Maiko Jackson njooo.... Kama hutaki nenda. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maiko Jackson njooo.... Kama hutaki nenda.

Discussion in 'Entertainment' started by Bujibuji, May 19, 2012.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,381
  Likes Received: 22,253
  Trophy Points: 280
  Naomba nijuzwe, huu wimbo uliimbwa na nani na unaitwaje?
   
 2. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,141
  Trophy Points: 280
 3. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Umenikumbusha mbali, enzi nikiwa mdogo mm na ndugu zangu tulikua tunashindana kucheza mabreka, na kuna huu mwingine wa Michael J. unaimba makusamba kusamba makusa, tulikua tunacheza mpaka basi. Utoto raha jamani, NATAMANI KUWA MTOTO TENA
   
 4. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #4
  May 19, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,141
  Trophy Points: 280
  Zamani kila wimbo mzuri tulikuwa tunajua wa Wacko Jacko
   
 5. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  Ha haa haaa those were the days!

  Ratiba yangu ilikuwa kama ifuatavyo,
  Jummosi kama leo mida kama hii nakwenda zangu kuogelea TTI Club Kidatu huko,
  saa saba nakwenda kuangua maembe Ng'ongo na makungu,
  Saa tisa tunakwenda kuendesha malingi ya magari,
  Saa 12 narudi TTI Club kuangalia Video ya KOmando john
  Saa 2 narudi home nyumba namba 28
  nikifika home napita mlango wa nyuma, mara naitwa na mshua kwa ajili ya bakora kwa nini sijakwenda Tuition kwa mwalimu Chacha?
  Nikitoka kwenye bakora za mshua naingia chumbani ili mshua aone kuwa ameniumiza sana najifunga vitambaa sehemu zote nilizovimba kwa ajili ya bakora za mshua, then nakwenda kula na vitambaa (bandeji) zangu.

  Hahaa haaaa.... Xmas sasa ikifika ngoma ndo hizo za kina Maiko Jackson, james Ingram, Mavin gaye, makali wetu wa ku-sakata dance alikuwa jamaa anaitwa Aigele na maulid mrisho washikaji ambao siku zote za sherehe kama hizo walikuwa wanachukua zawadi za Double cola na seven up!

  Zamani raha sana ilikuwa...
   
 6. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #6
  May 19, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Bjbj umenikumbusha....

  akusamba kusamba Mwakyusa
  katia kidole kanusa,
  kenda kusema kwa Mussah,
  Mussah nae kanusa. lol

  Naona ndio huyo huyo atakua kaimba na huo wako..
   
 7. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #7
  May 19, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Na ile nyimbo ya Maiko Jaksoni,
  Nataka binzali saba, nataka binzaliiii sabaaaa.
   
 8. L

  Luushu JF-Expert Member

  #8
  May 19, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 596
  Likes Received: 233
  Trophy Points: 60
  Hizo nyimbo zete zimeimbwa mkali wa pop MICHAEL JACKSON zikiongozwa na wimbo wa thriler ulimpatia umaarufu mkubwa na pesa nyingi kuliko albam zake zote.Kuna wimbo siukumbuki jina alipiga mwaka 1987 ujerumani magharibi,watu wa ujerumani mashariki waliparamia ukuta kuvuka wakaone shoo wengi walijeruhiwa na askari kipindi hicho nchi hizi zikuwa zimetengwa na ukuta uliojulikana kwa jina la BERLIN WALL,hakika umenikumbusha mbali nimewakumbuka akina EROTIKA MADONA,WHITNEY HOUSTON,MARVIN GEY,SIR ELTON JONH,LIEON RICH,UB 40,PETER TOSH,BOB MARLEY,JULIE EGLISHEZ,COOL AND THE GANG,CHAKACHAKA,na wengine wengi hako ndo kamchango kangu endeleaa
   
 9. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #9
  May 19, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,141
  Trophy Points: 280
  Mnazikumbuka zile kalata za kwenye chewing gum, zilitoka mwaka 1987/88 na kalata ngumu kabisa kuipata ilikuwa ya Michael Jackson?
   
Loading...