Binafsi nilichagua kuwa mtu wa peace and love. Kwa muda mrefu nimekuwa mtu mpole na mkimya hata pale inapotokea mtu kunikwaza siku zote nimekuwa wa kujishusha kwenye hali zote nazopitia.
ila nilichogundua ni kwamba ukiwa mnyonge haifanyi watu wakuheshimu Bali kukudharua na kila mtu atataka kugeuza kama ngazi ya kukupanda.
Nafikiri dunia imebadilika na ni muda wa Mimi kubadilika. Utachonifanyia na Mimi ntakufanyia hicho hicho. Ubaya ubayani.
Daaah, pole ndugu ila kumbuka wema ni akiba isiyo oza.
Katika dunia lazima pawepo watu agressive, cool na nutral. Bila hivyo mambo hayawezi kusonga na dunia haiwezi zunguka.
Haya maisha ni mafupi na hayajulikanai ni wapi kikomo cha uhai wetu, lililo bayana kwetu ni kuwa uhai wetu ni wa muda mfupi sana. Kuwapo duniani hii dakika hiileo ni rehema za Allah tu maana yawezekana sekunde upo na sekunde hiyohiyo umetoweka duniani.
Mimi huwa natenda wema kadiri niwezavyo ila silipizi kisasi kwa anaeniumiza bali hujitahidi kumwepuka maana keshanipa somo.
Sikuwahi jutia kwa wema niliowatendea watu baadae wakanijeruhi maana ninaamini katika Mungu na uwapo wake.
Nafanya hivi kwa sababu ndio wajibu wangu kama binadamu kwa binadamu mwenzangu lakininpia kwa ajili ya baraka za kizazi changu wakati ambapo sitokuwapo tena duniani.
Matunda ya wema yapo ila yawezekana nisifaidi mimi ila kizazi changu wataishi maisha yenye baraka kutokana na utu wema wa mimi mzee wao wakati wa uhai wangu.
Halikadhalika unaweza kuishi kifahari na kwa furaha hapa duniani ikiwa ni matokeo ya uovu kwa binadamu wengine, kumbuka unajenga laana kwako na kizazi chako miaka ambayo utakuwa umetangulia mbele ya haki nao wataishi kwa matunda ya uovu wako kwa binadamu wengine.
Ishi kwa haki kadiri Mungu akujaliavyo ,tenda haki kwa wenzako na dai haki zako kwa njia sahihi linda thamani ya utu wako, familia yako na jamii yako.
Kuwa mtu wa ibada kadiri Mungu akujaliavyo , jiweke karibu sana na Mungu hakika maisha ya dunia hii hayatakusumbua maana utayaona ni ubatili mtupu.
Namnukuu raisi wa Marekani hayati John F Kenedy.
"FORGIVE YOUR ENEMIES BUT DO NOT FORGET THEIR NAMES.