Mahakama Yazuia Kwa Muda Matumizi Ya Jina La 'ze Comedy'

Balantanda

JF-Expert Member
Jul 13, 2008
12,476
4,754
Mahakama kuu kitengo cha Biashara imelizuia kundi maarufu la vichekesho la Ze Comedy na kituo cha televisheni cha EATV kutumia jina la Ze Comedy kwa shughuli za kisanii wakati kesi kuu ikisubiri hukumu.....Mahakama imetoa huo baada ya kundi hilo kutoa ombi la kutaka mahakama itoe zuio dhidi ya kituo hicho cha EATV kuwazuia kufanya kazi zao za sanaa chini ya jina la Ze Comedy na pia lilitaka Mahakama itoe tamko kuwa jina hilo linamilikiwa kihalali na kundi hilo baada ya kuwepo kabla na baada ya kuingia mkataba na EATV.........Kundi hilo pia liliomba Mahakama kutoa amri ya kuizuia EATV kuingilia shughuli za kibiashara za kundi hilo pamoja na amri ya kuondoa alama za kundi hilo kutoka EATV kwenda Shirika LA Utangazaji Tanzania(TBC).................Jaji wa Mahakama hiyo Catherine Urio baada ya kupitia hoja za pande zote mbili amesema kwamba Mahakama imebaini kuwa hakuna mwenye haki ya kutumia alama na jina la Ze Comedy kwa kuwa mkataba wa pande zote hizo mbili uliisha tangu mwezi Juni mwaka huu............Kesi imesogezwa mbele hadi tarehe 21 Oktoba itakaposikilizwa tena.............Inakuwaje hii wakuu??????????????
 
Back
Top Bottom