Mahubiri ya kwanza ya Askofu Kilaini tangu sakata la Escrow(VIDEO)

Acha unafiki Jabulani nani asiyelifahamu kanisa katoliki hasa Roman Catholic? Huyu askofu anapaswa kusimamishwa hadi hili jambo lipatiwe ufumbuzi. Ni kosa sana muumini kama wewe unatanguliza ushabiki wa kijinga kwa kanisa tegemeo kama RC. Kipindi marehemu askofu Aloyces Balina yuko jimbo la Geita alikuwa anapata misaada mingi lakini aliiweka wazi na waumini tunafaidika hadi leo kwa huduma mbalimbali kama VETA yake,shule ya kisasa na kanisa kubwa nala kisasa lililopo Geita. Kilaini ni askofu wa kuchunguzwa sana kwa uhai wa kanisa la RC Tanzania kwani ndiye huyu alituaminisha Kikwete ni Chaguo la mungu kumbe chaguo lake kwa maslahi yake. Laiti ungepitia mafunzo tuliyokuwa tunafundishwa na baadae mtihani wa maswali ya papo kwa hapo unapopata ubatizo usingetetea upuuzi wa huyu askofu. Huna tofauti na muumini anayeogopa kumkosoa padri anayelewa pombe hadharani kwa kusema dunia itamfundisha. Kwa taarifa yako nimebatizwa,nikapata komunio na baadae kipaimara na hadi leo ni muumini nisiyeyumba katika kanisa la RC lakini siwezi kumfumbia macho padri au askofu anapoenda ndivyo sivyo. NB: asimamishwe na kama una namba za kadinali Pengo niwekee hapa nimwambie.

Nakubaliana na wewe mkuu lkn kwa taratibu za Kanisa Pengo hana madaraka juu ya Kilaini. Labda anaweza kumweleza Papa na kumpa ushauri amsimamishe Kilaini. Pengo hampi mtu uaskofu mtu yeyote ila anamshauri Papa.
 
Hili nilikuwa silifahamu ndugu yangu Kagalala.
 
Pamoja na kwamba Pengo hampi mtu uaskofu ila ana nguvu ya kuweza kumfanya askofu atolewe uaskofu wake kama ilivyotokea kwa Askofu Koda wa Jimbo la Same.
 
Maaskofu kama hawa wanatakiwa wasiongoze inada takatifu. Wapewe majukumu mengine kama vile kutunza mapadre wa zee na kutunza bustani za uaskofuni
 
Kilaini hata angechukua zote hakuna tatizo lolote.navyofahamu rc maskofu c wabinafsi wangelekeza kwenye maendeleo ya nch
 
Hivi bado kuna watu wanamsikiliza na kutoa sadaka huyu Askofu?
Acha unafiki Jabulani nani asiyelifahamu kanisa katoliki hasa Roman Catholic? Huyu askofu anapaswa kusimamishwa hadi hili jambo lipatiwe ufumbuzi. Ni kosa sana muumini kama wewe unatanguliza ushabiki wa kijinga kwa kanisa tegemeo kama RC. Kipindi marehemu askofu Aloyces Balina yuko jimbo la Geita alikuwa anapata misaada mingi lakini aliiweka wazi na waumini tunafaidika hadi leo kwa huduma mbalimbali kama VETA yake,shule ya kisasa na kanisa kubwa nala kisasa lililopo Geita. Kilaini ni askofu wa kuchunguzwa sana kwa uhai wa kanisa la RC Tanzania kwani ndiye huyu alituaminisha Kikwete ni Chaguo la mungu kumbe chaguo lake kwa maslahi yake. Laiti ungepitia mafunzo tuliyokuwa tunafundishwa na baadae mtihani wa maswali ya papo kwa hapo unapopata ubatizo usingetetea upuuzi wa huyu askofu. Huna tofauti na muumini anayeogopa kumkosoa padri anayelewa pombe hadharani kwa kusema dunia itamfundisha. Kwa taarifa yako nimebatizwa,nikapata komunio na baadae kipaimara na hadi leo ni muumini nisiyeyumba katika kanisa la RC lakini siwezi kumfumbia macho padri au askofu anapoenda ndivyo sivyo. NB: asimamishwe na kama una namba za kadinali Pengo niwekee hapa nimwambie.
Hoja yako ya pili haijajibu hoja yangu kwamba RC huwa hatutoi sadaka kwa mtu binafsi. Na hapa uwe makini, nazungumzia sadaka, sio misaada! Au hatuelewani katika hilo neno 'sadaka'?
 
Back
Top Bottom