Maisha kama Bongo Star Search..Uzushi mwingi....

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,885
Kwa Watanzania wengi wanaijua hii show ya Bongo sstar search na nyingine zinazofanana na hiyo ila ni watu wachache wanaoweza kujifunza kitu kwa kulinganisha maisha yao na show hiii. ukweli ni kuwa maisha meengi tunayoishi kuna vitu viingi mno vya kujifunza ambavyo ukitazama utaona ukweli na unaweza kukusaidia....

Kila mwaka hii show inaanza kwa kutafuta washiriki wanaanza watu maelfu na wanapunguzwa hadi anabaki mmoja ambae anatangazwa mshindi ukweli ni kuwa washiriki woote ni karibu sawa na mshindi haswa wa show hii ni 'muandaaji wa show' na sio washiriki. Washiriki hupewa tu title za kuwadanganya, mfano 'top ten' au 'top three' na kadhalika na wale wanaokosa kuingia hizi top ten au top three au wale ambao wako mikoani na walishindwa kuingia hatua ya pili ya kuja DSM 'hujiona wameshindwa kitu kikuubwa saana' na wanaofanikiwa 'hujiona wamepiga hatua kuubwa sana' kumbe mara nyingi ni 'uzushi mtupu'

sasa ukija kwenye maisha ni hivyo hivyo unakumbuka shule ilivyokuwa? unakumbuka kila mtihani ilionekana kama ni 'make or break' ya future yako? unakumbuka 'ulivyofaulu darasa la saba'? au 'ulivyofeli darasa la saba'?????? ulipoajiriwa je? wangapi hujutia kazi zao baadae? au waliofukuzwa kazi na 'wakaona ni kama mwisho wao umewadia' baada ya miaka michache walilitazama vipi?

'ulipompata the love of ur life'? miaka michache baadae mara ngapi ulijiuliza' if you made the right decision'? kila hatua tunayopitia in life huwa inatufanya tuone 'tukifanikiwa' dah.... na 'tukishindwa' duh......kumbe in few years 'kushindwa na kufanikiwa' hakutakuwa na tofauti kuubwa saana. Wangapi walifeli darasa la saba wakaja kupata div one form four? au waliofaul form six wakafeli chuo?
au walimaliza chuo na kushindwa maisha kwa ujumla?

ukweli ni kwamba maisha yetu yamejaaa 'show za aina ya BSS' kila hatua na ni watu wachache wanaojua hilo weengi 'tunaamini tunayoaambiwa na waandaji wa show hizi' kusoma kuna tests mitihani na kadhalika ajira zina interview na ukishapata kazi kuna 'probation time'

kuna barua za onyo ukikosea, na ukifanya kama muajiri anavyotaka'promotion na tuzo za kiofisi' ili mradi hakuna tofauti na 'kuingia top ten' au kuondolewa kwenye BSS... but 'anaefaidika zaidi' sio wewe wewe unatumika tu na ukishindwa kutumika vizuri wanaku dump asap lol

mitaani ni hivyo hivyo....watu wanatumika kununua bidhaa fulani fulani wakiamini wanafaidika tazama 'promotion za makampuni ya simu mfano' na makampuni mengineyo unaweza leo kuona umeshindwa saana au umefanikiwa saaana lakini kumbe uko kwenye
'show ya mtu au watu fulani hivi' mfano wa BSS

ukiweza kutumika 'wanaku promoti' ukishindwa wanaku timua na wanatafuta washiriki wapya...

thats life these days.....
 
Very insightful Boss. I think the only way to sail through is to remain constant and to focus on the greater goal. If you have a short sight of your possibilites, of your aspirations and of your life in general, you are likely to invest a lot of efforts into something that is not so useful, and is not helping you advance toward your ultimate goals.

Mafano umetoa hapo:Suppose you are a father and you consider your family to be the most important achievement of your life, and their hapiness to be the ultimate goal to reach: ikiwa utakomaa sana kazini, na ku-sacrifice zaidi kwenye kuhakikisha unamfurahisha mwajiri wako, bila kujali familia inakuaje, lazima baadae, ukija kupoteza/kuhama hiyo kazi utaona kama ulipoteza muda. Ila kama toka mwanzo ulielewa kua familia yako ni muhimu sana na kazi yako is only a mean to provide you with the necessary financial and self esteem comfort to deal intelligently with your family, then utachukulia challenges zingine simple tu, na unaposhindwa/faulu huwekei msisitizo sana. you put it in the broader context and realise it is only a tiny dot...
 
Thanks a lot kwa mchango wako
umeelewa my point
sasa weengi ninaokutana nao wanaaamini mno
'miongozo ya waandaaji wa shows'
ndo unakuta mtu awards za office au kuzungumza na bosi wake ni muhimu mno kwake
kuliko hata kuzungumza na watoto wake mfano
halafu akistaafu na kuanza tabu ya kufuatilia mafao ndo anagundua the mistake when its too late
 
Mimi nilifeli darasa la saba nikapelekwa kusoma shule ya private sekondari. Huko nako form four nikafeli (nilipata divisheni 4).

Baada ya hapo nikatimua zangu majuu kwenda kutafuta maisha. Well, kama wasemavyo...the rest is history.

Sasa hivi watu wenye mastaz zao nawakimbiza. Wale waliokuwaga wanakuwa wa kwanza darasani wengi wao ni choka mbaya tu. Nikikutana nao wananipiga mizinga.

Mashoree wengi waliokuwaga wakali enzi hizo sasa hivi wengi wao wameshazalishwa na kuachwa na wamekuwa vibibi tu. Usicheze na vumbi bana.

Haya maisha hayana kanuni na wala hayatabiriki.
 
the problem gets worse when a person who is not focused in life and lives for day to day moments of fame and glory, ignoring the big picture, meets a manipulative person who can take advantage of his short-sight and promote his own long term vision:

The perfect illustration is the tax payer who is milked by the tax authority, his money is used to finance a political party which appoints a candidate and provides him with substantial amount for his campaign. the candidate uses the money to buy t-shitrs and pay "transport" for his partisans in order to buy votes. The poor tax payer, for the pleasure of wearing a branded t-shirt with Mhe X picture, decides to vote for the same candidate and get milked again for another 5 years.

Because he is blinded by the t-shirt (wearing a t-shirt na kuonekana mjanja mtaani is the show here) he loses sight of the past 5 years, the future 5 years, and his contribution to the perpetuation of this vicious cycle.
 
Mimi nilifeli darasa la saba nikapelekwa kusoma shule ya private sekondari. Huko nako form four nikafeli (nilipata divisheni 4).

Baada ya hapo nikatimua zangu majuu kwenda kutafuta maisha. Well, kama wasemavyo...the rest is history.

Sasa hivi watu wenye mastaz zao nawakimbiza. Wale waliokuwaga wanakuwa wa kwanza darasani wengi wao ni choka mbaya tu. Nikikutana nao wananipiga mizinga.

Mashoree wengi waliokuwaga wakali enzi hizo sasa hivi wengi wao wameshazalishwa na kuachwa na wamekuwa vibibi tu. Usicheze na vumbi bana.

Haya maisha hayana kanuni na wala hayatabiriki.

wewe uliamua hutashiriki 'other people's show'
ulishiriki your own show
na sasa huna regrets
 
the problem gets worse when a person who is not focused in life and lives for day to day moments of fame and glory, ignoring the big picture, meets a manipulative person who can take advantage of his short-sight and promote his own long term vision:

The perfect illustration is the tax payer who is milked by the tax authority, his money is used to finance a political party which appoints a candidate and provides him with substantial amount for his campaign. the candidate uses the money to buy t-shitrs and pay "transport" for his partisans in order to buy votes. The poor tax payer, for the pleasure of wearing a branded t-shirt with Mhe X picture, decides to vote for the same candidate and get milked again for another 5 years.

Because he is blinded by the t-shirt he loses sight of the past 5 years, the future 5 years, and his contribution to the perpetuation of this vicious cycle.

hizi cycle hizi
afadhali huyo utasema hana 'education'
mimi huwa najiuliza unakuta mdada ana degree mbili au phd
anapewa ubunge au kupandishwa cheo kwa sharti la
'kutoa mwili wake mfano'
sasa faida ya kuumiza kichwa shuleni ilikuwa ya nini???????/

kama 'shule haikuti kwenye utumwa wa kutumika'?
 
Kwanza nimeipenda sana hii inakufanya uache kufikiri kimazoea.Nadhani swali la msingi ni kuwa,kufanikiwa kimaisha hasa ni nini?Kupata pesa?Au ni kusoma mpaka unazeeka?Kuoa?Kusomesha watoto?Je ni nini?
 
Nimependa ulivyoweza kulinganisha tv show, shule, ajira, love na maisha yetu ya kila siku. Ni maneno matamu kusoma, shida inabidi kutumia nguvu sana kuelewa ..... ngoja nisubiri kuona mifano nadhani nitaelewa zaidi
 
I got ur point buddy!
Ni kweli maisha ni kama 'vicious circle' fulani hivi!..Na kama ulivyosema kuna 'wakati' katika maisha unakuwa unaona unapatia..lakini ndani ya muda mchache unajiona ulikosea!..Na kadiri unavyoona umejirekebisha..then, unajikuta uko mbali na ile furaha uliyoitegemea...Wakati mwingine inabidi kuivunja hiyo 'vicious circle' and let life go the way you think it makes you happy!!

Mfano..huwa nashindwa kuelewa pale ambapo mtu hajiamni katika maisha yake mwenyewe..Unakuta anahangaika na kutumia nguvu kubwa kufkiria maisha ni kesho na sio leo!!..Kimsingi inabidi ifike hatua ukubali kuwa haya ndio maisha yangu na chochote kitakachokuja mbele kianzie hapa..lakini habari ya kudhani kukosa kile ama hiki ni 'big deal' mara nyingi inatufanya tuwe watumwa wa 'maisha yetu wenyewe' na mara tunapokuja kushtuka 'gharama' tuliyotumia kuyatafuta 'maisha' na 'kile tulicho nacho' inabaki huzuni tu..na ukifikiria sana unakuta muda umekwenda..na uliyemfaidisha ni mtu mwingine baki!

Kila 'step' katika maisha yako ina 'count'..furahia kuanzia hapo!!!
 
Nimependa ulivyoweza kulinganisha tv show, shule, ajira, love na maisha yetu ya kila siku. Ni maneno matamu kusoma, shida inabidi kutumia nguvu sana kuelewa ..... ngoja nisubiri kuona mifano nadhani nitaelewa zaidi

shule- mara ngapi uliambiwa usipofaulu huna future?
halafu ukafaulu na bado waliofeli walikuzidi kwa vitu viingi?

ajira- mara ngapi uliona ukipoteza ajira umekwisha na wapo walipoteza ajira
wakaenda kujiari wenyewe na kuishi better?

love- umeona watu wanavyofurahi siku ya harusi?
halafu few years latter unasikia wameachana kwa vipigo na matusi?
je mmoja angejiua labda kwa kukosa penzi la mwingine hapo kabla?

Bss- umewahi kuona watu wakiambia wamekuwa disqualified wanavyoona kama 'mwisho wa dunia'?
but walioshinda unawakumbuka woote?
 
Kwanza nimeipenda sana hii inakufanya uache kufikiri kimazoea.Nadhani swali la msingi ni kuwa,kufanikiwa kimaisha hasa ni nini?Kupata pesa?Au ni kusoma mpaka unazeeka?Kuoa?Kusomesha watoto?Je ni nini?
Nadhani kila mtu ana upeo wake wa maendeleo.Pale unapoweza fika mahali umetimiza ndoto zako kwa 100% hapo unaweza sema umeendelea(hii ni katika individual level)
 
shule- mara ngapi uliambiwa usipofaulu huna future?
halafu ukafaulu na bado waliofeli walikuzidi kwa vitu viingi?

ajira- mara ngapi uliona ukipoteza ajira umekwisha na wapo walipoteza ajira
wakaenda kujiari wenyewe na kuishi better?

love- umeona watu wanavyofurahi siku ya harusi?
halafu few years latter unasikia wameachana kwa vipigo na matusi?
je mmoja angejiua labda kwa kukosa penzi la mwingine hapo kabla?

Bss- umewahi kuona watu wakiambia wamekuwa disqualified wanavyoona kama 'mwisho wa dunia'?
but walioshinda unawakumbuka woote?

Vitisho kama hivi tulishaanza kuambiwa toka tupo tumboni..tunaenda shule bado tunaambiwa,tunaajiriwa bado tunaambiwa.Hadi kwenye familia story ni hizo hizo...Ndio maana inakuwa ngumu KUAMINI TOFAUTI(eg YES I CAN)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom