Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,636
- 220,350
Umefanikiwa kujenga kibanda cha vyumba viwili, chumba chako ni master bedroom na chumba cha pili ni cha kawaida. Unapata uhamisho, kwa sababu za kiusalama unamtafuta kijana wa kukaa. Chumba chako unafunga.
Kijana anakuta nyumba full furnished na king’amuzi juu, flat screen “60. Unamaliza mshahara kila mwezi na nje ana ki sehemu cha kupanda mihogo, viazi vitamu na mchicha. Hata kuku ameanza kufuga kwenye kibanda alichojenga.
Baada ya miaka miwili unarudi unamkuta anaishi na mwanamke na wamepata mtoto na kuna dada anawasaidia ulezi. Dada amewekewa godoro sebuleni. Chumba chako hawajagusa.
Hujakaa vizuri mtoto analetwa na kwa heshima wamempa jina lako. Maisha ya kijana ilibidi yaendelee akiwa amepata kibarua. Kijana ni muaminifu lakini unaona nyumba imekua ndogo. Utachukua uamuzi gani?