Mahusiano ya kidiplomasia kati ya Tanzania na Israel | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahusiano ya kidiplomasia kati ya Tanzania na Israel

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KIPOLE, Jan 13, 2010.

 1. K

  KIPOLE New Member

  #1
  Jan 13, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi karibuni nilisoma katika tovuti ya Michuzi kuwa Waisraeli wanataka kusaidia miradi mbalimbali Tanzania. Kwa bahati mbaya niliandika maoni kama blog wa Michuzi lakini inaonekana Michuzi ni mtu wa system kwa hiyo maoni yangu ambayo nayaambatanisha hapa, akayatia kapuni.

  Nikajaribu kumuomba ndugu Mjengwa katika blog yake nae pia hakuweza kuyaweka. Nikajua kuwa wote wanaganga njaa na hawako serious na kutoa forum kwa wananchi kutoa maoni yao. Haya hapa ndio maoni yangu kuhusu uhusiano wa Tanzania na Israel.

  Kitu kimoja kinanishangaza sana kuhusu hawa Waisraili.Udhalimu wanaoufanya kwa wapalestina wanapata wapi utu wa kuja kusaidia miradi ya Tanzania? Hapa lipo neno.

  Waisraili wanataka kudhibiti chanzo cha maji ya mto Nile ili kuwaadhibisha na kuwatia shindikizo watu wa Misri ambao uhai wao unategemea maji ya mto Nile. Walienda kwa Uganda na kufanikiwa. Huko walijenga bwawa kubwa linalotumia maji ya ziwa Victoria. Sasa wako Tanzania. Si kweli kuwa wana nia ya dhati ya kusaidia miradi, wana lao hawa. Wanachokitaka ni kuona maji ya Ziwa Victoria yanatumiwa sana ili kupunguza kina cha maji cha mto Nile na baadae kuifanya Misri ikose maji ya kutosha. Hii itawawezesha wao kuipiga kabari Misri ambayo kuna wakati hufurukuta ili kuwasaidia Wapalestina. Kwa mfano hivi karibuni Misri iliruhusu msafara wa misaada unaoelekea Gaza kupita nchini mwao. Jambo kama hili haliipendezi serikali ya Israel.

  Kwahiyo uhusiano huu na Israel una neno. Najua ingekuwa ni kipindi cha mwalimu Nyerere na uhai wa Yasser Arafat wasingeweza kuja kuingia kirahisi Bongo kutokana na msimamo wa mwalimu. Lakini mwalimu Nyerere hatunae tena na Yasser Arafat pia kwahiyo Israel wameutumia huu mwanya.

  Je, wadau wengine wanasemaje?

  =========
  Januari 2011:
  Agosti 2012:
  Aprili 2013:
  July 2014:
   
 2. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 667
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Hizo ni hisia zako tu ndugu kwani hazina ushahidi. Baniani mbaya kiatu chake dawa. Hata kama unamchukia mtu kiasi gani,siku akikufanyia zuri mshukuru.

  Waisrael tunajua wamepiga hatua katika teknologia za umwailiaji na kilimo. Kama watakuja kutusaidia kulitumia ziwa victira vizuri itakuwa jambo jema kuliko kuacha liendelee kufaidisha watu wengine huku sisi ambao liko kwetu hatufaidiki nalo.

  Wewe unaonyesha ni mzalendo zaidi kwa mataifa ya kiislamu kuliko hata Tanzania,inawezekana labda siyo raia wa Tz. Maana unaona sisi tukisaidiwa kutumia ziwa vizuri itakuwa vibaya kisa eti wamisri wanatumia maji yale.

  Acha mawazo mgando,mambo ya mlengo wa kushoto au kulia hayana maana,kama mtu anakusaidia bila masharti magumu yanayokufanya upoteze utu wako pokea msaada.
   
 3. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kutokana na maoni yako, ndio maana wakina michuzi hawakuweka bandiko lako kwani limejaa mizengwe.

  Kama wewe ni mpenda maendeleo ya nchi yako cha kuzingatia ni kuwa kama wewe mtanzania utafaidika vipi na hiyo miradi. Hata maandiko yalisema "Mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe".
   
 4. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #4
  Jan 13, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,857
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  WAYAHUDI wamesaidia sana nnchi hii kuliko Waarabu wote kwa ujumla wao......walijenga miundombinu mingi tu miaka ya sabini, walienga Ruvu sekondari, Kibiti Sekondari , Ifakara Sekondari, wamejenga jengo la BIMA makao Makuu, Walijenga Ardhi House na majengo mengi makubwa kwa msaada ....magomvi yao na waarabu sisi hayawezi kutunyima usingizi, watatue wenyewe matatizo yao kwa dhati sio kutuchagulia rafiki.
   
 5. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2010
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Waisraeli ni Watu wema sana
  Tungekuwa na uhusiano nao tangu awali tungekuwa tupo mbali sana kama Wamarekani na Wengineo ambao wanajua umuhimu wa "Taifa la Israeli"

  Wote wanaompinga Muisrael Wamelaaniwa laana ya Milele na wataendelea kuwa Maskini kama Watanzania tunavyoendelea kudidimia.

  Mungu tusaidie, muongezee Hekima Rais wetu ili UHUSIANO WA TANZANIA NA ISRAELI UDUMU MILELE.

  Mungu Ibariki Tanzania na Watu wake.
   
 6. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,056
  Likes Received: 3,416
  Trophy Points: 280
  Kwanza naomba kutokubaliana na mawazo yako ambayo yana kila chembe ya ubaguzi dhidi ya taifa la Israel. Inavyoelekea hujui taifa la Israel limewahi kusaidia miradi mikubwa ambayo mpaka leo bado inafaida kubwa kwa nchi inayokabiliwa na umasikini mkubwa ingawa imejaliwa utajiri wa rasilimali.

  Miradi ya ujenzi wa hotel ya Kilimanjaro, Seventy seven na makambi ya JKT ni baadhi ya mifano mizuri jinsi taifa la Israel lilivyosaidia Tanzania. Tangu tuvunje uhusiano na taifa la Israel na kujikita zaidi katika siasa za kuwasaidia waarabu hakuna faida ambayo tunaweza kujivunia au mafanikio tulipata kama nchi kwa kuziunga mkono nchi za kiarabu. Nchi nyingi za kiarabu zina uatajiri mkubwa wa mafuta lakini utajiri wa haujawa kutumika kuzisaidia nchi masikini za kiafrika ambazo mara nyingi zimekubali kutumika kidiplomasia kuzisaidia nchi za kiarabu.

  kuhusiana na matumizi ya maji ya ziwa Victoria unapaswa kuelewa kwamba Tanzania na nchi nyingine zinazozunguka ziwa hilo kubwa barani Afrika zina haki ya kutumia maji yake kwa faida ya wananchi wake. Upo mkataba uliowekwa enzi za ukoloni ambao uliipendelea Misri kwa kuipa haki ya kutumia maji ya mto Nile na kuziacha nchi nyingine kama watazamaji au waangalizi/ watunzaji wa chanzo cha maji ya mto Nile.

  Nitafurahi sana siku Israel itakapotoa msaada wa kutujengea mabwawa makubwa ya maji kutoka ziwa Victoria ili wananchi wanaopata shida ya maji katika maeneo yanayozunguka ziwa Victoria wapate maendeleo ambayo mwenyezi mungu alikusudia tangu kuumbwa kwa dunia hii badala ya kuyaachia maji hayo yaendelee kuwanufaisha waarabu wa Misri na Sudan pekee yao.
   
 7. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,035
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Jengo la ushirika, kilimanjaro hotel, Bugando Hospital, hata nyerere yamkini baadaye alijilaumu kuvunja uhusiano na israel.

  Kipole, ondokana na hisia za kidini na migogoro ya kihistoria ya karne nyingi ya mashariki ya kati ambayo wala huielewi hata chembe and be realistically a man of fact, a tanzanian. For your info hata Serikali ya Zanzibar mwaka jana ilipeleka wataalamu wake israel kujifunza namna ya kutengeneza umeme kwa kutumia upepo wa baharini unataka kuwaeleza nini wazanzibari?
  Porojo zako hazina kichwa wala miguu.

  Ndiyo maana michuzi na mjengwa walikotolea nje!
   
 8. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #8
  Jan 13, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Ningekuwa mbunge ningeomba private motion ya hii issue!South Africa,Nigeria,Angola,Kenya,Ethippia na Ivory Coast ambayo inawakilisha(Liberia,Togo,Burkina Farso,Benin) zote zina full diplomatic relationship na Israel.

  Why not Tanzania?Mgogoro wa Palestine upo,ni waarabu wenyewe!As a Tanzania mbantu,niko troubled na Sudan than Israel.Wausi wenzetu wanapata shida sana kule Darfur!Angalieni Southern Sudan ambayo wamepigana na waarabu wa kaskazini miaka yoyote.Ukiangalia Darfur ni humiliation of an african man,kwa sabauu ya skin colour.

  Ukiangalia waarabu kama Saud Arabia,wao ni kujaribu kueneza dini ya kiiislamu (Wahabism) na kuleta machafuko nchi nyingi.Michango ya Israel miaka ile ulikuwa mkubwa sana,wangetupa technical assistance mpaka sasa kwenye field nyingi sana.

  Waarabu wametuweka chini sana,mpaka sasa kuna capiatl flight toka Tz to Dubai,
  kununua magari na hata kuna fununu pesa za EPA zipo huko.
  Wake up Tanzania!
   
 9. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2010
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ndugu yangu Mmakonde, Umesema na mwenye Macho ya kusoma amesoma. Lakini atakaye pinga hii hoja ataipinga kwa sababu ya NJAA.
   
 10. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #10
  Jan 13, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,096
  Likes Received: 247
  Trophy Points: 160

  Kwani sisi wakati tunapambana na Iddi Amini Dada si hao hao Wapalestina na Walibya walikuwa upande wa Amini kijeshi kwa maana kwamba wanamgambo wa PLO na wale wa Libya walikuwa sehemu ya majeshi ya Amini? Sasa huo sio udhalimu wa Wapalestina wa kumsaidia yule nduli atuangamize sisi? Wapalestina waendelee kupambana kivyao, watuache sisi tupatiwe misaada na Waisraeli! Huku kuanza kuchambua utakuta hakuna taifa "zuri!" Yote ni mabaya na yote ni mazuri vile vile, it depends na intepretation ya mhusika!
   
 11. O

  Omumura JF-Expert Member

  #11
  Jan 13, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwanza mie naona tumechelewa sana kufungua ubalozi wetu kule israel simply because ya kufuata misimamo mingine isiyo na tija hata kidogo kwa ufanisi na maendeleo ya taifa letu, long live ISRAEL!
   
 12. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #12
  Jan 13, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,035
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Usisahau hata nchi za kiarabu na za kiislam - Jordan, Misri, Morocco, na hata Mauritania
   
 13. K

  KIPOLE New Member

  #13
  Jan 13, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nawashukuru wachangiaji wote kwa kutokunielewa. Lakini mchezo wanaoufanya waisraeli iko siku utakuja kusababisha vita vikubwa sana. You have been warned!

  Wale wanaowatetea kina Michuzi lakini hawakuwa na hoja.Ni woga tu ndio uliowafanya wasiweke maoni yangu. Kwani wangeweka na watu wakachangia kwa kutokukubaliana nami ingekuwaje? Si ingekuwa wamepanua wigo wa demokrasia. Sasa wanajifanya wana blog za jamii kumbe wanatangaza harusi na ziara za serikali na kwa Mjengwa, ziara zake za Dar na Iringa.
   
 14. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #14
  Jan 13, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,096
  Likes Received: 247
  Trophy Points: 160
  Bado hujatueleza kwamba wewe ugomvi wa Wapalestina na Waisraeli wewe unakuhusu nini? Na je, Wapalestina ni bora kuliko Watanzania? Mbona hao Wapalestina walimsaidia Idi Amini Dada 1978 - 1979 ili kupambana na Tanzania? Huo si udhalimu wa Wapalestina? Na hiyo vita unayoisema itatuhusu sisi peke yake au na nchi zote zenye uhusiano na Israeli zikijumuisha nchi za Kiarabu kama Jordan, Misri, Uturuki, nk? Bado hujatupa maelezo yanayoingia akilini ndugu Kipole! Kama Utanzania umekushinda unaweza kuhamia huko huko Palestina, acha kutupa vitisho vya bure!
   
 15. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #15
  Jan 13, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Kazi ipo
   
 16. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #16
  Jan 13, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  KIPOLE wewe ni mtanzania mweusi sio?Yana kuhusu nini Israel/palestine?
  Naomba mchango wako kuhusu DARFUR/southern sudan watu wanaofanana na wewe?
  Hawa wanasuffer zaidi mikononi kwa Waarabu wa North.

  Hii propaganda za kiaarabu hazikusaidii!Fungua ubongo wako?Tanzania inatakiwa tuwe na Ubalozi Israel.Sikujua Bugando ndio wao walijenga?????If so,ni jengo zuri sana,nilifika hapo miaka 20 ishirini iliyopita.Of course Kilimanjaro Hotel recently.

  Mwarabu wa nini???????????????????????????????
   
 17. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #17
  Jan 13, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,830
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Hana lolote huyu jamaa, ana UDINI kichwani mwake, na hilo limempofusha anashindwa kuangalia ndugu zake kule Darfur anashabikia MAARAB hawa hawa waliochukua babu zetu kama watumwa
   
 18. O

  Omumura JF-Expert Member

  #18
  Jan 13, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Huwezi kutumwa umlete binadamu mwenye akili timamu halafu ukambeba mwarabu,yapo hivyo hivo yalivo!
   
 19. J

  JOHN KITABI Member

  #19
  Jan 13, 2010
  Joined: Nov 10, 2007
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hata ifm wayahudi walijenga. na majengo ya wayahudi yako imara sana
   
 20. M

  Magezi JF-Expert Member

  #20
  Jan 13, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  Tena waisraeli wamechelewa nakumbuka mwalimu nyerere alipingana nao na akatunyima maendeleo kwani waisraeli walitaka kutujengea mradi wa maji mkubwa kutoka ziwa victoria hadi shinyanga, dodoma, na singida.

  Ina shangaza kuona sisi wenye ziwa victoria hatufaidiki lakini eti kwa sababu tukitumia maji yale wamisri watakufa......si bora wafe?

  Big up Israel.......njooni mtujengee miradi ya umwagiliaji kutoka ziwa victoria nasi tufaidike na raslimali zetu.......wamisri watafute vyanzo vingine......wasafishe maji ya bahari watumie.
   
Loading...