Abunwasi
JF-Expert Member
- Jun 25, 2009
- 5,486
- 3,468
Waesraeli na Waarabu wakuwa na tofauti hizi miaka karibu elfu tatu.Huna haja ya kutushukuru swala ni kwamba wewe una udini ktk akili yako. Akina Michuzi na mjengwa waliona unaongelea ujinga wakakupiga chini, lakini uzuri wa JF unaachiwa uwanja ili ukomeshwe na wanajamii wenyewe.
Huwezi ukawa na akili timamu ukawatetea waarabu kwa kuendelea kunufaika na ziwa victoria ili sisi tusitumie kwa manufaa ya wananchi wetu. Tena naomba tufungue ubalozi nchini Israel haraka mwaka huu.
Na tofauti walizokuwa nazo haziwezi kuondoka katika miaka mingine elfu tatu kama wote hawatobadilika kimtazamo/mila/tamaduni/siasa. Kwa hii miaka ya karibuni ukweli ni kuwa waarabu kipindi cha nasser walipiga mahesabu mabovu na kusababisha kupigwa vibaya sana na ardhi yao kutekwa na nadhani kwa vile nchi ya israel ni ndogo wanataka kutumia maeneo haya kama buffer zone.
Rais Anwar Sadat alijaribu sana kubadilisha mtizamo kwa kutambua kuwa israel ni lazima iendelee kuwepo na waarabu lazima wakubali hali hiyo. Lakini matokeo yake walimwita msaliti na kumua. Tangu hapo hakuna kinachoendelea kwa sababu hao wapalestina wenyewe hawaelewani. Kwa wasiofahamu hawa jamaa kuna nchi kadhaa za kiarabu haziwataki kutokana na matatizo yao.
Ukiangalia hata lebanon wamechangia kwa kiasi kikubwa matatizo ya nchi hiyo. Misaada ambayo waarabu wenzao wamewapa ingeweza kubadilisha kabisa hali yao kwenye maeneo ya westbank na gazza lakini wapi na wanafanyiana ushenzi ambao siyo rahisi sisi kuelewa. Kwa mfano wale wanao unga mkono kundi la PLO upande wa gazza hata kazi serikalini wanafukuzwa. Na katika kipindi kile ambacho Israel ilikuwa inaiharibu gazza wafuasi wa PLO walikuwa wanaogopa zaidi watu wa Hamas kuliko Israeli. na ukweli ni kuwa wa PLO wengi wailipigwa risasi za magoti [eti wasaliti].
Waafrika tuna matatizo ya kutosha hivyo wakati umefika tuangalie namna tutakavyoweza kuyatatua- IT TAKES 2 TO TANGO