MAHAKIMU nao njiani KUGOMA...

mahakimu hawaruhusiwi kugoma kisheria.
labda hawa wapya hawajui ethics zao
hela watapelekewa fungu lao limeshatengwa.
waliendaje kwenye vituo vya kazi bila fedha za kujikimu na usafiri? inatia shaka.
Tanzania hakuna mfanyakazi yeyote anayeruhusiwa chochote, kisheria, ndio maana migomo yote ikawa batili na kesi kufikishwa mahakamani.
 
Wale Mahakimu Wakaazi 300 walioajiriwa na Serikali mnamo mwezi wa sita na kusambazwa mikoani wako njiani kugoma.Taarifa nilizozipata zinaonesha kuwa Mahakimu hao,tangu kuajiriwa kwao hawajalipwa mshahara wowote au hata fedha za kujikimu. Taarifa zinaonesha kuwa hali zao sasa ni mbaya na wanateseka vya kutosha.

Kwakuwa wote wanajuana vyema,Mahakimu hao Wakaazi ambao wamepelekwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama za Mwanzo wamepanga kugoma ili kudai maslahi yao kwa Serikali 'sikivu'. Ifahamike kuwa Mahakimu wakaazi ni wale wenye elimu ya ngazi ya Shahada na kuendelea na hawakuwahi kuwepo katika Mahakama za Mwanzo.Kupelekwa kwao,kutaruhusu Mawakili Wasomi kujitokeza Mahakama za Mwanzo.

Wanasema 'liwalo na liwe'....


Ussu-Malya,Ananilea Nkya na Mama Bisimba hawajatoa tamko juu ya hili bado?Maana kwenye hizi ishu za kuigomea serikali ndiyo huwa tunawaona.
 
ukisoma vema sheria mpya ya kazi kuna makundi yameanishwa kule
kugoma ni haki ya mfanyakazi kushinika kitu fulani baada ya hatua zote muhimu kufuatwa
na kuna procedure wanatakiwa kutumia ili mgomo uwe halali
lakini kada kama wanajeshi, polisi, mahakimu hawaruhusiwi kugoma kwa njia yoyote ile
Tanzania hakuna mfanyakazi yeyote anayeruhusiwa chochote, kisheria, ndio maana migomo yote ikawa batili na kesi kufikishwa mahakamani.
 
Kama kweli wakigoma, sijui mahakama itahukumu vipi shauri hili.
 
ukisma vema sheria mpya ya kazi kuna makundi yameanishwa kule
kugoma ni haki ya mfanyakazi kushinika kitu fulani baada ya hatua zote muhimu kufuatwa
na kuna procedure wanatakiw akutumia ili mgomo uwe halali
lakini kada kama anajeshi, polisi, mahakimu hawaruhusiwi kugoma kwa njia yoyote ile
Hayo unayosema ni sawa kwani yamo katika vitabu na maandishi, lakini ukija katika utekelezaji wa sheria hizo, huo ni unafiki wa kisiasa na kidemokrasia, unaokupa haki kwa mkono mmoja na kukunyang'anya haki hiyo hiyo kwa mkono wa pili. Fikiria wewe mwenyewe na umri ulio nao, umewahi kusikia au kuona mgomo toka kada yoyote ambapo serikali imekubali kuwa ni mgomo halali?
 
Mahakimu hua wanatuonea sana kwenye kesi zetu kwa kuendekeza rushwa zaidi kwa hiyo hata siwasupport tena wakigoma ndo vizuri na kesi zisisikilizwe
 
Back
Top Bottom