwa na kiwango cha nauli kilichopandishwa na Sumatra.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini jana, Mwenyekiti wa Darcoboa, Sabri Mabrouk, alisema kuwa kiwango hicho ni kidogo sana ukilinganisha na baadhi ya magari ambayo yanakwenda umbali mkubwa, huku mafuta yakiwa yamepanda sana.

Alisema kuwa kutokana na upandaji huo, wameamua kuwa kila bei ya mafuta inavyoongezeka na wao wanapeleka mapendekezo yao ya kupandishwa kwa nauli hizo ili waweze kutoa huduma bora.

''Mafuta yamepanda sana, ukilinganisha na kipindi kilichopita, tumejaribu kupeleka mapendekezo yetu Sumatra ya kutupandishia nauli ili tuweze kutoa huduma bora, lakini mpaka wanatangaza juzi nauli hiyo ni ndogo na haiwezi kukidhi mahitaji ya vyombo vya usafiri,'' alisema Mabrouk.

Alisema kuwa katika mapendekezo yao waliomba nauli inanzie Sh 350 ambacho ni kima cha chini na Sh1,000 ambayo ni nauli kubwa kwa magari yanayokwenda zaidi ya kilomita 12, lakini upandaji huo umekuwa ni kinyume cha matarajio yao.

Alisema kuwa nauli iliyopandishwa ni ya kawaida, hivyo hategemei kuona wananchi wanailalamikia au kuwa na migogoro ya kutolipa kwa sababu imeongezeka kwa kiwango kidogo, ambacho wengi wao wanaweza kuimudu.

Hata hivyo, Mabrouk aliwataka madereva na makondakta wa daladala kuacha tabia ya kutoza nauli kinyume cha taratibu zilizowekwa na Sumatra.

"Makondakta wengi wamekuwa na tabia ya kupandisha nauli kinyume cha taratibu, tunawataka waache tabia hiyo, watoze nauli ambayo imetangazwa rasmi na Sumatra ili kuondoa migogoro ya usafiri," aliongeza.

Nao wananchi mbalimbali wametoa maoni tofauti, kufuatia uamuzi wa kupanda kwa nauli ifikapo Agosti Mosi.

wakizungumza na Mwananchi, walisema kuwa kiwango hicho kinamdidimiza mwananchi mwenye kipato cha chini, kwani nauli ni kubwa kuliko mahitaji ya wananchi.

Ziada Sadick, mtumishi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, mkoani Tanga, alisema kuwa wafanyakazi wanapokea mshahara wa kima cha chini kuongezeka kwa nauli ni kuwadidimiza zaidi.

"Mshahara tunaoupata ni mdogo ukilinganisha na matumizi, ulipe kodi, matumizi nyumbani, na bado hujalipa nauli ya daladala, hivi serikali inatoa maisha bora kwa kila Mtanzania kweli?" alihoji Sadick.

Eutropia Shilsya, mkazi wa Songea, alisema gharama za maisha zenyewe ni kubwa na wakulima hawataweza kupeleka mazao yao mjini kutokana na kupanda kwa gharama za usafirishaji.

''Ukilinganisha gharama za maisha na kiwango cha sasa cha nauli ni tabu kwa mwananchi wa kawaida, na tayari wamekipandisha hatutaweza kusafiri kama kiwango kitakuwa hivyo,'' alisema Shilsya.

Dickson Masena, fundi viatu, anasema iweje mwanafunzi alipe nauli kubwa wakati hafanyi kazi yoyote.

Karani wa Kampuni ya mabasi yanayosafiri kati ya Tanga na Dar es Salaam ya Raha Leo, Amos Mfalme, alisema nauli zinazopanda kuanzia Agosti Mosi ni kero kwa abiria.

Nacho Chama cha Kutetea Abiria Mkoa wa Dar es Salaam Chakuwada, kimepinga utaratibu uliotumiwa na Sumatra kupandisha nauli kwa wanafunzi kwa madai kuwa kiwango hicho kinamuongezea ugumu wa maisha mwanachi wa kawaida

Akizungumaza na Mwananchi Ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Chakuwada, Hassani Mchanjama, alisema katika ongezeko hili la nauli mwanafunzi hakupaswa kuongezewa kwa sababu anamtegemea mzazi kwa kila kitu.

Alisema ongezeko hilo kwa mwanafunzi ni mzigo mwingine kwa mwanachi wa kipato cha chini ambao wengi wao ni wakulima na kipato chao hakikidhi mahitaji ya kila siku ya kimaisha.

''Wote tunajua maisha ya Mtanzania kuwa ni duni, asilimia 80 ya Watanzania wanategemea kilimo ambacho nacho hakikidhi haja, kupandisha gharama za nauli kwa wanafunzi kutawaongezea mzigo Watanzania wa kawaida na inaweza kusababisha watoto wa masikini kukishindwa kupata elimu,'' alisema Mchanja

Vyama vya upinzani nchini vimeielezea hatua ya kupanda kwa nauli ya mabasi nchini kuwa ni matokeo ya uongozi mbovu wa serikali na kushindwa kuboresha maisha kwa wananchi wake.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, viongozi wakuu wa vyama hivyo nchini walipinga maamuzi ya Sumatra ya kupandisha nauli za mabasi nchini kote.

Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustino Mrema, alisema jana kuwa, hatua ya mamlaka hiyo kuridhia kupadishwa kwa nauli nchini kutazidi kumgandamiza mwananchi wa kawaida ambaye amekuwa akishindia mlo mmoja kwa siku licha ya serikali kuendeleza falsafa yake kuwa itaboresha maisha kwa wananchi wake.

"Hali inatisha, serikali ni lazima isalimu amri na kukukubali kuwa imeshindwa kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania, walalahoi wamezidi kugandamizwa huku viongozi wakitesa katika magari ya kifahari na kupata posho kila kukisha katika semina na makonngamano," alisisitiza Mrema.

Naye Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, Erasto Tumbo, alisema kuwa ongezeko la nauli ni matokeo ya utawala mbovu kwa kuwa serikali imeshindwa kuonyesha dhamira ya dhati katika kuboresha maisha ya wananchi wake.

Alisema kipato cha Mtanzania wa kawaida ni Sh 100,000 kwa mwezi hivyo hataweza kumudu gharama za nauli hiyo ikiwa ni pamoja na kuhudumia familia yake.

Juzi Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Israel Sekilasa, alitangaza ongezeko la nauli kwa wastani wa asilimia 20 kunzia Agosti mosi mwaka huu.

Imeandikwa na Patricia Kimelemeta, Saa Mohamed, Gofrey Nyang'oro, Midraji Ibrahimu na Tausi Mbowe.
 
kuna mtu humu aliwahi kusema watanzania ni vipofu. doh watu walifumuka kumpinga ile mbaya na wengine wakadiliki kumwita snitch but mi nilikuwa pamoja naye na mpaka mwisho ntakuwa nae coz alichokisema ni cha kweli.

je hebu tufikiri huku kupanda kwa gharama za maisha kiholela na serikali iliyochaguliwa kwa 80% iko kimya, je ingekuwa ni nchi ya jirani ya kenya ingewezekana?
kilo 1 ya unga ilikuwa 350 na ilipopanda ikafika 700 lakini wabongo wako kimya tu, sasa bei za nauli zimepanda na mishahara bado iko pale pale, je huku si kumtega mfanyakazi ili apokee rushwa pindi itakapojipitisha mbele yake?
 
Wakuu hizo zinaitwa nguvu za soko huru na huria. Kwa kifupi ni kwamba mfumuko wa bei ndio huo na huu mara nyingi ukishatokea katika nyanja au sehemu moja ya uchumi kama hautodhibitiwa (sio na serikali bali na mamlaka zinazojishughulisha na huduma za fedha na uchumi) una tabia ya kusambaa katika maeneo mengine.

Kiufupi ni kwamba, kutokana na uchumi wetu kuwa mchanga, nchi haina uwezo wa kujikinga na masahibu ya kiuchumi yatokenayo mahala pengine duniani.Huu mfumuko wetu wa bei unachangiwa kwa kiasi kikubwa sana na mfumuko wa bei katika chumi kubwa duniani.

Hapa ni kuomba tu waendesha dunia waweke mambo sawa KWAO labda na sisi huku Bongo ndio tutaweza kupona.

Patpending, you have said it all.
Hata angetawala malaika bado nauli na vitu vingine vingepanda tu.
 
Back
Top Bottom