Jodoki Kalimilo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 12,673
- 11,343
Watu kutumia kitu vibaya haimaanishi kuwa idea nzima ni mbaya.
Mahari yanatumiwa na wengi kuunganisha familia tu.
Kumfurahisha babu mjukuu wake kaolewa, basi anapewa shuka jipya; bibi anapata kanga mpya
Sidhani kama kuna asiyependa kupokea zawadi
Mbaya ni kwamba, wakati mwengine tunatumia mahari kama tupo kwenye biashara.
Na hii kwa mwanamme asiyetaadhima, ndipo anapoitumia kuwa kamnunua mwanamke.
Familia zinatakiwa kuwa careful hapo. Ionekane wazi kuwa hii ni a small token of appreciation na sio biashara
Yes hiyo ni kweli, hata kama hawaishi pamoja bado jamaa akikukuta na huyo mwanamke lazima ukatwe masikio kwa kushikwa ugoniHapa kuna ukweli, kuna wengine ile mahari inawapa kiburi hasa kama alitoa nyingi, japo si wote.
Pia mke anaweza kuwa anateseka ila anaogopa kusema sababu ya kuhofia mahari kurudishwa, ni aibu kweli kwa familia ya mke.
Mwanamke anakuwa mali ya mmewe kabisa.
Kwa mfano wakurya, mke akiolewa, akazaa watoto halafu akaachika kwa mmewe wa awali, ambaye ndio alimtolea mahari. Mwanamke huyo akaamua kuishi na mwanamme mwingine, wakazaa watoto, mume wa awali anakuwa na mamlaka kwa mkewe na watoto aliowazaa na mme mpya. Ana uwezo wa kwenda kuwachukua mkewe na watoto aliozaa huko na wote ni mali yake. Kisa? Yeye ndio aliyetoa mahari ya mwanamke yule, na yeye ndio anatambulika kwao. Cha ajabu hata mume wa pili wala halalamiki wanae kuchukuliwa.
Same scenario kwa nyumba ntobo, wanawake wanalazimika kuishi kwenye aina hii ya mahusiano sababu tu ya mahari aliyotolewa, hata akitamani kubadili aina ya maisha inawawia vigumu.
Ila ukiondoa mapungufu hayo, bado mahari ina nafasi yake.
Hii bomba sana kwa vijana wetu huku bara kama inge-apply maana vijana wengi wanaogopa kutangaza nia kuhofia hii kitu wanasahau sherehe (harusi) ni utaratibu kikubwa ni ndoa either kanisani, kwa mkuu wa wilaya au masjid
Ha ha ha ha, afu jacuzi la beseni la simba plastik, very romantic
Hahahahaa sasa bhana kuna zile harusi za uswahilini ambazo watu waliopoana miaka lukuki iliyopita, sasa wakiona mambo yamekuwa magumu wanatangaza kubariki ndoa (Hii ni kwa wakristo hasa RC) ndani yake kunakuwa na lengo moja tu kubwa, kupata zawadi na fedha za mtajiManeno mazuri hayo mkuu kwa kuongezea hapa wazee wetu walikuwa na alama za kujivunia na jamii nzima ilikuwa inazikubali hivyo inapotolewa mahari mfano ya mbuzi au ng'ombe kila mmoja kwenye familia aliona amethaminiwa pamoja na kwamba hata wao hiyo mifugo wanayo. Sasa zama hizi ndio kasheshe mtu kabila lake ni kwa ajili ya kujaza kwenye document au kama kakamatwa na polisi maana ndio huwa wanauliza kabila baada ya hapo hakuna kingine anachojua kuhusu kabila lake plus uwezekano wa kumwoa mtu wa kabila lake ambao wana-share mila na desturi unakuwa mdogo kutokana na mazingira ambayo amekulia hivyo inapofika suala la kuoana ndio yanakuja haya mambo ya mahari milioni kadhaa kwa kuwa wanadhani fedha ndio dhana nzima ya kuoana kumbe mahari ni sehemu ya kuonyesha familia hii na ile imekuwa kitu kimoja, naomba kuwasilisha
Rangi, elimu ya darasa la saba hivi muhimu sana (at least binamu zangu niliona wakati wanaolewa, mmoja hakumaliza la saba alikuwa hata familia haibageini kwa kujidai)
Vingine ni pamoja na kuolewa kwa kuchumbiwa(sio kutoroshwa-kulehiwa wala kubwakwa-kupondiwa), tena sifa huwa kubwa zaidi pale ambapo mchumba wala humfahamu, labda ni wa kijiji jirani kakuona gulioni akakufuatilia hadi kwenu then akaja kuchumbia. Chezeiya wamekuja na Phonex kama 4 zimepaki nje, sio waje wamebebana, kila mmoja aje na yake, ooh my God ni zaidi ya X6.
Vingine vinavyoongeza soko la binti kwenye kubargain mahari ni pamoja kama hajazaa, akiwa kazaa bargaining power inapungua.
Pia kuna vitu kama body size, meno, mwanya maana hizi vinajumuisha kwenye definition ya uzuri.
habari ya hapa kimila kwa mfano (unakotokea wewe) Mahari huwa ni ya nani? Nasikia kuna wengine mahari huwa ni ya muolewaji mwenyewe so mara nyingi ye ndiye huwa anaplay sehemu kubwa ya kuamua inakuwa kiasi gani. We unafikiri average mahari inatakiwa kuwa kiasi gani?
Hahahahaa sasa bhana kuna zile harusi za uswahilini ambazo watu waliopoana miaka lukuki iliyopita, sasa wakiona mambo yamekuwa magumu wanatangaza kubariki ndoa (Hii ni kwa wakristo hasa RC) ndani yake kunakuwa na lengo moja tu kubwa, kupata zawadi na fedha za mtaji
Hahahahaa haya mkuu, ila issue ya Mahari seems to be a very complicated matter kwa kweliTena wengine na kitchen party inakuwepo hapo ndio huwa ninashangaa maana ukiangalia picha za harusi ukaangalia na familia yaani baba, mama na watoto utaona mambo yapo inversely proportional, umri wa watoto ni mkubwa kuliko ndoa, nadhani ndoa kama hizi ni sehemu ya ku-formalize mambo hivyo hata issue za michango michango ni ya kupuuzia unless kama jamaa zako wameamua kukufanyia kutokana na umaarufu wako