Mahari kwa M pesa

Mahari kwa M pesa

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
79,036
Reaction score
168,674
Jamani,

Jana nilialikwa kwenye sherehe ya kupokea mahari.

Nikiwa kama mjomba wa anayetarajiwa kuolewa, bwana harusi alisema atatuma mahari kwa njia ambayo ilimuwezesha kukutana na binti yetu.

Alisema walikutana kwenye facebook, hivyo mahari atatuma kwa M pesa na harusi watafuna online.

Bwana harusi yuko Mwanza ambako anafanya biashara zake huko.

Baada ya baba wa binti kupata mashaka, bwana harusi akatuma shilingi milioni tano akitumia laini ofauti tofauti, baba akaingiwa na imani, na anaona ni jambo jema kufanya harusi ya kihistoria.

Hivi ndoa kama hii (iwapo itafungwa onine) je itatambuliwa kisheria?

Nimebaki na maswali mengi ambayo baada ya kujazwa mapesa, baba wa binti kaacha kujiuliza, na anasubiri kwa hamu mwanawe aolewe
 
Sijui huko nje, hapa kwenu, ndoa haifungwi mpaka wahusika wawepo. Labda zile za mauzauza za mtu kumuolea mwenzake ilhali hayupo, lkn hayo ni magumashi.
 
Huyu baba ni pnguani ama hamnazo?
5Mil ndio zimemsahaulisha shida zake?
Kweli hamna dhambi mbaya kama umasikini, na usiombeee umasikini wa kipato ukichaganyika na ule wa fikra, yaani ni hatari tupu
 
Nilishuhudia km hiyo mwaka 2011hapa dar.Bw harus nilikuwa nafanya nae kaz mchumba yupo kahama,kila kitu ni m pesa mpaka tulimuozesha jamaa yetu pale tbs.Mahali ilikuwa lak 8,tulituma 6 then tukamalizia 2 zote kwa m pesa.Naul ya wazaz pande zote kuja dar kwenye shughur ni m pesa.ULIMWENGU WA DIGITAL HUU.
 
Huyu baba ni pnguani ama hamnazo?
5Mil ndio zimemsahaulisha shida zake?
Kweli hamna dhambi mbaya kama umasikini, na usiombeee umasikini wa kipato ukichaganyika na ule wa fikra, yaani ni hatari tupu
Kwa hiyo wewe umeziona ndogo
 
Jamani,
Jana nilialikwa kwenye sherehe ya kupokea mahari.
Nikiwa kama mjomba wa anayetarajiwa kuolewa, bwana harusi alisema atatuma mahari kwa njia ambayo ilimuwezesha kukutana na binti yetu.
Alisema walikutana kwenye facebook, hivyo mahari atatuma kwa M pesa na harusi watafuna online.
Bwana harusi yuko Mwanza ambako anafanya biashara zake huko.
Baada ya baba wa binti kupata mashaka, bwana harusi akatuma shilingi milioni tano akitumia laini ofauti tofauti, baba akaingiwa na imani, na anaona ni jambo jema kufanya harusi ya kihistoria.
Hivi ndoa kama hii (iwapo itafungwa onine) je itatambuliwa kisheria?
Nimebaki na maswali mengi ambayo baada ya kujazwa mapesa, baba wa binti kaacha kujiuliza, na anasubiri kwa hamu mwanawe aolewe

mkuu hujawahi fanyiwa interview online? hujawahi sikia watu wanatoa ushahidi wa kesi wakiwa tanzania kesi ipo italia? inawezekana kabisa na ikawa halali ingawa sijawah sikia ndoa ya namna hiyo. ila sababu ni nn huyo bwana harusi kutokuja kwenye ndoa?
 
Jamani,
Jana nilialikwa kwenye sherehe ya kupokea mahari.
Nikiwa kama mjomba wa anayetarajiwa kuolewa, bwana harusi alisema atatuma mahari kwa njia ambayo ilimuwezesha kukutana na binti yetu.
Alisema walikutana kwenye facebook, hivyo mahari atatuma kwa M pesa na harusi watafuna online.
Bwana harusi yuko Mwanza ambako anafanya biashara zake huko.
Baada ya baba wa binti kupata mashaka, bwana harusi akatuma shilingi milioni tano akitumia laini ofauti tofauti, baba akaingiwa na imani, na anaona ni jambo jema kufanya harusi ya kihistoria.
Hivi ndoa kama hii (iwapo itafungwa onine) je itatambuliwa kisheria?
Nimebaki na maswali mengi ambayo baada ya kujazwa mapesa, baba wa binti kaacha kujiuliza, na anasubiri kwa hamu mwanawe aolewe

Hiyo sherehe ya kupokea mahali mliifanya online au mlikuwa pamoja na bwana harusi ana kwa ana? Ikiwa mliifanya online hakuna haja ya kushangaa yaliyojiri.
 
Kweli siku hizi thamani ya mahari imekwisha........... mahari imepoteza umaana. Zamani kutoa mahari ilijumuisha na kukutana na upande wa pili na aliyekuwa analeta mahari hakuwa muoaji bali wazee wake. Pengine kwa kuwa ilikuwa inaletwa in-kind sio cash but hata kwa kasha makabila mengine huwa na taratibu za kufuata mf. kuzifunga kwenye kitambaa cha mkononi wakati unakwenda kuziwasilisha. Ile sherehe ya kuipokea, ule upokeaji wake na mengineyo. Mwe siku hizi imekuwa rahis rahisi tu.............. eti tumekutana FB ndio mahari ulete kwa Mpesa? So kama alivyouliza mdau hapo juu na mwanangu utamdoia online au?
 
Huyu baba ni pnguani ama hamnazo?
5Mil ndio zimemsahaulisha shida zake?
Kweli hamna dhambi mbaya kama umasikini, na usiombeee umasikini wa kipato ukichaganyika na ule wa fikra, yaani ni hatari tupu

Kwa comment yako inaonyesha una mkwanja kweli. Yaani unadharau mil5, ungalijua kuwa wenzio wanaolewa kwa laki 2 na wengine bure usingali sema haya. Kila la heli mkuu na kila mbuzi hula urefu wa kamba yake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom