Maisha: Kwa hili namshukuru Mungu

Maisha: Kwa hili namshukuru Mungu

Kifai

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2013
Posts
816
Reaction score
173
Nimefanya kazi kwenye makampuni mengi ya uchimbaji madini, kwa miaka takribani mitano bila kujenga nyumba, kila nilipofika nyumbani kwa ajili ya likizo baba alikuwa ananiuliza swali ambalo lilikuwa linanichoma moyo sana....!

Mwanangu vip ushaanza ujenzi? Kwa masikitiko nilikuwa sina jibu la kumpa,

Kilichokuwa kinaniuma zaidi ni wenzangu nilianza nao kazi na wengine walikuja nyuma yangu walikwisha anza ujenzi, nilikuwa naumia sana ndani ya nafsi yangu bila kumweleza mtu, kwa sasa nilishaanza ujenzi na nipo kwenye lenta, Mungu ashukuriwe.
 
Jamani si anafurahi na wanajamii kwa mafanikio yake!! Je na yule alie changa hadi kapata pesa ya kununua kamera iiyo muwezha kupiga picha gari nzuri aipendayo?
 
Hivi kila mtu akianza ujenzi (wengine tulishaanza kitambo)na akawa na mawazo kama yako patatosha kweli humu?!
 
hii taarifa sisi inatuhusu nini!? moderators huu nao ni uzi wa kuachwa!? ngoja waje wengine watutaarifu wamenunua pedi

Roho mbaya hiyo!,haitakufokisha popote km haujaupenda uzi wa mwenzio si upite tu bila kukomment!,nani amekulazimisha kusoma na kukomment?,Hao walionunua Pedi ni wengine siyo wewe;Wewe ni wewe na wao ni wao acha hizo bhana!Kwanza kabisa jamaa Anamshukuru Mungu lkn cha ajabu Makamasi yanakutoka vipi weweee???.
 
Hongera ndugu kwa jitihada za kuangalia maisha ya baadae badala ya kuendeleza starehe. Kaza buti
 
Hivi kila mtu akianza ujenzi (wengine tulishaanza kitambo)na akawa na mawazo kama yako patatosha kweli humu?!

Kwanini pasitoshe?,si ni mambo ya maendeleo!!,hapa anatu-Inspire wengi kutokukata tamaa,halafu Wabongo sisi Vichwa maji kwelikweli Thread km hizi tunaziponda kinyama lkn Mtu akija na Thread ya Mapenzi hata km anasimulia namna alivyo sex usiku wa kuamkia leo ndo tunazichangia kweli tena very Postively!,Afrika Jinga sana sijui kwanini hatupendi maendeleo?,aah! Very hopless.
 
Amen, Mungu ashukuriwe. Endelea kumshukuru hivyo hivyo mpaka nyumba iishe, uongeze na nyingine na nyingine.
 
Hongera mkuu, ila dah nifanyeje na mimi nipate kazi migodini mkuu, hapaingiliki yan
 
Huu ni ushuhuda sio..

Naona kama haujakamilika ndio maana hauleweki.

Tujuze mwanzo uloshindwa vipi, na sasa umeweza vipi na unashauri nini kwa wanajukwaa. Hapo ndipo uzi utakuwa na mashiko.

Vinginevyo utakuwa nshomile wewe..
 
Hongera..

Ukihamia pia uje kutuambia.

Ushanunua gari? Kama bado ukinunua njoo utupe taarifa
 
Nimefanya kazi kwenye makampuni mengi ya uchimbaji madini, kwa miaka takribani mitano bila kujenga nyumba, kila nilipofika nyumbani kwa ajili ya likizo baba alikuwa ananiuliza swali ambalo lilikuwa linanichoma moyo sana....!

Mwanangu vip ushaanza ujenzi? Kwa masikitiko nilikuwa sina jibu la kumpa,

Kilichokuwa kinaniuma zaidi ni wenzangu nilianza nao kazi na wengine walikuja nyuma yangu walikwisha anza ujenzi, nilikuwa naumia sana ndani ya nafsi yangu bila kumweleza mtu, kwa sasa nilishaanza ujenzi na nipo kwenye lenta, Mungu ashukuriwe.

hongera sana mkuu,mi hapa limama lenye nyumba lina roho mbaya kama nini.n'way ukimaliza unipe na mimi maujuzi
 
hahahahaaa JF bhana, umenichekesha sana mkuu. kwamba 'mgodi' anaukalia afu analia njaa. Teh teh
Usishangae ni mwanamme ameweka hiyo ila pia usishangae ni afadhali ya jana kajitutumua na avatar ya KUBOTA... Mama/wake zetu baadhi hawajiamini na wanajiwekea support ili kujiamini.
 
Mungu akuzidishie kheri...umalizie ujenzi wako salama...na akuzidishie afya tele ili uhamie salama...na akuondolee wale wenye vijicho vya husda ili uishi kwenye nyumba yako salama.....na akujaze moyo wa imani ,subira na uvumilivu ili uzidi kufaidi matunda ya juhudi zako.....hao wanaokubeza ukiwaangalia unaweza kukuta ni watoto wa mama wanaokula na kulala bure majumbani mwao......hawajui hata bei ya kilo ya unga zaidi ya kujua bei za masuruali ya jinsi na mishahara ya wacheza soka la kulipwa ulaya.........kwa kifupi ni watoto wa kiume na wala si wanaume kwani mwanaume mtafutaji hawezi kubeza maendeleo ya mwanaume mwenzake kwani anajua wazi kuwa hakuna kitu kinachopatikana kwa URAHISI labda kwa wale ambao sio ridhki.........
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom