Mahusiano ya kimapenzi kati ya Reporters na Sources wao, nani wa kulaumiwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahusiano ya kimapenzi kati ya Reporters na Sources wao, nani wa kulaumiwa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bazobonankira, Jun 8, 2009.

 1. Bazobonankira

  Bazobonankira Senior Member

  #1
  Jun 8, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wasalaam,

  Kidogo ningependa kupata msaada katika hili. Kumekuwa na tetesi na hata mara nyingine ushahidi wa waziwazi au wa kimazingira juu ya kuwepo uhusiano wa kimapenzi kati ya waandishi wa habari na watoa habari wao.

  Binafsi, sidhani kama ni jambo jema kimaadili, hasa ya uandishi wa habari. Wapo wanaoamini kuwa uhusiano huu si tatizo, alimradi tu unakurahisishia kupata habari. Pia wapo wanaoamini kuwa huku ni kuidhalilisha taaluma na wadau wote! Wapo waliodiriki kutembea na mawaziri, wakurugenzi wa idara nyeti, wakuu wa wilana au mikoa, wanasiasa mashuhuri na wengine hata viongozi wao makazini au katika taasisi shirikishi.

  Wadau mnasemaje?
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,596
  Likes Received: 18,592
  Trophy Points: 280
  Mising ya uhusiano kati ya mwandishi na source wake ni fidutiary relationship inayohusiana na uwajibikaji kama boss na secretary wake, daktari na mgonjwa, mwanasheria na mteja, kiongozi wa dini na muumini, mwalimu na mwanafunzi etc.Mahusiano yanatakiwa yawe ya heshima na uwajibikaji, yanapogeuka kuwa mapenzi, basi mapenzi haya yawe ya kibinaadamu kama ambavyo unaweza jikuta bosi anampenda secretary wake kwa dhati na sio kwa sababu ni secretari wake, na mapenzi haya lazima yawe nje ya mahusiano ya uwajibikaji.Naomba tutofautishe mapenzi haya na hongo ya mapenzi ambapo mwandishi anajirahisi kwa source ili aweze kupata exclusive headline story kwa ajili ya kazi. Kwa upande wangu, this is ok, unatakiwa kutumia mbinu zozote, safi au chafu kupata unachokitaka.Hongo hii hutumika hata kwa polisi wasikufikishe kituoni, utahonga mapenzi kwa majani ili nduguyo usipate hukumu kali, atahonga penzi mpaka kwa muuza genge ili upate nyanya za bure.Akiondoa hongo ya penzi kupata unachokitaka, kuna mahusiano ya mapenzi kati ya mwandishi na source, sio ili apate habari, bali apate pesa na mafanikio kimaisha, huku sasa ni kujiuza. Wanaujiuza kwa masorce hao ni wauzaji, ina maana yoyote akifika bei, bidhaa anapatiwa. Mimi ni mmoja wa ninaowaunga mkono asilimia 100% hawa dada zetu wanaujiuza ili kupata maisha bora, gari nyumba na mahitaji muhimu, as long as dhamira zao haziwasuti.Kama mtoto wa kike anaweza kujitoa mwili wake utumike na yule anayemuona ni mpwenzi wake, na akishatumika anajisikia raha kutoa penzi kwa mpenziwe hata kama hajapata kitu, sio ubaya kutoa penzi huku unapata na kitu zaidi ya penzi, nyumba, gari mapesa kibao, tatizo liko wapi?.Mambo ya morals ni subjective, mwingine thamani mtu kwake ni utu wake na heshima kwake ni kujiheshimu, na mwingine thamani mtu kwake ni kitu sio utu hivyo ni kazi ya kula vichwa kwa kwenda mbele.
   
 3. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,087
  Likes Received: 1,733
  Trophy Points: 280
  Nani kasema kuwa 'sources' are always men and news 'seekers/reporters' are always women?
  A sheer misconception!
   
 4. Bazobonankira

  Bazobonankira Senior Member

  #4
  Jun 8, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kazi kwelikweli. Mwanzoni nilipowaza juu ya jambo hili, sikuweza kupata picha kwa kiasi wadau wanavyonieleza hapo juu.

  Nazidi kujifunza siku hasi siku!
   
Loading...