kluger
JF-Expert Member
- Jun 16, 2016
- 2,093
- 1,894
Wasalaam,
Maisha ya family na Ndoa yanahitaji hekima na Busara kwa wanandoa wenyewe na pande zote za muunganiko huo unaotengeneza family kubwa.
Rafiki zangu wengi au pengine hata wewe hapa kuachilia mbali mimi mwenyewe, kuna vitu huwa vimetukwaza kwa hali moja ama nyingine.
Leo napenda nigusie, upande wa ndugu wa mke au mume wanaotembelea family yenu. Wanawake katika nyumba wamekuwa na nafasi ya ustawishaji wa mahusiano ya pande mbili za Ndoa.
Si wote, bali walio wengi hawa wakina Mama, wamekuwa na tatizo sana linapokuja ugeni wa upande wa Mume, huku upande wa mke wakimiminika kila mara.
Yaani hakuna usawa kabisa wa upendo linapokuja wamekuja wageni ambao si ndugu wa mke. Kuanzia ukarimu hata namna ya mapokezi. Mtu unashindwa kuelewa ni Roho Mbaya au hata ni nini?
Wageni hawa si wakukaa siku zote, wala si wa mara kwa mara. Lakini hawa wa upande wake kila baada ya muda mfupi huyu kaja mara yule kaja na kwa upande wetu sisi wanaume tulio wengi hili si tatizo na kama mimi binafsi nafurahi kupata wageni wa family yetu.
Lakini siku zinavyoenda natambua ndugu wa upande wangu hata hawana Amani ya kuja tena kwangu, maana kuna ukarimu na matendo yanayoonekana ambayo hayastahili kwao. Ni kama vile mtu hapendi. Sasa hapa ndipo ikanistua, mbona binafsi sina shida na wageni hao bila kujali pande?
Isitoshe hawakai zaidi ya siku tatu, na katika mwaka pengine mara moja moja sana. Ila upande wake haipiti miezi miwili kuna mgeni. Tatizo ni nini nyinyi wapendwa wetu?? Kwa nini mnakosa upendo? Gharama zote nagharimia sasa shida ni nini?
Jambo hili linakera sana, na linapunguza upendo kwa kiasi kikubwa sana. Wanaotaka kuingia kwenye Ndoa jambo hili jitahidi kumjua mwenza wako, kama ni mtu mkarimu au Roho mbaya. Wanatesa nafsi zetu sana sana
Nawakilisha kwa mliowahi kutana na zahama hizi pengine mnazitatua vipi?
Family si Kisiwa, inahitaji mahusiano na ndugu wengine. Sisemi ndugu wa pande zote kuhamia na kuishi nanyi, la hasha! Yaani, upendo kwa ndugu wa pande zote.