Mahusiano mafupi kuliko yote ushawahi kuwa nayo

Nakadori

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
8,781
20,946
Wakuu habari zenu,

Huku tukiutafuta tafuta usingizi hebu tuambiane mahusiano ambayo umewahi kuwa nayo na yakawa mafupi kuliko yote.....

Ukitoa sababu ya kwanini mlidumu muda mfupi hivyo itakuwa vizuri. Binafsi mahusiano yangu mafupi kuliko yote yalichukua week moja.

Nlijiona tu siko sehemu salama nikaamua kukatisha kwa kumtafutia sababu isiyo na kichwa wala mguu na kuendelea na yangu.

Hadi leo yule kaka ananilaumu na ile sababu niliyomtafutia hajaikubali milele.
 
Mie siku mbili tu jamani, Jamaa yule alikua anapiga simu kama customer care. Alafu cha maana hakuna..mara umekula, unafanyaje, nimekumiss mfyuu ila si kosa lake alikua jobless yaan wanaume fanyeni kazi hata kama kuzibua choo wacheni ubishoo.
 
Mie siku mbili tu jamani,Jamaa yule alikua anapiga simu kama customer care.Alafu cha maana hakuna..mara umekula,unafanyaje,nimekumiss mfyuu ila si kosa lake alikua jobless yaan wanaume fanyeni kazi hata kama kuzibua choo wacheni ubishoo.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Kweli wanaume wafanye kazi...
Lakini jaman ss ke tukiwa hatupigiwi simu huwa tunalalamika..tukipigiwa pia tatizo...
Akiuliza umekula inabidi awe ametuma muamala ws chakula
 
Wakuu habari zenu,

Huku tukiutafuta tafuta usingizi hebu tuambiane mahusiano ambayo umewahi kuwa nayo na yakawa mafupi kuliko yote.....

Ukitoa sababu ya kwanini mlidumu muda mfupi hivyo itakuwa vizuri. Binafsi mahusiano yangu mafupi kuliko yote yalichukua week moja.

Nlijiona tu siko sehemu salama nikaamua kukatisha kwa kumtafutia sababu isiyo na kichwa wala mguu na kuendelea na yangu.

Hadi leo yule kaka ananilaumu na ile sababu niliyomtafutia hajaikubali milele.
Sababu gani wewe hiyo nasi wanaume tujihami tukiisikia
 
Kweli wanaume wafanye kazi...
Lakini jaman ss ke tukiwa hatupigiwi simu huwa tunalalamika..tukipigiwa pia tatizo...
Akiuliza umekula inabidi awe ametuma muamala ws chakula
Kujali ni muhimu ila isipitilize jamenii.Kuna mda mtu unahitaji kujishughulisha eti pata picha upo ofisin unapambana na simu ndo kama za hivyo zinaingia si unaeza kuwehuka
 
Mkitaka mapenzi yenu yadumu mmoja wenu inabidi ajifyatue akili bila hivo hamtoboi. Mapenzi na akili haviendi pamoja🚶🚶🚶
255694002377_status_17e0ad5c4233480dbdf211d6c6248842.jpg
 
Kujali ni muhimu ila isipitilize jamenii.Kuna mda mtu unahitaji kujishughulisha eti pata picha upo ofisin unapambana na simu ndo kama za hivyo zinaingia si unaeza kuwehuka
Hahahaha wapo wa hivi...unablokua mbali huko
 
Back
Top Bottom