Maharamia wa Kisomali na majumba mapya Mbezi

Si afadhali hawa wanaojenga hapa kuliko hawa maharamia wa madini ambao watatuachia mashimo na sumu ardhini baada ya kuondoka na kila kitu,Gwasika pia nahisi una personal vendetta baada ya kukwaruzana na mmoja kwenye biashara this is beyond hate.

Mkuu uporoto1, nashindwa kundi la kukuweka, pamoja na facts zote zilizochangiwa hapa.
Sijui kama ni ugumu wa kuelewa au kutokuwa na uwezo wa kufikiri sijui.
Pengine tuweke kwa lugha rahisi ambayo unaweza kuielewa vizuri.
Unaambiwa kitandani kwako kuna nyoka mwenye sume-wee unajibu upuuzi huo nyoka ataingiaje katika nyumba nzuri hii na ina magrilli.
Unaambiwa , jirani yako ameumwa na nyoka jana tu-wee unasema aah bahati mbaya tu.
Na wewe huchukui tahadhari yoyote.
Sasa mkuu kama wewe uporoto1 kuumwa na nyoka ni stahili yako.

Uporoto1 kuniweka katika kundi la kuwa na bifu na hawajamaa (Wasomali) ni kujiaibisha kwa upande wako kwa vile swali langu la kwanza ni kutafuta ukweli, kitu ambacho kimedhihirika kutokana na michango tofauti.
Mkuu uporoto1, una matatizo ya kimsingi na hakuna uafadhali wa maharamia wala wale wanaoacha sumu ardhini katika migodi.
Na hapo ndo unaonekana huna dira ya kimaisha kama mtanzania.
 
What a stupidity argument!Kwa nini wasiwekeze Mogadishu?Who need piracy money,kuendeleza nchi?Japan,South Korea hawajaendelea na hela za wizi,ni UBONGO ndio unaendesha nchi.Al Shabaab wapo bongo,ngoja siku waje wakulipue !
I think between Stuxnet and Mmakonde it is Mmakonde who is stupid because he can not think outside the box. There are various ways of wealth redistribution based on different schools of thought. Even Mwalimu Nyerere when he was chair of the South- South Commission, on repayment of loans to developed countries he said "countries of the south should refrain from paying loans to developed countries because, we are taking what they took from us during colonialism"
 
Hapana mkuu kama ni fedha chafu wanayotumia kuwekeza hapa kwetu lazima tuipigie kelele, tusishiriki dhambi yao maana Mungu atailaani nchi yetu kama tutaikumbatia hii dhambi. Isitoshe mhalifu ni mhalifu tu kesho atatugeukia watanzania na kuanza kutupora pale meli zitakapoimarisha ulinzi na wakashindwa kuendelea kupora. Huwezi kujua labda pia wanashiriki kwenye biashara ya madawa ya kulevya. Nyumba zinamushroom hadi najiuliza hawa watu wanaokota hizi hela? Mbona mie siziokoti? WaTanzania tuwe macho na hawa watu sio wazuri hata kidogo. Mafia ni mafia hata kama atakupa hela za kuishi!!!
 
Pesa chafu kama ya uharamia, ufisadi, dawa ya kulevya nk haiwezi kuwa halali iwe isiwe, na huwa haisadii jamii japo wachache (nina maana wauza madawa wa amerika ya kusini ambao kidogo waliweza kusaidia jamii inayowazunguka kama ombaomba). Ninadhani ni jambo la maana mkuu hapo kutoa wazo kama hili kwasababu intelijinsia kote duniani huanzia kwenye vyanzo vya ajabu sana ( wengine wameita hoja ya kijinga hapa:A S 114 Tunaona miradi mingi ya hawa wasomali inakwenda kasi isiyo ya kawaida mfano kisa cha karibuni maeneo ya kigamboni ambako kuna msomali mmoja alijenga uzio wa matofali usiku wakati wa sikukuu za Pasaka!! mafundi ujenzi walikuwa wanalipwa bila kujali kiasi cha kazi yaani pesa ilikuwa nje nje. baada ya serikali (serikali ya mtaa) kuuliza maswali mawili matatu huyu jamaa hajaonekana tena huku nyuma kaacha maswali mengi sana yasio na majibu...ukweli ni kwamba wapo tena wengi waliotoka somalia baada ya serikali kusambaratishwa ni matajiri wakubwa sana hapa nchini. hivyo sio kweli kwamba wabongo ni wavivu au wabaguzi... haya mambo yapo na serikali yetu inajua.......... :music:
 
Hivi unajua Uswis imefaidika sana na pesa chafu? Au wewe pesa chafu ni za maharamia wa kuteka meli tu?
 
Fedha chafu gani?huko majuu kwenyewe pesa za madictotar zimejaa kwenye mabenki na huwa wanazing'ang'ania na kuzitumia wao pesa na mali za libya,iran,abacha etc wamechimbia wazungu.
Hamna pesa chafu bwana
 
Fedha chafu gani?huko majuu kwenyewe pesa za madictotar zimejaa kwenye mabenki na huwa wanazing'ang'ania na kuzitumia wao pesa na mali za libya,iran,abacha etc wamechimbia wazungu.
Hamna pesa chafu bwana
Hal hala bwana, wakizifuata usijekuwa wa kwanza kukimbia nchi kama mkimbizi.
 
Utawala wa Jenerali Mohammed Siad Barre ulipopinduliwa, mawaziri wengi wa serikali yake walikimbilia Tanzania na kuanzisha miradi ktk vitongoji vya DSm vya Kigamboni na Buguruni kwa kutaja maeneo machache. Miradi hiyo ya wakimbizi hao waliokuwa ktk serikali ya Somali ni pamoja na majumba ya ghorofa, vituo vya petroli (sheli), mahoteli na usafirishaji.

Pia wasomali wenye asili ya Tanzania wametapakaa huko nchi za Scandinavia na Marekani ya Kaskazini na kutokana na shughuli zao za kibiashara na kuendesha magari makubwa huko ughaibuni sasa wameanza kurudisha mitaji nyumbani Tanzania ktk miji yao ya asili ya wasomali-wakitanzania yaani Arusha, Moshi na Dar-es-Salaam.
 

wewe naona ni jamii ya wasomali, ipo siku tutawarudisha kwenu somalia maana nia yenu ni mbaya kwetu watanzania
 
Kenya kuna nyumba za hatari sana, na sehemu wanazokaaa Wasomali nairobi inaitwa Isilii!, Kuna biashara haramu huko ni balaaa mpaka roho ya mtu unaweza kupata, Wanavifaaa vya umeme haieleweki vinatoka wapi afu ni cheap sana, ila ukinunua na ukaweza kutoka navyo kwenye eneo lao bila matatizo hapo utakuwa umewin!
 
Hakuna fedha chafu popote pale duniani, nawasihi wasomali wazidi kuzileta tu zikuze ajira, ziboreshe miundombinu na hatimaye uchumi ukue. Whether wanazipata kwa uharamia au wanaua watu sisi haituhusu kwani tuko sawa na mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa. Hana kosa wazazi wake ndiyo wana kosa
 

hata south c pia wamejazana....bei ya viwanja haishikiki south c!
 
hiyo TANSOMA (ambayo nadhani ni TANZANI-SOMALIA) ni kama vile nao wameshtuka maana ile ya Nkrumah St wamelitoa hilo jina na sasa inasomeka 'HOTEL' tu. Tatizo hizi sio reliable and consistent investments!
 
Ukiangalia hili neno la 'hela chafu' ni la kinafiki tu Mji wa las Vegas ulijengwa na hela za mafia serikali ya U S wakifahamu,Uswisi imejengwa na hela zilizoibwa Ujerumani wakati wa vita na kila jambazi na dictator anaweka hela zake huko bila maswali yeyote.CIA kuna wakati walikuwa wauzaji wazuri wa mihadharati ili kupata hela za kujiendesha ambazo hawataulizwa na serikali zimetoka wapi.Mwaka jana ilikamatwa ndege ya kijeshi ya Marekani ikwa na heroin nusu tani kutoka Afghanistan ilipotua Italia soo likazimwa.
 

Una akili sana bwana uporoto01, sijui lakini unatoka usweke upi.
Nenda LEO Marekani na usithibitishe pesa ulizonazo mfukoni kwako zikizidi dola 5000, na lupango ni yako.
Hayo yalimpata kigogo mmoja wa Uganda, Meya wa Jiji la Kampala baada ya kuto-declare dola 100,000 alizokuwa nazo mfukoni.Kwa hakika lupango alikwenda.
Tusipende kuiga historia ambazo tunajua fika hatuna utamaduni nazo.
 

Mkuu uporoto01, nashangazwa sana na akili ya namna hii.
Hivi unaweza kutetea vipi analogy hii kwa mazingira ya kiTanzania.
Las Vegas na miji mingine uliyoitaja ushoga, ukahaba na wizi na mauaji ni fair game.
Je hawa wageni wakikubebea mmoja wa familia yako mradi wanakupa pesa kweli utaona ni sawa tu?
Nafikiri Mkuu una matatizo.
 
Uporoto fikra zako ni sawa na zangu usiwasikie hao wanaolalama kuhusu fedha chafu. Hata taasisi za dini zenye nguvu kubwa na wafuasi wengi duniani ukizichunguza vyanzo vyao vya mapato utashangaa. Kasome kitabu cha David Yallop kinachoiywa "in the God's Name" utajua kwa nini Pope John 1 wa Kanisa Katoliki aliishi kwa siku zisizozidi 40 baada ya kutawazwa kama kiongozi mkuu wa imani hiyo pale mwaka 1978
 
Tangu mwanzo nilisema kuna kitu binafsi kinachokusukuma kwa hili angalia kwenye capitals,halafu pia dhana ya kuwa kila mwenye mawazo totauti ana matatizo ni potofu,tukubaliane kutofautiana.
 
Tangu mwanzo nilisema kuna kitu binafsi kinachokusukuma kwa hili angalia kwenye capitals,halafu pia dhana ya kuwa kila mwenye mawazo totauti ana matatizo ni potofu,tukubaliane kutofautiana.
Mimi nikifikiri naongea na watanzania wenye uchungu na nchi yao kumbe kuna wale wenye "upeo mpana zaidi" wa kuweza kuside na wageni katika mabo yahusuyo nchi yetu.
Wenye ufinyu wa uzalendo , lisipowahusu basi hilo ni la kwako na haliwahusu.
Wenye kujiona na umimi basi ukionya juu ya hatari mbeleni basi wewe una chuki binafsi.
Kuonya ni wajibu
Kuonyeka ni uchaguzi wako.
Idi Amin aliposhambulia nchi hii walikuwepo walioside naye , tena humuhumu nchini, Mwalimu hakufanya ajizi.
Wasomali waliposhambulia na kuua OCD kule sehemu za kaskazini , kuna walioopewa vijisenti, na waka side nao, nina uhakika nao walionja shubiri wanayostahili.
Mkuu uporoto01, watu wa aina yako mko wengi tu, alimradi matatizo ya waTanzania wengine hayawagusi basi nyie ni kula bata tu na wageni wa maangamizi-kama hawa ndugu.
Siku ikifika mgeni maangamizi na vibaraka wake watakuwa fair game.
 
Naomba kukumbushwa hawa wabunge wa jamhuri ya muungano waliothibitishwa kufacilitate usafirishaji wa akina mama wa kisomali kwenda ulaya(germany) kwa kufunga nao ndoa fake na kupewa diplomatic pasport, je waheshimiwa hao wana asili ya somakia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…