Mahindi

Mahindi

TODO

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2011
Posts
219
Reaction score
63
I salute u Wanajf! leo nimeshangaa sana, nilienda barabara ya 15 jiji la Tanga kupata huduma ya unga wa mahindi.Nilivofika nikamkuta mama mmoja wa kitanga nikamuuliza debe moja la mahindi ni bei gani akaniambia na nikamwambia nataka kusaga kabisa dona akanipa bei nikampa hela akaanza kusaga na baada ya muda unga ukawa tayar

Wakati nataka kutoka nikamuuliza haya mahindi ya sasa yanatoka wapi alichonijibu nilishangaaa san.Mama huyu anasema hapa Tanga mahindi tunayapata kutoka Kenya, zambia, Malawi na kwingine nimekusahau ila sio ndani ya TZ.nilichoshangaa ni kauli ya Mh Rais Kikwete akiwa Tabora juzi tu kwamba tuna chakula cha kutoshana hivyo hakuna wa kufa njaa.

Kama ndani ya tz mahindi hayatosh ma kulazimikakuagiza toka nje tutafika kweli au baadhi yetu tutakufa kwa njaa.

Nawasilisha, mwenye takwimu sahihi juu ya zao hili aje atujuze, tafadhali
 
Hilo la kutoka kenya sina uhakika nalo, ila kwa malawi na zambia ni kweli, Kenya mara nyingi hununua na kusaga na kuuza unga, huwa hawauzi mahindi wao
 
chacha nimekupata hapa Tanga wadau wanasema yapo mahindi ya kenya pia.ila hivi mahindi ya Rukwa huko vp yanaishia wapi? mbona wanasema huko wanalima sana mahindi kias cha kwamba hawana soko! au nawao wanataka yaweprocessed pale pale wasafilishe unga kama jamaa wa Mtwara kwenye gas yao
 
Hilo la kutoka kenya sina uhakika nalo, ila kwa malawi na zambia ni kweli, Kenya mara nyingi hununua na kusaga na kuuza unga, huwa hawauzi mahindi wao

Hata nguzo za umeme zilikuwa zinatoka Mafinga zinaingia nchi jirani kisha zinarudishwa Tanzania na nembo ya nchi ya mbali sana. Sisi tunanunua kama product ya nje kwa hela za kigeni !!!!!!!!
 
sidhani kama ni kweli yanatoka zambia na malawi. ninavyojua hizo nchi zinanjaa na hutegemea mahindi toka nyanda za juu kusini. au alifikiri akikwambia yanatoka nje ya nchi utaona yana quality!?. maana wabongo kwa kuthamini vitu vya nje!.

Malawi/zambia siku zote mahindi wanachukua hapo nyanda za juu kusini, kwa sasa mahindi/unga ya Rukwa yanasombwa kwa wingi kwenda drc. Kama kenya nao wanaweza kuingiza mahindi Tz, basi yaweza kuwa ni ile hadithi ya nguzo za umeme.
 
Kwa hakika hakuna mahindi yatokayo Malawi kwenda Tanga.
 
sidhani kama ni kweli yanatoka zambia na malawi. ninavyojua hizo nchi zinanjaa na hutegemea mahindi toka nyanda za juu kusini. au alifikiri akikwambia yanatoka nje ya nchi utaona yana quality!?. maana wabongo kwa kuthamini vitu vya nje!.

Mkuu Malawi wanalima sana Mahindi na Hata Kenya inachukua sana Mahindi Kutoka Malawi, na hii ni baada ya Tanzaniakuweka zengwe za kuuza mahindi Nje, kwa Zambia sijajua vizuri ila Malawi wanazalisha mahindi kwa wingi sana
 
Malawi/zambia siku zote mahindi wanachukua hapo nyanda za juu kusini, kwa sasa mahindi/unga ya Rukwa yanasombwa kwa wingi kwenda drc. Kama kenya nao wanaweza kuingiza mahindi Tz, basi yaweza kuwa ni ile hadithi ya nguzo za umeme.

Mkuu Malila Malawi inazalisha Mahindi kwa wingi na Kule kwao Kilimo kwanza kinatekelezwa kwa Vitendo sio huku Bongo na hata ishu za Mbegu na Mbolea za ruzuku kule wanafanya vizuri kuliko Bongo, Na Kenya wanachukua sana Mahindi Malawi kwa sababu kule hakuna vikwazo kama Tz
 
Kabla mutharika hajawa Rais hali ilikuwa mbaya sana, Mutharika akashusha bei ya pembejeo na wakulima wakalima sana na kupata ziada. Hii ilimsaidia kuingia awamu ya pili kwa turufu ya ziada ya chakula. Upepo uligeuka kiasi,hali haikuwa nzuri kama mwanzo, ni kama sisi ilivyo, Ngorongoro Wamasai wanakufa njaa, Katavi hawana pa kupeleka mahindi ndani ya nchi moja. Mgomo/maandamano ya Wamalawi mwaka jana kabla jamaa hajafa yalichangiwa pia na hali mbaya ya lishe.

Hata hivyo, Malawi wako juu sana ktk suala la kilimo kwanza kutuzidi.
 
Wiki iliyopita nilisikia kwenye taarifa ya habari nakumbuka ilikuwa Clouds Fm asubuhi kuwa kuna Malori 8 yamekatwa Sirari huko Mara kwa kuingiza mahindi nchini kinyemela tumeshazoe the other way round mahindi kutoka TZ kuvuka kwenda Kenya,Uganda nilishtuka sana kusikia mahindi yanatoka Kenya kwenda TZ so tusibishe hatuwezi jua nini kimetokea kuna uwezekano Wakenya walinunua mahindi kwa wingi sana TZ wakati wa Mavuno last year na wakayahifadhi then kuna scarcity TZ cause mahindi mengi tumeuza Kenya then mahindi hayo hayo tunarudishiwa tena najaribu tu kuja na hypothesis hapa ila mi mwenyewe sielewi nini kimetokea ila kuna hizo taarifa kuwa Mahindi yanatoka Kenya kuja TZ
 
Mahidi Tanga yanapatikana kuokoa Malawi, Kibaigwa, sina uhakika na Kenya lakini Njaa ipo.
 
mimi nafanya biashara za nafaka mahindi hatuchukui huko kulikotajwa mahindi yapo mbozi ,sumbawanga kibaigwa nk,ila ninacho jua bei ya mahindi malawi iko chini kuliko kwetu
na HAWA RUHUSU KUTOA NJE YA MALAWI. Tunaye jamaa yetu lory zima walitaifisha kwa kutaka kusafilisha kimagendo.
 
I salute u Wanajf! leo nimeshangaa sana, nilienda barabara ya 15 jiji la Tanga kupata huduma ya unga wa mahindi.Nilivofika nikamkuta mama mmoja wa kitanga nikamuuliza debe moja la mahindi ni bei gani akaniambia na nikamwambia nataka kusaga kabisa dona akanipa bei nikampa hela akaanza kusaga na baada ya muda unga ukawa tayar

Wakati nataka kutoka nikamuuliza haya mahindi ya sasa yanatoka wapi alichonijibu nilishangaaa san.Mama huyu anasema hapa Tanga mahindi tunayapata kutoka Kenya, zambia, Malawi na kwingine nimekusahau ila sio ndani ya TZ.nilichoshangaa ni kauli ya Mh Rais Kikwete akiwa Tabora juzi tu kwamba tuna chakula cha kutoshana hivyo hakuna wa kufa njaa.

Kama ndani ya tz mahindi hayatosh ma kulazimikakuagiza toka nje tutafika kweli au baadhi yetu tutakufa kwa njaa.

Nawasilisha, mwenye takwimu sahihi juu ya zao hili aje atujuze, tafadhali
Huko Rukwa yanaliwa na panya kwnye vihamba kwa kukosa soko,na hurusiwi kuuza nje,CCM Oyee,Oyee !Asenti
 
Swala la kutoka Mahindi Kenya au Malawi sina uhakika, ila nina uhakika kuwa Tanzania kuna mahindi mengi hatuwezi kuyamaliza, mengineyo labda soko huria! Last year ilichukua miezi mitatu kuhamisha Mahindi ya ziada kutoka Ruvuma pekee, na ilikuwa ni kazi ya non-stop usiku na mchana, nilishuhudia Lory nyingi za kutoka kenya zikipishana barabarani sambamba na Malori ya JW! Wakulima wengi waliuza mahindi kwa serikali na kupata pesa zao!
 
Mahindi Tz yapo yakutosha watu hapa arusha wana ghala zimejaa mahindi yakutosha, swala la kutoka kwa mahindi kenya au malawi labda huyo mama alikurusha tu uone kwamba wanabidhaa iliyo vuko border lakini kiukweli ni kwamba mahindi Tz yapo yakutosha hakuna kufa njaa.
 
Back
Top Bottom