Mahita 'aangukia pabaya' kortini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahita 'aangukia pabaya' kortini

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Jun 26, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,153
  Likes Received: 417,585
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Mahita 'aangukia pabaya' kortini
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Saturday, 25 June 2011 09:44 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  James Magai

  MKUU wa zamani wa Jeshi la Polisi Nchini, Omar Mahita, ameumbuka kwa mara nyingine baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, kutupilia mbali rufaa yake ya kupinga hukumu ya Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, kuhusu sakata la mtoto anayemkataa.

  Rufaa hiyo ya Mahita ilitupiliwa mbali jana na Jaji Dk Fauz Twaib, baada ya kuridhika na hukumu ya mahakama ya chini kuwa ilikuwa sahihi na kumwamuru Mahita kulipa gharama za kesi hiyo.

  Hata hivyo wakati hukumu hiyo ikitolewa, Mahita hakuwapo mahakamani na wakili wake Semgalawe, alifika wakati tayari jajiakiwa ameshamaliza kusoma hukumu.
  Septemba mwaka 2009 Mahakama ya Kinondoni ilimwamuru Mahita kutoa kiasi cha Sh100,000 kila mwezi kwa ajili ya kumhudumia mtoto na kulipa malimbikizo ya gharama za matunzo kuanzia mwaka 2003 hadi siku ya hukumu.

  Hukumu hiyo ilitokana na kesi ya msingi iliyofunguliwa katika mahakama hiyo na aliyekuwa mfanyakazi wa Mahita, Rehema Shabani, kupitia kwa Kituo cha Msaada wa Kisheria na Haki za Binadamau (LHRC).

  Katika kesi hiyo, Rehema alikuwa anadai matunzo ya mtoto Juma Omar Mahita, baada ya kumtelekeza na baadaye mahakama ilifikia uamuzi wa kumtaka Mahita kulipa gharama hizo.
  Mahakama pia iliamuru Mahita akachukuliwe vipimo vya vinasaba (DNA) lakini Mahita akakataa.

  Hata hivyo Mkuu huyo wa zamani wa Polisi, kupitia kwa wakili wake Charles Semgalawe aliamua kukata rufaa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, akipinga hukumu na adhabu hiyo.

  Katika rufaa hiyo, Mahita aliwasilisha sababu nne za kupinga hukumu na adhabu hiyo.
  Alidai kuwa pamoja na mambo mengine,mahakama ya chini ilikosea kisheria kuamua kwa kuwa shauri la matunzo ya mtoto halikufunguliwa nje ya wakati, kinyume cha Sheria ya Kuasili Watoto.

  Pia alidai kuwa mahakama ya chini ilikosea kusema kuwa mrufani ni baba halali wa mtoto kwa kuegemea katika ushahidi wa mjibu rufani kwa madai kuwa mrufani alikataa kuchukua vipimo vya DNA wakati si kweli.

  Mahita pia alihoji uhalali wa amri ya mahakama ya chini kumwamuru kumlipa mjibu rufani kiasi Sh100,000 kila mwezi kwa ajili ya matunzo ya mtoto wakati sheria inataja kiasi cha Sh100.

  Hali kadhalika, alilalamikia amri ya mahakama ya chini ya kumtaka kulipa fidia kuanzia mwaka 2003 hadi siku ya hukumu.Hata hivyo katika hukumu yake jana Jaji DK Twaib alitupilia mbali sabababu hizo baada ya kuziona kuwa hazina msingi na kuungana na baadhi ya hoja za wakili wa mlalamikaji, Fredrick Mkatambo kutoka LHRC.


  Wakili huyo alizipinga vikali sababu hizo wakati wa usikilizwaji wa rufaa hiyo.Jaji Dk Twaib alichambua sababu moja baada ya nyingine na kuzitolea maelezo ya kisheria ya sababu za kuzitupila mbali.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,153
  Likes Received: 417,585
  Trophy Points: 280
  malipo kweli ni hapa hapa duniani...........................when the former daredevil is caught in his own traps then you know God is fair 2 all.............................the rich and the poor too..................
   
 3. P

  PascalFlx Member

  #3
  Jun 28, 2011
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu kweli ni mzembe laki moja tu kwa mtu aliyewahi kuwa IGO anaziona nyingi eti sh 100, we shilingi mia moja utanunua nini huyo ni mtoto wako wa mwenyewe hivi akikua utamuambia nini akisoma habari kama hizi?
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  uwe unatulia wakati wa kuandika na wewe ..IGO ndo nini?
   
 5. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Ahsante sana Dr. Fauz Twalib kwa kuwa muadilifu na kutokutetereka kwa jina.
   
 6. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  wewe changundoa....
   
Loading...