Mahojiano (EXCLUSIVE INTERVIEW) ya JamiiForums na Khamis Kagasheki

Mahojiano (EXCLUSIVE INTERVIEW) ya JamiiForums na Khamis Kagasheki

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,249
Reaction score
5,743
Habari Wakuu,

Hivi karibuni tulifanya mahojiano na Mh. Hamis Kagasheki. Mahojiano hayo yalitokana na maswali yaliyowasilishwa na washiriki (members) wa JamiiForums kupitia mada hii -



Mapema hapo kesho (29/05/2015), ndiyo tunaanza kurusha rasmi video hizo za mahojiano hapa JamiiForums (Kwa maandishi, audio na Video zitawekwa YOUTUBE Channel).

Maswali yaliyoulizwa yalikusanywa na yalipangiliwa katika vipengele husika tokana na maswali ya wadau wa JamiiForums yaliyowasilishwa.

Mkusanyiko wa maswali hayo ulipangwa katika vipengele kumi na sita (16) kila kipengele kikiwa na maswali kadhaa hivyo kufanya kuwe na maswali zaidi ya sabini (70) kwa ujumbla wake. Kwa maana hiyo, hata vipande vya video hizo zimegawanyika katika vipande 70, kila kimoja kikijitosheleza katika sehemu yake.

Kwa wale ambao kuangalia video ni tatizo kwao (vifurushi/kasi ndogo ya mtandao), kutakuwepo na mahojiano hayo katika mfumo wa maandishi pia; hivyo tunawahakikishia kwa kila mmoja atakayependa kujua kilichojiri, ataweza kupata kwa namna moja ama nyingine.

KagashekiJF.png

Mhe. Balozi Khamis Kagasheki wakati wa Mahojiano na JamiiForums​
Mpangilio wa Maswali upo katika vipengele hivi:


A. Kagasheki ni nani?
B. Kagasheki na Ubalozi
C. Kagasheki na Ubunge
D. Kagasheki na Uwaziri
E. Kagasheki na Operation Tokomeza
F. Kagasheki na CCM
H. Kagasheki na Urais
I. Kagasheki na Siasa za Upinzani
J. Kagasheki na Tanzania yetu
K. Kagasheki Khamis Kagasheki (Yeye kama yeye)


Maswali ya kila kipengele tafadhali bofya
hapa

Asanteni

--------------------

Thread zenye mahojiano hayo;

*Mahojiano katika video na maandishi ya swali la kwanza (1) tembelea -



*Mahojiano katika video na maandishi ya swali la pili (2) na la tatu (3) tembelea -


*Mahojiano katika video na maandishi ya swali la nne (4) tembelea - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ji-wa-balozi-za-tanzania-nchi-za-nje-3-a.html

*Mahojiano katika video na maandishi ya swali la tano (5) tembelea - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-nyuma-katika-uchangamkiaji-wa-fursa-4-a.html

*Mahojiano katika video na maandishi ya swali la sita (6) na saba (7) tembelea - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...anikio-ya-mhe-kagasheki-bukoba-mjini-5-a.html

*Mahojiano katika video na maandishi ya swali la nane (8) na tisa (9) tembelea - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...isiasa-na-mhe-kagasheki-6-a.html#post12867298

*Mahojiano katika video na maandishi ya swali la kumi (10) na kumi na moja (11) tembelea - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-ihungo-kwa-kukosa-chakula.html#post12903774
 
MAHOJIANO NA MHESHIMIA BALOZI KAGASHEKI


(Mpangilio wa Maswali)​


A. KAGASHEKI NI NANI?

1. Tueleze historia ya Elimu yako kwa ufupi.
2. Ulipoanza kazi, ulifanya na nani na hali ilikuwaje?
3. Tueleze maisha yako ya kazi.

B. KAGASHEKI NA UBALOZI

4. Je, Balozi zetu nje zina Tija? Kuna malalamiko mengi; matatizo ya utendaji kazi kwao ni nini?
5. Katika suala la kuchangamkia Fursa, Watanzania unawaelezea vipi?

C. KAGASHEKI NA UBUNGE

6. Mh. tueleze mafanikio yako katika Jimbo la Bukoba Mjini
7. Ukoo wa Kagasheki una Historia ndefu Bukoba, Je hii ndio inayokubeba?
8. Tofauti zenu za kisiasa kati yako na Anatory Amani unatokana na nini? Ni kweli tofauti hizi zinachangia kuzorotesha maendeleo?
9. Vipi madai kuwa ulimpa Dr. Amani uraia wakati ukiwa Naibu Waziri wizara ya mambo ya ndani?
10. Unasemaje juu ya Shule ya Ihungo katika manispaa ya Bukoba kufungwa kutokana na ukosefu wa Chakula?
11. Hivi karibuni kumeripotiwa uchomwaji makanisa katika jimbo lako, Kuna hatua yoyote ulichukua?
12. Tueleze kuhusu hali ya usafiri Bukoba hasa ufufuaji wa MV Bukoba na ununuzi wa meli mpya.
13. Ni sababu zipi zilipelekea kuhamishwa kwa kiwanja cha ndege cha Mkoa toka Biharamulo hadi Bukoba?
14. Bado una nia ya kugombea tena Ubunge?
15. Utawaambia vipi watu wakuchague na hali yale uliyoahidi kama vile soko na stendi hujakamilisha?
16. Unasemaje juu ya wanaosema CCM ni Chama cha mafisadi? CCM isipokuchagua kugombea Ubunge utakubaliana nao?
17. Vuguvugu la Lwakatare kurudi na kugombea Jimbo lako unalisemeaje?
18. Je wewe na Wilfred Lwakatare mna uadui?
19. Una maoni gani juu ya Ripoti ya utafiti Tanzania ulofanyika hivi karibuni unaoonyesha jimbo lako kuwa nyuma sana kiuchumi na kimaendeleo.
20. Ikiwa utarudi katika ubunge, mambo yapi utazingatia?
21. Unazungumziaje bei ndogo ya kahawa na nini kifanyike?

D. Kagasheki na Uwaziri

22. Tupe tathmini yako fupi tu ya utendaji wako ulipokuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.
23. Ukiwa Naibu Waziri katika Wizara ya Mambo ya Ndani ulifanya nini kupunguza rushwa?
24. Kwa kumbukumbu zako ni jambo gani zuri ulilowahi kulifanya katika Wizara ya Maliasili na Utalii?
25. Inakuwaje Wizara ya Maliasili na Utalii inatoa vibali vya tafiti mbalimbali katika mbuga za wanyama wakati wizara hiyohiyo inazuia makazi ya watu?
26. Kwanini makazi kadhaa ya wananchi yamekuwa yakichomwa moto karibu na hifadhi lakini makambi ya watafiti na wanaotarajia kufungua yamejengwa katikati ya migodi?
27. Inasemekana kuwa idadi kubwa ya vitalu vinamilikiwa na viongozi wa serikali na CCM na wengine hukodishia watu binafsi, una maoni gani?
28. Je unaridhika na mfumo wa utendaji wa wizara zetu ikiwemo Wizara ya Maliasili na Utalii?
29. Ili kuendeleza sekta ya utalii Unafikiri mambo gani yafanyike?

E. Kagasheki na Operation Tokomeza

30. Operesheni tokomeza ilikuwa ni nini hasa na ni nini faida na hasara zake?
31. Unadhani Operesheni ile ilikuwa ina uwezo wa kumaliza kabisa tatizo la ujangili?
32. Je unakubaliana na hoja kuwa baadhi ya viongozi wamekuwa wakishiriki kwa namna moja au nyingine katika tatizo la ujangili wa maliasili?
33. Unasemaje kuhusu kiongozi mmoja wa Chama aliyekuwa ana kampuni ya usafirishaji na Meli yake ilikutwa na kontena likisafirisha meno ya tembo?
34. Kwanini ujangili wa meno ya tembo hauishi na kwanini wahusika wakuu hawakamatwi?
35. Ni kweli kwamba ulijuwa yote yaliyokuwa yakifanyika kwenye Operesheni Tokomeza lakini hukuchukua hatua zinazostahili?
36. Je kujiuzulu kwako ni uwajibikaji au ni kutolewa kafara tu ?

37. Tokana na kashfa kama Richmond, operesheni tokomeza, escrow n.k Ikisemwa serikali hii ipumzishwe, unakubaliana nalo?
38. Ni kwanini mawaziri mnaojiuzulu kwa kuwajibika baadae mkiwa bungeni mnasusa kuchangia bungeni?
39. Je, hao ambao hawachangii ndo kusema wamesusa? (Robert take note qn number 38 and prior 39 where the same na zimeunganishwa)
40. Ni kweli kuwa unajisikia fahari kuwatumikia wananchi kuliko Ukiwa Waziri kuliko ukiwa nje au umeondolewa?

F. Kagasheki na CCM

41. Huoni kuwa sasa ni wakati muafaka wa wewe kuhama na kugombea kutumia chama kingine?
42. Unasemaje kuhusu Baadhi ya viongozi kuogopa midahalo ya wazi, Je wewe upo tayari kushiriki?
43. Wananchi wengi wa Tanzania ni masikini sana. Unadhani CCM ina nia ya dhati ya kuwakomboa watanzania?
44. Miaka hamsini ya Uhuru Tanzania bado ni maskini. Je umaskini umeletwa na serikali ya CCM?
G. Kagasheki na katiba
45. Tunaomba mukhtasari wako kuhusu mchakato wa katiba.
46. Kwanini serikali ilishindwa kugundua mapema kuwa zoezi la upigaji kura kupata Katiba Mpya lisingeweza kufanikiwa katika muda ulopangwa?
47. Je, hiyo Katiba Pendekezwa kwa maoni yako imekidhi mahitaji ya watanzania?
48. Kwa muda huu mchache ulobakia unasema nini kuhusu kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura?
49. Una maoni gani kuhusu Mahakama ya Kadhi?
50. Nini maoni yako juu ya Mahakama ya Kadhi ilitumiwa na CCM kupata kura za Waislam?

H. Kagasheki na Urais

51. Mheshimiwa unafikiria kugombea urais?
52. Wewe unadhani sifa za raisi wa Tanzania hapa tulipofika ni zipi?
53. Je, una matumaini kuwa CCM itashinda katika uchaguzi wa October (2015)? Je, wanaotajwa kuna unaoona wanafaa?

Kagasheki na Siasa za Upinzani

54. Unauongelea vipi upinzani katika Siasa za Tanzania.
55. Una mtazamo gani kuhusu chama kipya cha ACT-Wazalendo?
56. Una maoni gani juu ya tetesi za wabunge wengi kuwa na Mpango wa kujiunga na ACT baada ya Bunge kuvunjwa?
57. Umesisitiza umuhimu wa kuchagua mgombea ambaye anapendwa na watu. Je, anayependwa na watu akikataliwa na CCM kuna madhara gani?

J. Kagasheki na Tanzania yetu

59. Kwanini Tanzania ni nchi masikini yenye kutegemea misaada ya wahisani wakati tuna maliasili na rasilimali nyingi? (Naona kama sawa na swali la 44)
60. Ni njia zipi unadhani zitakomesha mauaji ya watanzania wenye ulemavu wa ngozi (Albino)?
61. Nini kifanyike kwa vijana hasa wanaomaliza vyuo vikuu waweze kujiajiri?
62. Nini nafasi ya Siasa katika kutupeleka mbele kwa maendeleo ya mwananchi mmoja mmoja na jamii kwa ujumla?


K. Kagasheki Khamis Kagasheki

63. Ni kitu gani kilikufanya uhamasike kuwa mtumiaji wa mara kwa mara wa Mitandao ya Kijamii?
64. Mitandao ya Kijamii imekuathiri vipi kama Kiongozi, NA inaathiri vipi Siasa za siku hizi?
65. Mtazamo wako juu ya Wanawake katika jamii na Uongozi ni upi?
66. Ni mtu gani alikuwa ‘Role Model' wakati unakuwa, na je bado ndiye ‘Role Model' wako sasa?
67. Kama ungekuwa na uwezo wa kubadilisha kitu kimoja kuhusu Tanzania, ungebadilisha kitu gani? Ni nini unajivunia kama mafanikio makubwa kuliko yote uliyowahi kupata?
68. Ukiwa waziri na muonekano wako kwenye jamii unaonekana vizuri; "What is your fashion sense?"
69. Angependa jamii ikukumbuke kwa kitu gani?


- MWISHO -​

 
Nimeshawatumia ujumbe natumaini hizo video kuanzia kesho ntazipata asanteni sana JamiiForums
 
Nnatumia BB 9900 Bold, lakini whatsapp siipendi naona inazidisha udaku na majungu.

Udaku na majungu kwani umeambia vipo kwenye whatsapp wewe unatumia tecno cha mchina kuingia humu Jf .uko duniani gani wewe?
 
Nashukuru swali langu nimeliona , thanx JF
 
Duh acha uwongo weka picha hiyo yako au tecno za mchina zina whats app ?

Situmii simu nyingine zaidi ya BB kwa miaka kadhaa sasa. Lakini sioni kama kuna dhambi kwa mtu kutumia techno.

Nnapenda kukufahamisha kuwa line ninayotumia mimi huwa kila mwaka nnaulizwa nipewe simu ipi na Voda, bure. Nami huchaguwa BB kwa kuwa nimezizowea, sinunuwi simu huletewa mpaka kwangu, wala sitii vocha, kumbuka hilo.

Lakini hiyo whatsapp, ni feature tu kama features zingine za simu na mimi sikuipenda na siitumii. Na pia situmii FB.

Hivi hiyo shule ulienda kusomea ujinga? au ni ujinga wa kuzaliwa ulionao na hakuna shule inayoweza kuufuta?
 
Situmii simu nyingine zaidi ya BB kwa miaka kadhaa sasa. Lakini sioni kama kuna dhambi kwa mtu kutumia techno.

Nnapenda kukufahamisha kuwa line ninayotumia mimi huwa kila mwaka nnaulizwa nipewe simu ipi na Voda, bure. Nami huchaguwa BB kwa kuwa nimezizowea, sinunuwi simu huletewa mpaka kwangu, wala sitii vocha, kumbuka hilo.

Lakini hiyo whatsapp, ni feature tu kama features zingine za simu na mimi sikuipenda na siitumii. Na pia situmii FB.

Hivi hiyo shule ulienda kusomea ujinga? au ni ujinga wa kuzaliwa ulionao na hakuna shule inayoweza kuufuta?

Hongera kwa kupata wafadhili wanaokufanya uishi at zero cost
 
Back
Top Bottom