Mahusiano ya kidiplomasia kati ya Tanzania na Israel

KIPOLE

New Member
Jan 13, 2010
2
1
Hivi karibuni nilisoma katika tovuti ya Michuzi kuwa Waisraeli wanataka kusaidia miradi mbalimbali Tanzania. Kwa bahati mbaya niliandika maoni kama blog wa Michuzi lakini inaonekana Michuzi ni mtu wa system kwa hiyo maoni yangu ambayo nayaambatanisha hapa, akayatia kapuni.

Nikajaribu kumuomba ndugu Mjengwa katika blog yake nae pia hakuweza kuyaweka. Nikajua kuwa wote wanaganga njaa na hawako serious na kutoa forum kwa wananchi kutoa maoni yao. Haya hapa ndio maoni yangu kuhusu uhusiano wa Tanzania na Israel.

Kitu kimoja kinanishangaza sana kuhusu hawa Waisraili.Udhalimu wanaoufanya kwa wapalestina wanapata wapi utu wa kuja kusaidia miradi ya Tanzania? Hapa lipo neno.

Waisraili wanataka kudhibiti chanzo cha maji ya mto Nile ili kuwaadhibisha na kuwatia shindikizo watu wa Misri ambao uhai wao unategemea maji ya mto Nile. Walienda kwa Uganda na kufanikiwa. Huko walijenga bwawa kubwa linalotumia maji ya ziwa Victoria. Sasa wako Tanzania. Si kweli kuwa wana nia ya dhati ya kusaidia miradi, wana lao hawa. Wanachokitaka ni kuona maji ya Ziwa Victoria yanatumiwa sana ili kupunguza kina cha maji cha mto Nile na baadae kuifanya Misri ikose maji ya kutosha. Hii itawawezesha wao kuipiga kabari Misri ambayo kuna wakati hufurukuta ili kuwasaidia Wapalestina. Kwa mfano hivi karibuni Misri iliruhusu msafara wa misaada unaoelekea Gaza kupita nchini mwao. Jambo kama hili haliipendezi serikali ya Israel.

Kwahiyo uhusiano huu na Israel una neno. Najua ingekuwa ni kipindi cha mwalimu Nyerere na uhai wa Yasser Arafat wasingeweza kuja kuingia kirahisi Bongo kutokana na msimamo wa mwalimu. Lakini mwalimu Nyerere hatunae tena na Yasser Arafat pia kwahiyo Israel wameutumia huu mwanya.

Je, wadau wengine wanasemaje?

=========
Januari 2011:
Habari wa Jf,

Nimesikia Tanzania ilivunja uhusiano na Israel tangu 1960, jambo hili limenishtua kidogo kwa kufuatana na kitabu cha dini ninachokiamini kinasema ANAYEMBARIKI ISRAEL ANABARIKIWA NA UKIMLAANI UNALAANIWA NA MUNGU, nisaidieni jamani kwa anayejua kama tuna balozi hapa Tanzania.
Pole sana umepewa majibu laini sana ila ni kwamba kipindi fulani wakati wa utawala wa nyerere israel ilishambulia wapalestina sana na kuua watu wengi, sasa kwa vile nyerere alikua hapendi ukandamizani kama unaofanywa na marekani huko libya, alivunja uhusiano na israel kama inshara ya kupinga vitendo vyao dhidi ya wapalestina! Kabla ya hapo uhusiano ulikua safi sana, wao ndio waliojenga majengo ya maana ya zamani hapa dar es salaam kama kitega uchumi, jengo la ushirika, chuo kikuu cha dar es salaam na hospitali ya bugando mwanza!, sina uhakika na muhimbili ila nadhani ndio wenyewe! na ubalozi wao ulikua pale ubalozi wa marekani uliolipuliwa na magaidi ulipo! Shughuli zao za kijasusi kwa tanzania walitumia ubalozi wa marekani!

Waumini wa biblia wanasema tanzania ina laana kwani imeandikwa atakaemlaani israel amelaaniwa! Karibu sana

Serikali ya Nyerere ilivunja uhusiano na Israel mwaka 1967 kwa sababu Israel iliikalia Sinai Peninsula baada ya Six Day War.
Nasikia kabla ya hapo Israel walikuwa wametusaidia kwenye ujenzi wa majengo kadhaa likiwemo jengo la makao makuu ya Usalama wa Taifa to name the few.

With my little knowledge ubalozi wao ulikuwepo na ndiyo waliotujengea miundombinu kama ya AICC- kule Arusha; Bugando hospital MWanza na sehemu nyingi hasa public buildings na kulikuwepo na kampuni moja ikiitwa COSATA hii kampuni ni ya kiyahudi.

Ikumbukwe pia baada ya vile vita ya ^6 days war Wayahudi walikuja kumfuta JK na kumwuliza kama angependa kuuchimba mfereji wa kumwagilia kilimo cha mizabibu kule Dodoma na kumwagilia vijiji vya jirani basi wangeweza kuuchimba huo mfereji utakaomwaga maji yakitokea Lake Victoria kupitia Nyarugusu kote huko Igunga mpaka singida hadi Dom pia hata meli ndogo zingeweza kuutumia na kumaliza zogo la usafiri na samaki. Hata hivyo JK kushauriana na wakandarasi wake ndani ya ikulu walimweleza this is an issue kwani ziwa victoria liko mlimani na linamwaga maji kuelekea bondeni maana yake ukichimba mfereji kwa upande wa kusini unakausha Nile river and its tributaries na ndo mwi=sho wa Misri kwani Nile is Egypt and egypt is Nile.

Wamisri wakawa ndo victims wa vita vya 6 days war kwani they are one hosted that military base. Ndo hata juzi kama umeona wamisri walipoandamana kwenye ubalozi wao hata waliochukua nchi hawakusema kitu kwani wanajua kuna nini kitatokea wakiuvunja ule mkataba wa mwaka 1972. nao wayahudi hawajsema kama watauhamisha ubalozi wao kutoka Misri au la.. pengine kuna alieye na mpya zaidi kuhusu hii point ya Israili na egypt jamani atujuze..

Turudi kwenye point kule juu . Sisi ni taifa lisilofungamana na upande wowote, lina watu wake wenye dini tofauti na lenye kufuta haki za binadamu na halina dini kikatiba wala ubaguzi wa rangi. Mwaka 1975s bila kukosea kulitokea mauaji ya watoto wachanga wasiojua dini wala siasa waliuawa kule Gaza yaani mauaji ya kimbari yaliyo hitimishwa na majeshi ya Kiyahudi.

Wazee wakamfuata JK na kumwuuliza mbona sisi ni nchi ya watu isio na katiba ya dini na tunaheshimu nchi nyingine na zisizo fuata haki za binadamu siyo marafiki wetu? iweje hawa marafiki wetu wawauwe watoto wasio na dhambi na wasio jua dini wala siasa? kweli tuwakubali hawa watu??. Isareli haikujutia lile jaribio wala kuomba msamaha kwa watu Kipalestina.

Kambarage siku iliyofuata akina Butiku wakamweleza mzee chomoa ubalozi kule na waite Wapalestina. Ndo mpaka leo tunaitambua mamlaka ya kipalestina hapo Bongo.
Agosti 2012:
Swali la Asumpta Mshana; ameuliza "Kwanini Tanzania haina balozi nchini Israel, ikizingatiwa kuwa watanzania wengi wanaenda Israel kwa masuala ya kiimani na kibiashara?"

Naibu waziri amejibu kuwa Tanzania ina balozi Israel, lakini anaiwakilisha kutoka Misri.

kaaazi kweli!
Aprili 2013:
Asikofu Gamanywa leo kasema Tanzania haiwezi kufanikiwa kiuchumi na kisiasa sababu haina mahusiano mazuri na Israel. Kasema mataifa makubwa yote yana mahusiano mazuri na Israel ya kiuchumi.

Kayataja Marekani, China, Japan, India, Ujerumani, Urusi, Brazil, Uingereza, Ufaransa na Italia; lakini Tanzania haina hata balozi israel.
2% ya wamarekani ni wayahudi.

Ametoa ujumbe kwa serikali ya Tanzania kufungua mahusiano na Israel. Tuache kuingilia ugomvi wa Ishmael na Isaka sisi hautuhusu kasema Askofu.

=====

Askofu Gamanywa anasema tukiwa connected na Isaka, baraka za kiuchumi zitakuja.

Gamanywa anasema pigeni kelele na Israel lakini pataneni na Israel kiuchumi kama mataifa mengine ili Tanzania ifanikiwe.

Amesema Ishmail ni mwarabu na Isaka ndipo baraka zetu zilipo kutokana na mandiko katika biblia. Sisi ugomvi wa waarabu na wayahudi hautuhusu.

Tunachotakiwa ni kuinuka kiuchumi na hiyo haiwezekani bila kuwa na mahusiano mazuri na Israel. Waisrael wameahidiwa kuwa kichwa na sio mkia katika biashara.

July 2014:
TZ mnasema hakuna Balozi wa Israel na hapa kama picha inavyoonesha ni kwamba Balozi Seif Idi anamkabidhi zawadi ya mlango Balozi wa Israel nchini TZ baada ya kumaliza muda wake.

attachment.php
 
Hizo ni hisia zako tu ndugu kwani hazina ushahidi. Baniani mbaya kiatu chake dawa. Hata kama unamchukia mtu kiasi gani,siku akikufanyia zuri mshukuru.

Waisrael tunajua wamepiga hatua katika teknologia za umwailiaji na kilimo. Kama watakuja kutusaidia kulitumia ziwa victira vizuri itakuwa jambo jema kuliko kuacha liendelee kufaidisha watu wengine huku sisi ambao liko kwetu hatufaidiki nalo.

Wewe unaonyesha ni mzalendo zaidi kwa mataifa ya kiislamu kuliko hata Tanzania,inawezekana labda siyo raia wa Tz. Maana unaona sisi tukisaidiwa kutumia ziwa vizuri itakuwa vibaya kisa eti wamisri wanatumia maji yale.

Acha mawazo mgando,mambo ya mlengo wa kushoto au kulia hayana maana,kama mtu anakusaidia bila masharti magumu yanayokufanya upoteze utu wako pokea msaada.
 
Kutokana na maoni yako, ndio maana wakina michuzi hawakuweka bandiko lako kwani limejaa mizengwe.

Kama wewe ni mpenda maendeleo ya nchi yako cha kuzingatia ni kuwa kama wewe mtanzania utafaidika vipi na hiyo miradi. Hata maandiko yalisema "Mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe".
 
WAYAHUDI wamesaidia sana nnchi hii kuliko Waarabu wote kwa ujumla wao......walijenga miundombinu mingi tu miaka ya sabini, walienga Ruvu sekondari, Kibiti Sekondari , Ifakara Sekondari, wamejenga jengo la BIMA makao Makuu, Walijenga Ardhi House na majengo mengi makubwa kwa msaada ....magomvi yao na waarabu sisi hayawezi kutunyima usingizi, watatue wenyewe matatizo yao kwa dhati sio kutuchagulia rafiki.
 
Waisraeli ni Watu wema sana
Tungekuwa na uhusiano nao tangu awali tungekuwa tupo mbali sana kama Wamarekani na Wengineo ambao wanajua umuhimu wa "Taifa la Israeli"

Wote wanaompinga Muisrael Wamelaaniwa laana ya Milele na wataendelea kuwa Maskini kama Watanzania tunavyoendelea kudidimia.

Mungu tusaidie, muongezee Hekima Rais wetu ili UHUSIANO WA TANZANIA NA ISRAELI UDUMU MILELE.

Mungu Ibariki Tanzania na Watu wake.
 
Kwanza naomba kutokubaliana na mawazo yako ambayo yana kila chembe ya ubaguzi dhidi ya taifa la Israel. Inavyoelekea hujui taifa la Israel limewahi kusaidia miradi mikubwa ambayo mpaka leo bado inafaida kubwa kwa nchi inayokabiliwa na umasikini mkubwa ingawa imejaliwa utajiri wa rasilimali.

Miradi ya ujenzi wa hotel ya Kilimanjaro, Seventy seven na makambi ya JKT ni baadhi ya mifano mizuri jinsi taifa la Israel lilivyosaidia Tanzania. Tangu tuvunje uhusiano na taifa la Israel na kujikita zaidi katika siasa za kuwasaidia waarabu hakuna faida ambayo tunaweza kujivunia au mafanikio tulipata kama nchi kwa kuziunga mkono nchi za kiarabu. Nchi nyingi za kiarabu zina uatajiri mkubwa wa mafuta lakini utajiri wa haujawa kutumika kuzisaidia nchi masikini za kiafrika ambazo mara nyingi zimekubali kutumika kidiplomasia kuzisaidia nchi za kiarabu.

kuhusiana na matumizi ya maji ya ziwa Victoria unapaswa kuelewa kwamba Tanzania na nchi nyingine zinazozunguka ziwa hilo kubwa barani Afrika zina haki ya kutumia maji yake kwa faida ya wananchi wake. Upo mkataba uliowekwa enzi za ukoloni ambao uliipendelea Misri kwa kuipa haki ya kutumia maji ya mto Nile na kuziacha nchi nyingine kama watazamaji au waangalizi/ watunzaji wa chanzo cha maji ya mto Nile.

Nitafurahi sana siku Israel itakapotoa msaada wa kutujengea mabwawa makubwa ya maji kutoka ziwa Victoria ili wananchi wanaopata shida ya maji katika maeneo yanayozunguka ziwa Victoria wapate maendeleo ambayo mwenyezi mungu alikusudia tangu kuumbwa kwa dunia hii badala ya kuyaachia maji hayo yaendelee kuwanufaisha waarabu wa Misri na Sudan pekee yao.
 
WAYAHUDI wamesaidia sana nnchi hii kuliko Waarabu wote kwa ujumla wao......walijenga miundombinu mingi tu miaka ya sabini, walienga Ruvu sekondari, Kibiti Sekondari , Ifakara Sekondari, wamejenga jengo la BIMA makao Makuu, Walijenga Ardhi House na majengo mengi makubwa kwa msaada ....magomvi yao na waarabu sisi hayawezi kutunyima usingizi, watatue wenyewe matatizo yao kwa dhati sio kutuchagulia rafiki.

Jengo la ushirika, kilimanjaro hotel, Bugando Hospital, hata nyerere yamkini baadaye alijilaumu kuvunja uhusiano na israel.

Kipole, ondokana na hisia za kidini na migogoro ya kihistoria ya karne nyingi ya mashariki ya kati ambayo wala huielewi hata chembe and be realistically a man of fact, a tanzanian. For your info hata Serikali ya Zanzibar mwaka jana ilipeleka wataalamu wake israel kujifunza namna ya kutengeneza umeme kwa kutumia upepo wa baharini unataka kuwaeleza nini wazanzibari?
Porojo zako hazina kichwa wala miguu.

Ndiyo maana michuzi na mjengwa walikotolea nje!
 
Ningekuwa mbunge ningeomba private motion ya hii issue!South Africa,Nigeria,Angola,Kenya,Ethippia na Ivory Coast ambayo inawakilisha(Liberia,Togo,Burkina Farso,Benin) zote zina full diplomatic relationship na Israel.

Why not Tanzania?Mgogoro wa Palestine upo,ni waarabu wenyewe!As a Tanzania mbantu,niko troubled na Sudan than Israel.Wausi wenzetu wanapata shida sana kule Darfur!Angalieni Southern Sudan ambayo wamepigana na waarabu wa kaskazini miaka yoyote.Ukiangalia Darfur ni humiliation of an african man,kwa sabauu ya skin colour.

Ukiangalia waarabu kama Saud Arabia,wao ni kujaribu kueneza dini ya kiiislamu (Wahabism) na kuleta machafuko nchi nyingi.Michango ya Israel miaka ile ulikuwa mkubwa sana,wangetupa technical assistance mpaka sasa kwenye field nyingi sana.

Waarabu wametuweka chini sana,mpaka sasa kuna capiatl flight toka Tz to Dubai,
kununua magari na hata kuna fununu pesa za EPA zipo huko.
Wake up Tanzania!
 
Ndugu yangu Mmakonde, Umesema na mwenye Macho ya kusoma amesoma. Lakini atakaye pinga hii hoja ataipinga kwa sababu ya NJAA.
 
Kitu kimoja kinanishangaza sana kuhusu hawa Waisraili.Udhalimu wanaoufanya kwa wapalestina wanapata wapi utu wa kuja kusaidia miradi ya Tanzania?

Kwani sisi wakati tunapambana na Iddi Amini Dada si hao hao Wapalestina na Walibya walikuwa upande wa Amini kijeshi kwa maana kwamba wanamgambo wa PLO na wale wa Libya walikuwa sehemu ya majeshi ya Amini? Sasa huo sio udhalimu wa Wapalestina wa kumsaidia yule nduli atuangamize sisi? Wapalestina waendelee kupambana kivyao, watuache sisi tupatiwe misaada na Waisraeli! Huku kuanza kuchambua utakuta hakuna taifa "zuri!" Yote ni mabaya na yote ni mazuri vile vile, it depends na intepretation ya mhusika!
 
Kwanza mie naona tumechelewa sana kufungua ubalozi wetu kule israel simply because ya kufuata misimamo mingine isiyo na tija hata kidogo kwa ufanisi na maendeleo ya taifa letu, long live ISRAEL!
 
Ningekuwa mbunge ningeomba private motion ya hii issue!South Africa,Nigeria,Angola,Kenya,Ethippia na Ivory Coast ambayo inawakilisha(Liberia,Togo,Burkina Farso,Benin) zote zina full diplomatic relationship na Israel.

Usisahau hata nchi za kiarabu na za kiislam - Jordan, Misri, Morocco, na hata Mauritania
 
Nawashukuru wachangiaji wote kwa kutokunielewa. Lakini mchezo wanaoufanya waisraeli iko siku utakuja kusababisha vita vikubwa sana. You have been warned!

Wale wanaowatetea kina Michuzi lakini hawakuwa na hoja.Ni woga tu ndio uliowafanya wasiweke maoni yangu. Kwani wangeweka na watu wakachangia kwa kutokukubaliana nami ingekuwaje? Si ingekuwa wamepanua wigo wa demokrasia. Sasa wanajifanya wana blog za jamii kumbe wanatangaza harusi na ziara za serikali na kwa Mjengwa, ziara zake za Dar na Iringa.
 
Nawashukuru wachangiaji wote kwa kutokunielewa. Lakini mchezo wanaoufanya waisraeli iko siku utakuja kusababisha vita vikubwa sana. You have been warned!

Bado hujatueleza kwamba wewe ugomvi wa Wapalestina na Waisraeli wewe unakuhusu nini? Na je, Wapalestina ni bora kuliko Watanzania? Mbona hao Wapalestina walimsaidia Idi Amini Dada 1978 - 1979 ili kupambana na Tanzania? Huo si udhalimu wa Wapalestina? Na hiyo vita unayoisema itatuhusu sisi peke yake au na nchi zote zenye uhusiano na Israeli zikijumuisha nchi za Kiarabu kama Jordan, Misri, Uturuki, nk? Bado hujatupa maelezo yanayoingia akilini ndugu Kipole! Kama Utanzania umekushinda unaweza kuhamia huko huko Palestina, acha kutupa vitisho vya bure!
 
KIPOLE wewe ni mtanzania mweusi sio?Yana kuhusu nini Israel/palestine?
Naomba mchango wako kuhusu DARFUR/southern sudan watu wanaofanana na wewe?
Hawa wanasuffer zaidi mikononi kwa Waarabu wa North.

Hii propaganda za kiaarabu hazikusaidii!Fungua ubongo wako?Tanzania inatakiwa tuwe na Ubalozi Israel.Sikujua Bugando ndio wao walijenga?????If so,ni jengo zuri sana,nilifika hapo miaka 20 ishirini iliyopita.Of course Kilimanjaro Hotel recently.

Mwarabu wa nini???????????????????????????????
 
Hana lolote huyu jamaa, ana UDINI kichwani mwake, na hilo limempofusha anashindwa kuangalia ndugu zake kule Darfur anashabikia MAARAB hawa hawa waliochukua babu zetu kama watumwa
 
Huwezi kutumwa umlete binadamu mwenye akili timamu halafu ukambeba mwarabu,yapo hivyo hivo yalivo!
 
Hivi karibuni nilisoma katika tovuti ya Michuzi kuwa Waisraeli wanataka kusaidia miradi mbalimbali Tanzania.Kwa bahati mbaya niliandika maoni kama blog wa Michuzi lakini inaonekana Michuzi ni mtu wa system kwahiyo maoni yangu ambayo nayaambatanisha hapa,akayatia kapuni. Nikajaribu kumuomba ndugu Mjengwa katika blog yake nae pia hakuweza kuyaweka. Nikajua kuwa wote wanaganga njaa na hawako serious na kutoa forum kwa wananchi kutoa maoni yao. Haya hapa ndio maoni yangu kuhusu uhusiano wa Tanzania na Israel.

Kitu kimoja kinanishangaza sana kuhusu hawa Waisraili.Udhalimu wanaoufanya kwa wapalestina wanapata wapi utu wa kuja kusaidia miradi ya Tanzania? Hapa lipo neno.

Waisraili wanataka kudhibiti chanzo cha maji ya mto Nile ili kuwaadhibisha na kuwatia shindikizo watu wa Misri ambao uhai wao unategemea maji ya mto Nile.Walienda kwa Uganda na kufanikiwa. Huko walijenga bwawa kubwa linalotumia maji ya ziwa Victoria. Sasa wako Tanzania. Si kweli kuwa wana nia ya dhati ya kusaidia miradi, wana lao hawa.Wanachokitaka ni kuona maji ya Ziwa Victoria yanatumiwa sana ili kupunguza kina cha maji cha mto Nile na baadae kuifanya Misri ikose maji ya kutosha. Hii itawawezesha wao kuipiga kabari Misri ambayo kuna wakati hufurukuta ili kuwasaidia Wapalestina. Kwa mfano hivi karibuni Misri iliruhusu msafara wa misaada unaoelekea Gaza kupita nchini mwao. Jambo kama hili haliipendezi serikali ya Israel.

Kwahiyo uhusiano huu na Israel una neno. Najua ingekuwa ni kipindi cha mwalimu Nyerere na uhai wa Yasser Arafat wasingeweza kuja kuingia kirahisi Bongo kutokana na msimamo wa mwalimu.Lakini mwalimu Nyerere hatunae tena na Yasser Arafat pia kwahiyo Israel wameutumia huu mwanya.

Jee wadau wengine wanasemaje?

Tena waisraeli wamechelewa nakumbuka mwalimu nyerere alipingana nao na akatunyima maendeleo kwani waisraeli walitaka kutujengea mradi wa maji mkubwa kutoka ziwa victoria hadi shinyanga, dodoma, na singida.

Ina shangaza kuona sisi wenye ziwa victoria hatufaidiki lakini eti kwa sababu tukitumia maji yale wamisri watakufa......si bora wafe?

Big up Israel.......njooni mtujengee miradi ya umwagiliaji kutoka ziwa victoria nasi tufaidike na raslimali zetu.......wamisri watafute vyanzo vingine......wasafishe maji ya bahari watumie.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom