Mahubiri ya kwanza ya Askofu Kilaini tangu sakata la Escrow(VIDEO)

HarakatiNews

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
218
185
Tangu Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoriki la Bukoba Methodius Kilaini kutajwa kuwa ni miongoni mwa wanufaikaje katika sakata la Escrow hajawahi kujitokeza hadharani kuongelea lolote wala sauti yake kusikika,ikiwemo kuendesha misa takatifu.

Tazama mahubiri yake katika video,picha na yaliyojiri kwa ujumla hapa chini

Chanzo:HARAKATINEWS
 
Last edited by a moderator:
Mbona hajaongea lolote kuhusu escrow.?

Ama mnatangaza hicho ki web chenu kiaina harakat bla.bla tu ----
 
Acha unafiki Jabulani nani asiyelifahamu kanisa katoliki hasa Roman Catholic? Huyu askofu anapaswa kusimamishwa hadi hili jambo lipatiwe ufumbuzi. Ni kosa sana muumini kama wewe unatanguliza ushabiki wa kijinga kwa kanisa tegemeo kama RC. Kipindi marehemu askofu Aloyces Balina yuko jimbo la Geita alikuwa anapata misaada mingi lakini aliiweka wazi na waumini tunafaidika hadi leo kwa huduma mbalimbali kama VETA yake,shule ya kisasa na kanisa kubwa nala kisasa lililopo Geita. Kilaini ni askofu wa kuchunguzwa sana kwa uhai wa kanisa la RC Tanzania kwani ndiye huyu alituaminisha Kikwete ni Chaguo la mungu kumbe chaguo lake kwa maslahi yake. Laiti ungepitia mafunzo tuliyokuwa tunafundishwa na baadae mtihani wa maswali ya papo kwa hapo unapopata ubatizo usingetetea upuuzi wa huyu askofu. Huna tofauti na muumini anayeogopa kumkosoa padri anayelewa pombe hadharani kwa kusema dunia itamfundisha. Kwa taarifa yako nimebatizwa,nikapata komunio na baadae kipaimara na hadi leo ni muumini nisiyeyumba katika kanisa la RC lakini siwezi kumfumbia macho padri au askofu anapoenda ndivyo sivyo. NB: asimamishwe na kama una namba za kadinali Pengo niwekee hapa nimwambie.
 
Roman Catholic huwa hatutoi sadaka kwa mtu binafsi

Acha unafiki Jabulani nani asiyelifahamu kanisa katoliki hasa Roman Catholic? Huyu askofu anapaswa kusimamishwa hadi hili jambo lipatiwe ufumbuzi. Ni kosa sana muumini kama wewe unatanguliza ushabiki wa kijinga kwa kanisa tegemeo kama RC. Kipindi marehemu askofu Aloyces Balina yuko jimbo la Geita alikuwa anapata misaada mingi lakini aliiweka wazi na waumini tunafaidika kwa huduma mbalimbali kama VETA yake,shule ya kisasa na kanisa kubwa nala kisasa lililopo Geita. Kilaini ni askofu wa kuchunguzwa sana kwa uhai wa kanisa la RC Tanzania kwani ndiye huyu alituaminisha Kikwete ni Chaguo la mungu kumbe chaguo lake kwa maslahi yake. Laiti ungepitia mafunzo tuliyokuwa tunafundisha na baadae mtihani wa maswali ya papo kwa hapo unapopata ubatizo usingetetea upuuzi wa huyu askofu. Huna tofauti na muumini anayeogopa kumkosoa padri anayelewa pombe hadharani kwa kusema dunia itamfundisha. Kwa taarifa yako nimebatizwa,nikapata komunio na baadae kipaimara na hadi leo lakini siwezi kumfumbia macho padri au askofu anapoenda ndivyo sivyo. NB: asimamishwe na kama una namba za kadinali Pengo niwekee hapa nimwambie.
teh teh teh..
Ngoma inogile, ngoja nichukue popcorn na fwantha baridi..
 
Huyu Askofu amekosa sifa za kuwa askofu na mhubiri wa neno la Mungu. Kanisa linataratibu za kuwawajibisha hawa watu. Naona hapa kigugumizi kinakuwa kirefu. Waumini mkataeni.
 
Nadhani hakuna alie juu ya sheria, askofu ajitokeze na kusema bayana pesa aliyopewa na Mt. Mwenye Heri alipewa kwa minajili ipi? Kukaa kimya hakumsaidii.
 
Acha unafiki Jabulani nani asiyelifahamu kanisa katoliki hasa Roman Catholic? Huyu askofu anapaswa kusimamishwa hadi hili jambo lipatiwe ufumbuzi. Ni kosa sana muumini kama wewe unatanguliza ushabiki wa kijinga kwa kanisa tegemeo kama RC. Kipindi marehemu askofu Aloyces Balina yuko jimbo la Geita alikuwa anapata misaada mingi lakini aliiweka wazi na waumini tunafaidika hadi leo kwa huduma mbalimbali kama VETA yake,shule ya kisasa na kanisa kubwa nala kisasa lililopo Geita. Kilaini ni askofu wa kuchunguzwa sana kwa uhai wa kanisa la RC Tanzania kwani ndiye huyu alituaminisha Kikwete ni Chaguo la mungu kumbe chaguo lake kwa maslahi yake. Laiti ungepitia mafunzo tuliyokuwa tunafundishwa na baadae mtihani wa maswali ya papo kwa hapo unapopata ubatizo usingetetea upuuzi wa huyu askofu. Huna tofauti na muumini anayeogopa kumkosoa padri anayelewa pombe hadharani kwa kusema dunia itamfundisha. Kwa taarifa yako nimebatizwa,nikapata komunio na baadae kipaimara na hadi leo ni muumini nisiyeyumba katika kanisa la RC lakini siwezi kumfumbia macho padri au askofu anapoenda ndivyo sivyo. NB: asimamishwe na kama una namba za kadinali Pengo niwekee hapa nimwambie.

Toa upuuzi wako hapa...yani kupata communion, kipaimara ndo unalijua kanisa...??

Hebu peleka vichekesho kule jokes
 
Askofu ni kielelezo cha juu kabisa katika kanisa, ni kioo cha kanisa, uchafu wake unaathiri waumini wengi sana, haitakuwa sawa Askofu mwenye kashfa ya uhujumu uchumi, rushwa na ufisadi akaendelea kuhubiri. Akiiachwa atazalisha mafisadi wengi sana ndani ya kanisa, kwani kila mwizi atatumia mfano wa askofu huyu ndani ya kanisa. Lazima atoke. Na kama kweli jimbo la kagera lina waumini wacha Mungu wasusie misa zake.

Waumini waliweza kumkimbiza Padre Luambano Mburahati baada ya yeye kukiuka kiapo chake cha upadre. Askofu Kilaini hayuko juu ya kanisa. Waumini onyesheni kwa vitendo mnakataa dhambi na mnamkataa shetani na anasa zake zote. Mkataeni Askofu Kilaini kwa vitendo.
 
Asiudanganye umma huyo askofu,mi ni miongoni mwa wakatoliki na nmebahatika kusoma na kuijua miiko ya makasisi wa kanisa letu;amekosa maadili na anastahili auambie umma huo ubia na rugemalila ulikuwa kwenye hisa au ukabila na ujiografia watokako??asilichafue kanisa na tamaa zake za kisiasa!hakuna sadaka ya mtindo huo haipo..watanzania wana matatizo chungu nzima,serikali imewaweka rehani yeye anatajwa kwenye kashfa....tuelewe nini km viongozi wa dini nao wameungana na wanasiasa kutuibia na kutangaza hadharani kuwa si pesa za umma wakati majibu yapo nje kuwa zilikuwa hela za pande mbili???kilaini uambie umma wewe umepokea hela hzo kwa minajili ipi,mbona mwenzio amejitahid amejtetea kuwa zililenga shule yake,japo hatujamwelewa.
 
Back
Top Bottom