life expectancy kwa mtanzania wakati kikwete anachukuwa madaraka ilikuwa ni chini ya miaka 50?
Wakati wa nyerere?
Baada ya miaka 8 ya kikwete ni 62 years.
Bila maisha kuwa bora tusingeyaona hayo/ fikiri.
Mpaka wakati wa mkapa kuwa na usafiri binafsi ilikuwa ni anasa, baada ya miaka 5 tu ya kikwete imekuwa ni necessity, dogo hilo?
Jiko la kutumia gas ilikuwa ni kwa wenye uwezo tu, leo hii wakati wa kikwete imekuwa ni kawaida, dogo hilo?
Bima ya afya ilikuwa ni kwa akina fulani tu, leo hii wakati wa kikwete mpaka vijijini inaenea, dogo hilo?
Kabla ya kikwete ukitaka kwenda mwanza kutokea dar mpaka uzungukie kenya, leo unapuyanga tu hata kwa bajaji, dogo hilo?
Kabla ya kikwete usafiri wa ndege ulikuwa ni wa kuhadithiana kwa walioipanda au kuiona ndani tu, leo wakati wa kikwete kuna mpaka ya bei nafuu na si ajabu tena, dogo hilo?
Kuna vijiji kabla ya kikwete walikuwa hawajawahi kuuona taa za umeme toka kuzaliwa, leo rea inasambaza umeme kila pahala, dogo hilo?
Kuna vijiji na miji ilikuwa haijawahi kuona shule ya sekondari na ilibidi mtu ahame kwao kwenda kutafuta elimu japo ya sekondari tu, leo wakati wa kikwete sekondari kila kata, dogo hilo?
Kuna watanzania walikuwa hawajawahi kuziona huduma za afya toka wanazaliwa mpaka wanakufa, leo wakati wa kikwete zahanati kila kata, dogo hilo?