Just Distinctions
JF-Expert Member
- May 5, 2016
- 3,322
- 6,990
Maisha huwa yana namna ya kumjaribu mtu , ukiona unakaribia kukata tamaa jua neema inakaribiaHabari za jioni
Maisha mnayaonaje ndugu zangu,dada zangu,Kaka zangu.
Kila nilichopanga kufanya mwaka huu naona kabisa hakitimii.
Dada yangu mmoja hapa mtaani anasema nisijipe presha bado mdogo,nitafanikiwa tu kwa uwezo wa Mungu, lakini Mimi mwenyewe nina marafiki kibao,naona kama wanaendelea vizuri na mambo yao.
Na Mimi kila siku najiuliza nawezaje kufanikiwa na Elimu yangu ya kuunga unga ?
Kudanga siwezi,
Kutapeli ni mwiko kwangu,
Pamoja na hivi nilivoo naenjoy Kula pesa ya jasho halali iliyo na Baraka za Mungu. Je nitafanikiwa vipi.
Nawaombeni ushauri.
Maria D.
Muhimu ni kufanya yale yaliyo halali na kwa bidii, yaliyobaki muachie Mungu
Na kamwe usithubutu kujifananisha na yoyote hata kama ni mtu mliecheza nae utotoni
Watu wana mengi nyuma yao usione mtu kafanikiwa hata kama mnashinda nae mtaani, subiri yako ya halali