SoC01 Maisha baada ya kuhitimu Chuo Kikuu

Stories of Change - 2021 Competition

SAKA25

Member
Jul 15, 2021
12
22
Habari wana JF,Kwanza Tumshukuru Mungu kwa neema ya uhai anayoendelea kutujalia hapa

Pili niwashukuru watendaji wa JF Kwa kutuletea changamoto hii, tatu niende moja kwa moja kwenye story challenge yangu inayohusu Maisha baada ya kuhitimu Chuo kikuu.

Vijana wengi baada ya kuhitimu vyuo vikuu wanaishia mitaani kwa sababu hakuna ajira za kutosha serikalini na hata sekta binafsi na hata kama zikitokea basi wachache wenye connection wanapata nafasi hizo za ajira

Tumeshuhudia hivi karibuni serikali ilitangaza ajira elfu sita za walimu na afya lakini waombaji wa ajira hizo walikuwa zaidi ya elfu 90 na hata baada ya hao elfu 6 kupangiwa vituo vya kazi je hawa wengine zaidi ya elfu 80 wanaenda wapi?

Nini cha kuwashauri wahitimu wa vyuo vikuu. Kwanza kabisa kuhakikisha tunaondoa ile dhana ya kwamba lazima nikimaliza chuo kikuu naenda kuajiriwa,pili baada ya kufika mtaani basi tujichanganye na jamii na kuweka pembeni kabisa degree zetu.

Lakini pia kuchangamkia fursa zinazoizunguka jamii yetu tunaweza kufanya ufugaji mdogo wa kuku,kilimo cha mboga mboga,na hata kama nyumbani mmebarikiwa kuwa na mashamba makubwa basi omba nafasi ya kusimamia mashamba hayo.

Tatu kuna baadhi ya familia zimebarikiwa kuwa na uwezo mzuri basi omba mtaji kidogo kwenye familia na fanya kijibiashara chochote kila ambacho unaona kinaweza kufanya maisha yako yakaenda.

Nne kwa wale ambao wana ubunifu mdogo mdogo nao ni wakuutumia kuhakikisha mkono unaenda kinywani.

Kikubwa kabisa ni kuhakikisha haukai nyumbani bure ukisubiri ajira.

Mwisho mwishoni niwashauri serikali kubadili mfumo badala ya kuwapeleka wahitimu wa kidato cha sita Jeshini basi wawapeleke veta kujifunza ufundi na ujasiriamali na aakitoka hapo akaenda chuo kikuu kuongeza elimu akihitimu chuo hawezi kosa cha kufanya.

Mwisho niwashauri serikali kuhusu bodi ya mikopo Uwekwe utaratibu utakaowafanya wale wanaafunzi wanaopata mikopo basi kiwango kile kiongezeke na kigawiwwe katika makundi mawili kundi laa kwanza liwe na wakati mwanafunzi yupo chuo na kundi la pili baada ya kuhitimu chuo mfano mimi mpaka namaliza chuo kikuu nimetumia pesa ya bodi ya mikopo 11,745,778/= katika hicho kiwango kiongezeke walau million 4 ambazo mwanafunzi atapewa na kwenda kujiajiri huko mtaani hapo ningekuwa na deni la million 15 ambazo zingekuja kulipwa baadae kwa mifumo yao kuliko kumwambia tu muhitimu akajiajiri na hana hata mtaji wa kwenda kujiajiri.

Asanteni karibu unipigie kura.
 
Nimesibitisha kuwa hakuna kipya chini ya jua. Nilikua nawaza same idea kwann serekali Kama in nia wa yasomi wajiajiri isitengeneze mazingira ya kumpatia kiasi flan muhitimi ili akaanzia maisha Kama mtaji wa kujiajiri. Halaf deni ilo liuganishwe kwenye mkopo wa kosomea. Hi ingesaidia kusolve tatizo la mtaji. Ikitokea muhitimu akiutumia vibaja bas ni uzembe wake lakin angelikua kasaidiwa kwa njia moja au nyengine.
Tofauti na kusema kwenye majukwaa watu wajiajiri halaf mitaji hakuna.
Chengine wasomi wengi hawana elimu za ubunifu na kujiajiri need sehemu ya kuangalia sana hii
 
Unapomaliza chuo unakuwa na expectations za hali ya juu..but ukifika kitaa uwanja umeinama ....wazo la kuwapa wahitimu pesa ni zuri but trust me wengi watatumia vbaya....

Boom tu mtu akipata anakuwa mwehu...hapo kaingiziwa 500k ...vp akipewa 4M.. vjn weng wa ki bongo n hadi upitie msotoo flan ndoo huyaelewa maisha...all in all mleta mada kaleta wazo zuri...
 
Nikweli. Lkn ingesaidia kupush kwa wale wenye idea za biashara.
 
Unapomaliza chuo unakuwa na expectations za hali ya juu..but ukifika kitaa uwanja umeinama ....wazo la kuwapa wahitimu pesa ni zuri but trust me wengi watatumia vbaya....

Boom tu mtu akipata anakuwa mwehu...hapo kaingiziwa 500k ...vp akipewa 4M.. vjn weng wa ki bongo n hadi upitie msotoo flan ndoo huyaelewa maisha...all in all mleta mada kaleta wazo zuri...
Wataenda kushinda kidimbwi hapa dar hawatotoka kwenda hata kusalimia makwao
 
Kila mhitimu anapoelekea kuhitimu kungewekwa mfumo wa wa kuandika project proposal za entrepeneurshp kuanzia mwaka wa pili wa masomo na zikawa financed na bodi ya mkopo kwa awamu kutokana na ukuaji unaoridhisha,na pesa ya mtaji itolewe kwa phases,hadi kuhitimu tayari projects zinakua zimesimama,lakini pia iundwe tume ya kusimamia hizi projects
 
Agiza soda nitalipa
 
Back
Top Bottom