Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 950
- 2,866
Nikiwa ndio nimeajiriwa NBC mwaka 2008 kuelekea 2009 kwenye mkutano mmoja NBC MD's road tour, nilimsikia mtu mmoja anahutubia anasema "Mtaimba sana Solidarity forever lakini mtabaki hapo hapo,Mimi nimeomba nafasi ya COO wa NBC nimeitwa kwenye interview nimekutana na makaburu tu hakuna Mtanzania, nikaenda South Africa nikawagaragaza makaburu kwenye interview na nikapata nafasi hii niliyonayo sasa, sasa Nina nyumba ya privilege na gari ya privilege lakini ninyi mnalalamika hampandishwi vyeo na Watanzania wanasema kazi hamna wakati nafasi ya ukurugenzi wa Posta bank imetangazwa mwaka wa pili sasa hakuna aliyeomba?" nikauliza wenzangu huyu nani wakasema Maharage Chande,Chief Operating Officer,COO niliguswa sana na maneno yake,
Maharage Chande akaendelea "Mimi sikai milele kwenye hiki cheo nakaa miaka miwili na nataka ukurugenzi kama sio hapa basi popote pale,akageuka kumcheki Lawrence Mafuru aliyekuwa Head of Finance nae alikuwa anautaka ukurugenzi wa NBC na wote wakageuka kumtazama Vermaas aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NBC,kaburu alitikisa kichwa kukubaliana nao, Lawrence Mafuru alianza kukaimu nafasi ya Ukurugenzi Mkuu wakati Vermaas akienda Christmas Holiday,na mwaka mmoja mbele Lawrence Mafuru akawa Mkurugenzi Mkuu wa NBC na mwaka mmoja mbele Maharage Chande akawa Mkurugenzi Mkuu wa Multichoice Afrika Mashariki.
Nimalizie kwa kusema,story hii iitwe Mr Beans our inspiration.