Mahudhurio Bungeni ni hafifu sana

CORONAZ

Senior Member
Apr 26, 2020
181
337
Nimekuwa nikifuatilia mara kwa mara mikutano ya bunge kila ninapopata nafasi.

Kinachonisikitisha ki kuona viti vina wabunge wachache mnooo.

Sasa najiuliza maswali yafuatayo:

1. Wote wanalipwa posho bila mahudhurio? Sio kufoji huko?

2. Hivi hakuna utaratibu wa kusign kwa kidole au uso kwenye malango ya Bunge kuondoa udanganyifu kama upo?

3. Ndani ya chama au bunge hakuna kanuni inayomtaka mbunge kuhudhuria sio chini ya 80% ya vikao?

4. Kama mbunge ni mtoro bungeni, spika hana utaratibu wa kukiarifu chama anakotoka mbunge kuhusu mwenendo huo wa kutohudhuria vikao?

5. Kwanini wakati wa vikao vya bunge wasisitishe shuhuli nyingine kwa wabunge ili wapate muda wa kutimiza jukumu hili lao kuu lililowapa hata jina wanalotumia?

6. AOB: Kuna wabunge wasiochangia chochote kila mkutano wa bunge kipindi chote. Hawa tuwafanyeje?

Screenshot 2023-11-09 at 04-09-45 Serikali Sehemu zenye maambukizi ya ugonjwa wa malaria kwa w...png
 
Unashauri mawaziri watokane kwa utaratibu upi?
Rais apendekeze raia wanaofaa kuwa mawaziri na wawe wamefikia levels za serior officials kama watatoka serikalini na wale wasio serikalini wawe na impacts zinazoshikika. Kisha majina yepelekwe Bungeni kwa vetting na usaili kabla hawajapewa Uwaziri.

Waziriakipishwa anakuwa Mbunge automatically na akitenguliwa ubunge wake unakoma hapo hapo.

Mafao ya Waziri yasitokane na Ubunhe wake bali kazi yake ya Uwaziri kwa Mujibu wa standing orders za Hazina.

Caution, waziri wa Ulinzi awe na historia ya kuhudumu senior levels za jeshini.

Mbunge abaki ktk nafasi hiyo ili apambanie maendeleo ya jimbo na wilaya yake
 
Kwa minajili ya tija, ukitoa Waziri Mkuu, mawaziri wote wasitokane na Wabunge. Serikali itabinywa inavyopaswa.

Sasa wanalindana na kubebana
Tupe mfano wa nchi gani ya kiafrica iliyotawaliwa na uingereza.
 
Mimi ningependa speaker kuulizwa hili swali, kwa maana wabunge muda mwingi wako nje kukiwa hakuna bunge. unategemea kwenye vikao wahudhurie maana ndio kazi yao.
 
Back
Top Bottom