Mahakama yamuumbua waziri Magufuli na sheria zake za uongo

WATANABE

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
1,092
466
Katika siku za hivi karibuni umeibuka mgogoro mkubwa wa kijamii hapa nchini uliosababishwa na maamuzi ya kibabe ya Mhe John Magufuli kuhusiana na malori na mabasi, hivi sasa mgogoro huo unapelekea kuathiri vibaya uchumi wa nchi na kusababisha mfumuko wa bei na kuathiri ajira za wananchi wengi sana.

Ndani ya jamii zipo pande mbili zinazolumbana moja ikiwa ni pamoja na mtani wangu Jackton Manyerere wakimuunga mkono Mhe Magufuli kutokana tu na kauli zake za mdomoni kuwa "analinda, kusimamia na kufuata sheria" pasipo wahusika kuchukua hatua zozote kujiridhisha kama ni kweli kiongozi huyu analinda na kusimamia sheria kama anavyojigamba. Na kundi la pili ni lile linalomuoona kiongozi huyu kama mtu mbabe na asiye na busara wala hekima hata kidogo kutokana na matendo na kauli zake za kibabe. Itakumbukwa kuwa hata Mhe Jakaya Kikwete aliwahi kumwambia hadharani Mhe John Magufuli kuwa apunguze ubabe, japo wakati ule watu wengi sana walimpinga Jk japo upo msemo wa wahenga kuwa "mnyonge mnyongeni haki yake mpeni" leo ukweli umejidhihiri.

Wote tunakumbuka sakata la "Hifadhi ya Barabara" ambapo Mhe Magufuli kwa muda mrefu sana amekuwa akidai kuwa anasimamia na kulinda Sheria ya barabara "The Highway Ordinance Cap 161 of 1967 GN 161 of 5/5/1967" (na wakati huo huo akipuuza Sheria ya Ardhi ya Vijiji Namba 5 ya 1999 aliyoshiriki kuipitisha akiwa mbunge), hivyo mara kwa mara kwa kuzingatia sheria hiyo tu amekuwa akichukua maamuzi mazito ya kibabe na yasiyo na utu ndani yake kwa kuiagiza TANROAD nchi nzima kuingia isivyo halali katika ardhi na makazi ya wananchi, kuweka alama za "X" kwa maana ya "kucondemn ardhi za wananchi na hivyo kuwasababishia athari mbali mbali za kijamii na kiuchumi na mara nyingine kubomoa nyumba za wananchi maskini kiasi cha kupeleka baadhi ya kaya kukosa kabisa makazi, kukosa vipato, watoto kushindwa kuendelea na masomo na athari zingine nyingi. Kutpokea mwaka 2002 alipoanza umyama huo watu kadhaa wameshapoteza maisha kwa magonjwa ya mshtuko wa moyo, shinikizo la damu na mengine kama hayo baada ya nyumba zao kuwekewa alama za X na kisha kubomolewa isivyo halali, aidha wengi zaidi wameathirika vibaya kiakili na kisaikolojia kwa kushindwa kutumia ardhi na majengo yao yaliyoko mbali kabisa na barabara (Mita 120 toka katikati ya barabara ya Morogoro) yaliyovamiwa na TANROAD isivyo halali kwa maelekezo ya Mhe Magufuli. Kwa maelekezo haya haramua ya Mhe Magufuli ardhi na majengo haya ya wananchi wanyonge na maskini hayawezi tena kutumika kwa ajili ya kupangishwa, kama dhamana benki n.k

Hivi karibuni Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi imetoa hukumu katika kesi namba 80 ya 2005 iliyofunguliwa na Ndg Proches Tarimo na wenzake dhidi ya Wizara ya Ujenzi kupinga amri ya kuboma nyumba za wananchi zilizoko Mita 120 toka katika ya barabara pande zote mbilia eneo la Mbezi Mwisho katika barabara kuu ya Morogoro. Amri hiyo ilitolewa na TANROAD mwaka 2004, ikidai eneo hilo ni hifadhi ya barabara kwa mujibu wa sheria hiyo haramu. Itakumbukwa kuwa amri hiyo ya TANROAD ilitolewa miaka mitatu tu baada ya Mhe John Magufuli kuteuliwa kwa mara ya kwanza kushika wadhifa wa Waziri wa Ujenzi na Rais Benjamin Mkapa, ilihali wananchi hao wamekuwa wakiishi maeneo hayo miaka nenda rudi pasipo usumbufu wowote kutoka kwa mawaziri wa ujenzi wa Serikali za awamua ya kwanza na ya pili wakati huo Mhe John Pombe Magufuli akiwa bado mtoto mdogo.

Itakumbukwa kuwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa barabara ya Morogoro na barabara zingine hapa nchini, ambao hivi sasa wanaitwa "wavamizi wa barabara" na Mhe Magufuli, walihamishiwa katika maeneo hayo kwa nguvu tena wengine kwa kuchomewa makazi yao huko walikotolewa na Serikali ya awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere katika "Operesheni Vijiji Vya Ujamaa" iliyofanyika miaka ya 1970s wakati huo Mhe John Magufuli akiwa bado mtoto mdogo. Hivyo si kweli hata kidogo kuwa walivamia barabara, hizi ni kauli za kichochezi zenye lengo la kuwawezesha viongozi wa Serikali kutumia vibaya nyadhifa zao kuwapora wananchi ardhi kama walivyofanikisha njama ya kujitwalia nyumba na viwanja vya Serikali bure na kwa bei chee.

Mhe John Magufuli akijigamba "kufuata, kulinda na kutetea sheria feki ya "The Highway Ordinance Cap 161 of 1967" ambayo katika hukumu hiyo Mahakama Kuu imetamka kuwa ilipoteza uhai tokea mwaka 1999; kuaniza mwaka 2002 Mhe Magufuli amewasababishia wakazi waishio pembezoni mwa barabara ya Morogoro madhara makubwa ya kisaikolojia, Kijamii na Kiuchumi kwa kuvamia Mita 120 za ardhi na makazi ya wananchi toka katikati ya barabara pande zote mbili; na kuzuia maendelezo ya aina yoyote tokea wakati huo hadi sasa. Aidha kwa katika nyakati mbali mbali amekuwa akiwaagiza TANROAD kuboma nyumba za wananchi, amri ambazo Mahakam Kuu imetamka imeziona kuwa si halali bali zilikuwa haramu mbele ya sheria. Walioathrika wanastahili kulipwa fidia za aina mbali mbali ili kuwafidia dhidi ya ubabe wa kiongozi huyu kutumia madaraka yake vibaya.

Kifupi katika hukumu yake Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi imemuunga mkono Raisi Jakaya Kikwete kwa kutambua kuwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa barabara kuu hapa nchini sio "wavamizi wa barabara" kama ambavyo Mhe Magufuli amekuwa akidai na kutumia wadhifa wake kuuaminisha umma wa watanzania hivyo. Na badala yake imetamka kuwa ardhi husika ni mali ya wananchi kupitia Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na 5 ya 1999 Kifungu cha 15, kwa kuwa waliwekwa hapo pembezoni mwa bara ya Morogoro na zinginezo na Serikali hiyo hiyo anayoitumikia Mhe Magufuli chini ya Chama hicho hicho kilichoasisi na kutekeleza Sera ya Vijiji vya Ujamaa miaka ya 1970.

Mahakama hiyo pia imetamka kuwa kwa kuzingatia Sheria ya Mipango Miji eneo la hifadhi ya barabara kwa Jiji la Dar es Salaam ni Mita 30 tu toka katika ya barabara pande zote mbili hivyo si sahihi kwa mtu yoyote kudai kuwa eneo zaidi hilo kuwa ni hifadhi ya barabara; na kwa kuwa wanaoishi pembezoni mwa barabara waliwekwa hapo na Serikali katika operesheni Vijiji wanapaswa kulipwa fidia kwa mujibu wa Sheria za Ardhi na Mahakama ikaelekeza utaratibu wa kufuatwa na TANROAD kuhamisha ardhi husika kutoka "Ardhi ya Kijiji" kuwa "Hifadhi ya barabara". Kwa maana ingine Mahakama imetupilia mbali utetezi uliotolewa na Wizara ya Ujenzi kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kuwa zipo sheria za kuanzia mwaka 1932 hadi 1967 zinazotamka kuwa hifadhi ya barabara ni zaidi ya hapo. Kichekesho kilikuwa Mahakanai pale Wizara ya Ujenzi iliposhindwa kuithibitishia Mahakama wapi "Morogoro Road" ilikuwa ikipita kwa nyakati mbali mbali chibni ya sheria hizo feki za Mhe Magufuli. Chini ya Sheria hizo za kikoloni barabara ya Morogoro ilikuwa ikipita sehemu tofauti kabisa na ilipo sasa.

Kwa faida ya wasomaji wangu na kwa lengo la kutompatia fursa Mhe John magufuli kuwadanganya watanzania kuwa kwa hukumu hii sasa sekta ya barabara hapa nchini itashindwa kuendelezwa. Ibara ya 27 (1) ya Kanuni ya Sheria ya Barabara Namba 13 ya 2007 zilizotolewa kupitia GN Notice No 21 ya tarehe 23 Januari 2009 inaeleza upana wa njia za barabara za lami (Lanes) hapa nchini. Na kwa njia moja ya barabara kuu (Trunk Roads) upana huo usipungue Mita 3.25. Hivi sasa upana njia za barabara ya Morogoro Road yenye njia mbili ni Mita 6.5.

Hivyo katika upana halali wa hifadhi ya barabara uliotamkwa na Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kupitia hukumu hii wa Mita 30 kila upande wa barabara ya Morogoro unatosha kujenga njia (lanes) 8 mpya za barabara za kuelekea Mlandizi, na njia 8 mpya za kuja Dar, hivyo kuifanya Morogoro Road kuwa ya njia (lanes) 18 kama tutakuwa na uwezo wa kifedha wa kuzijenga, kabla ya TANROAD kuwafikia wananchi walioko nje ya Mita 30 toka katikati ya barabara ambao ndio hifadhi ya barabara iliyotamkwa na Mahakama.

Katika kuthibitisha kuwa Mhe John Magufuli si muumini wa dhana za "kulinda, kusimamia na kufuata sheria" tokea arejeshwe katika wadhifa wa Waziri wa Ujenzi na Raisi Jakaya Kikwete mwaka 2010, kwa makusudi amekuwa akivunja Sheria ya barabara Na 13 ya 2007 na Kanuni zake 2009. Ibara ya 27 (2) inamtaka kuwa mara baada ya Waziri wa Ujenzi kuridhika kuwa ardhi fulani inahitajika kwa ajili ya maendeleo ya barabara, atafanya mawasiliano na Wizara wa Ardhi, kwa ajili ya ardhi hiyo kuhifadhiwa baada ya wamiliki wake kulipwa fidia. (5) Siku 60 baada ya wananchi walioko katika emaeneo husuika kulipwa fidia ndipo Mamlaka ya barabara (TANROAD) itawaarifu wananchi kuondoka katika ardhi husika au kutofanya maendelezo mengine yoyote.

Mwaka 2009, Sheria mpya ya barabara Na 13 ya 2007 iliongeza eneo la hifadhi ya barabara kutoka Mita 22.86 za zamani hadi Mita 30 kila upande kwa barabara zote kuu hapa nchini ikwa ni ongezeka la takribani Mita 8 kila upande kuingia katika ardhi na makazi ya wananchi. Tokea Mwaka 2011 Mhe Magufuli ameanza kuvunja
Sheria mpya ya barabara Na 13 ya 2007 kwa kuwaagiza Mameneja wa TANROAD nchi nzima kuingia isivyo halali Mita 8 toka Mita 22.86 hadi Mita 30 toka katikati ya barabara zote hapa nchini na kuwawekea alama za X katika nyumba zao. Aidha katika kuashiria ni namna gani Magufuli alivyo mbabe amediriki kuwaagiza Mameneja wa TANROAD nchi nzima kuvamia ardhi na makazi ya wananchi walioko pembezoni mwa vijichochoro, vijibabara vya mitaa, barabara za vijiji, barabara za Kata, tarafa, Wilya na Mikoa ambazo wananchi walizianzisha wenyewe na hazihusika kabisa na Sheria hii. Huu ni ubabe uliopituiliza kabnisa na umefika wakati wananchi wakachukua hatua stahiki.

Sheria ya barabara Na 13 ya 2007 iliyopendekezwa na Wizara yake na kupitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwekwa sahihi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa sheria iko wazi kabisa kuwa kama ataona ardhi yoyote inafaa kuwa barabara atafanya mawasiliano na Wizara ya Ardhi kwa ajili uhifadhi na utolewaji wa haki za wananchi wanaomiliki ardhi husika.
Kama Mhe Magufuli kweli ni muumini wa dhana ya "kulinda, kusimamia na kufuata sheria" ni wapi alipata madaraka ya kuwaagiza mameneja wa TANROAD nchi nzima kuingia isivyo halali katika ardhi na makazi ya wananchi yaliyoko nje ya Mita 22.86 lakini ndani ya Mita 30 ya barabara kuu zote hap nchini? Na mabarabara mengine yote na kuwawekea wananchi alama za X kabla ya mchakato wa wao kulipwa fidia kwa mujibu wa sheria ya barabara na zingine? Hivi sasa wananchi hawa nchi nzima hawaweza tena kutumia ardhi zao kupangisha majengo yao, kutumia ardhi na majengo yao kama dhamana n.k ili kujiondolea umasikini.


Kwa kuwa ibara 107A (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 inatamka kuwa "The Judiciary shall be the authority with final decision in dispensation of justice in the United Republic of Tanzania".

Kupitia hukumu iliyotajwa hapo juu ni wangapi humu JF watakubalina na mimi kuwa Mhe Magufuli hafai tena kuwa na sifa "kufuata, kulinda na kusimamia sheria" kutokana na ukweli kuwa alishiriki kama mbunge kupitisha Sheria ya Ardhi za Vijiji Namba 5 ya mwaka 1999 na katika utendaji wake kwa muda wote tokea ateuliwe kuwa Waziri wa Ujenzi kwa mara ya kwanza mwaka 2000 na Rais Benjamin Mkapa na hivi karibuni aliporejeshwa katika Wizara hiyo na Rais Jakaya Kikwete amekuwa akiipuuza sheria hiyo na kutoa kipaumbele kwa "Kanuni" katika kusigina haki za wananchi katika brabara ya Morogoro na nchi nzima; Kanuni ambayo Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi imetamka kuwa ilipoteza nguvu kutokea 1999
ilipopitishwa Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na 5. Hii ni kabla hajateuliwa kushika madaraka hayo kwa mara ya kwanza.


Maana ya hukumu hii ni kuwa tokea Mhe John Magufuli ateuliwe kuwa Waziri wa Ujenzi kwa mara ya kwanza mwaka 2000 hadi sasa popote anapodai kutumia "The Highway Ordinance Cap 161 of 1967 GN 161 of 5/5/1967" anakuwa akitenda na kutekeleza mambo "batili hapo WIZARANI". Hii ni pamoja na utitiri wa mabango yaliyowekwa na TANROAD nchi nzima (hususan Mkoa wa Pwani) kuwafahamisha wananchi uwepo wa sheria hiyo ambayo ilipoteza nguvu tokea 1999.

Ni kwanini na kwa vipi wabunge wetu toka Chama tawala na hata upinzani ambao walishiriki kutunga Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na 5 ya 1999 na ambao ni wananchi wao wanaonyanyswa hawachukui hatua dhidi ya Waziri huyu mbabe? Umefika wakati Mhe John magufulia akakubali kuwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa barabara wana haki kamili ya kutumia ardhi yao hadi pale atakapowalipa fidia wapate kuondoka. Hii ni kutokana na ukweli kuwa kama angekuwa na uchungua wa fedha za Serikali kama anavyotaka tuamini asingekubali kukaa katika Chama, Serikali na Baraza la Mawaziri n.k ambao wanaficha mabilioni huko Uswisi au kukubali kuwa sehemu Serikali yeney kuingia mikataba ya kufanya ya malipo makubwa ya ukodishaji wa mitambo ya umeme IPTL, DOWANS, RICHMOND AGGREKO n.k au kuwa sehemu ya Serikali iliyolipa fefha za RADA. Lanpokuja suala la haki ya msingi ya wananchi wanaoishi pembezoni mwa barabara kulipwa fidia Mhe John Magufuli aache kutuzuga.

Naomba kuwasilisha kuwa "Sheria" sio kama "Menu" katika migahawa ambapo mlaji huchagua anataka kula nini na nini aache nini.
 

Attachments

  • Mandele letter to TANROAD.pdf
    94.2 KB · Views: 398
  • Road Reserve Land Case Judgement.pdf
    2.1 MB · Views: 617
Yawezekana yapo maeneo ambayo magufuli amekiuka sheria!! Lakini si kwa kiwango ambacho unaeleza wewe! Sijawahi kumsikia magufuli akitaja mt120 za barabara ambavyo unasema wewe, huwa anaongelea mita 60 (30+30) labda kama una ushahidi huo utuletee.

Pia watu wanaobomolewa ni waliovamia eneo la 45mt..linalotamkwa na sheria ya zamani. Watu walioko nje ya mt 22.5 lakinj ndani ya mt 30 kutoka katikati ya barabara kuu wamewekewa alama ili waweze kupewa fidia kwa mujibu wa sheria.lakini km umejenga ndani ya eneo hilo baada ya seheria basi wewe hustahili kupewa fidia! Na ndiyo anayoyahubiri magufuli!!
 
Kutoa data vizuri kwa kuweka mifano na takwimu hata kutaja vifungu vya sheria umemuiga huyo huyo Magufuli
 
Mkuu. Huenda serikali ikakata rufaa na kushinda. Kuwekwa na serikali ni tofauti na kuwa kwenye eneo lililopimwa. Mfano watu wa mabwepande wamewekwa pale hawajapewa eneo. Wanaweza kunywanganywa wakati wowote. Kama umefika nchi za wenzetu utaona umbali wa makazi na highways. Moshi wamejitahidi sana. Super highways inakuwa na eneo kubwa zaidi la hifadhi. Cha msingi kama una uwezo usinunue kiwanja ambacho hakijapimwa na epuka viwanja karibu na barabara kuu.
 
Yawezekana yapo maeneo ambayo magufuli amekiuka sheria!! Lakini si kwa kiwango ambacho unaeleza wewe! Sijawahi kumsikia magufuli akitaja mt120 za barabara ambavyo unasema wewe, huwa anaongelea mita 60 (30+30) labda kama una ushahidi huo utuletee.
Pia watu wanaobomolewa ni waliovamia eneo la 45mt..linalotamkwa na sheria ya zamani. Watu walioko nje ya mt 22.5 lakinj ndani ya mt 30 kutoka katikati ya barabara kuu wamewekewa alama ili waweze kupewa fidia kwa mujibu wa sheria.lakini km umejenga ndani ya eneo hilo baada ya seheria basi wewe hustahili kupewa fidia! Na ndiyo anayoyahubiri magufuli!!

Kama ungekuwa makini ungekuwa unafahamu mikurupuko ya wazi Magufuli kila mara anapotafuta sifa za kijinga! Hili la mita 120 amelisema mara nyingi tu labda wewe ulikuwa uhamishoni ndo maana hujawahi kumsikia.
 
Jamani Mh Magufuli siyo mwnasheria labda wanasheria walimshauri vibaya. Maana amekuwa anasimamia sheria na kuzilinda, sioni kwa nini wanasheria wa serkali hawakuona mkanganyiko huu ulivyoonekana katika hukumu. Kwa nini hawakumtaadharisha mapema ili kuokoa gharama, maana sasa ninaona uwezekano mkubwa wa serkali kulipa fidia kubwa kwa watu walioonewa.
 
Katika siku za hivi karibuni umeibuka mgogoro mkubwa wa kijamii hapa nchini uliosababishwa na maamuzi ya kibabe ya Mhe John Magufuli kuhusiana na malor na mabasi, hivi sasa mgogoro huo unapelekea kuathiri vibaya uchumi wa nchi na kusababisha mfumuko wa bei na kuathiri ajira za wananchi wengi sana.

Ndani ya jamii zipo pande mbili zinazolumbana moja ikiongozwa na mtani wangu Jackton Manyerere ikimuunga mkono Mhe Magufuli kutokana tu na kauli yake ya mdomoni kuwa "analinda kusimamia na kufuata sheria" pasipo wahusika kuchukua hatua zozote kujiridhisha kama ni kweli kiongozi huyu analinda na kusimamia sheria kama navyojigamba. Na kundi la pili ni lile linalomuoona kiongozi huyu kama mtu mbabe na asiye na busara wala hekima hata kidogo kutokana na matendo na kauli zake za kibabe. Itakumbukwa kuwa hata Mhe Jakaya Kikwete aliwahi kumwambia hadharani kuwa apunguze ubabe, japo watu wengi sana walimpinga japo upo msemo wa wahenga kuwa "mnyonge mnyongeni haki yake mpeni" leo ukweli umejidhihiri.

Wote tunakumbuka sakata la "Hifadhi ya Barabara" ambapo Mhe Magufuli kwa muda mrefu sana amekuwa akidai kuwa anasimamia na kulinda Sheria ya barabara "The Highway Ordinance Cap 161 of 1967 GN 161 of 5/5/1967" (na wakati huo huo akipuuza na Sheria ya Ardhi ya Vijiji Namba 15 ya 1999 aliyoshiriki kuipitisha akiwa mbunge), alichukua maamuzi ya kibabe na yasiyo na utu ndani yake kwa kuiagiza TANROAD nchi nzima kuingia isivyo halali katika makazi ya wananchi, kuweka alama za "X" kwa maana ya "kuicondemn ardhi za wananchi na hivyo kuwasababishia athari mbali mbali za kijamii na kiuchumi na mara nyingine kubomoa nyumba za wananchi maskini kiasi cha kupeleka baadhi ya kaya kukosa kabisa makazi, kukosa vipato, watoto kushindwa kuendelea na masomo na athari zingine nyingi. Wapo watu waliopoteza maisha kwa magonjwa ya mshtuko wa damu baada ya kubomolewa nyumba zao isivyo halali, kuathiri kiakili kwa kushindwa kutumia ardhi zao kujiondolea umaskini n.k.

Hivi karibuni Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi imetoa hukumu katika kesi namba 80 ya 2005 iliyofunguliwa na Ndg Proches Tarimo na wenzake dhidi ya Wizara ya Ujenzi kupinga amri ya kuboma nyumba za wananchi zilizoko Mita 120 toka katika ya barabara pande zote; eneo la Mbezi Mwisho katika barabara kuu ya Morogoro iliyotolewa na TANROAD mwaka 2004, ikidai eneo hilo ni hifadhi ya barabara kwa mujibu wa sheria hiyo. Itakumbukwa kuwa amri hiyo ya TANROAD ilitolewa miaka mitatu baada ya Mhe John Magufuli kuteuliwa kwa mara ya kwanza kushika wadhifa wa Waziri wa Ujenzi na Rais Benjamin Mkapa na wananchi hao wamekuwa wakiishi maeneo hayo mika nenda rudi pasipo usumbufu wowote.

Itakumbukwa kuwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa barabara ya Morogoro na barabara zingine hapa nchini, ambao hivi sasa wanaoitwa wavamizi wa barabara na Mhe Magufuli, walihamishiwa katika maeneo hayo kwa nguvu tena wengine kwa kuchomewa makazi yao huko walikotolewa na Serikali ya awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere katika "Operesheni Vijiji Vya Ujamaa" iliyofanyika miaka ya 1970s wakati Mhe John Magufuli akiwa bado mtoto mdogo.

Huku Mhe John Magufuli akijigamba "kulinda na kutetea sheria" ya "The Highway Ordinance Cap 161 of 1967" Mahakama Kuu iliyoitamka kuwa batili tokea mwaka 2002 amewasababishia wakazi waishio pembezoni mwa barabara ya Morogoro madhara makubwa ya kisaikolojia, Kijamii na Kiuchumi kwa kuvamia Mita 120 za ardhi za wananchi toka katika ya barabara pande zote mbili za barabara na kuzuia maendelezo ya aina yoyote. Aidha kwa wakati mbali mbali amekuwa akiwaagiza TANROAD kuboma nyumba za wananchi isivyo halali kama ambavyo Mahakam Kuu imetamka.

Kifupi katika hukumu yake Mahakam Kuu Kitengo cha Ardhi imemuunga mkono Raisi Jakaya Kikwete kwa kutambua kuwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa barabara kuu ahpa nchini sio wavamizi wa barabara kama ambavyo Mhe Magufuli amekuwa akidai na kutumia wadhifa wake kuuaminisha umma wa watanzania hivyo. Na imetamka kuwa ardhi husika ni mali ya wananchi kupitia Sheria ya Ardhi ya Vijiji Kifungu cha 15 kwa kuwa waliwekwa hapo walipo na Serikali hiyo hiyo anayoitumikia Mhe Magufuli.

Mahakama hiyo pia imetamka kuwa kwa kuzingatia Sheria ya Mipango Miji eneo la hifadhi ya barabara kwa Jiji la Dar es Salaam ni Mita 30 tu pande zote mbili toka katika ya barabara; na kwa kuwa wanaoishi pembezoni waliwekwa hapo na Serikali katika operesheni Vijiji wanapaswa kulipwa fidia kwa mujibu wa Sheria za Ardhi na ikaeleza utaratibu wa kufuatwa na TANROAD kuamisha ardhi husika kutoka "Ardhi ya Kijiji" kuwa "Hifadhi ya barabara"

Kwa faida ya wasomaji wangu, ibara ya 27 (1) ya Kanuni ya Sheria ya Barabara Namba 13 ya 2007 zilizotolewa kupitia GN Notice No 21 ya tarehe 23 Januari 2009 inaeleza upana wa njia za barabara za lami hapa nchini. Na kwa barabara kuu upana huo usipungue Mita 3.25. Hivyo hivi sasa upana njia za barabara ya Morogoro Road yenye njia mbili ni Mita 6.5.

Hivyo katika upana halali wa hifadhi ya barabara uliotamkwa na Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kupitia hukumu hii wa Mita 30 kila upande wa barabara ya Morogoro. Upo uwezekano wa kujengwa njia 8 mpya za barabara kila upnde na kufanya barabara ya Morogoro Road kuwa ya njia 18 kabla ya TANROAD kuwafikia wananchi walioko nje ya Mita 30 za hifadhi ya barabara zilzotamkwa na Mahakama.

Kibaya zaidi Mhe John Magufuli anavunja hata Sheria ya barabara Na 13 ya 2007 na Kanuni zake 2009 ambzo katika ibara ya Ibara ya 27 (2,4,5) zinamtaka kuwa mara baada ya Waziri wa Ujenzi kuridhika kuwa ardhi fulani inahitajika kwa ajili ya maendeleo ya barabara, atafanya mawasiliano na Wizara wa Ardhi, kwa ajili ya ardhi hiyo kuhifadhiwa baada ya wananchi wanaomiliki ardhi hiyo kulipwa fidia. Na kuwa siku 60 baada ya wananchi kulipwa fidia ndipo Mamalaka ya brabara (TANROAD) itawataka wananchi kuondoka katika ardhi husika.

Baada ya Sheria mpya ya barabara ya 2007 kuongeza eneo la hifadhi ya barabara kutoka Mita 22.86 za zamani hadi Mita 30 kila upande kwa barabara zote kuu. Je Waziri Magufuli aliitia Sheria yake ya barabara kama ilivyofafanua haki za wananchi hapo juu au mara tu aliporejea kuwa Waziri katika Wizara hiyo mwaka 2010/11 aliwaagiza Mameneja wa TANROAD nchi nzima kuweka alama za X katika nyumba za wananchi zilizoko katika hizo Mita 8 zilizoongezeka kutokea 2009?.
Kama alifanya hivyo ukandamizaji wa haki za wananchi wa kiasi hicho ndio ""kulinda kusimamia na kufuata sheria"?


Kwa kuwa ibara 107 107A (1) ya Katiba ya Jamahuri ya Muungano wa Tanzania inatamka "The Judiciary shall be the authority with final decision in dispensation of justice in the United Republic of Tanzania". Kupitia hukumu iliyotajwa hapo juu ni wangapi humu JF watakubalina na mimi kuwa Mhe Magufuli hawezi kuwa na sifa ya "kufuata, kulinda na kusimamia sheria" kutokana na ukweli kuwa alishiriki kama mbunge kupitisha Sheria ya Ardhi Namba 15 mwaka 1999 na katika utendaji wake kwa muda wote tokea ateuliwe kuwa Waziri wa Ujenzi kwa mara ya kwanza mwaka 2000 na Rais Benjamin Mkapa hadi sasa amekuwa akiipuuza sheria hiyo na kutoa kipaumbele kwa "Kijikanuni" ambayo Mahakama Kuu imetamka kuwa ilipoteza nguvu kutokea 1999 lipotungwa, kupitishwa na kuwa Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na 15. Sheria sio kama Menu katika migahawa ambapo mlaji huchagua anataka kula nini.

1. Binafsi nakuona umeguswa na Dr.Magufuli kufuta 5% ya uzito wa magari

2. Umejitahidi kuandika lakini unatia huruma kupoteza muda wako, naijua sana sheria ya barabara unayoisema, Morogoro road ni barabara pekee yenye upana tofauti tofauti ukiacha barabara zingine zote inchini.

3. Uongo mkubwa kuwa Morogoro road itajengwa 18 lanes

4. Mengine wenzangu watanisaidia kwa vile naona umeumizwa, but pole piga ua Dr.Magufuli hakuna sehemu utakuta ana tatizo kisheria, yangu macho.

 
Last edited by a moderator:
Nchi hii inaeleka watu hataki maendeleo, mtu hata ajihidi vipi kuleta maendeleo, bado kuna wengine wanakubeza. Nakumbuka mwanza dar ilikuwa siku tatu leo ni siku moja bado watu hawakubali. Hakuna maendeleo yatakayokuja kwa kuchekeana na kuvunja sheria
 
Back
Top Bottom